Sunday, July 14, 2019

SERA YA VIWANDA YASAIDIA KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA


MKAZI wa kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Leonard Nkamba anayejishughulisha na uchongaji wa vyombo mbalimbali vya jikoni ameishukuru Serikali kwa kuanzisha sera ya viwanda kwa kuwa imesaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Ameyasema hayo leo  (Jumapili, Julai 14, 2019) baada ya kukabidhiwa kiasi cha sh. milioni 2.5 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili aweze kuongeza mashine itakayomuwezesha kuchonga bidhaa zenye ubora zaidi. Makabidhiano hayo yamefanyika mjini Kigoma.

Bidhaa anazochonga ni vikombe, chupa za chai, hot pot kwa kutumia mti aina ya jakalanda. Mbali na kutengeneza vyombo hivyo, pia mjasiriamali huyo ambaye ameajiri vijana watatu anachonga vibao na kuandika ujumbe mbalimbali kwa kutumia unga wa ngano.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Waziri Mkuu, mjasiliamali huyo amesema anaushukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambao uliona kazi zake na kumuagiza atengeneze seti za vyombo kwa ajili ya zawadi za kumpelekea Rais Dkt. John Magufuli.

“Uongozi wa UWT mkoa wa Kigoma Taifa ulivutiwa na kazi zangu na kuniagiza nitengeneze chupa ya chai, vikombe na hot pot kwa ajili ya kumpa zawadi Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu ndipo Waziri Mkuu jana aliona kazi zangu na akavutiwa na bidhaa ninazotengeneza ndipo akaniuliza kama kuna changamoto zinazonikabili nikamwabia nahitaji mashine moja yenye thamani ya sh. milioni mbili na nusu akasema umepata na leo sijaamini alivyoniita na kunikabidhi. Namshukuru sana.”

Nkamata ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wengine hususani vijana waache kulalamikia suala la ukosefu wa ajira na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wataziuza na kujipatia kipato.

Pia amewaomba Watanzania wajenge utamaduni wa kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vya ndani kwa kuwa vina ubora wa kutosha na pia watakuwa wanachangia kukuza uchumi wa wajasiriamali na Taifa kwa ujumla. Amesema bidhaa anazotengeneza ni rafiki wa mazingira kutokana na malighafi anazotumia.

Kwa upande wake Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini. Pia amesema Serikali ipo tayari wakati wowote watakapohitaji msaada.
Waziri Mkuu amempongeza mjasiriamali huyo  kwa bidhaa mbalimbali anazotengeneza ambazo ni nzuri na za kipekee. Amesemma amefurahi kuona vikombe, chupa za chai pamoja na hot pot zilizotengenezwa na Mtanzania kwa kutumia miti.
 (mwisho)
Read More

Saturday, July 13, 2019

SUALA LA KUWAONDOA WATUMISHI WALA RUSHWA, WAZEMBE NI ENDELEVU-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema suala la kuwaondoa kazini watumishi wa umma ambao ni wazembe, wala rushwa na wasiotimiza majukumu yao ipasavyo ni endelevu.

‘Serikali inahitaji watumishi wenye heshima na nidhamu ya kazi ili waweze kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote iwe wa kiuchumi, kidini au kikabila.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Julai 13, 2019) wakati akihutubia mwananchi katika kongamano la kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani.

Kongamano hilo limeandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ili kumpongeza Rais Dkt. Magufuli lilifanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi watoe taarifa iwapo watabaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na rushwa.

"Watumishi wa umma tunataka watambue kwamba wao ni watumishi wa wananchi, hivyo hawana budi kutambua wajibu wao ambao ni kuwatumikia mwananchi ipasavyo."

Amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi amesema kongamano hilo ni muendelezo wa makongamano mengine ya kumpongeza Rais yaliyofanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Unguja na Pemba.

Amesema viongozi hao wameonesha dhamira ya kweli ya kuwaletea wananchi maendeleo. "Tutaendelea kushirikiana na viongozi wetu na hatupo tayari kugawanyika."

Awali, Mawaziri na Manaibu Waziri mbalimbali walipata fursa ya kuelezea namna ilani ilivyotekelezwa katika maeneo mbalimbali kupitia wizara zao.

Katika kongamano hilo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali walivihama vyama vyao na kujiunga na CCM akiwemo na aliyekuwa Kalibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

 (mwisho)
Read More

Friday, July 12, 2019

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA VIETNAM


*Awakaribisha Waviet Nam waje kuwekeza katika bandari, usafiri wa anga na kilimo


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekuna na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Viet Nam, Trinh Dinh Dung na amewakaribisha wawekezaji kutoka Viet Nam waje kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya mipango miji, madini, bandari, usafiri wa anga, ufundi stadi, kilimo pamoja na uvuvi.

Amesema kuwa anatambua kwamba nchi ya Viet Nam inafanya vema katika suala la mazao ya kilimo kwa kuongeza tija kwenye mazao hayo na kukifanya kilimo kuwa cha biashara, hivyo amezialika kampuni za Viet Nam zenye teknolojia mahsusi katika maeneo tajwa ili kushirikiana na Tanzania katika mikakati yake ya kuendeleza kilimo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 12, 2019) wakati wa mkutano wake na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam , ambapo ametumia fursa hiyo kumuhakikishia kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Viet Nam kwa manufaa ya watu wa nchi mbili hizo.

Amesema uwepo wa kampuni ya Viettel PLC (Halotel) ya kutoka nchini Viet Nam ni ishara tosha ya imani ya uwekezaji iliyopo kwa wawakilishi wa Viet Nam. “Nawakaribisha sana wawekezaji kutoka Viet Nam kuja kuwekeza Tanzania kwani kwa kufanya hivyo hawatojutia uamuzi wao wa kuwekeza Tanzania.”

Waziri Mkuu amesema Viet Nam imeendelea kuwa mshirika muhimu wa kiuchumi kwa Tanzania, hivyo ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Viet Nam kwa kuendelea kuunga mkono Serikali ya Tanzania katika jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo.

“Kwa mfano, kampuni ya mawasiliano ya Viettel PLC (maarufu kama Halotel) ambayo imewekeza nchini tangu mwaka 2014 inafanya vizuri katika sekta ya mawasiliano. Kampuni hiyo, imewezesha mawasiliano ya simu kuwafikia Watanzania wengi hususan wale waishio vijijini.”

Waziri Mkuu amesema kampuni hiyo ya Halotel imeweza kuzalisha ajira takriban 1,600 za moja kwa moja kwa wazawa na ajira takriban 100,000 zisizokuwa za moja kwa moja hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018;

Amesema lengo la Serikali ya Tanzania ni kuendelea kushirikiana na Serikali ya Viet Nam katika masuala ya mawasiliano na masuala mengine ikiwemo biashara na uendelezaji na masoko ya mazao ya kilimo hususan korosho, kahawa, kilimo mseto cha mpunga na uvuvi wa samaki ambako Viet Nam inafanya vizuri zaidi.

Akizungumzia kuhusu sekta ya utalii, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi nzuri, watu wake ni wakarimu na pia imebarikiwa vivutio vingi vya utalii. Hivyo, amezikaribisha kampuni za Viet Nam kuja kuwekeza katika sekta ya utalii na utamaduni nchini.

“Halikadhalika, sina shaka kwamba wengi wenu mmewahi kusikia kuhusu Visiwa vya Zanzibar, Mlima Kilimanjaro, pamoja na Mbuga za Serengeti na Ngorongoro. Hivyo ni baadhi tu ya vivutio vingi vya utalii tulivyojaliwa kuwa navyo nchini mwetu.”

Kwa upande wakeNaibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, Trinh Dinh Dung ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushgirikiano na kwamba ameomba ushirikiano huo uimarishwe kupitia ziara za viongozi wa wakuu wa nchi mbili hizo.

Naibu Waziri Mkuu huyo wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Serikali ya Viet Nam itazidi kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania hususani katika sekta za kilimo, biasdhara na uvuvi.

Kadhalika kiongozi huyo amesema kuwa nchi ya Viet Nam iko tayari kununua mazao mbalimbali ya kutoka nchini Tanzania yakiwemo ya korosho na pamba. Amesema lengo la Serikali yao ni kuhakikisha kwamba biashara kati ya Tanzania na Viet Nam inafikia dola bilioni moja ifikapo 2020.

 (mwisho)
Read More

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATAKA DHANA YA AFYA MOJA KUTEKELEZWA KWA WAKATI

 Na; MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amewataka waratibu wa dawati la Afya Moja kutekeleza dhana ya Afya Moja kwa wakati sambamba na kuweka mikakati mahususi itakayowaongoza katika utendaji wa dhana hiyo.  
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya moja na wataalam kutoka sekta ya Afya, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira kilichofanyika Julai 12, 2019, Jijini Dodoma.
Alieleza kuwa dhana ya afya moja inajumuisha wataalam na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa dhana hiyo ikiwemo kutoa fursa ya kushirikiana pamoja katika kukabiliana na madhara au magojwa hatarishi nchini.
“Nimepitia Sera ya Afya moja na kuona suala hili linatakiwa kusimamiwa vyema, ikiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu wa Dawati la Afya moja kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa mahala salama,” alieleza Mwaluko
Aliongeza kuwa, suala la kujenga uwezo kwa waratibu wa dawati la afya moja inatakiwa kuangalia ofisi kwa ujumla na si mjumbe mmoja tu ambaye atakuwa anasimamia masuala hayo ya Afya moja wakati wote.
“Mnatakiwa mtambue kuwa mkiwa kama wafanyakazi mna majukumu mengine ya kiofisi ambayo mnatakiwa kuyatekeleza, hivyo mtoe fursa kwa wafanyakazi wengine waliopo kwenye ofisi zenu kujifunza na kuelewa dhana hii ya afya moja,” alieleza Mwaluko.
Aidha, alitoa wito kwa waratibu wa dawati hilo kuelimisha umma kuhusu maana ya Afya Moja na dhana nzima ya Afya moja ili wananchi waweze kuwa na ufahamu wa suala hilo.
Pia, aliwahimiza washauri elekezi wa dawati hilo kutimiza majukumu yao kwa weledi na kutoa ushauri mapema kuhusu dhana ya Afya Moja.
Kwa upande wake, Prof. Robinson Mdegela ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja alisema kuwa kukutana kwao katika kikao hiko ni kuonesha utayari wa kila mtaalamu katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Afya Moja.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe mara baada ya kikao kilichowakutanisha na Wadau wa Afya Moja kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akielezea jambo kwa wadau wa Afya Moja walioshiriki kikao hiko kilichofanyika Hoteli ya Morena, Jijini Dodoma.
Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja Dkt. Kunda John akichangia mada kuhusu umuhimu wa dhana ya Afya Moja wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2019 Jijini Dodoma.
Baadhi ya wataalamu wa Dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.
Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afya Moja nchini walipokutana Jijini Dodoma.
Sehemu ya wataalamu wa dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka (hayupo pichani).



Read More

Thursday, July 11, 2019

MAPAMBANO YA RUSHWA YANG’ARISHA OFISI YA RAIS NA OFISI YA WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema juhudi za Serikali za kupambana na rushwa, kudhibiti upotevu wa mapato, matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma ni sababu zilizowezesha Ofisi ya Rais pamoja na Ofisi ya Waziri  kuaminika zaidi.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na viongozi wa Umoja wa Wanake Tanzania (UWT)  akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Amesisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni endelevu.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation iliyotolewa hivi karibuni.

Ripoti hiyo mpya iliyotolewa Julai 11, mwaka huu inaonesha kwamba kwa sasa Tanzania inaongoza katika nchi 35 za Afrika  baada ya kupungua kwa vitendo vya rushwa katika sekta nyingi, ambapo Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu zimeonekana kuaminika zaidi.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatahadharisha watumishi wa umma kwamba Serikali kamwe haitomvumilia mtumishi atakayebainika  anayejihusisha na vitendo vya rushwa na aliwataka wahakikishe kuwa wanatekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi wasisite wakati wote kutoa taarifa kwa vyombo husika pale watakapobaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.

“Watumishi wa umma wanatakiwa kutambua kwamba jukumu lao kubwa ni kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maadili na kanuni za utumishi wa umma zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na si vinginevyo. Serikali hii kamwe haitowaonea haya au kuwafumbia macho watumishi wa hovyo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa suala la kuwaondoa kazini watumishi wazembe, wasiotimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma ni endelevu kwa sababu Serikali inahitaji watumishi wa umma wenye heshima na nidhamu ya kazi.

Suala la kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi zikiwemo ofisi za Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia jambo hilo.

(mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI TANZANIA TOKEA NCHINI MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, tokea nchini Misri, alipokua kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 11.2019. Kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Ngalayainisi. 

Read More

Wednesday, July 10, 2019

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA MISRI

*Wazungumzia namna ya kuimairisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah Al- Sisi, ambapo wametumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Misri.

Mbali na kuzungumzia masuala hayo ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pia Waziri Mkuu amemfikishia Rais wa Misri salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yamefanyika leo (Jumatano, Juni 10, 2019) Ikulu jiji Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Misri. Katika ziara hiyo ameambatana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi nchini Misri ambapo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo ameagwa na Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi wa Misri, Dkt. Ezz Eldien Abo Setit.

Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Pia, Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo, mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez Canal na kiwanda kikubwa cha ngozi.

 (mwisho)

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini CairoJulai 10.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini CairoJulai 10.2019.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini CairoJulai 10.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fatah Al Sisi, katika Ikulu ya Rais, mjini CairoJulai 10.2019.

Read More

ZIARA YA WAZIRI MKUU NCHINI MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa ya ngozi, wakati alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki, kilichopo katika mkoa wa Sharkia, nchini MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa ya ngozi, wakati alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki, kilichopo katika mkoa wa Sharkia, nchini MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya ngao, kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Canal, Admiral Mohab, wakati alipotembelea mfereji huo mpya nchini MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa kwenye boti,wakati alipotembelea mfereji wa Suez Canal, katika mji wa Ismailia, Misri Julai 9.2019.






Read More

Tuesday, July 9, 2019

WAZIRI MKUU ATEMBELEA PIRAMIDS MISRI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo MisriJulai 9.2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitembea nje ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo Misri,Julai 9.2019. kulia ni mwenyeji wakeWaziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa za wajasiriamali, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi mjini Cairo MisriJulai 9.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Kilimo Japhet HasungaWaziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (katikati) Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa anashuka kwenye Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo MisriJulai 9.2019
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ndani ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri,Julai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amepanda juu ya Piramidi, akionesha jambo wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo MisriJulai 9.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishika jiwe lililotumika kujengea Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo MisriJulai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kushoto), wakati alipotembelea Piramidi mjini Cairo MisriJulai 9.2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy.

Read More

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA NGOZI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Julai 9, 2019) alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi za kutosha.

Waziri Mkuu ambaje jana alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania inamifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri, ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola bilioni 8.2).

(mwisho)
Read More