Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe, Ummy Nderiananga amepongeza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es salaam kwa jitihada mbalimbali za kurejesha hali katika maeneo ambayo miundo mbinu ya barabara imeathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa
ziara yake leo Mkoani humo alipotemebelea na kujionea athari za mvua
zilizonyesha usiku wa kuamkia tarehe 20/ januari/2024 na kuathiri maeneo
mabalimbali ya wilaya ya Kindondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Jiji la Ilala.
Naibu Waziri Ummy alisema
anampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abert Chalamila kwa uongozi ambao wameuonesha
katika kurejesha halina kazi waliyofanya.
“Naomba tufanye kazi hii usiku
na mchana ili tuweze kurejesha hali mapema bila kuathiri shughuli za biashara na
shughuli nyingine za uchumi zinazofanyika katika Mkoa wa Dar es saalam,”
alihimiza.
Sisi kama serikali
tunawahakikishia wana Dar es salamu kwamba tutafanya kazi hii ya urejeshaji wa
hali kwa nguvu bila kuchoka,
Naye Mkuu wa wilaya ya
Kindondoni Mhe. Saad Mtambule amesema kazi waliyofanya ni kusimamia usafishaji
wa mitaro na usawishaji wa mito na hivyo kusaidia maji kutotuwama kwa muda
mrefu.
“Tumeendelea kuwaeleza
wananchi walio katika maeneo ya pembezoni mwa mito kama; Mto Nyakasangwa, Mto Mpiji,
Mto Tegeta, Mto Mlalakuwa na Mto Ng’ombe kuhamia maeneo ya juu ili kuepeuka
athari za mvua,”alibainisha
Ujenzi wa nyumba holela
umesababisha Watu kujenga mpaka kwenye mapito asili ya maji na kusababisha maji
kukosa sehemu za kupita na kuingia maeneo ya watu
“Lakini pia tuna kazi ya
kuendelea kuwaelimisha wananchi ili wafuate misingi ya ujenzi wa maeneo kulingana
na ramani ya mipango Miji,” alisisitiza
Akizungumza katika ziara hiyo
Mkazi wa Ununio Bw. James Koyi ameishukuru serikali kwa kazi kubwa inayofanya
ya urejeshajji wa hali katika maeneo yaliyoathirika mafuriko kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha mkoa wa Dar es salaam.