Monday, January 28, 2019

SERIKALI KUENDELEA KUKABILIANA NA MAJANGA NCHINI


NA.MWANDISHI WETU
Serikali kwa ushirikiana na wadau wengine imejipanga kuendelea kukabiliana na majanga yanayoikumba nchi ili kuhakikisha inashughulikia na kutatua majanga hayo pindi yanapotokea.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi Januari 28, 2019 wakati akifungua warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Tarishi alibainisha jitihada zinazofanywa na Serikali ili kukabili maafa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili kwa kuongeza idadi ya wilaya zenye mipango ya kupunguza madhara ya maafa, kuboresha mifumo ya tahadhari za awali, kuongeza utoaji wa elimu kwa umma na kuimarisha shughuli za kujiandaa, kukabili na kuimarisha mfumo wa uratibu wa masuala ya maafa.
“Kwa kuzingatia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17- 2020/21 tutaendelea kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili pamoja na kukabili majanga kwa kuzingatia utekelezaji wa malengo ya msingi ya Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030, tumedhamiria kuhakikisha tunakabiliana na majanga ili kujiletea maendeleo,”alisema Tarishi
Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia majanga yanayoikabili nchi ikiwemo mafuriko nchi haina budi kuwa mikakati hiyo ili kuhakikisha inakabili na kuweka mikakati yenye tija katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Tarishi alibainisha kuwa, mafuriko yamekuwa na athari nyingi kwa kulinganisha na majanga mengine yanayoikabili nchi mara kwa mara kwa kuzingatia takwimu zilizopo kwa sasa.
 “Takwimu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2018 mafuriko yameathiri wilaya 50 na kusababisha vifo kwa watu 71, majeruhi kwa watu 64, kuharibiwa nyumba 15,802 kwa viwango tofauti, kuathiri miundombinu katika shule 43, mashamba ya mazao mbalimbali, na vituo vya afya,”alisisitiza Tarishi
Alieleza kuwa, takwimu zilizopo tangu tupate uhuru nchi imeathiriwa na ukame zaidi ya mara 18 ikimo yale  ya mwaka 2006/2007 na 2007/2008 ambayo yaliathiri zaidi mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Lindi, Singida, Tabora na Mwanza.
Sambamba na hilo Ukame mwingine mkubwa ulitokea mwaka 2008/2009 ulioathiri zaidi mikoa ya kaskazini ya nchi hasa Arusha na Manyara. Mikoa ambayo mara nyingi huathiriwa na ukame ni Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga, ambayo kawaida hupata mvua ya chini kwa kiwango cha kati ya milimita 200 - 600 kwa mwaka.
Naye Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar, alieleza mipango mikakati ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzingatia ongezeko la madhara yatokanayo ya maafa ikiwemo vifo, upotevu wa makazi, pamoja na uharibifu wa mali za watu.
“Tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunakabili na kuzuia maafa yasitokee pale itakapotokea ili kuendelea kuwa na maendeleo endelevu katika mazingira tuliyonayo,”alieleza Abbashar
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Alvaro Rodriques, aliwataka wajumbe kuitumia fursa ya warsha hiyo kwa kuzingatia mada zitakazowasilishwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na wataalam na mikakati yenye kutatua madhara yatokanayo na majanga na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kushughulikia maafa.
AWALI
Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara imeratibiwa na Idara ya Usimamizi wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa na Taasisi ya Utafiti ya CIMA kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya. Aidha warsha inatarajiwa kudumu kwa siku tano hadi Februari 01, 2019 Jijini Dodoma. Warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Umoja wa Ulaya (EU) katika nchi za Africa, Caribbean na Pacific (ACP), ambayo inalenga kupunguza majanga katika nchi hizo.
Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar akizungumza kuhusu namna bora za kukabili majanga  wakati wa warsha hiyo.

Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriques akiwasilisha hotuba yake wakati wa warsha hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Alvaro Rodriques wakati wa warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika  ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano Dodoma hoteli Januari 28, 2019.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi pamoja na wajumbe wa meza kuu wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa warsha hiyo.

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bwana Alvaro Rodriques (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki katika warsha hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza jambo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar (wa kwanza kushoto) na katikati ni Mratibu wa Maafa wa Idara ya Maafa Bw.Charles Msangi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akiteta jambo na Watendaji wa Ofisi yake, katikati ni Kanali Matamwe Said, Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Maafa na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Utafiti Bw.Bashiru Taratibu

Sunday, January 27, 2019

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA WADAU WA KOROSHO MJINI MTWARA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako aliongoza kikao cha wadau wa zao la korosho, Januari 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mtwara ambako aliongoza kikao cha wadau wa zao la korosho, Januari 27, 2019.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha wadau wa zao la korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza katika kikao hicho alichokiitisha mjini Mtwara, Januari 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  kikao alichokiitisha cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika mjini Mtwara, Januari  27, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba.

Baadhi ya washiriki wa kIkao cha wadau wa zao la korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza katika kikao hicho alichokiitisha mjini Mtwara, Januari 27, 2019.

Saturday, January 26, 2019

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA TANZANIA BARA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Madini, Dotto Biteko, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019, kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, wakati akiwasili kwenye mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019, katikati ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Januari 26, 2019.

Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Januari 26, 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo, kabla ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, uliofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, mara baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019. Katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, nje ya  ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Januari 26, 2019.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu (kulia), akimsikiliza  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara jijini Dodoma Januari 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.

Friday, January 25, 2019

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA CWT TAIFA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taifa, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 25, 2019. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais , Deus Seif, Mweka Hazina , Abubakar Allawi, Katibu Mkuu, Christopher Banda na Wapili kulia ni  Rais wa CWT , Leah Ulaya.

Thursday, January 24, 2019

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA MPONDE WILAYANI LUSHOTO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde  katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 24, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde  katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 24, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde  katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 24, 2019.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAJUMBE WA BODI YA MISHAHARA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini.

Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye  utumishi wa umma.

“Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”

Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi  katika Utumishi wa Ummam, kwenye  Makazi ya Waziri Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya  Mishahara na Maslahi  katika Utumishi  wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni  Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa.

Saturday, January 19, 2019

MHE. MAVUNDE AWATAKA KAZI SACCOS KUWA NA MIRADI YENYE TIJA

 NA; Mwandishi Wetu - Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) Mhe. Anthony Mavunde ameutaka uongozi wa Kazi SACCOS kubuni miradi yenye tija ili kuboresha mfuko wao na kuleta manufaa kwa wanachama wake.
Ametoa rai hiyo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanachama wa SACCOS hiyo uliofanyika Januari 19, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TAKWIMU Jijini Dodoma.
Ameutaka uongozi wa chama hicho kubuni miradi ya kimkakati inayotekelezeka na kuendana na mazingira, na hali ya kiuchumi ya eneo husika.
“Ni vyema uongozi kuangalia fursa za kiuchumi zilizopo Dodoma ili kuanzisha miradi itakayoendana na hali halisi ya kiuchumi pamoja na kukikwamua chama chenu kuendelea kuwa na tija,” alisisitiza Mavunde.
Lengo la mkutano hilo lilikuwa ni kupeana taarifa za uendeshaji wa chama, kufanya uchaguzi wa viongozi wapya katika bodi ya uongozi na kamati ya usimamizi pamoja na kujadili namna bora ya kuendelea kuboresha Chama hicho ili kuendelea kuwa na tija kwa wanachama wake.
Aidha aliwatoa hofu wanachama kwa kueleza kuwa, uwepo wa vyama hivi ni kisheria na kikanuni za utumishi wa umma na kuwataka kuviheshimu ili kuendelea kuwa wanachama hai.
“Ieleweke kuwa ukiwa katika chama hiki, bado upo katika utaratibu na kanuni za utumishi wako hivyo muendelee kufanya vyema katika chama ili kujipatia heshima ndani na nje ya ofisi yako,” alisema Mavunde.
Aliwapongeza viongozi pamoja na wanachama wote kwa mchango wanaoutoa kwa ofisi yake kuzingatia mchango wa Chama kwa watumishi wote.
“Ninashawishika na kuona mchango wenu kwetu kama ofisi, kwani mmechangia kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wetu, ambao vinginevyo wangeshindwa kutoa huduma bora yenye tija kwa wadau wetu kutokana na changamoto za kifedha huwenda ingechangia kuwaingiza katika matendo ya utovu wa nidhamu kama vile rushwa”,alisisitiza Mavunde.
Pia aliwataka viongozi wa Ofisi yake kuendelea kuunga mkono jitihada hizo ambazo chama kimezionesha hususani uanzishwaji wa miradi ikiwemo ikiwemo kuwekeza katika viwanda.
Naye Bw. Omari Sama mwenyekiti wa chama hicho aliunga mkono maagizo hayo kwa kuanzisha miradi endelevu itakayoleta maendeleo ya kiuchumi kwenye chama, kuongeza wanachama na kukifanya chama hiko kitambulike zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo, Bw. Peter Kalonga aliuasa uongozi mpya kuendelea kutoa elimu ya ushirika kwa wanachama ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu Wanachama wa Kazi SACCOS Januari 19, 2019.Jijini Dodoma.


WAZIRI MKUU KUWAPOKEA WATALII 300 KUTOKA CHINA

   
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.

Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na kampuni ya TouchRoad International Holding Group ya China.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumamosi, Januari 19, 2019) alipokutana na Mwenyekiti wa Touchroad Group, Bw. Liehui He na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa na Bw. He huyo kwamba kundi hilo la watalii likiwa Djibouti litapokelewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na likienda Zimbabwe, litapokelewa na Rais wa nchi hiyo.

“Tanzania imeamua kuweka mkakati wa kuongeza idadi ya watalii nchini kwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza utalii kupitia vivutio vya vyakula vya asili, mavazi ya asili, wanyama, fukwe za bahari na milima. Kwa hiyo, ujio wa kundi hili kubwa, unatoa fursa mpya ya kutangaza vivutio vya nchi yetu,” amesema.

“Nitoe wito kwa Watanzania wanaoishi maeneo ya jirani na vivutio vyetu, wachangamkie fursa ya ujio wa watalii hawa katika maeneo mbalimbali. Wakifika Dar es Salaam, wanaweza kwenda Kigoma kuona Ziwa Tanganyika, mbuga zilizoko Nyanda za Juu Kusini, Arusha au vivutio vya Zanzibar. Tujiandae, tuwe tayari kuwauzia bidhaa mbalimbali,” amesema.

Pia amesema amefurahishwa na wazo lao la kuifanya Dar es Salaam iwe kitovu cha utalii (tourist hub) kwa makundi ya watalii ambayo yatakuja Tanzania na baadaye kutoka Tanzania kwenda Lusaka, Harare, Johannesburg na Djibouti.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwasili nchini juzi, ameambatana na ujumbe wa watu 31 ambao unajumuisha waandishi wa habari, wasanii, wanamuziki na watu mashuhuri.

Akiwa Beijing, China, wakati akishiriki mkutano wa Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na China lililofanyika Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu alikutana na uongozi wa kampuni ya TouchRoad ambayo ilionesha nia ya kutangaza fursa za utalii zilizopo hapa nchini.

Ziara ya Bw. He ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa kati ya kampuni ya TouchRoad na Bodi ya Utalii ya Tanzania, Novemba 2018.

Mapema, Bw. He alimweleza Waziri Mkuu nia ya kampuni hiyo kutekeleza makubaliano yao ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika soko la China ili kuvutia watalii wapatao 10,000 waitembelee Tanzania katika mwaka 2019.

“Tumepanga kuleta watalii 10,000 kwa mwaka huu wa 2019 na tumeweka lengo la kuongeza idadi hiyo kwa asilimia 20 kila mwaka kwa muda wa miaka mitano. Pia tuna lengo la kuitumia ndege ya ATCL ili ilete watalii moja kwa moja kutoka Shanghai, China,” alisema.

Akielezea ujio wa kundi la kwanza la watalii, Bw. He alisema kundi hilo litakaa Djibouti kwa siku moja, Tanzania siku nne (tatu za kulala) na Zimbabwe siku tatu (mbili za kulala) na kisha kurejea China.

Alisema wanapanga kila mwezi wawe na kundi kubwa la watalii ambao watakuwa wanafikia Tanzania na kupelekwa nchi nyingine kwa sababu Wachina wengi hupenda kufanya utalii kwa siku walau 10, lakini wapelekwe maeneo matatu au manne tofauti kuona vivutio vya aina nyingine badala ya kukaa sehemu moja kwa kipindi chote hicho.

“Watalii hawa wakija kwa siku tatu au nne, wana uhakika wa kutumia dola za Marekani zaidi 2,000, wakienda eneo jingine watatumia fedha pia, namna hiyo tuna uhakika wa kuongeza pato la Taifa, lakini pia tuna uhakika wa kutengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.

MAJALIWA AKUTANA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA TOUCHROAD GROUP YA CHINA, BW.He LIEHUI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dodoma, Januari 19, 2019.

Friday, January 18, 2019

WAZIRI MKUU AITAKA BODI YA PAMBA IFANYE KAZI KARIBU NA WAKUU WA MIKOA



*Ataka viongozi wote wasimamie kilimo hicho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Bodi ya Pamba ifanye kazi kwa karibu na Wakuu wa Mikoa ili kuhakikisha msimu huu zao hilo linafikia malengo ya uzalishaji.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa mikoa nane ya Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, Singida na Tabora inayolima pamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga.

Waziri Mkuu ameendesha kikao hicho kwa njia ya video (video conference) kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ili aweze kupata picha halisi ya kilimo cha pamba na hatua zilizofikiwa hadi sasa katika msimu huu wa kilimo.

“Lego letu mwaka huu 2019 ni kuzalisha tani zisizopungua 600,000. Wote mmeeleza kuwa wakulima wako kazini, pamba inalimwa, mnachosubiria ni dawa za kuuza wadudu waharibifu, na Bodi imeeleza kuhusu upatikanaji wa dawa hizo.”

Waziri Mkuu pia amesema viongozi wote wanapaswa kuwa karibu na wakulima ili waweze kubaini shida zao na kuzitatua kwa haraka. “Viongozi wote huko tuliko, zaidi ya asilimia 75 ya wa wananchi wetu ni wakulima. Kwa hiyo basi, tunapaswa tutenge asilimia zaidi ya 50 ya muda wa wetu kwenye mpango kazi ili tuweze kusimamia kilimo,” amesema.

“Wakuu wa mikoa peke yenu hamuwezi kufika kila mahali. Ni lazima maafisa ugani, maafisa kilimo na maafisa ushirika kwenye Halmashauri zetu waende kwa wakulima. Nikisema viongozi siyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya peke yao, Wizara nayo ina jukumu la kusimamia, viongozi wa AMCOS, vyama vikuu vya ushirika wote wawajibike kushirikiana na Serikali, waangilie ni nini tufanye ili kumkomboa mkulima.”

“Warajis wasaidizi, Ma-Ras wasaidizi wanaohusika na kilimo ni lazima washirikane kuhakikisha wakulima wetu wanajikwamua kutoka hapo walipo,” amesisitiza.

Mapema, akitoa taarifa ya maandilizi ya kilimo cha pamba kwa msimu huu, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba alisema hadi sasa wamekwishasambaza tani 27,000 za mbegu ambao ni zaidi ya asilimia 37 ikilinganishwa na usambazaji wa mbegu wa msimu uliopita.

“Hadi sasa mikoa yote imepata mbegu na zimeshapandwa na hali ya uotaji ni asilimia 100 kwani hatujapata malalamiko yoyote,” alisema.

Kuhusu dawa za viuadudu, Mkurugenzi huyo alisema wameshanunua chupa milioni sasa na vinyunyizi 23,000.

Wakichangia mjadala kwenye kikao hicho, kwa nyakati tofauti, Wakuu hao wa mikoa waliunga mkono dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kufufua ushirika kama njia pekee ya kumkomboa mkulima.

Walisema kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kuwatoa wakulima wa pamba kwenye utegemezi wa mikopo ili waweze kupata mbegu na pembejeo na badala yake wapewe elimu ya kujiwekea akiba tangu wanapovuna na lkuuza mazao yao.

MAJALIWA AKAGUA ENEO ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA UHURU KATIKA KIJIJI CHA MADUMA WILAYANI CHAMWINO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine.

“Uamuzi wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.

Wazee waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5 zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange na kila mmoja ajipange kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akihimiza. “Ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea hivi sasa ni fursa kwenu. Na ujio wa hospitali hii ni fursa nyingine kwa wana-Chamwino hasa kwa vile ujenzi wake utatumia mfumo wa force account ambao unatoa fursa kwa wanajamii kushiriki kazi za miradi ya eneo husika,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa hospitali hiyo yenye hadhi ya wilaya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza wananchi wapatiwe huduma za matibabu huko huko waliko. “Hadi sasa tumeshajenga vituo vya afya 350 ili kusogeza huduma kwa wananchi na jumla ya hospitali za wilaya 67, zinajengwa nchi nzima kwa mwaka huu,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji jirani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo alisema eneo la ujenzi wa hospitali hiyo liko umbali wa kilometa mbili kutoka barabara kuu ya Dar es Salaaam-Dodoma na kilometa tatu kutoka Ikulu ya Chamwino.
Naye, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa hiyo kwa kusomba mawe, mchango, maji na kwamba Kamati za usimamizi wa ujenzi zitapaswa kusimamiwa na wanakijiji.

Aliwataka wakazi hao wasiishie kwenye lengo la kuwa na hospitali ya wilaya, bali walenge kujenga hospitali yenye hadhi ya mkoa kwa kadri bajeti itakavyoruhusu.

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith Mahenge alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni wa hadhi ya wilaya ikiwa na nyongeza ya huduma za wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi (Emergency Department and Critical Care Unit).

Alimshukru Rais Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali hiyo sh. milioni 995.18 ambazo zilipaswa kutumika kwenye maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9, mwaka jana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuongezea kiasi kingine cha fedha cha sh. bilioni 2.35 na kutufanya sasa tuwe na sh. bilioni 3.22 za ujenzi huo,” alisema.




IDARA YA URATIBU MAAFA YARIDHISHWA NA HATUA ZA KUREJESHA HALI DARAJA LA DUMILA.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akimsikiliza Mratibu wa Kurejesha Hali Daraja la Dumila, Mhandisi wa TANRODS- Morogoro, Deogratius, akimueleza hatua walizochukua katika kurejesha hali ya  hilo ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa  maafa  ya mkoa na wilaya  zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akikagua sehemu ya kingo za daraja la Dumila, ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa  maafa  ya mkoa na wilaya  zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.

Muonekano wa mawe yaliyowekwa katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, ikiwa ni hatua ya kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ya  kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kuweza kupitika. Daraja hilo liliathirika  kingo zake kutokana  na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi.
Vyombo vya Usafiri, ikiwa ni magari, pikipiki na baiskeli pamoja na watembea kwa miguu wakipita  katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, baada ya kingo za daraja hilo zilizo kuwa zimeathiriwa na mvua  kujengwa kutokana na  mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi.  Hatua hiyo ilifanywa kwa wakati na kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro .