Wednesday, June 21, 2017

MAJALIWA AWASILI MWANZA AKIWA NJIANI KUELEKEA CHATO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Juni  21, 2017 akiwa njiani kueleakea Chato ambako atakuwa na ziara ya siku mbili.

Read More

Tuesday, June 20, 2017

BUNGENI DODOMA LEO TAREHE 22 JUNE,2017

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, bungeni mjini Dodoma juni 20, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, bungeni mjini Dodoma juni 20, 2017.


Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA USHIRIKIANO, UPENDO, KWA DINI ZOTE TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017.
 Baadhi ya Wabunge wakibadilishina mawazo  wakati wa  futari iliyo andaliwa na Spika wa Bunge la Tanzania Job  Ndugai , kutoka  kulia,  Mbunge wa Ilala  Idd Zungu.  katikati  Mbunge wa  Bariadi Magharibi  Andrew Chenge .na kushoto ni Mbunge  wa Mbarali  Haroon Mulla  .Futari hiyo ilifuturiwa katika viwanja vya  Bunge  June 20, 2017 Mjini Dodoma.
 Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa . akitoa salamu za Shukurani  kwaniaba ya WaBunge na wafanyakazi wa Bunge , kwa  Spika wa Bunge  Job  Ndugai , Kwakuwafuturisha  , June. 20 .2017 katika Viwanja vya  Bunge Mjini  Dodoma


Read More

Monday, June 19, 2017

MAJALIWA AZINDUA KAMUSI KUU YA KISWAHILI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 19, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017 (kushoto)  ni  Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kamumusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuizindua kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala,  Mussa Azan Zungu. Kushoto ni Balozi wa Kiswahili Afrika, Mama Salma Kikwete. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu nakala ya Kamusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuzindua kamusi hiyo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, Juni 19, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Kamumusi Kuu ya Kiswahili baada ya kuizindua kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala,  Mussa Azan Zungu. Kushoto ni Balozi wa Kiswahili Afrika, Mama Salma Kikwete. Wapili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe

Read More

BUNGENI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017.


Read More

Tuesday, June 6, 2017

MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wazazi wote nchini ambao wana watoto wenye ulemavu wasiwafiche na badala yake wahakikishe wanapata elimu na kutimiza ndoto zao.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumanne, Juni 6, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, walimu na wanafunzi kwenye uzinduzi wa usambazaji wa vifaa vya elimu maalum uliofanyika kwenye viwanja vya ya msingi Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam.

Nikiwa mwalimu kitaaluma, natambua kwamba mapungufu ya kimwili, kisaikolojia, kiakili au ulemavu wa aina yoyote si kikwazo cha kutimiza ndoto za watoto wetu. Hili linadhihirika kwenye maeneo mbalimbali nchini,” alisema na kutoa mfano wa utumishi Serikalini ambako kuna viongozi wenye mahitaji maalum, lakini wamekuwa wakitoa mchango mkubwa bila kujali hali yao kimwili au vinginevyo.

“Hivyo, nawasihi wazazi wenzangu, msikatishe ndoto za watoto wenu wenye mahitaji maalum kwa kuwaficha. Wapelekeni shuleni wakapate elimu, iwafae maishani,” alisema.

Waziri Mkuu alisema usambazaji wa vifaa hivyo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania mwenye umri wa kwenda shule, anapata huduma hiyo bila kujali hali yake ya kimwili, kiakili, kiafya na uwezo wa kifedha.

Waziri Mkuu pia alimwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene ahakikishe anandaa utaratibu wa kuwatambua watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupangiwa bajeti kulingana na mahitaji yatakayoainishwa.

“Tunapoendelea na jitihada hizi za kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu, ni vizuri tukawa na utaratibu endelevu wa kubaini idadi kamili ya watoto hao kupitia uandikishaji wa watoto shuleni. Bila kubaini idadi yao, itatuwia vigumu kupanga bajeti kwa ajili ya watoto wetu hao. Zoezi hili linaweza kufanyika wakati wa uandikishaji na likawa endelevu kadiri wanavyopanda vidato,” alisema.

Waziri Mkuu alisema mbali ya vifaa vya wanafunzi wasioona na wenye baki ya usikivu (hard of hearing), Serikali pia imenunua vifaa kwa ajili ya walimu wao ili vitumike kufundishia na kupimia ili kubaini mahitaji maalum ya ujifunzaji kwa watoto wanaoandikishwa shuleni.

Alisema vifaa vinavyoanza kusambazwa, vitasaidia kuinua kiwango cha taaluma kwenye shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum na pia vitasaidia watoto wengi zaidi wenye mahitaji maalum wapate elimu na kuongeza hamasa kwa walimu wanaofundisha kwenye shule husika.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia hadhira hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa utahusisha mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na kwamba zoezi hilo litazinufaisha shule za msingi 213 kati ya 408; na shule za sekondari 22 kati ya 43 zenye wanafunzi wa mahitaji maalum.

Alisema vifaa vilivyonunuliwa vimegharimu sh. bilioni 3.6 kutokana na michango ya washirika wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa (DfID) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Sweden (SIDA) na kwamba wizara hiyo itaendelea kununua vifaa zaidi kulingana na bajeti inayotolewa.

Alivitaja vifaa vilivyoninunuliwa kuwa ni mashine za nukta nundu 932; vivunge vya kufundishia wasioona 1,495; karatasi za kuandikia nukta nundu (ream) 2,548; karatasi za kurudufishia (ream) 1,150; shime sikio (hearing aid) 1,150 na vivunge vya upimaji wa mahitaji maalum ya kielimu 78.

Naye Mratibu wa Elimu kutoka SIDA, Bi. Helena Reutersward akitoa salamu kwa niaba ya washirika wa maendeleo alisema wao wamedhamiria kuboresha sekta ya elimu hapa nchini na hasa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

“Elimu ni muhimu ni kwa kila mtu lakini ni muhimu zaidi kwa watu wenye mahitaji maalum. Washirika wa maendeleo tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuchangia jitihada zake za kuboresha elimu nchini Tanzania,” alisema.


Read More

WAZIRI MKUU AZINDUA USAMBAZAJI VIFAA KUFUNDISHIA SAYANSI

Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akiangalia Mtoto wa Darasa la asaba Uhuru  Mchanganyiko Mariana  Alex  Mwenye  ulemavu  wa macho, anavyo weza kuandika  kwakutumia  mashine  maalumu  ya kuandika, June 6 2017 Waziri  Mkuu  alikabidhi  vifaa  vya Kujifunzia   katika shule mbali mbali hapa Nchini Shughuli hiyo imefanyika  Jijini  Dar es salaam

Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akijaribu  kuandika  kwa kutumia  kifaa maalumu  cha kujifunzia  kuandika  watoto wenye Ulemavu  wa  Macho leo 6 june 2017, Kulia ni Waziri wa Elimu na Sayansi  Profesa  Joyce  Ndalichako, Waziri  Mkuu  alikabidhi  vifaa  vya Kujifunzia   katika shule mbalimbali hapa Nchini Shughuli hiyo imefanyika  Jijini  Dar es salaam. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa wa Banki ya Dunia anayeshughulikia  Elimu  nchini  Tanzania  Bibi  Cornelia  Jesse , katikati ni Ofisa  wa  Ubalozi Swiden Nchini Tanzania  anayeshughulikia Elimu Bibi Helena  Reutersward , Maofisa hao walishiriki katika  Uzinduzi  wa Usambaziji  vifaa   vya  kufundishia  Masomo ya  Sayansi , Shughuli hiyo ilifanyika leo 6 june 2017  katika  Viwanja  vya  Jeshi  Lugalo  Dar es salaam.





Read More

WAZIRI MKUU AAGIZA UJENZI WA MAABARA UKAMILISHWE HARAKA

*Azindua usambazaji vifaa vya sayansi
*Ni kwa ajili ya shule za sekondari nchini
          
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene ahakikishe Halmashauri zote zinakamilisha ujenzi wa maabara za sayansi ili vifaa vilivyoletwa visikae bohari kwa muda mrefu.

“Vifaa vya maabara vitatolewa katika shule za Tanzania Bara zilizokamilisha majengo na miundombinu muhimu ya maabara. Hivyo, ni vizuri sasa Halmashauri zote ambazo shule zake hazijakamilisha ujenzi wa maabara ziongeze bidii ili ziweze kunufaika na utaratibu huu. Mheshimiwa Waziri wa Nchi TAMISEMI simamia suala hili,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Juni 6, 2017) wakati akizungumza na viongozi, walimu na wanafunzi wa shule za sekondari wanaosoma masomo ya sayansi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa usambazji wa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari Tanzania bara iliyofanyika kwenye viwanja vya Lugalo jeshini, jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu pia alimwagiza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ahakikishe anawasiliana na Waziri mwenzake wa Zanzibar ili wabadilishane uzoefu na utaratibu huo uweze kuzinufaisha pande mbili za Muungano.

Tunapoimarisha elimu nchini ni vizuri jitihada hizi zikahusisha pande zote mbili za Muungano. Hivyo, wekeni utaratibu wa kubadilishana uzoefu na wenzetu wa Zanzibar, ili jitihada hizi zinufaishe pande zote mbili za Muungano,” amesema.

Akizindua mpango huo, Waziri Mkuu amesema usambazaji wa vifaa hivyo ni kwa ajili ya shule 1,696 za sekondari nchini ambazo zilikamilisha ujenzi kabla ya tarehe 30 Desemba mwaka jana.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia hadhira hiyo, Prof. Ndalichako alisema ununuzi wa vifaa hivyo umegharimu sh. bilioni 16.9 kutokana na michango ya washirika wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa (DfID) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Sweden (CIDA).
Alisema usambazaji wa vifaa hivyo utafanyika kwenye kanda 11 za kielimu na utahusisha shule za wananchi 1,625 na shule kongwe 71. “Wizara ya Elimu imenunua vifaa hivyo chini ya programu ya Lipa Kulingana na Matokeo. Vifaa hivi, vinakidhi ufundishaji kwa vitendo kwa asilimia 100 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita,” alisema.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi alisema Jeshi la Wananchi wa Tanzania litahakikisha linavisambaza vifaa hivyo katika kanda zote 11 zilizoteuliwa.

Akifafanua kuhusu maghala ya jeshi kutumika kutunzia vifaa hivyo na kemikali, Dk. Mwinyi alisema Serikali imepata unafuu mkubwa kwa kutumia maghala hayo na hivyo kuokoa fedha ambazo zingetumika kulipia sehemu nyingine.

Naye Mshauri wa Elimu kutoka DfID, Bi. Tanya Zebroff akitoa salamu kwa niaba ya washirika wa maendeleo alisema wamefurahi kupata fursa ya kuisaidia Seriakli ya Tanzania na watoto wa Kitanzania katika suala la elimu.

Tulipata fursa ya kutembelea mabanda na kuangalia vifaa vya maabara vilivyooneshwa, pia tumezungumza na wale watoto. Tumeona hamasa waliyonayo watoto wale ambao ni wanasayansi wa siku zijazo, tumefarijika sana,” alisema.


Read More

Saturday, June 3, 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI GAIRO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe. 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. 

Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. 

Read More

WAZIRI MKUU AAGIZA KILOSA WAILIPE GAIRO DENI LA0

* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30.
          
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.

“Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini.

“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.

Mapema akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel Mchembe alisema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo  inaanzishwa na hawakuwa wamefungua akaunti ya wilaya.

“Fedha hizi zilikuwa zinapitia Kilosa wakati wilaya ya Gairo imeanzishwa kwa kuwa kipindi hicho wilaya ya Gairo ilikuwa bado haijafungua akaunti. Fedha hizi zinajumuisha ruzuku ya uendeshaji, mapato ya ndani na miradi ya maendeleo,” alisema.

Alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliagiza wilaya ya Kilosa ilipe deni hilo kabla ya Juni 2016 lakini hadi sasa wameshalipa sh. milioni 20 tu ambapo sh. milioni 10 zililipwa Desemba 2015 na nyingine milioni 10 zililipwa Mei 2017.

Akisisitiza kuhusu makusanyo ya mapato, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi hao kuwa Serikali imekwishatoa agizo la kutumia mashine za kielektroniki kukusanya mapato ifikapo Julai mosi.

“Makusanyo ya mapato ya ndani ni eneo muhimu sana. Tumeshaagiza, mwisho wa kutumia mifumo ya kawaida ni Juni 30. Kuanzia Julai mosi, kila eneo ni lazima litumie mashine za kielektroniki,” alisema Waziri Mkuu.

Alihoji ni kwa nini Halmashauri ya Gairo ililenga kukusanya sh.milioni 889.5 lakini kufikia Aprili mwaka huu, makusanyo halisi yalikuwa ni sh. milioni 356.2 sawa na asilimia 40.

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) ya wilaya hiyo ambao hadi kufikia Aprili, 2017 wameweza kukusanya sh. milioni 601.5 ikilinganishwa na makadirio yao ya kukusanya sh. milioni 471 kwa mwaka. Waziri Mkuu aliwapongeza kwa sababu wamevuka lengo kwa asilimia 127.6.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku ya wilaya hiyo, asubuhi alipanda mti kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa maadhimisho ya siku ya upandaji miti hapa nchini.

Pia alikagua mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale, na mradi wa visima 10 ambayo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu. Pia atazungumza na wananchi wa Gairo mjini kwenye mkutano wa hadhara.

Read More

Friday, June 2, 2017

MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA IJUMAA KWENYE MSIKITI WA AL - GADDAF

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa  Al- Gadaf mjini Dodoma Juni 2, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislaam, (kulia) na ujumbe wake, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma  Juni  2, 2017. 



Read More

Thursday, June 1, 2017

TUMEBAINI MADAI HEWA YA BILIONI 21/-

* Ni kwenye malipo ya mawakala wa mbolea, awali yalifikia sh. bilioni 65. 
*Akiri kukutana nao, asema wenye madai halali wote watalipwa
           
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini madudu katika uhakiki wa madeni ya mawakala wa mbolea kwa sababu baadhi yao hawakuwa waaminifu.

“Tulipoanzisha mfumo wa kutoa pembeje kwa njia vocha kwa kuwatumia mawakala kupeleka pembejeo vijijini, tulibaini kuwa baadhi yao walikuwa siyo waaminifu. wakiorodhesha majina ya wakulima na kuandika kuwa wamewapa madawa napembejeo wakati hawapo.”

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni mosi, 2017) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Morogoro), Bi. Devotha Minja kwenye kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma. 

Bi. Minja alitaka kujua ni kwa nini Serikali haijawalipa mawakala hao hadi sasa licha ya kuwa inatambua kwamba walifanya kazi ya kusambaza pembejeo hizo.

“Tulijikuta tuna deni la shilingi bilioni 65. Nilipokutana na mawakala wiki mbili zilizopita, niliwaahidi kwamba tutawalipa lakini ni lazima watupe muda tufanye uhakiki ili kubaini kama kweli pembejeo zilifika. Kati ya shilingi bilioni 35 za madeni ya awali, imebainika kuwa sh. bilioni 6 tu ndiyo za halali. Na bado kuna sh. bilioni 30 nyingine zinafanyiwa uhakiki,” amesema Waziri Mkuu.

“Tumewasihi waendelee kuwa wavumilivu ili tukamilishe zoezi hili na tujue Serikali inadaiwa kiasi gani. Napenda niwahakikishie kuwa kazi hiyo inaendelea na tuko kwenye hatua za mwisho, na wale wote wenye madai halali ambao ni waaminifu watalipwa na Serikali.”  

Akijibu swali la nyongeza ni kwa nini Serikali isiharakishe malipo hayo kwani kuna baadhi nyumba zao zimepigwa mnada na mabenki, na wengine wamepoteza maisha kwa sababu ya mshtuko, Waziri Mkuu alisema siku ya mwisho ya kufanya uhakiki ilikuwa jana Mei 31 kwa hiyo anasubiri taarifa kutoka Halmashauri zote kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Alisema wenye mabenki wameisikia kauli ya Serikali kwa hiyo hawana sababu ya kukimbilia kuuza mali za mawakala kwa njia ya mnada kwani hatua zinazochukuliwa na Serikali ni nzuri na zimeokoa mabilioni ya fedha. 

Alisema watumishi wote wa umma waliohusika kwenye ubadhirifu huo, watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wawekezaji nchini wasihofu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusiana na usafirishaji wa mchanga wenye madini kwenda nje ya nchi.

Akijibu swali ya Bw. Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora “Ninawasihi wawekezaji wasiwe na shaka kwa sababu lengo la Serikali ni jema. Tunataka tujiridhishe kuwa kuna nini hasa ndani yake. Hatuna jambo ambalo tumelifanyia kazi isipokuwa kwa watu wetu wa ndani,” amesema.

“Kila kitu kitakuwa wazi, ninawaomba Watanzania na wawekezaji wawe watulivu. Kazi tunayoifanya ni kwa manufaa ya Watanzania. Nia yetu ni kulinda rasilmali za nchi yetu, na hadi sasa bado hatujatoa taarifa rasmi, bado tunasubiri taarifa ya kamati ya pili,” alisisitiza.

Akijibu swali la nyongeza ni mikakati gani Serikali imeweka kwa kufunga mashine kwenye chanzo ili kuhakikisha tatizo hilo haijirudii tena, Waziri Mkuu alisema Serikali imekuwa inapokea wawekezaji ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye eneo hilo. Alisema zamani kulikuw ana usiri wa kupata wawekezaji wa aina hiyo lakini hivi sasa kumeanza kuwa na uwazi katika eneo hilo.

“Tutaamua kujenga mashine zetu hapa hapa nchini au kuwakaribisha wawekezaji katika eneo hili au kuona uwezo wa Serikali ili tuweze kutatua tatizo la kupoteza mchanga ambao tunalazimika kuupeleka nje ya nchi kwa ajili ya uyeyushaji wa madini yaliyomo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ni mwitikio wa kilio cha siku nyingi cha wananchi wa maeneo husika pamoja na waheshimiwa wabunge ambapo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimtuma aende Kahama kuchukua sampuli za mchanga na alipompa taarifa, Rais akaunda tume mbili za kufuatilia suala hilo.

Read More

Wednesday, May 31, 2017

WAZIRI MKUU AHIMIZA UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU

*Ataka VIGUTA iende kwenye halmashauri, ihamasishe watumishi
*Asema Watanzania wanataka nyumba bora, hawana muda wa kusimamia ujenzi
          
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri za wilaya nchini ziangalie uwezekano wa kuwapatia watumishi wake nyumba za bei nafuu kwa malipo kidogo kidogo.

Amesema Halmashauri za wilaya kupitia mapato ya ndani, japo si makubwa zinaweza kuandaa mazingira yatakayowawezesha watumishi wake kupata nyumba kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na Muungano wa Vikundi vya Vicoba Tanzania (VIGUTA).

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Mei 31, 2017) mara baada ya kutembelea maonyesho ya Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za Waheshimiwa Wabunge (Low Cost Housing) yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. 
         
Waziri Mkuu aliwashauri  viongozi wa VIGUTA wafanye mawasiliano na Halmashauri zote na akawataka watenge muda wa kuzitembelea  Halmashauri hizo ili kuonyesha nia na uwezo wao wa kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo malipo yake hulipwa kidogo kidogo kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.

“Watanzania wengi hivi sasa wanapendelea nyumba ndogo, nzuri na ambazo zimekamilika. “Wengi wao, na hasa wafanyakazi, siku hizi wana shughuli nyingi na hawana muda wa kujenga nyumba na kuzisimamia wenyewe kama zamani. Hivyo, wanahitaji makampuni yanayoweza kuwanjengea nyumba na wao wakalipa kidogo kidogo,” amesisitiza.
         
Aliwaaasa viongozi wa VIGUTA wahakikishe kuwa wanajenga nyumba zenye ubora unaokubalika ili waweze kuaminika hali ambayo itawawezesha kupata wateja wengi zaidi.

“Katika kipindi hiki ambacho Serikali inahamia Dodoma, Muungano wa Vikundi vya VICOBA au VIGUTA unayo nafasi kubwa ya kuwapatia watumishi wanaohamia nyumba za kuishi kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,” Waziri Mkuu alisema.

Alisema watumishi wengi wanaoingia gharama kubwa kwa kuishi katika nyumba za kupanga huku wakilipa kodi, sasa wamepata kimbilio kwani  wanaweza kujengewa nyumba kwa muda mfupi na kwa bei nafuu na wakalipa kidogokidogo kwa kipindi cha hadi miaka 15.

Naye, Mwenyekiti wa VIGUTA Taifa, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana uwezo wa kujenga nyumba kwa gharama ya shilingi milioni 12, milioni 15, milioni 25 na milioni 60 kutegemeana na ukubwa wa nyumba.

Alisema wameweka viwango tofauti ili kuwawezesha Watanzania wenye kipato cha chini kumiliki nyumba zao wenyewe.

(
Read More

Tuesday, May 30, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA UJENZI WA NYUMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa  Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto  ni  Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa  Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto  ni  Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.


Read More

Monday, May 29, 2017

BUNGENI LEO MEI 29,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Asha Abdullah Juma (kushoto) na Taska Mbogo kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 29, 2017.


Read More

Sunday, May 28, 2017

RAMADHAN KAREEM

Salaam za kheri ya mfungo wa Ramadhani  kwa Waislam wote Duniani kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Read More

Friday, May 26, 2017

MATUKIO PICHA BUNGENI LEO 26 MEI,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu  Vijijini, Fratei Massay kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Wapili kulia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makumira kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kushoto ni  Mbunge wa Newala Mjini, Capt. George Mkuchika.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makiragi na Anna Lupembe kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Pikipiki na Vipuri  vyake pamoja na baadhi ya wabunge, ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango. 


Read More

Tuesday, May 23, 2017

MAJALIWA: BENKI VIKOPESHENI VIKUNDI VYA WAKULIMA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki mbalimbali nchini ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo kutoa mikopo kwa vikundi vya kilimo ili viweze kupata fedha za kununulia matrekta.

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na adhma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Mei 23, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha kuunganisha Matrekta URSUS-TAMCO, Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kiwanda hicho kinalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani kwa kuwa wakulima watakuwa na zana za kisasa.

Aidha, amevitaka vyuo vya kilimo nchini kununua matrekta hayo kwa lengo la kufundishia wanafunzi wake ili wanapohotimu wawe na uwezo wa kutumia zana hizo vizuri na kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yao.

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Halmashauri nchini kuendelea kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, uwekezaji, makazi, biashara na huduma za jamii, hivyo kuepuka migogoro ya ardhi kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema wataunganisha matrekta 2,400,  harrow 2,400 na majembe 2,400 katika mradi huo wa kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO ikiwa ni mkataba wa awali.

Amesema kiwanda hicho kina wafanyakazi 27 kwa hatua za mwanzo. Aidha, idadi hiyo itaongezeka kutokana na mahitaji ambapo baadhi ya wafanyakazi watapewa mafunzo nchini Poland na watakaporudi watakuwa wakufunzi wa watakaoajiriwa.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kiwanda hicho kimeazima wafanyakazi wengine wakiwemo watano kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 10 kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi nchini, wawili kutoka CAMARTEC ambao wanashirikiana na wataalamu 10 kutoka URSUS kuunganisha matrekta.

Bw. Mkucha amesema wafanyakazi 10 kutoka Tanzania wanatarajiwa kwenda nchini Poland kufanya mafunzo mahsusi na watakaporejea watakuwa wakufunzi kwa watumishi wengine watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.

Amesema mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha kuunganishia matrekta ya URSUS, mradi unahusisha uanzishwaji wa vituo vinane kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja na kuuzia matrekta, zana na vifaa vingine.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda mkoani humo ni pamoja na kukatika kwa umeme, hivyo ameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANECO) kuongeza vituo vya kupozea umeme.

Awali Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage amesema kwa sasa nchini kuna viwanda vikubwa 393 kati yake 84 viko mkoani Pwani, ambapo amewaomba viongozi wa mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya wanawake na vijana kuanzisha viwanda vidogo.

Mara baada ya kutembea kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO Waziri Mkuu alitembelea eneo la uwekezaji la Kamal (Kamal Indusrial Estate) lililoko katika Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo.
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS KILICHOPO KIBAHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Bagamoyo wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege mkoani Pwani Mei 23, 2017.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia  kwake  ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Charles Mwijage.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei  23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia  kwake  ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Charles Mwijage.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka baada ya kutembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrual Estate lililopo Kerege, Bagamoyo Mei 23, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. 


Read More