Thursday, June 28, 2018

SERIKALI KUBORESHA MFUMO WA HUDUMA ZA VIBALI VYA AJIRA NA UKAAZI NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao kuzungumzia azma ya Serikali ya kuboresha mfumo wa huduma za vibali vya ajira na ukaazi nchini hii leo Juni 28, 2018 Jijini Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipokutana Bungeni Dodoma Juni 28, 2018

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipokutana Bungeni Dodoma Juni 28, 2018.  
NA MWANDISHI WETU
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (Idara ya Uhamiaji) imekusudia kufanya mabadiliko ya kimfumo ambayo yatahusisha utoaji wa vibali ya ajira nchini pamoja na vibali vya ukaazi ili kuhama kutoka mfumo wa zamani na kuwa na mfumo wa kielektroniki.

Maboresho hayo yanakwenda sambamba na matumizi ya TEHAMA, ambapo kutakuwa na utaratibu wa kuwa na kadi moja (smart card), ambayo itakuwa na taarifa za muhusika kuhusu kibali cha ajira pamoja na hati ya ukaazi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama alikukutana na waandishi wa habari hii leo Mjini Dodoma (Juni 28, 2018).
Waziri Mhagama alieleza kuwa, kuanzishwa kwa mfumo huo utasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni nchini zenye uhakika na zitakazo patikana kwa wakati ili kudhibiti mianya yote rushwa kwa watendaji kwa kuwa taarifa zote zitapatikana katika kanzidata maalum.
“Uwepo na mfumo huu mpya utasaidia kuondokana na mianya yote ya rushwa kwa Watendaji wa Serikali pamoja na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wageni na malengo ya ujio wao hapa nchini kwani taarifa zote zitapatikana kwenye kanzidata maalum,”alisisitiza Mhagama
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba alieleza kuwa mfumo huu wa kadi moja utasaidia hutatua changamoto ya uchuleweshaji wa vibali ili kuondokana na usumbufu wa ufuatiliji wa vibali hivyo kwa wageni.

“Lengo kubwa la mabadiliko haya ni kuwa na kadi moja itakayomruhusu mgeni kufanya kazi kulingana na sheria na taratibu zilizopo na kuwaondolea usumbufu usio wa lazima na kuongeza ufanisi kwa watendaji wa Serikali,” alisisitiza Mwigulu
Aidha alitoa rai kwa Taasisi zote zinazotumia wageni kuhakikisha wanafanya uhakiki wa taarifa za wageni hao hususan uhalali wa kuwepo kwao pamoja na kazi wanazozifanya ili kuepuka udanganyifu unaoweza kujitokeza.
“Nitoe rai kwa Taasisi zote zinazotumia wageni katika ofisi zao kuhakiki na kujiridhisha taarifa za vibali vya ajira na ukaazi wa wageni hao ili kuepuka taarifa zisizo sahihi na kuhakikisha kila kila mgeni anakuwa na kibali halali kinachomruhusu kuwepo nchini,”alisisitiza Mwiguli
Read More

Wednesday, June 27, 2018

WAZIRI MKUU ATOA MWEZI MMOJA KWA WATUMISHI BAHI

*Ataka apewe majina ya watakaokiuka agizo hilo
*Akataza magari ya Serikali kulala nyumbani kwa mtu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo Julai 30, mwaka huu.

“Tunataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo Julai 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao,” amesisitiza.

Pia ameagiza magari yote ya Serikali baada ya kuisha muda ya kazi yawe yameegeshwa kwenye ofisi za halmashauri na ni marufuku kwa magari hayo kulala nyumbani kwa mtu.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali inataka watumishi wote wa umma nchini waishi kwenye vituo vyao vya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ukaribu katika maeneo husika.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Bibi. Rachel Chuwa aanzishe mradi wa upimaji wa viwanja na viuzwe kwa watumishi na wananchi kwa gharama nafuu.

Waziri Mkuu amesema ni vema wilaya hiyo ikachangamkia fursa ya Serikali kuhamia Dodoma kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo nyumba za kuishi, hoteli na sehemu za burudani ili watumishi waliohamia Dodoma wapate sehemu za kujipumzisha pindi wamalizapo majukumu yao.
Read More

WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA

WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.

Amesemakuwa kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”. 

Vituo hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”. 

Amesema kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe. 

“Pia, mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za mafuriko         na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda Wizara nyingine,” amesema. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.
Read More

SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA MAFUTA YA KULA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kufanya mageuzi makubwa katika zao la michikichi, alizeti na ufuta.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Balozi Dkt. Ramadhan Dau ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma.

’’Tunataka kufanya mageuzi makubwa ya zao la michikichi, tunataka kuondoa miti ya zamani na kupanda miche mipya. Tutafanya kampeni ya kuhamasisha upandaji wa miche mipya ya michikichi ili tuondoe tatizo la upatikanaji wa mafuta nchini,’’.

Waziri Mkuu amesema licha ya kuwepo kwa michikichi mingi nchini ila uzalishaji wake unafanyika kwa njia kienyeji, hivyo Serikali imedhamiria kuboresha kilimo hicho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili liweze kuleta manufaa makubwa kwa Taifa na wakulima.

Amesema mbali na zao la michikichi, pia Serikali imedhamiria kuboresha mazao mengine ya mbegu za kukamua mafuta kama alizeti na ufuta, ambayo itayafuatilia kuanzia hatua za awali za uandaaji wa mashamba hadi masoko.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania bado ipo chini kwenye uzalishaji wa mbegu za kukamulia mafuta na inahitaji wawekezaji katika mazao hayo, hivyo amemuagiza Balozi wa Tanzania nchini Malaysia atafute wawekezaji hao.

’’Inawezekana kujitosheleza kwa mafuta ya kula kwa sababu Tanzania tuna ardhi ya nzuri yenye rutuba na watu ambao kilimo ndiyo shughuli yao kubwa. Na hivi karibuni nitafanya ziara mkoani Kigoma kwenda kuhamasisha kilimo cha michikichi,’’.

Kwa upande wake, Balozi Dkt. Dau amesema Malaysia ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kilimo cha michikichi na inatengeneza zaidi bidhaa 400 kutokana na zao hilo, yakiwemo mafuta ya kuendeshea magari.

Balozi Dkt. Dau amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba atatafuta wawekezaji kutoka nchi za Malaysia na Indonesia ili waje kuwekeza kwenye mashamba na viwanda vya mafuta na sukari.
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA, DKT. DAU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Juni 27, 2018.
Read More

MAJALIWA AZINDUA VITUO 51 VYA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA WILAYNI BAHI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.   Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wanne kushoto ni Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly.
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika  uzinduzi wa vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.  Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo cha kupima wingi wa mvua baada ya kuzindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama,Waziri wa Maji, Mhandisi Isaack Kamwele, Mwakilishi Mkaazi wa Mpango  wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie  Boucly na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma, Felista Bura.

Read More

Tuesday, June 26, 2018

WAZIRI MKUU KUZINDUA VITUO 51 VYA HALI YA HEWA VINAVYO JIENDESHA VYENYEWE, VITUO 15 VYA KUPIMA WINGI WA MAJI MTONI, KANZIDATA YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA KITUO CHA OPERESHENI NA MAWASILINO YA DHARURA.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Vituo 51 vya Hali ya Hewa vinavyojiendesha vyenyewe, Vituo 15 vya Kupima wingi wa maji Mtoni, Kanzidata ya Taarifa za Hali ya Hewa pamoja na Kituo cha Operesheni na Mawasilino ya Dharura. Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, tarehe 27 Juni, 2018 katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma. 

Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) litaonesha shughuli hiyo mubashara kuanzia saa sita mchana. Akizungumza wakati wa maandalizi ya Uzinduzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na kuwakaribisha wananchi wote kushiriki katika uzinduzi huo, amebainisha kuwa Kuzinduliwa kwa vituo hivyo , kanzidata na kituo cha Operesheni na Mawasiliano nchini ni baadhi ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha menejimenti ya maafa inaimarika nchini.

 “Vituo hivyo vitawasaidia Watanzania ambao ni wadau wakubwa wanaotumia Taarifa za Hali ya Hewa katika kupata taarifa za awali za utabiri wa uwepo wa majanga au kutokuwepo ili kujiandaa, kuyakabili endapo majanga yatatokea pamoja na kusaidia katika maandalizi ya shughuli za maendeleao ikiwemo upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kusaidia kupanga aina za mazao yanayofaa kulimwa kulingana na mabadiliko ya tabia nchi”, amesema Mhagama Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali, imeweza kuimarisha miundombinu na mazingira ya kufuatilia taarifa za mabadiliko ya tabianchi na kutengeneza mifumo imara ya kutoa tahadhari za awali, usimamizi wa maafa na kuchangia katika mipango ya maendeleo endelevu. 

Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali, Uliandaliwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kufadhiliwa kupitia Mfuko wa Uboreshaji wa Mazingira Duniani (GEF). Mradi umetekelezwa na Wizara na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania, tangu mwaka 2014 hadi Juni mwaka 2018. 
Read More

KIKOSI KAZI CHA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA CHATEMBELEA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA DODOMA

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Salome Kassanga akitoa maelezo kuhusu wodi maalum ya viongozi wa Serikali iliyopo katika hospitali hiyo kwa wajumbe wa Kikosi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea Juni 25, 2018.

Baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakipata maelezo ya kuhusu hospitali ya Benjamini Mkapa kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa hospitali hiyo Dkt. walipotembelea Juni 25, 2018 Dodoma.

Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika dirisha la mapokezi hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Chuo kikuu cha Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Salome Kassanga akitoa maelezo kwa baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea hospitali hiyo kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Salome Kassanga akitoa maelezo ya matumizi ya mitambo ya kuchunguza, kuzibua na Kutibu mishipa ya moyo  iliyopo katika Hospitali hiyo walipotembelea kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.

Muonekano wa mashine za upasuaji wa matundu madogo (endoscopys) vilivyofungwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Muonekano wa mashine ya CT-Scaniliyofungwa katika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Muonekano wa Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma.

Katibu wa Kikosi kazi cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Salome Kassanga juu ya matumizi ya mashine za upimaji wa mfumo wa chakula (Fluoroscopy) iliyopo katika hospitali hiyo Juni 25,2018.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Salome Kassanga akionesha sehemu ya ujenzi unaoendelea katika hospitaliya Benjamin Mkapa ikiwa ni moja ya Mpango wa kuongeza jengo la kutolea huduma za afya.

Read More

UZINDUZI WA VITUO VYA HALI YA HEWA NA KITUO CHA OPERESHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA


Read More

Monday, June 25, 2018

BUNGENI LEO 25.06.208

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwanamuziki Mkongwe Mzee Makassy  na wasanii wenzake katika Viwanja vya Bunge , Juni 25/2018 .Kulia ni Mbunge wa Viti maalumu Martha Mlata
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba , bungeni jijini Dodoma  Juni 25/2018

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki)  na wasanii wenzake  katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma  Juni 25/2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, kushoto mwenye kofia nyekundu ni Mzee Makassy na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wanamuziki wakongwe kwernye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma  Juni 25/2018


Read More

SHEREHE ZA KUHITIMISHA KUWEPO MADARAKANI KWA MTUKUFU AGAKHAN

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akigonganisha glasi kumtakia afya njema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli na Mtukufu Agakhan, katika sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma Juni 25, 2018. Kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai na katikati ni   Mwakilishi Mkazi wa Mtandao wa Mashirika ya Maendeleo ya Agakhan (AKDN) Amin Kurji.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa na Bw. Mehboob Chamsi pochi iliyotengenezwa Tanzania, katika  sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, zilizofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma Juni 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia shati lililotengenezwa Tanzania, katika sherehe za kuhitimisha kuwepo madarakani kwa Mtukufu Agakhan, zilizofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma Juni 25, 2018, kutoka kushoto ni Muwakilishi Mkazi wa Mtandao wa Mashirika ya Maendeleo ya Agakhan (AKDN) Amin Kurji akifuatiwa na Bw. Mehboob Chamsi. 

Read More

Sunday, June 24, 2018

PROF KAMUZORA ATEMBELEA MRADI WA MFUMO UNGANISHI WA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA ARDHI(ILMIS) WILAYA YA KINONDONI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati wa ziara fupi kukagua ujenzi wa chumba kitakachokuwa kinatoa huduma za Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi (ILMIS)  katika Mradi wa Mfano Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Katibu  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akieleza jambo kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta wakati wa ziara fupi  kukagua ujenzi wa chumba kitakachotumia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi (ILMIS)  katika Mradi wa Mfano Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akioneshwa namna jalada ambalo taarifa zake tayari zimeshafanyiwa kazi na mfumo huo linavyoonekana katika Mradi wa Mfano unaotekelezwa katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Read More

Saturday, June 23, 2018

MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikali kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema watakaobainika kuhujumu mifumo hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia watumishi wasio waadilifu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 23, 2018) mara baada ya kuzindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU) ni  “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu”.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini, wananchi, Sekta Binafsi, Sekta ya Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa na Wadau mbalimbali,  kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.

“Hii ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa  ambayo yamehimizwa na Kaulimbiu ya mwaka huu,”.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza Watendaji  Wakuu wa Taasisi zinazosimamia mifumo hiyo pamoja na maafisa waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kupitia mifumo hiyo, wahakikisha wanailinda na kuitumia vema ili iweze kuwa na tija na manufaa yaliyokusudiwa.

Mifumo hiyo aliyoizundua inahusu utoaji Huduma Serikalini ambayo ni Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa Kumbukumbu za Kielektroniki na Mfumo wa Ofisi Mtandao.

Mingine ni Mfumo wa Ankara Pepe na Ulipaji wa Serikali, Mfumo wa Utoaji Huduma za Serikali Kupitia Simu za Mikononi, Mfumo wa Barua Pepe wa Serikali na Mfumo wa Vibali vya Kusafiri.

Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali la kutumia mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali za kila siku.

“Hivyo basi, mtakubaliana nami kuwa, Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA ili kutekeleza kwa vitendo azma ya kuwapatia wananchi hususani wa vijijini huduma bora na kwa wakati,” amesema.

Kwa upande wa wananchi,Waziri Mkuu amewataka  waendelee kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejipambanua kwa vitendo pamoja na kuwa na dhamira ya dhati ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Uzinduzi huo umehudhuliwa na waziri wa nchi, ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Bw. George Mkuchika, waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage, naibu waziri Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, na naibu waziri wa nchi OR-TAMISEMI Josephat Kakunda, wabunge, muwakilishi wa benki ya dunia, makatibu wakuu, watendaji na viongozi wa taasisi za umma.
Read More

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 23.6.2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Cuthbert Simalenga, wakati akikagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Shukran George kwa niaba ya mwanae Magreth Msomba, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

Katibu Muhtasi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Kholuu Ramadhan, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Johari Swalehe kwa niaba ya mwanae Seif Ramadhan, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kwenye uzinduzi wa mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

Read More

Monday, June 18, 2018

TANZANIA INAONGOZA KWA UCHUMI KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema hali hiyo, imetokana na Tanzania kufungua fursa za ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara milioni tatu zinazokuwepo kila mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua na unamgusa kila Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.

Waziri Mkuu ameyasena hayo leo (Jumatatu, Juni 18, 2018) wakati akifunguaKongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF, jijini dodoma.

“Pia, huduma za fedha jumuishi ni kigezo ambacho kimeiweka Tanzania mahala pazuri kwenye uchumi jumuishi ambapo zaidi ya Watanzania milioni 30 wamekuwa wakifanya miamala mbalimbali ya fedha kupitia simu za mkononi na hivyo kuongeza huduma za fedha kufikia asilimia 65,” amesema. 

Amesema huduma za msingi za kijamii kama vile elimu, afya na kupungua kwa rushwa katika utoaji huduma za umma pamoja namtandao wa miundombinu ya barabara ambayo huwezesha wananchi wengi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ni kigezo kingine kilichozingatiwa katika kuipatia Tanzania nafasi hiyo. 

Waziri Mkuu ameongeza kwamba Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema suala la uchumi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni moja ya ajenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo amezitaka sekta zote zihakikishe zinatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa viwanda.

Pia amesema suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi lazima liende sambamba na uwezeshaji vijana kujiajiri kama inavyoelekeza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015. “Ilani inatambua kwamba kuwawezesha wananchi kiuchumi ni hatua ya msingi katika kujenga Taifa lililoimarika kiuchumi na lenye lengo la kujitegemea,”. 

Aidha, Ilani pia, inasisitiza kuhusu umuhimu wa kuhamasisha ushiriki wa Sekta binafsi katika kuwezesha wananchi kiuchumi, hivyo ni muhimu kukamilisha taarifa ya uwezeshaji kutoka kwa wadau wa sekta binafsi, ili Serikali iweze kuona mchango wa sekta binafsi katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa malengo hayo ya uwezeshaji wananchi katika maeneo ya fursa za mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ya masharti nafuu ni muhimu sana katika kupambana na umaskini wa kipato. 
         
Amesema kwa kutambua umuhimu wa ajenda ya uchumi wa viwanda, ndiyo maana makongamano ya uwezeshaji yamekuwa yakiweka mkazo kwenye masuala ya viwanda. Hali hiyo pia, inajidhihirisha katika kaulimbiu ya Kongamano la Tatu ambayo ni: “Viwanda: Nguzo ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi”. 

Hivyo Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema, “tuendelee kuhimiza kuhusu kutekeleza uchumi wa viwanda kwa lengo la kuwawezesha wananchi wetu kiuchumi na kuhakikisha kuwa tunafikia lengo la kuwa na  uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,”.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba, Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Bw. Suleiman Jafo.

Wengine ni Wakuu wa Mikoa mbalimbali, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Makatibu Tawala wa Mikoa, Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Wakurugenzi wa Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’ Issa, wadhamini wa Kongamano hilo na Wawakilishi kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta binafsi.
Read More

KILIMO CHA PAMBA KUNOGESHA MAPINDUZI YA VIWANDA

*Ni kutokana na juhudi za Serikali za kuhamasisha kilimo cha pamba 


 ZAO la pamba ni miongoni mwa mazao makubwa ya biashara yaliyokuwa yakiliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni na kuchangia kukuza uchumi wa wananchi miaka ya 1970.

Kwenye miaka ya 1970 kulisheheni vyama vingi vya ushirika wa zao la Pamba na viwanda vya kuchambua nyuzi na kukamua mafuta, ambavyo vilibadili  hali halisi ya kipato cha wananchi wa eneo linalolimwa zao hilo na kulifanya kujulikana kama dhahabu nyeupe.
Kilimo hicho kilianza kudorora miaka ya hivi karibuni kutokana na kulegalega kwa vyama vya ushirika na matokeo yake pamba iliuzwa ikiwa chafu bila kuzingatia ubora  na madaraja yaliyopo.
Kutokana na sababu hizo Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, iliamua kufufua zao hilo ili kuhakikisha upatikanaji wa malighafi ya viwanda vya nguo na mafuta yatokanayo na mbegu za pamba zinapatikana pamoja na kuinua uchumi wa wakulima nchini.
Katika kufanikisha suala hilo Serikali ilianza kwa kuwaagiza viongozi wa mikoa yote inayolima pamba kuhakikisha wanawahamasisha wakulima kufufua mashamba yao na ilihakikisha inafuatilia jambo hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, ugawaji wa pembejeo hadi utafutaji wa masoko.

Baada ya kutoa agizo hilo ambalo lilifanyiwa kazi na tayari mafanikio yameanza kuonekana katika msimu wa mwaka huu, kwa wakulima  kuanza kuvuna na kuuza kwa mafanikio.

Akizungumzia kuhusu hali ya zao hilo mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella, anasema msimu wa mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na hamasa iliyotolewa na viongozi wakuu wa Serikali.

Bw. Mongella anasema kutokana na hamasa hiyo, mwaka huu wanatarajia kupata mavuno makubwa kutoka katika kilimo  hicho kwa sababu wakulima wengi wamelima na baadhi yao tayari wameshaanza kuvuna.

Anasema Rais Dk. Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, walitoa maelekezo mahususi na walifanya ufuatiliaji wa karibu wa kilimo cha mazao makuu matano ya biashara nchini, likiwamo na zao la pamba.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya zao hilo jijini Mwanza hivi karibuni, Bw. Mongella amesema zao la pamba litasaidia kufufua viwanda vya mafuta ya kula, nguo pamoja na kuongeza ajira.

Amesema baada ya Rais Dkt. Magufuli kuhamasisha kilimo cha zao hilo, ambacho kilianza kusuasua nchini, viongozi waliitikia na kuwahimiza wakulima wachangamkie fursa hiyo, ambao walikubali.

“Tunashukuru kwa hamasa na miongozo iliyotolewa na viongozi wetu kwa sababu iliongeza ari kwa wakulima kulima zao la pamba kwa wingi na mwamko kwa wananchi kulima mazao mengine, likiwamo la mpunga,” anasema.

Hata hivyo, kiongozi huyo ameishukuru Serikali kwa kuagiza pamba itakayovunwa iuzwe kupitia minada itakayosimamiwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) katika kila eneo, jambo ambalo limesaidia  kufufuka kwa vyama hivyo.

“Tunashukuru kwa maelekezo na miongozo iliyokuwa inatolewa na viongozi wetu wakuu. Sasa AMCOS zetu zimefufuka na huu ni mwanzo tu mapinduzi makubwa katika biashara ya zao la pamba na yajayo yanafurahisha zaidi,” anasisitiza Bw. Mongella.

Bw. Mongella anatarajia kuwahamasisha wakulima wote wa mkoa huo pamoja na wafugaji na wavuvi wajiunge katika AMCOS zilizoko katika maeneo yao, ili kuweza kuirahisishia Serikali kufanyanao kazi.

Mkuu huyo wa mkoa pia anatumia fursa hiyo kuwapongeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maofisa Kilimo kuanzia ngazi ya wilaya hadi kijiji na wakulima kwa kuhakikisha kilimo cha zao la pamba kinapata mafanikio.

Bw.Mongella anaamini ushirikiano wao kupitia vikosi kazi mbalimbali vilivyoundwa kuanzia ngazi ya mkoa ambapo alikuwa Mwenyekiti watendaji hao walitoa ushirikiano mkubwa ulichangia mafanikio ya zao hilo.

Hata hivyo, Bw. Mongella amewashauri wakulima watumie taasisi za kifedha kuhifadhi fedha zao na wajijengee nidhamu ya matumizi, ambayo itawapa fursa ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo, ikiwa pamoja kujenga nyumba bora.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mkoani Mwanza, Bw. Juma Sweda anasema anaishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kulifufua zao hilo pamoja na kuwahamasisha wananchi kulima na kutoa maelekezo ya uuzwaji wake.
“Naishukuru Serikali kwani baada ya kuwahamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la pamba nasi tuliungana na wananchi kuhakikisha maelekezo hayo tunayatekeleza kwa vitendo, lengo letu kubwa ni kuona zao hili linarudi kama zamani.

‘’Mbali na kuwahamasisha wananchi kulima zao la pamba, pia Watumishi wa Halmashauri  nao wamelima jumla ya ekari 306 za zao la pamba kwenye kijiji cha Ikoma katika Kata ya Kijima. Mashamba yaliongeza hamasa kwa wananchi,’’ anasema Sweda.

Bw. Sweda anasema kabla ya wakulima kuanza kuanda mashamba ya kilimo cha pamba, Wilaya ya Misungwi yenye vjjiji 113 ilitoa mafunzo kwa wakulima wawili kila kijiji, ambao wameshirikiana na vikosi kazi vya vijiji husika na Maafisa Ugani kusimamia kilimo cha zao hilo.

Anasema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.

Anasema baada ya Serikali kuhamasisha kilimo cha zao la pamba kwa mikoa yote inayolima zao hilo, pia iliagiza kuanzishwa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) katika maeneo yote, ambapo AMCOS 50 zilianzishwa wilayani Misungwi.

Bw. Sweda anasema AMCOS zimesaidia kuimarisha ubora wa pamba, ambapo viongozi wake hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi pembeni kabla ya kupima na kulipwa. 

Mkuu huyo wa Wilaya anaongeza kuwa, mbali na kukagua usafi na ubora wa pamba ili kuhakikisha hakuna pamba chafu inayouzwa, pia wanasimamia zoezi la malipo kwa wakulima na kwamba wanaouza wote wanalipwa hapo hapo na ni marufuku mnunuzi kumkopa mkulima.

Pia, anasema wilaya yao imeanzisha mikakati mbalimbali ya kutoa motisha kwa Maafisa Kilimo na wakulima waliofanya vizuri, ambapo hutoa zawadi za pikipiki kwa mkulima na afisa aliyeongoza katika kata yake.

Anaongeza kuwa Maafisa Kilimo Wasaidizi wapo nchini Brazil kwa mafunzo ya miezi mitatu, ambapo wanajifunza namna ya kilimo bora cha zao la pamba. Viongozi hao ambao ni John Choto, Haika Kimambo na Bahati Mchele walichaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo baada ya kuonyesha jitihada kubwa katika kusimamia zao hilo.

Mkuu huyo wa wilaya anasema wilaya ina Maafisa Ugani 90 ambao wamesambazwa kuanzia wilayani hadi vijiji, lengo likiwa ni kupata nafasi ya kusimamia vizuri na kwa ukaribu zao la pamba.

Anasema wilaya ina jumla ya kata 27 ambapo Maafisa Kilimo wake wote walipatiwa pikipiki ili ziwawezeshe kuwafikia wakulima kwa urahisi na kuwahudumia kwa wakati lakini atakayeshindwa kuwajibika atanyang’wanywa pikipiki.

Sambamba na hayo, Bw. Sweda aliwashauri wakulima kutumia vizuri fedha wanazozipata baada ya kuuza mazao yao. Anasema ni vema wakatumia fedha hizo kujiletea maendeleo katika familia zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora za kisasa na kuwaendeleza watoto wao kielimu.

Anasema kwa sasa wapo katika hatua ya uvunaji na uuzaji, ambapo wamejipanga kukagua kikamilifu ili kuona zoezi hilo linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.

Anasema viongozi wa Vyama vya Msingi vya AMCOS, hukagua pamba kabla ya kuipokea na iwapo mkulima atabainika kupeleka pamba chafu hulazimika kuisafisha kwanza kwa kutenga safi na chafu ndipo hupima na kulipwa.

Mkuu huyo wa wilaya anaongeza kuwa zao la pamba mbali ya kuwapatia wakulima kipato, pia litaimarisha hali ya usalama wa chakula kwa sababu fedha watakayoipata baada ya kuuza pamba itawawezesha kumudu ununuzi wa mahitaji mengine katika familia na hawatouza vyakula walivyonavyo.

Hata hivyo, Bw. Sweda aliwaomba wadau wa sekta binafsi wasaidie katika kuliongezea thamani zao hilo kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa viwanda vya nyuzi, nguo na vya kukamua mafuta ya pamba badala ya kuuza malighafi.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Kata ya Mondo, Bw. Sebastian Mbandi anasema mafanikio ya zao hilo kwa mwaka huu ni makubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, hata hivyo wameshindwa kufika lengo walilojiwekea kutokana na mazao mengi kushambuliwa na wadudu aina ya thrips.

Bw. Mbandi anasema walitarajia kuvuna wastani wa tani 1.5 kwa ekari moja lakini kutokana na changamoto ya ugonjwa iliyosababishwa na mdudu huyo wanatarajia kuvuna wastani wa kilo 800 kwa ekari hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia wakulima kwa kuwatafutia dawa itakayowawezesha kupambana na thrips msimu ujao.

Kwa upande wao, wakulima wakizungumza kwa nyakati tofauti, walitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kuhamasisha wananchi walime zao la pamba, ambapo nao waliitikia wito huo na sasa wameanza kuona mafanikio.

Miongoni mwa wakulima hao ni pamoja na Bw. Hoja Ngole mkazi wa Kijiji cha Mondo ambaye amelima ekari sita na tayari ameshavuna na ameenda kuuza na anatarajia kutumia fedha atakazozipata kwa kujenga nyumba ya kisasa.

Bw. Ngole na mkewe Bibi Sara waliahidi kuongeza ukubwa wa shamba katika msimu ujao na wamewaomba wananchi wengine kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa kuwa ni mkombozi wa maisha yao.   ’’Tumehamasika kuongeza ukubwa wa shamba baada ya Waziri Mkuu kututembelea na tunataka akija tena akute tumebadilika, tuwe na nyumba bora,’’ anasema. 
Mkulima mwingine,mkazi wa kijiji cha Mondo Bw. Michael Masalamunda ambaye alikuwa amepeleka pamba yake katika kituo cha mauzo cha Mwanimo AMCOS amesema anatarajia kutumia fedha atakazozipata baada ya mauzo hayo kwa kuongeza mtaji wa biashara ya ng’ombe.

Bw. Masalamunda naye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwahamasisha walime zao la pamba pamoja na na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye naye aliwahamasisha na kufuatilia maendeleo ya zao hilo.
Mkulima huyo anaishukuru Serikali kwa kuagiza mauzo ya zao hilo yasimamiwe na vyama vya ushirika kwa sababu vimewezesha wakulima kuwa na soko la uhakika la pamba yao na wakiuza tu wanalipwa fedha zao hakuna anayekopwa. “Mimi leo nakuja kuuza kwa awamu ya pili na fedha zote nimelipwa.”

Naye mkulima mwingine, mkazi wa kijiji cha Maganzo Bw. Swalala Nteminyanda anaiomba Serikali kuwatafutia dawa nzuri itakayoweza kuwaangamiza wadudu aina ya thrips ambao wameonyesha usugu baada ya kupuliziwa dawa mbalimbali bila ya kufa.

Nteminyanda pia anawashauri wakulima wenzie wafuate maelekezo yanayotolewa na Maafisa ugani wanaowatembelea katika mashamba yao ili waweze kupata mavuno mengi na yenye viwango vya ubora vinavyotakiwa. Mkulima huyo amelima ekari saba na anatarajia kujenga nyumba bora kwa fedha atakazozipata.

Kwa upande waowanunuzi wa zao hilo wanaishukuru  Serikari kwa kuweka mfumo mzuri wa ununuzi wa zao hilo, ambalo kwa mwaka huu linauzwa kupitia katika minada inayosimamiwa na AMCOS.

Miongoni mwa wanunuzi hao ni pamoja Meneja Mkuu wa Kampuni ya NGS Investment LTD, Bw. Emmanuel Dandu alipokuwa akizungumzia kuhusu kuanza kwa uchambuaji wa pamba kwa msimu wa mwaka huu.

Bw. Dandu ambaye kampuni yao ya NGS Investment LTD, licha ya kujishughulisha na biashara nyingine, pia inamiliki kiwanda cha kuchambua pamba cha Majahida kilichopo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, ambayo tayari imeshaanza zoezi ya uchambuaji pamba.

Anasema pamba inayochambuliwa katika kiwanda hicho wanainunua kupitia AMCOS walizopangiwa, ambapo alipongeza mfumo huo kwa sababu unawawezesha kupata malighafi kwa urahisi na kwa wakati.

“Wanunuzi wote tunanunua pamba kupitia AMCOS. Serikali imeweka mfumo mzuri unaotuwezesha wote kununua pamba kadiri ya uwezo wetu. AMCOS zimeagizwa kuuza pamba kwa wanunuzi wote bila ya ubaguzi, tofauti na miaka ya nyuma” anasema Bw. Dandu.
  
Anasema awali kabla pamba haijaanza kuuzwa kupitia AMCOS suala la ubora lilikuwa halizingatiwi sana na wakulima kwani  pamba yake ikikataliwa na kampuni moja alikuwa na uhuru wa kuipeleka kwenye kampuni nyingine jambo ambalo lilichangia kuishusha thamani.

Hata hivyo, wanunuzi hao wanaiomba Serikali kuziwezesha AMCOS kuwa na maghala makubwa na ya kisasa ya kuhifadhia pamba, lengo likiwa ni kuhakikisha pamba inahifadhiwa kwenye maeneo salama na kuifanya isipoteze ubora.

Mbali na maombi hayo, pia wameiomba Serikali kuwajengea uwezo viongozi wa Ushirika ili waweze kutekeleza majuku yao kikamilifu na pia isaidie kutoa elimu kwa wanachama juu ya umuhimu na faida za AMCOS ili wakulima wengi waweze kujiunga.

Akizungumzia kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, anasema kina uwezo wa kuchambua tani 40,000 za pamba kwa mwaka, lakini wanalazimika kuchambua wastani wa tani tano  hadi 12 kutokana na changamoto ya upatikanaji wa pamba ya kutosha pamoja na changamoto ya umeme wa uhakika.

Pia anaiomba Serikali iwasaidie wakulima kwa kuwapatia pembejeo kwa wakati pamoja na kuwapa elimu ya mara kwa mara juu ya kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao la pamba, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa wakati ili waweze kujiongezea tija.

Anasema kwa sasa kiwanda hicho kina jumla ya wafanyakazi 300, ambao kati yao 62 ni waajiriwa wa kudumu na waliosalia ni vibarua. 

Bw. Dandu anasema marobota yanayotengenezwa kiwandani hapo yanakuwa na uzito wa kilo 200 hadi 220, huku wateja wao wakubwa ni Cotton Distributors Inc (CDI) ya nchini Uswisi, Saurashtra Cotton and Agro Product PVT LTD ya nchini India.

Wengine ni Awatac Impex PTE LTD ya nchini Singapore pamoja na viwanda vya nguo vya ndani ya nchi kikiwemo cha Mwatex cha jijini Mwanza. Alisema matarajio ya kampuni hiyo ni kuanzisha kiwanda cha kutengeza nyuzi ili kuongezea thamani ya pamba kabla ya kuiuza.

Aidha, Meneja huyo anasema mbegu zinazopatikana baada ya pamba hiyo kuchambuliwa zinapelekwa moja kwa moja katika kiwanda cha kukamua mafuta ya kula na mashudu huuzwa kama chakula cha mifugo na mabaki yanayopatikana baada ya mafuta kuchujwa, anasema yanatumika kwa kutengeneza sabuni za kufulia, ambazo wanaziuza kwa wananchi. 
Read More