Home
All posts
Wednesday, June 21, 2017
Tuesday, June 20, 2017
BUNGENI DODOMA LEO TAREHE 22 JUNE,2017
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, bungeni mjini Dodoma juni 20, 2017. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, bungeni mjini Dodoma juni 20, 2017. |
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA USHIRIKIANO, UPENDO, KWA DINI ZOTE TANZANIA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017. |
| Baadhi ya Wabunge wakibadilishina mawazo wakati wa futari iliyo andaliwa na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai , kutoka kulia, Mbunge wa Ilala Idd Zungu. katikati Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge .na kushoto ni Mbunge wa Mbarali Haroon Mulla .Futari hiyo ilifuturiwa katika viwanja vya Bunge June 20, 2017 Mjini Dodoma. |
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . akitoa salamu za Shukurani kwaniaba ya WaBunge na wafanyakazi wa Bunge , kwa Spika wa Bunge Job Ndugai , Kwakuwafuturisha , June. 20 .2017 katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma |
Monday, June 19, 2017
MAJALIWA AZINDUA KAMUSI KUU YA KISWAHILI
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Kamusi Kuu ya Kiswahili kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 19, 2017. |
BUNGENI DODOMA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Juni 19,2017. |
Tuesday, June 6, 2017
MSIWAFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU - WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wazazi wote
nchini ambao wana watoto wenye ulemavu wasiwafiche na badala yake wahakikishe
wanapata elimu na kutimiza ndoto zao.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumanne, Juni 6,
2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, walimu na
wanafunzi kwenye uzinduzi wa usambazaji wa vifaa vya elimu maalum uliofanyika
kwenye viwanja vya ya msingi Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam.
“Nikiwa mwalimu kitaaluma, natambua kwamba
mapungufu ya kimwili, kisaikolojia, kiakili au ulemavu wa aina yoyote si
kikwazo cha kutimiza ndoto za watoto wetu. Hili linadhihirika kwenye maeneo
mbalimbali nchini,” alisema na kutoa mfano wa utumishi Serikalini ambako kuna
viongozi wenye mahitaji maalum, lakini wamekuwa wakitoa mchango mkubwa bila
kujali hali yao kimwili au vinginevyo.
“Hivyo,
nawasihi wazazi wenzangu, msikatishe ndoto za watoto wenu wenye mahitaji maalum
kwa kuwaficha. Wapelekeni shuleni wakapate elimu, iwafae maishani,” alisema.
Waziri Mkuu alisema usambazaji wa
vifaa hivyo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuhakikisha kuwa kila mtoto wa Kitanzania mwenye umri wa kwenda shule, anapata
huduma hiyo bila kujali hali yake ya kimwili, kiakili, kiafya na uwezo wa
kifedha.
Waziri Mkuu pia alimwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi
Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene ahakikishe anandaa utaratibu wa
kuwatambua watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupangiwa bajeti kulingana
na mahitaji yatakayoainishwa.
“Tunapoendelea na jitihada hizi za
kuwawezesha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu, ni vizuri tukawa na
utaratibu endelevu wa kubaini idadi kamili ya watoto hao kupitia uandikishaji
wa watoto shuleni. Bila kubaini idadi yao, itatuwia vigumu kupanga bajeti kwa
ajili ya watoto wetu hao. Zoezi hili linaweza kufanyika wakati wa uandikishaji
na likawa endelevu kadiri wanavyopanda vidato,” alisema.
Waziri Mkuu alisema mbali ya vifaa
vya wanafunzi wasioona na wenye baki ya usikivu (hard of hearing), Serikali pia
imenunua vifaa kwa ajili ya walimu wao ili vitumike kufundishia na kupimia ili
kubaini mahitaji maalum ya ujifunzaji kwa watoto wanaoandikishwa shuleni.
Alisema
vifaa vinavyoanza kusambazwa, vitasaidia kuinua kiwango cha taaluma kwenye
shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum na pia vitasaidia watoto wengi
zaidi wenye mahitaji maalum wapate elimu na kuongeza hamasa kwa walimu
wanaofundisha kwenye shule husika.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia hadhira hiyo, Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema uzinduzi wa zoezi la
usambazaji wa vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa utahusisha
mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na kwamba zoezi hilo litazinufaisha shule za
msingi 213 kati ya 408; na shule za sekondari 22 kati ya 43 zenye wanafunzi wa mahitaji maalum.
Alisema vifaa vilivyonunuliwa
vimegharimu sh. bilioni 3.6 kutokana na michango ya
washirika wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, Shirika la Misaada ya Maendeleo
ya Kimataifa (DfID) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Sweden (SIDA) na kwamba wizara hiyo itaendelea
kununua vifaa zaidi kulingana na bajeti inayotolewa.
Alivitaja vifaa vilivyoninunuliwa
kuwa ni mashine za nukta nundu 932; vivunge vya kufundishia wasioona 1,495; karatasi
za kuandikia nukta nundu (ream) 2,548; karatasi za kurudufishia (ream) 1,150;
shime sikio (hearing aid) 1,150 na vivunge vya upimaji wa mahitaji maalum ya
kielimu 78.
Naye Mratibu wa Elimu kutoka SIDA, Bi. Helena
Reutersward akitoa salamu kwa niaba ya washirika wa maendeleo alisema wao
wamedhamiria kuboresha sekta ya elimu hapa nchini na hasa elimu kwa watoto
wenye mahitaji maalum.
“Elimu ni muhimu ni kwa kila mtu lakini ni muhimu
zaidi kwa watu wenye mahitaji maalum. Washirika wa maendeleo tutaendelea
kushirikiana na Serikali katika kuchangia jitihada zake za kuboresha elimu
nchini Tanzania,” alisema.
WAZIRI MKUU AZINDUA USAMBAZAJI VIFAA KUFUNDISHIA SAYANSI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa wa Banki ya Dunia anayeshughulikia Elimu nchini Tanzania Bibi Cornelia Jesse , katikati ni Ofisa wa Ubalozi Swiden Nchini Tanzania anayeshughulikia Elimu Bibi Helena Reutersward , Maofisa hao walishiriki katika Uzinduzi wa Usambaziji vifaa vya kufundishia Masomo ya Sayansi , Shughuli hiyo ilifanyika leo 6 june 2017 katika Viwanja vya Jeshi Lugalo Dar es salaam.
|
WAZIRI MKUU AAGIZA UJENZI WA MAABARA UKAMILISHWE HARAKA
Saturday, June 3, 2017
WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI GAIRO
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe. |
| Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. |
WAZIRI MKUU AAGIZA KILOSA WAILIPE GAIRO DENI LA0
* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.
“Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.
Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini.
“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.
Mapema akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel Mchembe alisema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo inaanzishwa na hawakuwa wamefungua akaunti ya wilaya.
“Fedha hizi zilikuwa zinapitia Kilosa wakati wilaya ya Gairo imeanzishwa kwa kuwa kipindi hicho wilaya ya Gairo ilikuwa bado haijafungua akaunti. Fedha hizi zinajumuisha ruzuku ya uendeshaji, mapato ya ndani na miradi ya maendeleo,” alisema.
Alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliagiza wilaya ya Kilosa ilipe deni hilo kabla ya Juni 2016 lakini hadi sasa wameshalipa sh. milioni 20 tu ambapo sh. milioni 10 zililipwa Desemba 2015 na nyingine milioni 10 zililipwa Mei 2017.
Akisisitiza kuhusu makusanyo ya mapato, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi hao kuwa Serikali imekwishatoa agizo la kutumia mashine za kielektroniki kukusanya mapato ifikapo Julai mosi.
“Makusanyo ya mapato ya ndani ni eneo muhimu sana. Tumeshaagiza, mwisho wa kutumia mifumo ya kawaida ni Juni 30. Kuanzia Julai mosi, kila eneo ni lazima litumie mashine za kielektroniki,” alisema Waziri Mkuu.
Alihoji ni kwa nini Halmashauri ya Gairo ililenga kukusanya sh.milioni 889.5 lakini kufikia Aprili mwaka huu, makusanyo halisi yalikuwa ni sh. milioni 356.2 sawa na asilimia 40.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) ya wilaya hiyo ambao hadi kufikia Aprili, 2017 wameweza kukusanya sh. milioni 601.5 ikilinganishwa na makadirio yao ya kukusanya sh. milioni 471 kwa mwaka. Waziri Mkuu aliwapongeza kwa sababu wamevuka lengo kwa asilimia 127.6.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku ya wilaya hiyo, asubuhi alipanda mti kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa maadhimisho ya siku ya upandaji miti hapa nchini.
Pia alikagua mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale, na mradi wa visima 10 ambayo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu. Pia atazungumza na wananchi wa Gairo mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Friday, June 2, 2017
MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA IJUMAA KWENYE MSIKITI WA AL - GADDAF
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Al- Gadaf mjini Dodoma Juni 2, 2017.
|
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Nurdin Kishik ambaye ni Mhadhiri wa Kimataifa wa Dini ya Kiislaam, (kulia) na ujumbe wake, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Juni 2, 2017. |
Thursday, June 1, 2017
TUMEBAINI MADAI HEWA YA BILIONI 21/-
* Ni kwenye malipo ya mawakala wa mbolea, awali yalifikia sh. bilioni 65.
*Akiri kukutana nao, asema wenye madai halali wote watalipwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini madudu katika uhakiki wa madeni ya mawakala wa mbolea kwa sababu baadhi yao hawakuwa waaminifu.
“Tulipoanzisha mfumo wa kutoa pembeje kwa njia vocha kwa kuwatumia mawakala kupeleka pembejeo vijijini, tulibaini kuwa baadhi yao walikuwa siyo waaminifu. wakiorodhesha majina ya wakulima na kuandika kuwa wamewapa madawa napembejeo wakati hawapo.”
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni mosi, 2017) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Morogoro), Bi. Devotha Minja kwenye kipindi cha maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma.
Bi. Minja alitaka kujua ni kwa nini Serikali haijawalipa mawakala hao hadi sasa licha ya kuwa inatambua kwamba walifanya kazi ya kusambaza pembejeo hizo.
“Tulijikuta tuna deni la shilingi bilioni 65. Nilipokutana na mawakala wiki mbili zilizopita, niliwaahidi kwamba tutawalipa lakini ni lazima watupe muda tufanye uhakiki ili kubaini kama kweli pembejeo zilifika. Kati ya shilingi bilioni 35 za madeni ya awali, imebainika kuwa sh. bilioni 6 tu ndiyo za halali. Na bado kuna sh. bilioni 30 nyingine zinafanyiwa uhakiki,” amesema Waziri Mkuu.
“Tumewasihi waendelee kuwa wavumilivu ili tukamilishe zoezi hili na tujue Serikali inadaiwa kiasi gani. Napenda niwahakikishie kuwa kazi hiyo inaendelea na tuko kwenye hatua za mwisho, na wale wote wenye madai halali ambao ni waaminifu watalipwa na Serikali.”
Akijibu swali la nyongeza ni kwa nini Serikali isiharakishe malipo hayo kwani kuna baadhi nyumba zao zimepigwa mnada na mabenki, na wengine wamepoteza maisha kwa sababu ya mshtuko, Waziri Mkuu alisema siku ya mwisho ya kufanya uhakiki ilikuwa jana Mei 31 kwa hiyo anasubiri taarifa kutoka Halmashauri zote kupitia kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alisema wenye mabenki wameisikia kauli ya Serikali kwa hiyo hawana sababu ya kukimbilia kuuza mali za mawakala kwa njia ya mnada kwani hatua zinazochukuliwa na Serikali ni nzuri na zimeokoa mabilioni ya fedha.
Alisema watumishi wote wa umma waliohusika kwenye ubadhirifu huo, watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wawekezaji nchini wasihofu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusiana na usafirishaji wa mchanga wenye madini kwenda nje ya nchi.
Akijibu swali ya Bw. Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Tabora “Ninawasihi wawekezaji wasiwe na shaka kwa sababu lengo la Serikali ni jema. Tunataka tujiridhishe kuwa kuna nini hasa ndani yake. Hatuna jambo ambalo tumelifanyia kazi isipokuwa kwa watu wetu wa ndani,” amesema.
“Kila kitu kitakuwa wazi, ninawaomba Watanzania na wawekezaji wawe watulivu. Kazi tunayoifanya ni kwa manufaa ya Watanzania. Nia yetu ni kulinda rasilmali za nchi yetu, na hadi sasa bado hatujatoa taarifa rasmi, bado tunasubiri taarifa ya kamati ya pili,” alisisitiza.
Akijibu swali la nyongeza ni mikakati gani Serikali imeweka kwa kufunga mashine kwenye chanzo ili kuhakikisha tatizo hilo haijirudii tena, Waziri Mkuu alisema Serikali imekuwa inapokea wawekezaji ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye eneo hilo. Alisema zamani kulikuw ana usiri wa kupata wawekezaji wa aina hiyo lakini hivi sasa kumeanza kuwa na uwazi katika eneo hilo.
“Tutaamua kujenga mashine zetu hapa hapa nchini au kuwakaribisha wawekezaji katika eneo hili au kuona uwezo wa Serikali ili tuweze kutatua tatizo la kupoteza mchanga ambao tunalazimika kuupeleka nje ya nchi kwa ajili ya uyeyushaji wa madini yaliyomo,” alisema.
Waziri Mkuu alisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ni mwitikio wa kilio cha siku nyingi cha wananchi wa maeneo husika pamoja na waheshimiwa wabunge ambapo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alimtuma aende Kahama kuchukua sampuli za mchanga na alipompa taarifa, Rais akaunda tume mbili za kufuatilia suala hilo.
Wednesday, May 31, 2017
WAZIRI MKUU AHIMIZA UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU
*Ataka VIGUTA iende kwenye halmashauri, ihamasishe watumishi
*Asema Watanzania wanataka nyumba bora, hawana muda wa kusimamia ujenzi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri za wilaya nchini ziangalie uwezekano wa kuwapatia watumishi wake nyumba za bei nafuu kwa malipo kidogo kidogo.
Amesema Halmashauri za wilaya kupitia mapato ya ndani, japo si makubwa zinaweza kuandaa mazingira yatakayowawezesha watumishi wake kupata nyumba kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na Muungano wa Vikundi vya Vicoba Tanzania (VIGUTA).
Ametoa wito huo leo (Jumatano, Mei 31, 2017) mara baada ya kutembelea maonyesho ya Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za Waheshimiwa Wabunge (Low Cost Housing) yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu aliwashauri viongozi wa VIGUTA wafanye mawasiliano na Halmashauri zote na akawataka watenge muda wa kuzitembelea Halmashauri hizo ili kuonyesha nia na uwezo wao wa kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo malipo yake hulipwa kidogo kidogo kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.
“Watanzania wengi hivi sasa wanapendelea nyumba ndogo, nzuri na ambazo zimekamilika. “Wengi wao, na hasa wafanyakazi, siku hizi wana shughuli nyingi na hawana muda wa kujenga nyumba na kuzisimamia wenyewe kama zamani. Hivyo, wanahitaji makampuni yanayoweza kuwanjengea nyumba na wao wakalipa kidogo kidogo,” amesisitiza.
Aliwaaasa viongozi wa VIGUTA wahakikishe kuwa wanajenga nyumba zenye ubora unaokubalika ili waweze kuaminika hali ambayo itawawezesha kupata wateja wengi zaidi.
“Katika kipindi hiki ambacho Serikali inahamia Dodoma, Muungano wa Vikundi vya VICOBA au VIGUTA unayo nafasi kubwa ya kuwapatia watumishi wanaohamia nyumba za kuishi kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,” Waziri Mkuu alisema.
Alisema watumishi wengi wanaoingia gharama kubwa kwa kuishi katika nyumba za kupanga huku wakilipa kodi, sasa wamepata kimbilio kwani wanaweza kujengewa nyumba kwa muda mfupi na kwa bei nafuu na wakalipa kidogokidogo kwa kipindi cha hadi miaka 15.
Naye, Mwenyekiti wa VIGUTA Taifa, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana uwezo wa kujenga nyumba kwa gharama ya shilingi milioni 12, milioni 15, milioni 25 na milioni 60 kutegemeana na ukubwa wa nyumba.
Alisema wameweka viwango tofauti ili kuwawezesha Watanzania wenye kipato cha chini kumiliki nyumba zao wenyewe.
(
Tuesday, May 30, 2017
MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA UJENZI WA NYUMBA
Monday, May 29, 2017
BUNGENI LEO MEI 29,2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Asha Abdullah Juma (kushoto) na Taska Mbogo kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 29, 2017.
|
Sunday, May 28, 2017
RAMADHAN KAREEM
![]() |
| Salaam za kheri ya mfungo wa Ramadhani kwa Waislam wote Duniani kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa Kassim Majaliwa. |
Friday, May 26, 2017
MATUKIO PICHA BUNGENI LEO 26 MEI,2017
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Wapili kulia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makumira kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kushoto ni Mbunge wa Newala Mjini, Capt. George Mkuchika. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makiragi na Anna Lupembe kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Pikipiki na Vipuri vyake pamoja na baadhi ya wabunge, ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango. |
Tuesday, May 23, 2017
MAJALIWA: BENKI VIKOPESHENI VIKUNDI VYA WAKULIMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki mbalimbali nchini ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo kutoa mikopo kwa vikundi vya kilimo ili viweze kupata fedha za kununulia matrekta.
Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na adhma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Mei 23, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha kuunganisha Matrekta URSUS-TAMCO, Kibaha mkoani Pwani.
Amesema kiwanda hicho kinalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani kwa kuwa wakulima watakuwa na zana za kisasa.
Aidha, amevitaka vyuo vya kilimo nchini kununua matrekta hayo kwa lengo la kufundishia wanafunzi wake ili wanapohotimu wawe na uwezo wa kutumia zana hizo vizuri na kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yao.
Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Halmashauri nchini kuendelea kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, uwekezaji, makazi, biashara na huduma za jamii, hivyo kuepuka migogoro ya ardhi kwa siku zijazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema wataunganisha matrekta 2,400, harrow 2,400 na majembe 2,400 katika mradi huo wa kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO ikiwa ni mkataba wa awali.
Amesema kiwanda hicho kina wafanyakazi 27 kwa hatua za mwanzo. Aidha, idadi hiyo itaongezeka kutokana na mahitaji ambapo baadhi ya wafanyakazi watapewa mafunzo nchini Poland na watakaporudi watakuwa wakufunzi wa watakaoajiriwa.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kiwanda hicho kimeazima wafanyakazi wengine wakiwemo watano kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 10 kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi nchini, wawili kutoka CAMARTEC ambao wanashirikiana na wataalamu 10 kutoka URSUS kuunganisha matrekta.
Bw. Mkucha amesema wafanyakazi 10 kutoka Tanzania wanatarajiwa kwenda nchini Poland kufanya mafunzo mahsusi na watakaporejea watakuwa wakufunzi kwa watumishi wengine watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.
Amesema mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha kuunganishia matrekta ya URSUS, mradi unahusisha uanzishwaji wa vituo vinane kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja na kuuzia matrekta, zana na vifaa vingine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda mkoani humo ni pamoja na kukatika kwa umeme, hivyo ameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANECO) kuongeza vituo vya kupozea umeme.
Awali Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage amesema kwa sasa nchini kuna viwanda vikubwa 393 kati yake 84 viko mkoani Pwani, ambapo amewaomba viongozi wa mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya wanawake na vijana kuanzisha viwanda vidogo.
Mara baada ya kutembea kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO Waziri Mkuu alitembelea eneo la uwekezaji la Kamal (Kamal Indusrial Estate) lililoko katika Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo.
MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS KILICHOPO KIBAHA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Bagamoyo wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege mkoani Pwani Mei 23, 2017. |
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
|
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
-
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiuliza jambo kwa Kaimu Meneja wa Uwa...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.
