Wednesday, September 6, 2017

MAJALIWA AKABIDHIWA NA SPIKA WA BUNGE TAARIFA TA KAMATI YA KUCHUNGUZA BIASHARA YA TANZANITE NA ALMASI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Spika wa  Bunge, Job Ndugai Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.  Katikati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza Biashara ya Tanzaniate wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge Job Nduga  Taarifa hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Baadhi ya Wabunge walioshiriki katika hafla ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Spika wa Buge, Job Ndugai baada ya kukabidhiwa na Spika Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Spika wa Buge Job Ndugai akizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Spika wa  Bunge, Job Ndugai Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.  Katikati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza baada ya  kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza baada ya  kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Maalum iliyoundwa na Spika ya  Kuchunguza Biashara ya Tanzanite baada ya Spika kupokea Tarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai.

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Malum iliyoundwa na Spika   Kuchunguza biashara ya  Almasi baada ya Spika kupokea Taarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septembea 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai.

Read More

MAJALIWA AZINDUA MPANGO MKAKATI JUMUISHI WA KITAIFA WA LISHE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu,  kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza kabla ya kuzindua  Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Baadhi ya Washiriki wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango  nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe  baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba  6, 2017.  Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na kushoto  ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini nakala ya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya kuzindua Mpango huo kwenye ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango(kushoto kwake) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia kwake) wakionyesha vitabu vya Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe baada ya Waziri Mkuu kuuzindua kwenye ukumbi wa hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, watatu kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo, wapili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF nchini, Minaz Zaman na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID nchini, Andy Karas.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katia Uzinduzi wa Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe uliofanywa na Waziri Mkuu,  kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Septemba 6, 2017.

Read More

Tuesday, September 5, 2017

FANYENI TATHMINI YA ZAO LA KOROSHO – WAZIRI MKUU


*Apiga marufuku biashara ya kangomba, makato ya unyaufu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania zifanye tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kwa wakati na zimpatie taarifa mara moja.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana usiku (Jumanne, Septemba 5, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma kujadili mwenendo wa zao la korosho na ununuzi wa pembejeo.

“Lipo tatizo la tathmini ya maandalizi ya msimu kutofanyika kwa wakati na kusababisha matatizo kutotatuliwa kwa wakati. Bodi na Wizara zitoe tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kuhusu vyama vya ushirika vilivyojipanga, upatikanaji wa vifaa kama magunia na nyuzi, maghala, masoko, mizani, minada, malipo na mfumo wake,” alisema.

Waziri Mkuu pia alizitaka Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Korosho zitoe tathimini ya maandalizi ya msimu ujao katika maeneo ya mashamba, miche, pembejeo na viatilifu. 

Alisema tangu Serikali iamue kusimamia mazao makuu matano ya pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku hajapata muda wa kukaa na kuongea na wadau wote. “Serikali imeamua kufuatilia usimamizi wa mashamba; kusimamia upatikanaji wa mbegu, miche na pembejeo; kufuatilia uvunaji na mfumo wa masoko ya korosho na pia kufuatilia mfumo wa ushirika katika baadhi ya mazao,” alisema.

Alisema hivi sasa zao la korosho linalimwa katika wilaya 50 kwenye mikoa 11 ya Dodoma, Iringa, Lindi, Mbeya, Morogoro na Mtwara. Mingine ni Njombe, Pwani, Ruvuma, Singida na Tanga. 

“Katika msimu wa mwaka 2016/2017 zao la korosho lilikuwa ni moja kati ya mazao ya kibiashara yenye tija na faida nyingi kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni kiasi cha dola za Marekani milioni 346.6,” alisema na kuongeza kuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 watendaji hawana budi kujipanga vizuri ili zao la hilo liendelee kuliingizia Taifa dola nyingi zaidi kwa kuwa Serikali imetoa viatilifu bure.  

“Ninasisitiza eneo hili kwa sababu tumebaini kuwa korosho inachangia zaidi ya asilimia 50 ya mapato kwenye Halmashauri zinazolima kwa wingi zao hilo. Kwa kuwa zao hili ni la kimkakati, naitaka Wizara inipatie taarifa sahihi na kwa wakati,” alisisitiza.

Alisema Agosti mwaka huu, alipofanya ziara mkoani Tabora, alielezwa kwamba wilaya ya Uyui na Tabora Manispaa zimeanza kulima zao hili kama zao mbadala ili kuinua uchumi wa wananchi wake. “Tabora itakuwa mkoa wa 12, kwa hiyo Wizara ya Kilimo itembelee maeneo haya na kuona inawezaje kuwasaidia, ikaangalie uzalishaji ukoje kwani mti unaweza kukubali kuota pale Tabora lakini usizae kwa wingi kama ilivyo kwa mikoa mingine,” aliongeza.

“Viongozi wa juu Serikalini hadi kwa mtendaji wa kijiji ni lazima tusimamie zao la korosho, kila mtendaji ashirikiane na taasisi ambata, wizara mama iimarishe vyuo vya kilimo na utafiti. Kila mtendaji ni lazima ajue na wakulima wangapi, je kila mkulima ana ekari ngapi na kila ekari ina miche mingapi,” aliongeza.

Ili kurekebisha dosari zilizojitokeza katika msimu uliopita na kuboresha utendaji katika msimu ujao, Waziri Mkuu alisema Wizara na Bodi zinapaswa kufanya tathmini ya uhakika kwa kushirikiana na ofisi za mikoa. 

“Tumepata matatizo ya msimu kutoanza kwa wakati kwa sababu ya kukosekana kwa tathmini za nyuma, hatuna pa kuanzia kufanya marekebisho kwa sababu hatuna uzoefu wa yaliyojiri kwenye msimu uliotangulia. Siyo Bodi, Wizara wala Ofisi ya Mrajisi ambayo imekwishafanya tathmini. Kazi zote zimeacha kwa Wakuu wa Mikoa kupitia Sekretarieti za Mikoa.”

Akielezea kuhusu mwenendo wa biashara ya zao hilo, Waziri Mkuu alisema ili wakulima waweze kuwanufaika zaidi, Serikali imeendelea kuimarisha mfumo wa malipo wa stakabadhi ghalani na kupambana na watu wasio waaminifu wanaotumia kangomba. Kangomba ni kopo linalotumiwa na wanunuzi binafsi ambalo ujazo wake haufikii hata kilo moja, lakini wao wanalitumia kama kipimo cha kilo moja kununulia korosho kwa wakulima.

“Kuanzia sasa, biashara ya kangomba ni marufuku, kangomba ni wizi na yeyote atakayekamatwa, achukuliwe hatua za kisheria. Kila mkoa uweke mkakati makini wa kudhibiti biashara ya kangomba,” aliagiza.

“Hatutaki kusikia biashara ya kangomba. Viongozi wa Serikali msiwatumie vijana kwa kuwapa mitaji ili wafanye biashara hii. Mkizikamata korosho za kangomba, piga mnada na fedha ziende kwenye chama cha ushirika cha pale zilipokamatwa,” alisema.

Kuhusu makato ya unyaufu (shrinkage), Waziri Mkuu alisema kuanzia sasa, vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) na Chama Kikuu haviruhusiwi kutoza hela ya unyaufu kwa wakulima.

“Sheria ya unyaufu inasema utauza korosho kwa asilimia 0.5 ya bei halisi ya korosho iliyokaa kwa zaidi ya miezi sita. Sasa hapa kwetu msimu wa kuuza ni Oktoba hadi Desemba, unyaufu hapo unatoka wapi? Hili haliwahusu wakulima wetu kabisa,” alisema.

Alisema suala la unyaufu litawahusu wanunuzi ambao watakuwa wamenunua korosho na kuzihifadhi kwenye maghala kwa muda mrefu.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI, Bw. George Simbachawene; Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage; Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha; Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Tito Haule; Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Mama Anna Abdallah; Warajis Wasaidizi wa Mikoa; Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Mkurugenzi wa Maghala na Mizani, Wajumbe wa Bodi ya Korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Vyama vya Msingi, na Mameneja wa Vyama Vikuu.
Read More

WAZIRI MKUU AONYA WATAKAOKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mifumo miwili ya kielektroniki itakayosaidia kuandaa bajeti kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa na ameonya kwamba mifumo hiyo isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za Serikali .

Mifuyo iliyozinduliwa ni Kupanga Mipango, Kuandaa Bajeti na Kutolea taarifa za hatua za Utekelezaji wa Bajeti (Planning, Budgeting and Reporting System- PlanRep) pamoja na mfumo wa Kufanya Malipo na Kutoa Taarifa za fedha ambazo zimetumwa kwenye Vituo vya Kutoa Huduma (Facility Financial Accounting and Reporting System-FFARS).

Akizindua mifumo hiyo leo (Jumanne, Septemba 5, 2017) mjini Dodoma, Waziri Mkuu  amesema lengo la mifumo hiyo mipya ni kuongeza uwajibikaji na ufanisi na kamwe isiwe kikwazo katika utoaji wa huduma kwa jamii.
                              
“Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha Viongozi na Watendaji pamoja na Wananchi wote kwamba, lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali na isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za Serikali.”

Amesema ni muhimu mifumo hiyo itumike kwa ufasaha ili kuleta tija inayotarajiwa na kila muhusika kwa ahakikishe anailinda, anaitunza na kuitumia mifumo hiyo ili iweze kudumu na kuwa endelevu kwa manufaa ya Taifa.

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri na Vituo vya kutoa huduma za Elimu na Afya kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa mamlaka zinazohusika kwa wakati.
                    
Amesema ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa zitoe taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi wanaowahudumia kupitia mikutano, mbao za matangazo, tovuti, vyombo vya habari na njia nyinginezo.

Waziri Mkuu amesema kwa sasa Serikali haitarajii kuona kituo chochote cha kutoa huduma za Elimu na Afya kilichopo chini ya Halmashauri kinakuwa na matumizi yasiyozingatia taratibu na kanuni za fedha za umma.

“Hatutarajii kuona viongozi wa mikoa na halmashauri wakibadilisha matumizi ya fedha bila kuwasiliana na Mamlaka husika. Matumizi ya fedha yafanyike kutegemea chanzo cha fedha kilichopokelewa kwa wakati na kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa kwa mwaka husika.”

Amesema mifumo hiyo imeshirikisha Wizara za Kisekta na Taasisi za Serikali      ikiwemo Wakala wa Serikali Mtandao (e-Government Agency-eGA) kuanzia hatua za awali za ukusanyaji wa mahitaji hadi utengenezaji wa mifumo na ndiyo itakayotumika katika Halmashauri na Vituo vya kutolea Huduma za Jamii.

Waziri Mkuu amesema iwapo kuna mdau anataka kushirikiana na Serikali anapaswa kutumia na kuboresha mifumo hiyo na siyo kuleta mifumo mingine kwa sababu uwingi wa mifumo huondoa ufanisi na uwajibikaji.

“Serikali ina matarajio makubwa na mifumo hii, na nitapenda Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Ofisi yangu zipate taarifa zote za mipango, bajeti pamoja na taarifa za fedha zinazopelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati na zikiwa katika ubora wa hali ya juu.”

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bi. Inmi Patterson amesema mifumo hiyo iliyozinduliwa leo itaisaidia Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na uboreshaji wa huduma za jamii.

Amesema Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi kwa sababu vinakwamisha utoaji wa huduma mbalimbali za maendeleo kwa jamii.

“Ufisadi ni ugonjwa hatari na unaua kama magonjwa mengine yanavyoua. Ufisadi unazuia maendeleo ya jamii katika nchi husika pamoja na kukwamisha ukuaji wa uchumi na pia unaua ushindani na ndoto za vijana.”

Amesema anatambua namna ambavyo Rais Dkt. John Magufuli na wasaidizi wake wanavyopambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ili kuhakikisha fedha zote za maendeleo zinazotolewa zinatumika vizuri.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi Bw. George Simbachawene amesema mifumo hiyo itaziwezesha Halmashauri kupunguza gharama kubwa katika kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa Mipango na Bajeti kwani zilikuwa zikitumia muda mrefu na gharama kubwa kwenye kuandaa na kuwasilisha Bajeti.

Hesabu za mwaka 2017/2018 zilizotolewa zinaonyesha kuwa gharama za mchakato wa maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya mwaka kwa Halmashauri 185 ni takriban sh. Bilioni 8.32 za kulipia usafiri (Mafuta), posho ya kujikimu, shajala na gharama za kudurufu Vitabu.

Read More

MAJALIWA AZINDUA MFUMO WA KUAANDAA MIPANGO NA BAJETI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017 Kuzindua Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma . Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana. 
 Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Bi. Inmi Patterson akizungumza  katika Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa LAPF mjin Dodoma Septemba 5, 2017.
Baadhi ya washiriki wa Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozindua  mfumo huo  kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza  katika Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa LAPF mjin Dodoma Septemba 5, 2017.


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza  katika Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa LAPF mjin Dodoma Septemba 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya  Kuzindua Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma nchini. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017.


Baadhi ya washiriki wa Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozindua  mfumo huo  kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017.

Baadhi ya washiriki wa Uzinduzi wa  Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozindua  mfumo huo  kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya  Kuzindua Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma nchini. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma ulifanyika kwenye Ukukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Mrekani nchini, Bi. Inmi Patterson.Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Wapili kushotoni ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na watatu kushoto kwa Waziri Mkuu, ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuzindua Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma uliofanyika kwenye Ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Mrekani nchini, Bi. Inmi Patterson.Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Wapili kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na watatu kushoto kwa Waziri Mkuu, ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watalaam walioandaa Mfumo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma baada ya kuzindua mfumo huo kwenye ukumbi wa LAPF mjini Dodoma Septemba 5, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa marekani Nchini,  Bi. Inmi Pattersson. Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana.

Read More

Saturday, September 2, 2017

WAZIRI MKUU AMUAGIZA RC MORO KUFUATILIA UTENDAJI WA KAMPUNI YA ZHONG FENQ

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt Steven Kebwe na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kwenda katika kijiji cha Maseyu kufuatilia utendaji wa kampuni ya Zhong Fenq kama inafuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 2, 2017), wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa kiwanda cha Philp Morris kinachotengeneza sigara aina ya Marlboro akiwa  katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mkoani Morogoro.

Agizo hilo limefuatia malalamiko ya mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mheshimiwa Omary Mgumba kuwa wawekezaji hao kutoka China wanaendesha shughuli za uchimbaji wa mabo katika kijiji cha Maseyu wilayani Morogoro bila ya kuwa na kibali.

Mheshimiwa mgumba amesema tangu mwaka 2011 wawekezaji hao wameendesha shughuli zao bila  kulipa kodi za Serikali na tozo za Halmashauri, hivyo kuikosesha Serikali mapato.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kijiji cha Maseyu kuna Wachina wa kampini ya Zhong Fenq wanachimba mabo na hawana kibali na hakuna kodi yoyote wanayolipa Serikalini tangu mwaka 2010 walipoanza uzalishaji.”

Mbunge huyo ambaye machimbo hayo yako jimboni kwake aliongeza kwamba licha ya uongozi wa mkoa kwenda katika eneo hilo na kuizuia kampuni kuendelea na uchimbaji hadi itakapopata vibali walikaidi na kuendelea na shughuli.

Waziri Mkuu amesema hakuna muwekezaji anayeruhusiwa kufanya kazi bila ya kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hivyo ameagiza kesho Mkuu wa Mkoa afuatilie Wachina hao na kuona namna gani wamezingatia sheria za nchi.

Amesema iwapo watabaini kwamba wawekezaji hao  hawajafuata sheria, kanuni na taratibu hatua zichukuliwe dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika eneo hilo chini ya ulinzi na kuwasiliana na ubalozi wa China  Nchini.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema ni faraja kuona kiwanda cha Philp Morris kikiwa kimekamilika tayari kwa kuanza uzalishaji wa sigara aina ya Marlboro hivyo kuwezesha wakulima wa tumbaku nchini kuwa na soko la uhakika.

Amesema miaka ya nyuma uzalishaji wa tumbaku ulipungua nchini kutokana na wakulima kukata taama baada ya kukosa soko la uhakika pamoja na kuchoshwa na ubadhilifu wa mali za ushirika uliokuwa ukifanywa na viongozi wa vyama vya ushirika wa tumbaku.

Pia Waziri Mkuu alitembelea ujenzi wa kiwanda cha sukari kilichopo katika Gereza la Mbigiri wilayani Kilosa na kukagua shamba la miwa lenye ukubwa wa hekta 4,800 ambapo hekta 320 zimelimwa na kati yake hekta 125 tayari zimepandwa miwa na imeshaota.

Kiwanda hicho kinajengwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Magereza na mifuko ya hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia mradi wa Mkulazi ambao unatarajia kuzalisha tani 250,000 za sukari kwa mwaka kati yake tani 50,000 zitazalishwa katika kiwanda cha Mbigiri na tani 200,000 katika kiwanda cha Ngerengere.

Amesema uwepo wa viwanda nchini utawezesha watanzania kulima kilimo chenye tija kwa kuwa watauza mazao yao viwandani na mmoja atashiriki kulima zao ambalo ataliuza katika kiwanda cha jirani.
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akishiriki kupanda mbegu za miwa katika Shamba la  Gereza Mbigiri kwa ajili ya maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro jana Septemba 2, 2017.

Read More

MAMA MAJALIWA AHIMIZA BIDII YA MASOMO

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewataka watoto wanaojiandaa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, waongeze bidii kwani dunia ya sasa hivi inataka wasomi.

Mama Majaliwa ametoa wito huo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) wakati akizungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Martin Luther, kwenye sherehe za mahafali ya 10 zilizofanyika shuleni hapo katika Manispaa ya Dodoma.

“Ninawapongeza wanafunzi wanaohitimu lakini ni lazima mtambue kwamba huu siyo mwishi wa safari yenu ya masomo kwani dunia ya sasa inataka wasomi. Kwa hiyo, muongeze bidii hadi mfike elimu ya vyuo vikuu,” alisisitiza.

Aliushukuru uongozi wa shule hiyo na walimu wote kwa malezi mema wanayoyatoa kwa watoto hao na kwamba mafunzo yao yanadhihirika miongoni mwa watoto kwa jinsi walivyolelewa kimwili, kiroho na kiakili.

“Mtoto wangu nilimleta akiwa na miaka mitano, ameanza elimu ya chekechea na sasa anahitimu darasa la saba. Sasa hivi amekua na ana hofu ya Mungu, anatambua mema na mabaya, tunawashukuru sana,” alisema.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Gilbert Nhuguti wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji ya shule, alisema kwa zaidi ya miaka mitano, shule hiyo ambayo ni ya kutwa na ya bweni, imekuwa na rekodi ya kufanya vizuri kiwilaya na kimkoa kwa kushika nafasi za kwanza.

“Mwaka jana tulishika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya saba kitaifa kwa wastani wa daraja la ‘A’. Hata mwaka huu, kwenye mitihani ya majaribio (mock exams) tumeshika nafasi ya kwanza, tumepania kuchukua nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mwaka huu,” alisema.

Alisema mafanikio hayo yanachangiwa na ubora wa walimu wa shule hiyo ambao wana shahada, astashahada na stashahada.

Aliwataka wahitimu hao wawe mfano huko waendako, wamtangulize Mungu katika kila walifanyalo na wasiwe watu wa kutaka kupata makubwa bila kufanya kazi kwa bidii. “Fanyeni kazi kwa bidii na mafanikio yatakuja,” alisisitiza. Pia aliwataka waendeleza tabia ya kutunza  mazingira popote pale waendapo.

Naye Mbunge wa Mtera, Bw. Livingstone Lusinde ambaye alipewa nafasi kutoa nasaha kwa niaba ya wazazi, aliwataka wahitimu hao watambue kuwa wanapohitimu elimu ya msingi wajione kuwa wamejengewa msingi imara.

“Kuhitimu elimu ya msingi ni sawa na kujengewa msingi imara wa nyumba. Kwa hiyo, mkauendeleze kwa kujenga matofali imara, hautakuwa na maana kama mtaujenga kwa kutumia matofali mabovu juu yake,” alisema.

Wanafunzi wa darasa la saba kote nchini, wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kitaifa Septemba 6 na 7, mwaka huu.
Read More

FUATILIENI MAENDELEO YA VIWANDA KATIKA MAENEO YETU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo yao.

Amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) alipozungumza na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro alipofanya ziara katika kiwanda cha Moproco.

Alisema licha ya kukuza uchumi wa Taifa, viwanda vitasaidia katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana kwani vinauwezo wa kuajiri watu wengi.

“Viwanda hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa sababu vinauwezo wa kuajiri watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji wake.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya kilimo kuwa na tija.

Alisema kwa muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa soko.

Hata hivyo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji.

Pia aliwataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili kuviwezesha viwanda kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi ndani ya chini.

Awali Meneja Mkuu wa kiwanda cha Moproco, Bw. Arif Abood aliiomba Serikali kuongeza kodi kwa mafuta yanayotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.

Alisema uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kwa kiasi kukubwa ulichangia kufungwa kwa viwanda vya ndani vya mafuta kutokana na kukosa soko.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali. 
Read More

‘SERIKALI INATOA SH. BILIONI 22 KILA MWEZI KUBORESHA ELIMU’

SERIKALI imesema hivi sasa inatoa sh. bilioni 22.2 kila mwezi ili kuboresha elimu ya msingi na sekondari hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. George Simbachawene wakati akizungumza na wahitimu 166 wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Martin Luther, kwenye sherehe za mahafali ya 10 zilizofanyika shuleni hapo katika Manispaa ya Dodoma.

Waziri Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema Serikali itaendelea kuboresha elimu ya sekondari kwa kuajiri walimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi.

“Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu tunawakaribisha kwenye shule za sekondari kwa sababu zote zina walimu wa kutosha, madawati na vifaa vya kufundishia. Kila mwezi tunatenga sh. bilioni 22.2 kuendesha shule za msingi na za sekondari hadi kidato cha nne,” alisema.

Alisema hivi sasa, baadhi ya shule zinakabiliwa na changamoto ndogo ya upungufu wa walimu wa sayansi lakini nayo itatuliwa hivi karibuni kwa sababu vibali vya ajira vimeanza kutolewa.

“Tunaendelea kuziboresha na tumeshuhudia miaka ya karibuni wanafunzi bora kitaifa wakitoka katika shule za Serikali ambazo wengi wamezoea kuziita ni shule za kata. Hakuna shule za kata. Zote ni zimejengwa na Serikali,” alisisitiza.

“Ukienda vyuo vikuu, wanafunzi na ufaulu wa juu wengi wao ni wale waliotoka kwenye shule za Serikali,” aliongeza.

Aliwataka wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao Septemba 6 na 7, wasiwe na hofu kwani kufanya hivyo ni chanzo cha kuwafanya wachanganye mambo na kisha kufeli.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule hiyo, Bw. Rabbiely Mmanga aliwaasa wazazi na kuwaomba wasiwaingize watoto kwenye migogoro kwani matendo hayo yanawajisi watoto na kuwaathiri kisaikolojia hata wawapo shuleni.

“Ninawaomba sana wazazi, tofauti zenu ziishie chumbani na zisifike masikioni mwa watoto kwa sababu zinawasumbua kisaikolojia na kuwaharibia concentration yao kimasomo. Tumewahoji baadhi na wamesema wanaumia kwa kukumbuka adha ambayo mama anaipata kutoka kwa baba, au baba anaipata kutoka kwa mama,” alisema.

Katika mahafali hayo, wanafunzi mbalimbali walipewa vyeti kwa kufanya vizuri kwenye masomo mbalimbali huku Ismail Milambo na Nise-Magreth Malila wakiibuka kidedea kwenye masomo yote (best academic performers). Tuzo za nidhamu bora (discipline) zilichukuliwa na Michael Nyalusi na Sayuni Kampuni.

Wanafunzi wengine waliopata tuzo na masomo yao kwenye mabano ni Ismail Milambo (Hisabati), William Terry William (Kiingereza), Majaliwa K. Majaliwa (Sayansi), Nise Malira (Kiswahili), Clinton Dotto (Social Studies) na Justin Kilimali (Kompyuta).

Wengine walipewa tuzo kwenye vipengele vya michezo, uchoraji na sanaa, usafi, uongozi shuleni, uimbaji na uongozi wa ibada.

Katika risala yao, wanafunzi wanaohitimu walisema  wanaamini misingi ya elimu walioipata kwenye shule ya Martin luther haitapotea bure na wakaahidi kufanya mitihani yao kwa umakini ili watoke na ufaulu wa hali ya juu.

Wanafunzi wa darasa la saba kote nchini, wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya kitaifa Septemba 6 na 7, mwaka huu.
Read More