Wednesday, April 4, 2018

WAZIRI MKUU: VIWANDA 3,306 VYAANZISHWA NCHINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kaulimbiu yake ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda na kwamba hadi kufikia Februari 2018, viwanda vipya 3,306 vimekwishaanzishwa nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika viwanda kwa kutoa vivutio vya kodi na visivyo vya kodi kwa wawekezaji mahiri (strategic investors); kuendeleza na kuboresha miundombimu wezeshi kama vile barabara, reli, bandari, umeme na maji. “Serikali itaendelea kuhuisha sera, sheria na kanuni pamoja na kufuatilia utendaji wa viwanda vilivyobinafsishwa na kuchukua hatua stahiki kwa wamiliki walioenda kinyume na mikataba ya mauzo,” amesema.

Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba mikoa na Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya viwanda na kwamba katika mwaka 2018/2019, Serikali itatoa kipaumbele katika kutekeleza miradi ya kielelezo, uanzishwaji wa kanda maalum za kiuchumi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa sekta ya hifadhi ya jamii kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema pamoja na miradi mingine NSSF na PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wanatekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa sukari mkoani Morogoro.

“Lengo la mradi huo ni kuzalisha tani 250,000 za sukari na umeme megawati 40. Mradi huo unatekelezwa katika shamba la Mkulazi lililopo Ngerengere lenye ukubwa wa hekta 63,000 na shamba la gereza la Mbigiri lenye ukubwa wa ekari 12,000 lililopo Dakawa,” alisema.

“Hadi sasa ekari 2,000 za mashamba ya miwa zimetayarishwa katika eneo la Mkulazi na ekari 1,100 zimepandwa miwa. Lengo la Serikali ni kukamilisha awamu ya kwanza ya ufungaji wa mitambo ya kiwanda cha Mbigiri ifikapo mwezi Desemba, 2018 ili uzalishaji uanze mwaka 2019,” alisema na kuongeza kuwa miradi hiyo itakapokamilika, itazalisha zaidi ya ajira 100,000.

Waziri Mkuu alisema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo Juni 2017, ajira za moja kwa moja 780 na ajira zisizo za moja kwa moja  24,000 ikijumuisha wakulima wadogo wa mbegu na kilimo cha nje zimezalishwa.

Akifafanua kuhusu ujenzi wa barabara kuu, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kuboresha mtandao wa barabara nchini ambapo katika kipindi cha Julai 2017 hadi Februari 2018, ujenzi wa Km. 776.45 za barabara kuu kwa kiwango cha lami umekamilika na Km. 1,760 zinaendelea kujengwa. Pia barabara zenye urefu wa Km. 17,054 zilikarabatiwa katika kipindi hicho.

Kuhusu ujenzi wa madaraja, Waziri Mkuu alisema madaraja ya Kilombero na Kavuu ujenzi wake umekamilika na kwamba ujenzi unaoendelea hivi sasa ni wa madaraja ya Sibiti, Mto Mara, Lukuledi, Ruhuhu, Momba na Mlalakuwa. Alisema madaraja mengine 996 katika maeneo mbalimbali nchini yamekarabatiwa.

Kuhusu jitihada za Serikali kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema hadi kufikia Februari 2018, ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la TAZARA ulikuwa umefikia asilimia 70 na ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange) umeanza.

“Maandalizi ya awamu ya pili hadi ya nne ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka yanaendelea. Katika mwaka 2018/2019, Serikali imepanga kujenga kilometa 597 za barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami na kilometa 72 za kiwango cha lami zitakarabatiwa,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuliarifu Bunge juu ya uanzishwaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Roads Agency – TARURA) kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji na kuongeza kasi ya wananchi kujiletea maendeleo.

Alisema TARURA imepewa jukumu la kusimamia ujenzi na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 108,946.2 za vijijini na mijini. “Katika mwaka 2017/2018, TARURA imesimamia matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 4,183.3, madaraja 35, makalavati makubwa 43 na madogo 364 na drift nne,” alisema.

Waziri Mkuu aliliomba Bunge likubali kupitisha sh. 143,618,762,698 zikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2018/2019 ambapo sh. 74,527,321,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 69,091,441,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Vilevile, Waziri Mkuu aliliomba Bunge liidhinishe sh. 125,521,100,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo sh. 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,315,613,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Read More

MAJALIWA: SERIKALI YAAJIRI WAKAGUZI WA MAZINGIRA 450

Asema Serikali imeimarisha mifumo ya taarifa za ardhi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeongeza idadi ya Wakaguzi wa Mazingira kutoka 62 hadi kufikia 512 ili kuimarisha ukaguzi wa masuala ya hifadhi ya mazingira nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

Amesema katika mwaka wa fedha uliopita, jumla ya kaguzi 380 zimefanyika kwenye viwanda kwa lengo la kufanya tathmini za mazingira pamoja na kutoa elimu na uelewa kuhusu uendeshaji endelevu wa viwanda unaozingatia utunzaji bora wa mazingira.

“Kama nilivyoeleza katika Mkutano wa Kumi wa Bunge hili, halmashauri zote nchini zinapaswa ziweke mpango mahsusi wa kuhifadhi mazingira unaojumuisha kupanda na kutunza miti. Serikali itaweka utaratibu wa upimaji wa utendaji wa wakuu wote wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri unaozingatia uendelezaji na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao,” alisisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali inachukua hatua madhubuti za kuendeleza ardhi kutokana na umuhimu wake kama kitovu cha uzalishaji mali.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni kutekeleza mpango kabambe wa majiji, manispaa na miji; kudhibiti migogoro baina ya watumiaji wa ardhi na kuimarisha mfumo unganishi wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi nchini.

“Napenda kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba Mipango Kabambe ya Manispaa za Iringa, Singida na Mji wa Kibaha imekamilika na mipango mingine 20 ipo katika hatua mbalimbali za uandaaji. Hadi sasa, michoro 1,110 ya mipango miji imeshaidhinishwa kati ya 1,148 iliyopokelewa kutoka Halmashauri za miji mbalimbali,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wote wanapofanya shughuli za maendeleo, wazingatie mipango kabambe inayoandaliwa na mamlaka za upangaji miji kwenye maeneo yao husika.


Alisema Serikali imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na changamoto ya migogoro ya ardhi miongoni mwa watumiaji ikiwemo migogoro ya mipaka ya vijiji, wakulima na wafugaji, wanavijiji na hifadhi na mapori ya akiba.

“Moja ya hatua zilizochukuliwa ni kuunda timu ya kisekta ya kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo imetembelea mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Morogoro na Tabora na kufanya majadiliano na wadau 1,106. Hatua mbalimbali za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinaendelea kuchukuliwa.”

Kuhusu utendaji wa bandari nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali imeendelea kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ili kuifanya Tanzania iwe kitovu cha usafiri wa majini. Alisema uboreshaji huo utaanza na gati namba moja hadi saba; kuongeza kina na upana wa lango la kuingilia meli na eneo la kugeuzia meli; kuimarisha mtandao wa reli bandarini pamoja na kujenga gati maalumu la kuhudumia meli za magari.

“Vilevile, Mamlaka ya Bandari Tanzania imefungua ofisi katika baadhi ya nchi jirani kwa lengo la kuongeza urahisi wa kutoa huduma. Katika mwaka 2018/2019, Serikali itaendelea na uboreshaji wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara,” alisema.

“Serikali itatekeleza mradi wa dirisha moja la forodha (Tanzania Electronic Single Window System-eSWS) ili kuwaweka pamoja wadau wote wa kuondosha shehena bandarini na mipakani. Kukamilika kwa mradi huo, kutarahisisha na kupunguza muda na gharama za utoaji na upitishaji wa shehena bandarini,” alisema Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umejumuisha ujenzi wa mtandao wa miundombinu ya itifaki (Internet Protocol – Multiplier Label Switching) pamoja na ujenzi wa kituo cha kuhifadhi data ambacho hadi sasa mifumo ya taasisi 27 imeunganishwa ukiwemo mfumo wa ukusanyaji mapato wa TRA.

“Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaongeza usalama, usiri wa data, kujikinga na majanga na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali na muingiliano wa mifumo katika Kituo cha Data cha Taifa na vituo vingine vitakavyojengwa nchini,” alisema.

Kuhusu huduma ya mawasiliano vijijini, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ambapo vijiji 1,921 vimepatiwa huduma hiyo. “Serikali imeimarisha huduma za simu na intaneti katika taasisi za umma zikiwemo shule, vituo vya afya, vituo vya polisi na ofisi za posta.

“Katika mwaka 2018/2019, Serikali itaendelea kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kupanua matumizi yake hadi katika ngazi ya wilaya na kuzisimamia kampuni za simu nchini ili ziweze kutoa kumbukumbu sahihi kwa lengo la kukokotoa mapato yatokanayo na malipo ya huduma za simu za kitaifa na kimataifa,” alisema.
Read More

MAJALIWA AWASILISHA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye eneo la kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.
Baadhi ya wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipowasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua hotuba   kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba  baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi kwenye viwanja vya Bunge Mini Dodoma baada ya hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mini Dodoma Aprili 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa akipongezwa na Makatibu Wakuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Faustin Kamuzora -Sera na Uratibu(wapiti kulia), Eric Shitindi - Kazi, Akira na Wenye Ulemavu (kulia) na Maimuna Tarishi- Waziri Mkuu na Bunge (wapili kushoto) baada ya kuwasilisha   hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mini Dodoma Aprili 4, 2018. Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Kazi Uchumi na Jamii(LESCO), Det. Samwel Nyantahe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika (Katikati)  na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kwenye  viwanja  bunge baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Mtetezi CCBRT Bw. Fredrick Msigala kwenye viwanja vya Bunge baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabunge wa Viti Maalum, Faida Mohammed Bakari  (katikati), Azza Hilal Hamad (kulia) na Aisharose Matembe kwenye viwanja vya Bunge baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.


Read More

KAMATI ZA WATU WENYE ULEMAVU ZA MKOA KUTAMBULIKA KISHERIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Mtetezi CCBRT Bw. Fredrick Msigala kwenye viwanja vya Bunge baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu kwa kuzingatia sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kusimamia uundwaji wa kamati zinazoshughulikia masuala yao hapa nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) wakati akiwasilisha hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni dodoma.

Amesema Serikali itaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha uundwaji wa kamati zao zinazotambulika kisheria ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili na kuhakikisha kila mkoa unaunda kamati hizo ambapo hadi sasa mikoa 12 imekamilisha zoezi la uundwaji wa kamati hizo.

“Tayari Serikali imeunda kamati za watu wenye ulemavu katika mikoa 12 ya Geita, Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Njombe, Pwani, Singida, Rukwa, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Ufuatiliaji unaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa mikoa mingine nayo inaunda kamati hizo,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha uboreshaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, Serikali imeendelea kutoa vifaa zaidi ili waweze kushiriki katika shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa vifaa saidizi kwa jamii ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kufanya shughuli zao bila utegemezi kwa kuwapatia baadhi ya vifaa ikiwemo viti mwendo 240, bajaji 6, magongo ya kutembelea 350, kofia pana 128, fimbo nyeupe 175, miwani maalum kwa wenye uoni hafifu 70, shime sikio 20, vyerehani 8, vifaa vya kukuzia maandishi 65, mafuta maalum ya kukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua 35, viti maalum vya kuogea 50 na nyenzo nyingine za kujimudu,” alisema.

Alisema Serikali imeendelea kuviboresha vyuo vya watu wenye ulemavu vya Yombo, Dar es Salaam na Sabasaba, Singida ili kuhakikisha wanashiriki katika fursa zote ikiwemo za elimu ili wawe na ujuzi utakaowawezesha kushiriki katika fursa za ajira nchini ikiwa ni utekelezaji wa Sheria Na. 9 ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2010.

Alisema Serikali itaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kukamilisha uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Maendeleo wa Watu wenye Ulemavu, kuanzisha madawati ya watu wenye ulemavu, kuhamasisha sekta binafsi na umma kuweka miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu na kuwataka waajiri wote wawaajiri watu wenye ulemavu wenye sifa kwenye nafasi mbalimbali.
Read More

Tuesday, April 3, 2018

MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA STAR TIMES BUNGENI MJINI DODOMA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni  ya Star Times Group, Bw. Pang Xin Xing kabla ya mazungumzo yao, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Pang Xin Xing (watatu kushoto) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Star Media Tanzania Limited,Wang Xiao Bo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Makampuni ya Star Times Group,Zhang Ye  na kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Star Media Tanzania Limited, Juma Suluhu Sharobaro.

Read More

WABUNGE MTULIA WA KINONDONI NA MOLLEL WA SIHA WAAPISHWA

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akiingia Bungeni, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 
Mheshimiwa Maulid Mtulia akiapa kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.
Mheshimiwa Godwin Aloyce Mollel akiapa kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Maulid Mtulia kuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akizungumza na Mbunge wa Busega, Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Maulid Mtulia, (kushoto kwake) na  ujumbe wa wapenzi na mashabiki wa CCM kutoka Kinondoni waliomsindikiza mbunge huyo kutoka Dar es salam hadi bungeni Dodoma Aprili 3, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, Godwin Aloyce Mollel, (kushoto kwake) na  ujumbe wa wapenzi na mashabiki wa CCM kutoka Kinondoni waliomsindikiza mbunge huyo kutoka mkoani Kilimanjaro hadi  bungeni Dodoma Aprili 3, 2018.

 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akimwapisha, Godwin Aloyce Mollel kuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. 




Read More

MAJALIWA AZINDUA MBIO ZA MWENGE GEITA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipunga mkono kwa wananchi wakati aliposhiriki sherehe za kuwasha  Mwenge wa Uhuru,leo katika uwanja wa Magogo ,mjini Geita.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2,  2018. Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel  wakati alipotoa  salamu za mkoa huo katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita Aprili 2, 2018.

Watoto wakionyesha halaiki katika sherehe za kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru zilizoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana  sita watakaokimbiza Mwenge huo,Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. 

Read More

Sunday, April 1, 2018

MAJALIWA AWASILI MWANZA AKIWA NJIANI KWENDA GEITA KUWASHA MWENGE

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Aprili 1, 2018 akiwa njiani kuelekea Geita ambako Aprili 2, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha Mwenge wa Uhuru. Kiulia ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Aprili 1, 2018 akiwa njiani kwenda Geita ambako Aprili 2 , 2018 anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha Mwenge wa Uhuru.

Read More