Thursday, November 23, 2017

WAZIRI MKUU AKABIDHI CARRY KWA TIMU YA AFISI KUU ZANZIBAR

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi zawadi ya gari aina ya carry kwa timu ya mpira wa miguu ya Afisi Kuu Zanzibar baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya mpira wa miguu ya Majimbo.

Mashindano hayo yaliyohusisha majimbo 18 ya kisiwani Unguja yaliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambayo yalizinduliwa Machi 23, 2017 na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein.

Alikabidhi zawadi hiyo jana (Jumamosi, Novemba 25, 2017) katika mechi ya fainali iliyozikutanisha timu ya Afisi Kuu na timu ya Jimbo Kwahani. Katika mechi hiyo ya fainali Afisi Kuu iliibuka na ushindi wa magoli matatu na Jimbo Kwahani iliambulia goli moja.

Waziri Mkuu aliipongeza CCM Zanzibar kwa kubuni mashindano hayo ambayo yaliwakutanisha vijana. Alisema mbali na kuimarisha afya zao pia ni chanzo cha ajira hivyo ameishauri CCM upande wa Bara kuiga ubunifu huo.

“Ubunifu huu wa kuanzisha mashindano ya majimbo unapaswa kuigwa na Tanzania Bara, waanzishe mashindano haya kwa kuyakutanisha majimbo yote. Ni vema jambo hili likawa la Kitaifa ili kunufaisha vijana wengi.”

Pia Waziri Mkuu alimpongeza Muwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mohammed Raza ambaye ndiye alikuwa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, pia aliwashauri vijana walioshiriki mashindano hayo kuendelea kufanya mazoezi.

Katika mashindano hayo timu ya Jimbo Magomeni ilipewa tuzo ya timu iliyoonyesha hamasa kubwa, timu ya Jimbo Mfenesini iliibuka kidedea kwa kuongoza kwenye nidhamu na golikipa wa timu ya Afisi Kuu, Vuai Makame Jecha alipewa tuzo ya mchezaji bora.
Read More

Tuesday, November 21, 2017

WAZIRI JENISTA ATEMBELEA VITUO VYA HALI YA HEWA ARUMERU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano na baadhi ya Watendaji wa Serikali alipofanya ziara Wilayani Arumeru kujionea Vituo vya Hali ya Hewa vinavyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Novemba 21, 2017.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika ziara na Baadhi ya Watendaji wa Serikali walioongozana naye kutembelea Vituo vya Hali ya Hewa vilivyofungwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari Arumeru.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mwikolojia Bi.Clara Manase alipokuwa akieleza faida ya kituo cha Utoaji wa Taarifa za Hali ya Hewa kilichojengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha mkoani Arusha


Read More

WAZIRI MHAGAMA AITAKA HALMASHAURI YA BAHI KUKAMILISHA UJENZI WA SOKO LA KIGWE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.

“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.
Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.

“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel
Kwa upande wake mkazi wa Kigwe Bi.Anastazia Mkatato alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo litatatua changamoto iliyopo ya kukosa soko la kudumu kwani yaliyopo ni madogo yanayomilikiwa na watu binafsi.

“Ninaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua kutujengea soko hapa Kigwe na hii itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa wingi kupelekea kukuza uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.

Naye Mratibu wa Mradi Taifa Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko hili ni muhimu kwa wana Kigwe na maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa sokoni.
 “Tayari Ofisi yangu itachukua changamoto hii ya kukosekana kwa meza za kuuzia na kuitatua ndani ya mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza haya.”Alisisitiza Bw.Swai

AWALI:
Ujenzi wa soko la Kigwe  umegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 68 ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ilitoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo kuchangia jumla ya  shilingi Milioni 15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo rasmi la kufanyia biashara na kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleao yao.
Read More

WAZIRI MHAGAMA AITAKA HALMASHAURI YA BAHI KUKAMILISHA UJENZI WA SOKO LA KIGWE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi Dodoma.

Afisa Mtendaji Kata Bw. John Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko Kigwe kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Bahi kuona maendeleo ya ujenzi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe lililofadhiliwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na Halmashauri wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama Wilayani Bahi Dodoma.


Mratibu Taifa wa Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) Bw. Walter Swai akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Kigwe walipotembelea Kijiji hicho kuona ujenzi wa soko la Kigwe unavyoendelea.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi Bi. Rachel Chuwa wakati wa ziara yake Kigwe.

Read More

Monday, November 20, 2017

WAZIRI MHAGAMA : UHABA WA SUKARI NCHINI WAPATA MWAROBAINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa MbigiriKinachoendelea kujengwa Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa kufufuliwa kwa kiwanda sambamba na shamba la Miwa la Mbigiri itasaidia kuondoa uhaba wa sukari nchini kwa kuzingatia uwepo wa kiwanda hicho na shamba la miwa Mbigiri.

Ameyasema hayo mapema mwishoni mwa wiki hii walipokuwa katika ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kujionea namna uboreshaji wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza unavyoendelea.

Alieleza kuwa, Tayari hekari 300 zimeshapandwa miwa kati ya Hekari 1200 na hekari 700 zimeshalimwa ambapo hii itasaidia sana kuongeza uzalishaji wa sukari nchini tofauti na ilivyo sasa na kuwaomba Watanzania kuunga mkono jitihada za Mifuko ya Hifadhi ya PPF na NSSF ambao wamechangia asilimia hamsini kwa hamsini katika kuhakikisha kiwanda na shamba vinafikia malengo ya kuzalisha sukari kwa wingi nchini.

“Ninaipongeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kwa kuona umuhimu wa kukiboresha kiwanda hiki ili kukidhi hitaji la nchi katika kutatua changamoto ya sukari nchini ambapo matarajio ni kuvuna miwa tani 500,000 na uzalishaji wa sukari utakuwa Tani 30,000”Alisisitiza Mhagama

Sambamba na hilo,  Waziri Mhagama alifafanua kuwa uwepo wa viwanda hivi ni moja ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Miaka mitano unaoelekeza kuwa na uchumi wa viwanda.

“Kiwanda hiki kikianza kufanya kazi kitakuwa kimekidhi matakwa ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa ya miaka Mitano ambao unaeleza uchumi wetu wa viwanda uwe uchumi utakaotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini na bidhaa zitakazo zalishwa ziwanufaishe Watanzania”Alisema Mhagama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa alieleza kuwa Kiwanda hiki kikimalizika kitasaidia kuongeza uzalishaji wa sukari nchini na kupata masoko mpaka nchi za nje.

“Jambo hili likifanikiwa litaweza kutatua changamoto ya sukari hapa nchini basi sisi kama Kamati na kwa niaba ya wajumbe wenzangu tunaipongeza sana Serikali kwa hatua kubwa iliyofanya na hii itasaidia pia kujikwamua kiuchumi sisi kama Nchi ” alisisitiza Mtengerwa

Aidha Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara alieleza kuwa lengo jingine la kukifufua kiwanda hicho ni pamoja na kukuza uchumi wananchi kwa kuuza sukari ndani na nje ya nchi.

“Tunatarajia kupata soko la ndani na nje hususani kuuza ukanda wa Afrika ya Kati hivyo sukari itakayozalishwa lazima iwe ya viwangi vya juu na mfano mzuri ni nchi ya Congo ambao wanazalisha tani elfu 70 ingawa hitaji lao kwa mwaka ni tani laki moja hii ni picha halisi la uwepo wa siko la sukari barani Afrika” Alieleza Prof.Kahyarara

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe alipongeza juhudi za Serikali kufufua kiwanda hicho cha Mbigiri na shamba la miwa ambapo vitaleta tija kwa jamii kwa ujumla na kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge kuona umuhimu wa kutembelea Kiwanda hicho na Shamba la Miwa.
Read More

MAVUNDE: WATU WAKIKOSA MAADILI TAIFA LINAKUFA


                               
 *Ataka vijana waweke malengo maishani mwao
NAIBU WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Anthony Mavunde amesema Taifa lenye maadili ndilo linaloishi na watu wanapokosa maadili Taifa linakufa.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akiwahutubia vijana zaidi 3,500 wanaosoma vyuo vya elimu ya juu vya mkoa wa Dodoma ambao walishiriki mkesha wa kusifu na kuabudu (Campus Night 2017) kwenye ukumbi wa Chimwaga, mjini Dodoma.

“Naendelea kuiona Tanzania yenye ustawi mkubwa sana kama tutakuwa na vijana wenye kumjua Mungu, wenye hofu ya Mungu na wenye kufuata maadili mema kwani kukosa maadili kunaua Taifa,” alisema Naibu Waziri huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Aliwataka vijana hao watambue kuwa wameletwa vyuoni kusoma na siyo kujihusisha na mambo ambayo ni kinyume na maadili. “Katika maisha lazima utambue njia yako, usipoijua utapata shida tu. Ukiifahamu njia yako ni lazima unaitunza hadi ikufikishe mwisho,” aliongeza.

Akitoa mfano, Naibu Waziri Mavunde aliwaeleza wanavyuo kwamba hakuna jambo baya kama mtu kufikia hatua ya kuingia chuo kikuu au chuo kingine cha elimu ya juu lakini asijue anapaswa kufanya nini.

“Hakuna jambo baya kama hivi sasa uko chuo kikuu lakini hujajua unataka kufanya nini maishani mwako. Ni sawa na kufanya biashara ya kununua mablanketi na kwenda kuyauza Dar es Salaam ambako kuna joto wakati wote au kuamua kufanya biashara ya ice cream katika maeneo ya baridi kama vile Mafinga,” alisema.

Mapema, akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wanafunzi hao, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ICC Dodoma, Dk. Gerald Ole Nguyaine alisema hatma ya Taifa la Tanzania iko mikononi mwa vijana na ndiyo maana wazazi, walimu na jamii wanawekeza kwenye maisha yao.

Aliwaeleza vijana hao umuhimu wa wao kutambua kusudi la Mungu kwenye maisha yao. “Na sisi tunaamini bila uwepo wa Mungu, hamtaweza kuifikia hiyo hatma mkiwa salama. Kuna kusudi aliloliweka Mungu katika maisha yako wewe ambaye ni kijana, na kamwe usikubali kwenda kaburini kabla hujatimiza hilo kusudi,” alisema. 

“Mungu ana makusudi na maisha yako na sisi ndiyo maana tunawekeza kwenye maisha yako kwa sababu tunajua lipo kusudi maalum la Mungu kukuleta duniani. Tunatumia muda wetu, na rasilmali za Taifa ili kuhakikisha tunawaonyesha njia iwapasayo. Hakuna jambo litafanikiwa maishani mwako kama hauna mahusiano mazuri na Mungu wako,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CAMPUS NIGHT DODOMA, Bw. Ibrahim Kisungwe alisema mwaka huu wamefanya tamasha la campus night kwa mwaka wa saba mfululizo na kila mwaka kumekuwa na mafanikio ya aina tofauti.

Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Made Complete’ yaani umekamilishwa ambayo inaendana na namba saba ambayo ni namba ya ukamilifu.

Wakati huo huo, mhubiri aliyehudumu katika tamasha hilo, Mchg. Pascal Mande wa kanisa la TAG Msasani aliwaeleza vijana hao kwamba wanapaswa kujitambua wao ni akina nani na wapo vyuoni kwa kusudi gani ndipo waweze kufikia kusudi la uwepo wao.

“Kama huwezi kujitambua wewe ni nani, hauwezi kutimiza kusudi la Mungu. Hauwezi kutembea kwenye maono ya Mungu kama hajakubali kukamilishwa na Bwana Yesu,” alisema.

Tamasha hilo lilipambwa na waimbaji mbalimbali wakiwemo Mass Choir (Dodoma), Worship Experience (Dodoma), Angel Benard (Arusha), New Life Band (Arusha), Enos Lazaro (Dar es Salaam) na waimbaji wengine wadogo kama Sakina Naftari (Moshi) na Jerome Venance (Arusha).
Read More

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA MBIGIRI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe wakiangalia mashina ya miwa wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri Wilayani Kilosa Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe akiwakaribisha baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Novemba 18, 2017.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na Mhe. Siuleman Zedi mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri kilichopo Wilaya ya Kilosa Morogoro.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.Suleman Zedi akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) wakati wa ziara yao katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri mkoani Morogoro Novemba 18, 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) walipotembelea katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri kilichopo Morogoro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri Kinachoendelea kujengwa Morogoro.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.Ally Sallehe (mb) akiulizwa swali wakati wa mkutano wa kamati hiyo ilipotembelea katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa katika gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Novemba, 18, 2017.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Taska Mbogo (mb) akichangia hoja wakati wa mkutano wa kamati hiyo walipotembelea katika Sukari na Kilimo cha Miwa katika gereza la Mbigiri mkoani Morogoro Novemba 18, 2017.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia uwasilishaji wa mada kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Stephen Kembwe walipotembelea kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri Mkoani Morogoro Novemba, 18, 2017.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri Morogoro.


Picha ya pamoja ya Baadhi ya Wajumbe wa Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria waliotembelea katika kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa Mbigiri Wilayani Kilosa Morogoro Novemba 18, 2017.

Read More

Saturday, November 18, 2017

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU MKUU WA CWT


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wanafamilia, Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) katika kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Yahya Msulwa nyumbani kwa marehemu, Tuangoma Jijini Dar es Salaam. 
Bw. Msulwa  amefariki dunia juzi (Alhamisi, Novemba 16, 2017) katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Katika maombolezo hayo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali kwa sababu marehemu alishirikiana nayo vizuri akiwa kiongozi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya watumishi wa umma.

Waziri Mkuu amesema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi na mwenye ushirikiano mzuri na wenzake, ambapo Novemba 12, 2017 alipokea barua kutoka CWT iliyosainiwa na marehemu akimualika kushiriki kwenye shughuli za chama.

“Wote tumeguswa na msiba huu, marehemu alikuwa mtumishi wa muda mrefu wa Chama cha Walimu Tanzania tangu mwaka 1996 na alikuwa rafiki na ndugu wa kila mmoja. Alikuwa na tabia njema, hivyo tunatakiwa kuyaenzi mambo mema aliyotuachia”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema. Nawaomba wanafamilia, mke wa marehemu na watoto kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.”
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam
Read More

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU MKUU WA CWT

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma jijini Dar es salaam.Aliye simama kwa kwa Waziri Mkuu ni Mke wake Mama Mary Majaliwa .
Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Katibu Mkuu. Wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu, Alhaji Yahya Msulwa .aliye simama kushoto kwake ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa  pamoja na Mke wake  leo Novemba,18. 2017. Nyumbani kwa marehemu Toangoma Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa Pole, Bi. Sharifa Msulwa. kufuatia kifo cha Mume wake aliye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Marehemu Alhaji Yahya Msulwa  ,Waziri Mkuu alifika nyumbani kwa Marehmu Toangoma  jijini Dar es salam leo November 18, 2017

Read More

Friday, November 17, 2017

SERIKALI YAKARABATI VYUO 10 KWA SH. BILIONI 12

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia sh. bilioni 11.9 kufanya ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na mabweni katika vyuo 10 vya ualimu nchini.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Morogoro, Mpwapwa, Butimba, Kasulu, Songea, Tukuyu, Marangu, Kleruu, Korogwe na Tabora. “Ukarabati huu umewezesha wanachuo 5,920 waliokuwa wanasoma Stashahada maalum ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuhamishiwa katika vyuo hivyo,” ameongeza.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Januari 30, mwakani.

Amesema ili kuongeza fursa za wanafunzi kusomea ualimu, Serikali imepanga kujenga na kukarabati vyuo vya ualimu vya Kitangali, Ndala, Mpuguso na Shinyanga kwa thamani ya sh. bilioni 36.47. 

Amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2016/2017 - 2018/2019, unalenga kuongeza fursa kwa wanafunzi wenye sifa kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya ualimu.

“Ujenzi na ukarabati huu utasaidia kuongeza udahili katika vyuo vya ualimu vya Serikali kutoka wanachuo 20,535 katika mwaka 2017 hadi kufikia wanachuo 23,835 katika mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la wanachuo 3,300,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza maandalizi ya awamu ya pili ya ukarabati wa vyuo saba vya ualimu vya Serikali. Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Tandala, Nachingwea, Tarime, Kinampanda, Mandaka, Patandi na Ilonga.

Amesema vyuo vya ualimu vya Murutunguru, Kabanga na Mhonda vitalazimika kujengwa upya baada ya wahandisi kubaini kuwa vyuo hivyo havifai kukarabatiwa kutokana na uchakavu mkubwa wa majengo yake.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema ili kukabiliana na upungufu wa wahadhiri kwenye vyuo vya elimu ya juu, katika mwaka 2017/18, Serikali imepanga kusomesha wahadhiri 100 katika ngazi za shahada za umahiri na uzamivu.

Waziri Mkuu amesema kati ya mwaka 2016/17 na 2017/18, Serikali imeratibu upatikanaji wa wanafunzi wa Kitanzania wanaofadhiliwa kusoma nchi za nje ambapo China wapo wanafunzi 86, Uingereza (17), Misri (4), Korea (3), Urusi (13) na Thailand (2) huku baadhi ya wanufaika wakiwa ni wahadhiri wa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu nchini.

Vilevile, kupitia kuimarika kwa mahusiano yetu ya kidiplomasia, Waziri Mkuu amesema, Septemba, mwaka huu, Serikali ilitia saini makubaliano na nchi ya Hungary ambapo itakuwa inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 kwa kipindi cha miaka mitatu kuanza mwaka 2018/2019.
Read More

SERIKALI YATOA MAFUNZO KWA VIJANA ZAIDI YA 11,000


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweza kutoa mafunzo kwa vijana 11,492 katika fani mbalimbali kupitia vyuo vya umma, binafsi na makampuniikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi.

Amesema programu hiyo ambayo ilianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2016/17, inalenga kuweka maeneo mahususi ya kuwezesha vijana wawe na ujuzi stahiki wa kuajirika au kujiajiri katika soko la ajira la ndani na la nje ya nchi.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 17, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa tisa wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Januari 30, mwakani.

Amesema katika kutekeleza programu hiyo, Serikali imejikita katika maeneo ya kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (apprenticeship); kutoa mafunzo ya ujuzi na uzoefu kazini (internship) kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo hususan wale wa vyuo vikuu; kutoa mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo; na kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini.

Waziri Mkuu amesema katika kujenga ujuzi wa vijana kushiriki kwenye shughuli za kilimo, Serikali imeandaa mafunzo maalum ambayo yataanza rasmi Desemba, 2017 katika Halmashauri zote zilizowasilisha maombi.

“Tumeshirikisha Wakuu wa Mikoa yote na kuwaelekeza waandae maeneo ya kujifunzia vijana hao kwenye Halmashauri zote za mikoa yao,” amesema.

Amesema ofisi yake imepokea maombi ya kushiriki kutekeleza programu ya kukuza ujuzi katika eneo la kilimo kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House) kutoka mikoa mitano ya Kagera, Manyara, Ruvuma, Kilimanjaro na Shinyanga. “Ofisi yangu imefika katika Halmashauri zote za mikoa hii ili kujiridhisha kuwa imetenga maeneo kwa ajili ya kujenga vitalu vyumba vya kufundishia,” ameongeza. 

Amesema katika mwaka huu wa fedha (2017/18), Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imetoa fursa za mafunzo mbalimbali ya vitendo kupitia Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kukubaliana kuwa ifikapo Desemba, 2017 vijana wote wawe wamepatiwa fursa za mafunzo katika maeneo ya kazi.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa viwanda na taasisi mbalimbali zishirikiane na Serikali kuwapa nafasi kwa vijana ili wajifunze kwa vitendo katika maeneo ya kazi  na kupata uzoefu  na ujuzi stahiki. 

“Tuna vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu walioomba kushiriki mafunzo ya vitendo na kupata uzoefu wa kazi. Natoa wito kwa waajiri watoe nafasi kwa vijana wetu hawa kujifunza kwa vitendo. Serikali itaendelea kugharamia mahitaji ya msingi ya vijana hawa wakati wa mafunzo hayo,” amesisitiza. 
Read More

MAJALIWA:MWENENDO WA UKUAJI UCHUMI WA TAIFA UNARIDHISHA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Taifa unaridhisha, ambapo katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 17, 2017) wakati akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Bunge, mjini Dodoma.

“Mwenendo wa uchumi wetu ni wa kuridhisha, mfano, ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2017 ulikua kwa asilimia 5.7, robo ya pili ilikuwa asilimia 7.8 na nusu ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa ni asilimia 6.8.”

Amesema hali hiyo inafuatia kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na usimamizi thabiti wa matumizi ya Serikali, ambapo nakisi ya bajeti ya Serikali imeshuka na kufikia asilimia 1.9 kwa mwaka 2016/2017

Pia amesema akiba ya fedha za kigeni inatosheleza kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitano, ikiwa ni zaidi ya lengo la miezi minne.

Akizungumzia kuhusu kasi ya upandaji bei, Waziri Mkuu amesema takwimu zinaonyesha kwamba katika nusu ya mwaka 2017, mfumuko wa bei uliendelea kubaki katika kiwango cha tarakimu moja. 

“Takwimu zinaonyesha kwamba mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Oktoba 2017 ulikuwa ni asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilima 5.3 mwezi Septemba, 2017.”

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa bei wa bidhaa za vyakula, ambavyo vimepungua kutoka wastani wa asilimia 9.3 mwezi Septemba, 2017 hadi asilimia 8.8 mwezi Oktoba, 2017.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii ianzishe Mamlaka ya Fukwe za Bahari na Maziwa ili kutangaza na kuendeleza fukwe ambazo hazina shughuli.

Amesema fukwe za bahari ni eneo mojawapo ambalo likiendelezwa vizuri, linaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi, hivyo ni lazima zipewe kipaumbele.

Pia ametoa wito kwa wizara hiyo iongeze kasi ya kuleta mabadiliko katika sekta nzima ya maliasili ili iweze kuchangia zaidi kwenye uchumi. 

Ametolea mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 60.1 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi bilioni 102 mwaka 2016/2017.

Waziri Mkuu amesema ongezeko hilo la mapato limekuja baada ya Serikali kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki.

Read More