Saturday, May 5, 2018

WATAALAM WA AFYA MOJA WAITAKA WIKI YA CHANJO KWA MIFUGO NCHINI

Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  mkutano  wa “Cross-Border” uliowakutanisha wataalamu  hao kutoka katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma kujadili  mikakati ya  kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Timothy  Wonanji ,akisisitiza jambo  wakati wa Mkutano wa mkutano wa “Cross-Border” uliowakutanisha wataalamu  wa Afya moja kutoka katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma  kujadili  mikakati ya  kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha.

Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janneth Mghamba,akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa mkutano wa “Cross-Border” uliowakutanisha wataalamu wa Afya moja kutoka katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma kujadili mikakati ya  kudhibiti ugonjwa wa Kimeta , Jijini, Arusha.

Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja  kutoka katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma wakifuatilia mkutano  wa “Cross-Border” uliowakutanisha kujadili mikakati ya  kudhibiti ugonjwa wa Kimeta, Jijini, Arusha.

Katika kuhakikisha kunakuwepo na udhibiti wa ugonjwa wa Kimeta na  Kichaa cha mbwa nchini wataalamu wa Afya moja ambao  ni wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, Afya ya Wanyama wafugwao na wanyamapori pamoja na sekta ya Mazingira, wameitaka serikali kuanzisha wiki ya chanjo kwa mifugo nchini ili kuhamasisha chanjo hizo kwa kuwa na mkakati wa pamoja na kwa wakati mmoja na hatimaye kuweza kudhibiti maaambukizi ya magonjwa hayo kwa binadamu.
Ugonjwa huu huwapatawanyama na binadamu kwa njia ya kung’atwa na Mbwa, Paka, Fisi au mnyama mwingine anaye ugua kichaa cha mbwa. Ugonjwa huu hauna tiba ila unazuilika kwa njia ya chanjo.

Wakiongea jijini Arusha  wakati wa Mkutano wa Ujirani wa kujiandaa, kujikinga na udhibiti wa magonjwa, uliowakutanisha wataalamu hao kutoka katika mikoa ya  Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dodoma, wamebainisha kuwa wameamua kutoka na azimio hilo kutokana na kuwa katika baadhi ya wilaya za mikoa hiyo milipuko ya  ugonjwa  wa kimeta imekuwa ikijirudia hata ndani ya mwaka moja.
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janneth Mghamba,amesema Wizara imekuwa ikipokea taarifa za ugonjwa  wa Kimeta mara kadhaa katika baadhi ya Wilaya za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro hali inayodhihirisha hakuna mikakati ya kutosha ya udhibiti wa ugonjwa huo.
“Kinga ni bora kuliko matibabu, hivyo ili kudhibiti haya magonjwa yanayotoka kwa wanyama hatuna budi kujikita katika chanjo ya wanyama hao ili kupunguza maabukizi ya wanyama hao kwa binadamu ,  Chanjo ya Kimeta na kichaa cha mbwa kwa wanyama ni ndogo kuliko matibabu yake. Tukiwa na uhamasishaji mzuri wa chanjo na hasa kupitia hata wiki ya chanjo, serikali itaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika katika tiba ya magonjwa hayo” Alisema Mghamba.
Aidha Mghamba aliongeza kuwa , katika kuhakikisha kunakuwepo na mikakati ya udhibiti wa ugonjwa huo imewakutanisha wataalamu wa afya wa mikoa husika  kwa kutumia dhana ya afya moja ili waweze kujadili kwa pamoja na kuwa na mipango ya udhibiti ya pamoja kwani magonjwa hayana mipaka, Aidha hatua hiyo ya kuwa na mikakati ya pamoja itaweza kupunguza gharama za udhibiti wa magonjwa.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Timothy Wonanji  na Daktari wa wanyamaWilayani Monduli,Dkt. Yandu Marmo  wamefafanua kuwa upo mwingiliano mkubwa wa wanyama na binadamu, katika hali hiyo uwezekano wa magonjwa ya wanyama kuwaambukiza binadamu ni mkubwa. Aidha walieleza kuwa kukiwepo na kampeni maalum ya kuhamasisha kuchanja wanyama kutapunguza maabukizi ya magonjwa hayo.
Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 60% ya magonjwa wanayoyapata binadamu yanatoka kwa wanyama. Kwa kulitambua hilo,Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini, Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.


Read More

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA JENGO LA HUDUMA ZA MATUNZO NA TIBA KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI MANYARA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI linalojengwa katika Halimashauri ya Wilaya ya Simanjaro ,Mkaoani  Manyara Mei 05, 2018.
Mganga Mfawidhi Hassan Ishabailu akitoa ufafanuzi wa huduma za afya zinazotolewa na  Kituo cha Afya Mirerani kwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  alipozindua Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wagonjwa aliyekuwa akisubiri huduma za matibabu katika Kituo cha Afya Mirerani wakati wa Uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mei 05, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati wa Uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mei 05, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwapongea baadhi ya wazazi waliojifungua katika Kituo cha Mirerani Mkoani Manyara wakati wa Uzinduzi wa Jengo la jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akifafanua jambo wakati wa mkutano na wananchi wa Simanjiro (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.

Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ulemavu Wilayani Simanjiro Bw Robert Songa akieleza masuala yao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wauzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.

Mwenyekiti wa UVCC mkoa wa Manyara, Moses Komba akieleza masuala ya vijana wa mkoa wa Manyara kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake anayeshughulikia Waziri Mkuu na Bunge Bi.Maimuna Tarishi wakati wa uzinduzi wa jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.

Mbunge wa Viti Maalum Manyara, Mhe.Ester Mahawa akikabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mirerani kilichopo Wilaya ya Simanjiro kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama

Read More

Thursday, May 3, 2018

MAAMUZI YA RAIS YA KUUPANDISHA HADHI MJI WA DODOMA NA KUWA JIJI NI SAHIHI-MAJALIWA

*Asisitiza kwamba hakuna sheria iliyokiukwa

WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema maamuzi ya  Rais Dkt John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria iliyokiukwa.

Aprili 26, 2018 Rais Dkt Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 3, 2018) wakati akijibu swali la Bibi Felista Bura (Viti Maalumu) katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Bibi Felistaalitaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuupandisha hadhi mji wa Dodoma.

Amesema kuwa Rais Dkt Magufuli hakukiuka sheria kwa sababu ana mamlaka kwa mujibu wa katiba ibara 2 na sheria ya Mamlaka  ya Serikali za Mitaa sura ya 288 kupandisha hadhi mji au eneo lolote kadiri ya mahitaji yatakavyohitajika .

Waziri Mkuu amesema hata kitendo cha Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali pamoja na upatikanaji wa miundombinu muhimu kama ya afya, maji, umeme, barabara na kuendelea kukua kwa ukusanyaji mapato ni vigezo tosha vya kuufanya mji wa Dodoma kuwa Jiji.

"Pia Dodoma inajitosheleza kwa mahitaji mengi ikiwemo uwepo wa taasisi mbalimbali muhimu kama Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, vyuo vikuu zaidi ya vitano, Ofisi ya UN, hivyo nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt Magufuli kwa uamuzi wake kwani unaleta tija kwa wananchi. Nashauri jambo hili lipongezwe badala ya kubezwa”. 

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufuatilia utaratibu wa uingizwaji wa mafuta ya kula nchini kutokana  na uwepo wa baadhi ya wafanyabishara wasiokuwa waaminifu kuingiza mafuta safi na kudai ni ghafi. 

Waziri Mkuu amesema ghalama za kulipia kodi mafuta hayo inatofautiana, mafuta ghafi yanalipiwa asilimia 10 na safi ni asilimia 25 hivyo lazima Serikali ifuatilie ili wahusika waweze kutozwa kodi inayostahili.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kulinda viwanda vya ndani vya mafuta, hivyo ni lazima taratibu za uingizwaji wa mafuta ukazingatiwa wakati huu ambao nchi inahitaji mafuta ya nje kwa kuwa uzalishaji wa ndani bado haujajitosheleza. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbles Lema aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali isione umuhimu wa ungizwaji wa mafuta kutoka nje  ili kusaidia kupunguza  bei ya mafuta ya kula ambayo bei yake imeongezeka kwa asilimia 15 hadi 30.
Kuhusu suala la kuongezeka kwa bei ya sukari nchini hususan katika kipindi cha kukaribia kuanza kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa mikoa, wilaya na Maofisa biashara kuhakikisha wanawasimamia wafanyabiashara hawapandishi bei za bidhaa kiholela.
Amesema kitendo cha wafanyabiashara kupandisha bei za baadhi ya bidhaa katika kipindi hicho hususani sukari kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuwapa adhabu waumini wa madhehebu ya kiislamu watakaokuwa kwenye mfungo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kuteuliwa Bw. Abdalla Bulembo ambaye alisema mwezi Mtukufu wa Ramadhani umekaribia na bei ya bidhaa kama sukari imeanza kupanda  na kufikia 2,800 , 3,000 na 3,200, hivyo Serikali inatoa tamko  gani  juu ya suala hilo.
Waziri Mkuu amesema Serikali  inalifanyia kazi suala hilo na tayari vibali vya kuagiza sukari vimeshatolewa ilikuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana wakati wote, ambapo Bodi ya Sukari kupitia Wizara ya Kilimo inaedelea kufuatilia mwenendo wa uingizwaji wa sukari nchini ili iweze kusambazwa hadi kwenye vijiji.
Read More

MATUKIO BUNGENI 3.5.2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza, bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia Bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Anne Kilango Malecela, Bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikalikwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Mei 3, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayengakwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Mei 3, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Mei 3, 2018, kutoka kushoto ni Godfrey Nago, Abdulhamid Nzota na Mtumishi wa Wizara ya Ujenzi, Stanford Matovolwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Mei 3, 2018.

Read More

Tuesday, May 1, 2018

WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU KUENDELEA KUTOA HUDUMA KWA UFANISI KWA WATANZANIA

Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipita katika viunga vya jiji la Dodoma kuelekea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri kushiriki seherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, leo tarehe 1 Mei, 2018.

Baadhi ya Wafanyakazi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakishiriki maandamano ya kuelekea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri kushiriki seherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, leo tarehe 1 Mei, 2018, Jijini Dodoma.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipita mbele ya mgeni rasm wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani  zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 1 Mei, 2018.

Baadhi ya Wafanyakazi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri leo tarehe 1 Mei, 2018, Jijini Dodoma.
na Mwandishi wetu
Katika kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani, wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameungana na wafanyakazi wote Duniani kwa kujumuika na wafanyakazi wengine wa hapa nchini jijini  Dodoma na kuahidi  kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi kwa Watanzania.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe hizo wafanyakazi hao, wamesema kuwa ofisi ya Waziri Mkuu kama mratibu wa shughuli zote za serikali nchini na kama mratibu wa shughuli za Kazi na ajira nchini wataendelea kutekeleza majikumu hayo kwa uadilifu na ufanisi ili huduma zinazotolewa na serkali ziwe zenye tija kwa Watanzania.
Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na kuratibu Shughuli zote za serikali ndani na nje ya Bunge pia inaratibu masuala mtambuka, kama  shughuliza maafa, Udhibiti wa matumizi ya madawa ya Kulevya, Vita dhidi ya UKIMWI, Huduma kwa watu wenye Ulemavu. Aidha inahusika na  kuchapa nyaraka za uendesheshaji shughuli za serikali, masuala ya Vyama vya siasa, Masuala ya Uchaguzi, Masuala ya kazi, Ajira na maendeleo ya vijana, pamoja na masuala ya uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Maadhimisho ya sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu zimebebwana kauli mbiu ya “Uunganishaji wa Mifuko ya Jamii ulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi”

Read More