Tuesday, March 19, 2019

WAZIRI MKUU AAGIZA MSAKO KWA WALIOMUIBIA MKANDARASI MISUNGWI

 
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza ihakikishe inafanya msako wa watu wote waliohusika na wizi wa fedha na vifaa katika eneo la ujenzi wa mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Misungwi mkoani Mwanza.

Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Machi 19, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira uliopo wilayani Misungwi, ambapo ametumia fursa hiyo kuiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza iimarishe ulinzi katika eneo la mradi huo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya uvamizi wa mara kwa mara kwenye eneo hilo la mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Nyahiti wilayani Misungwi, Mwanza.

“Hawa waliofanya tukio hilo la uvamizi katika eneo la mradi si tu wanamuhujumu mkandarasi na kampuni yake, bali wanahujumu jitihada za Serikali ili miradi ya maendeleo kwa wananchi isikamilike hatutakubali, wananchi tushirikiane katika kuwabaini wote waliohusika.”

Ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza Serikali kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 95 wakazi waishio mijini na waishio vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.

Awali,Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi wa maji katika mji wa Misungwi unatekelezwa kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Viktoria, ambao unatekelezwa katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi kwa gharama ya Euro milioni 104.5 sawa na wastani wa sh. bilioni 276.

Amesema katika kiasi hicho cha fedha, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) zinachangia Euro milioni 90 sawa na sh. bilioni 238 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu, ambapo Serikali ya Tanzania inachangia Euro milioni 14.5 sawa na sh. bilioni 38.

Profesa Mbarawa amesema mradi wa maji na usafi wa mazingira katika mji wa Misungwi unagharimu kiasi cha Euro milioni 4.85 ambazo ni sawa na wastani wa sh. bilioni 12.85 ambazo zinatumika katika ujenzi wa kituo cha uzalishaji na kutibu maji, ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 53.7.

Pia, fedha hizo zitatumika kwenye ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji yenye ukubwa wa lita 600,000 na lita 300,000, ujenzi wa kituo cha kutibu majitaka, ununuzi wa magari mawili moja la kunyonya majitaka na Toyota pick up na pikipiki mbili pamoja na ujenzi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji na nyumba mbili za watumishi katika kituo cha uzalishaji.

Waziri Profesa Mbarawa amesema mbali na ujenzi huo pia watajenga maabara ya kupima ubora wa maji na karakana ya matengenezo. Mradi huo pia utaunganisha kaya 2,158 katika mfumo wa maji pamoja na kuwafungia mita za maji na ujenzi wa vituo 13 vya kuchotea maji.

Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) ya China chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya Egis ya Ufaransa na unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA) ulianza Mei, 2017 na unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.


(mwisho)
Read More

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA WA MJI WA MISUNGWI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga kuhusu michoro ya Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi huo, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na wa pili kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mji  wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019. Kushoto  kwake ni Waziri wa Maji, Profesa, Makame Mbarawa na  kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa   (kulia) wakimsikiliza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji  na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji na Usafi  wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa   (kulia) wakimsikiliza, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji  na Usafi wa Mazingira  Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji na Usafi  wa Mazingira  wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteremka kutoka kwenye chujio la maji wakati alipokagua ujenzi wa  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua mashine za  za kusukuma maji kabla ya kuweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa  Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Maji  na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Misungwi katika kijiji cha Nyahiti Mkoani Mwanza, Machi 19, 2019.  Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Daallo.

Read More

MAJALIWA AKABIDHI MATREKTA KWA WENYEVITI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA MSINGI MWANZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha trekta aina ya Ursus  wakati alipokabidhi matrekta16 yenye thamni ya shillings bilioni 1.8  kwa wenyeviti wa baadhi ya  Vyama vya Ushirika via Msingi mkoani Mwanza    katika hafla fupi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina ya Ursus, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Ugata wilayani Magu, Bw. Enock Ng'ombe katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shilingi bilioni 1.8  kwa Vyama vya Ushirika vya  Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa  (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi  19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina Ursus, Mwenyekitiu wa Chama cha Msingi cha Mgundama, Bibi Getrude John katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shiliüngi bilioni 1.8 kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina ya Ursus, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Busisi wilayani Sengerema, Bibi  Amina Makone katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shiliüngi bilioni 1.8 kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.

Read More

MAJALIWA AFUNGUA UJENZI NA UKARABATI MKUBWA WA KITUO CHA AFYA CHA KOROMIJE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Grace Fabian aliyejifungua mtoto wa kiume katika Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi wakati alipofungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo hicho, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata  utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019.  Wapili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi Machi 19, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Misungwi, Gambadu Samwel.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua Mradi wa Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua Mradi wa Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019.

Read More

Monday, March 18, 2019

WAZIRI MHAGAMA AWAFUNDA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU.

NA.MWANDISHI WETU
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, Sera, Bunge na Uwekezaji wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kwa umakini katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na ufanisi wa hali ya juu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi hiyo kilichofanyika Machi 18, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa ufanisi kwani hakuna haki pasipo wajibu, hivyo kila mtumishi azingatie hayo ili kuwa na utendaji wenye manufaa kwa ofisi na Serikali kwa ujumla,”alisema Mhagama
Aidha Waziri Mhagama ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi ikiwemo watumishi wazembe na wenye tabia ya kuchelewa kazini.
“Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,inasisitiza utendaji uliotukuka na bidii kwa kuzingatia adhima ya HAPA KAZI TU, hivyo kila mmoja ajitathimini kwa kina kuona namna anavyoenenda na endapo akaona kuna kasoro arekebishe mapema kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa juu yake,”alisisitiza Waziri Mhagama.
Naye Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki alipongeza watumishi wa ofisi hiyo kwa mafanikio yanayoonekana katika Ofisi hiyo na kutoa wito kwa watumishi kuendeleza jitihada hizo ili kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.
“Kipekee niwapongeze watumishi wa Ofisi hii kwa kuendelea kutekeleza vizuri majukumu ya kila siku kwa weledi kwa kuzingatia ukubwa wa ofisi hii, na tuendelee kutekeleza vya ufanisi ili kuvutia wawekezaji nchini waweze kuona fursa na kuwekeza,”alieleza Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia kikao na kuongezea kuwa Ofisi ya waziri Mkuu inapaswa kuwa mfano katika kusimamia shughuli za mabaraza ikiwa ni sambamaba na kuwataka waajiri kuendelea kuyathamini mabaraza kwa vitendo kwa kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya yenye kuimarisha utendaji wa kazi za kila siku.
“Nawaomba watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira nasi tunatoa shime kwa  waajiri kuendelea kuzingatia umuhimu wa kuundwa kwa mabaraza haya na kuyatumia kwa usahihi kama ilivyokusudiwa” asisitiza Bibi.Tarishi
=MWISHO=

Read More

WAZIRI MHAGAMA AWAFUNDA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia watumishi wa Ofisi yake walioshiriki katika mkutano wa baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo uliofanyika Machi 18, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo Machi 18, 2019 Jijini Dodoma.
Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi hiyo, anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo Bw.Pascal Vyagusa nyaraka za utendaji kazi katika nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na wajumbe wa baraza hilo.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa. akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/2020 wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Amina Simbaulanga akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angella Kairuki wakikata utepe nyaraka za utendaji kazi kwa viongozi wa baraza la wafanyakazi wa ofisi hiyo wakati wa mkutano wa baraza lao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki (mwenye koti jeusi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi la ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao chao kilichofanyika Machi 18, 2019.

Read More

WAZIRI MKUU AWATAKA MAAFISA HABARI WAJITATHMINI

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikaliniwajitathmini kwa kina zaidi kuhusu namna walivyotekeleza wajibu wao na watafakari njia bora ya kuyatangaza na kuyatetea mafanikio ya mageuzi makubwa yanayoendelea nchini. 

Pia, amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikaliniwahakikishe wanatumia vizuri taaluma zao na nyezo wanazopatiwa kusema mambo yanayofanywa kwenye sekta zote na wasipofanya hivyo watatoa fursa kwa taarifa zinazosemwa na wapinga maendeleo kuonekana kuwa ni kweli. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Machi 18, 2019)katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, kinachofanyika katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza. Kikao hicho kinahudhuriwa na Maafisa Habari na Mawasiliano takbaribani 400.

Amesema maafisa hao wanatakiwa wakumbuke kuwa wanapaswa kuueleza umma wa Watanzania kwa kina masuala yanayofanywa na Serikali hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017 – 2020/2021) wenye kuweka msisitizo kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda. 

“Mkumbuke kuwa kazi ya utoaji taarifa kwa wananchi kwa sasa si utashi binafsi wa mtoa habari bali hainabudi kufanywa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Mathalan Sheria mpya ya Haki ya Kupata Taarifa Na. 12 ya mwaka 2016 yenye kuzitaka mamlaka za umma kuwapa wananchi taarifa zinazowahusu”. 

Waziri Mkuu amesema sheria hiyo, inakwenda sambamba na sheria nyingine ya kumlinda mwananchi asilishwe taarifa za uongo, uchochezi na uzushi yaani Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016.

Amesema lengo la katiba na sheria hizo mbili, pamoja na mambo mengine, ni kuwahakikishia wananchi haki ya kupata habari tena zilizothibitishwa kwa maana ya usahihi wake na kwa wakati. “Sababu hizo, ndizo zilizofanya niguswe sana na kauli mbiu yenu isemayo: “utoaji habari sahihi na kwa wakati ni chachu katika kuifikia Tanzania ya kipato cha kati”. 

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hususan Idara yake ya Habari - MAELEZO) na timu za habari za viongozi wakuu kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na watendaji wengine. 

Pia, Waziri Mkuu amesema ameguswa na baadhi ya mada ambazo zitajadiliwa katika kikao kazi hiko, ikiwemo ya namna ya kushughulikia habari za uongo, kutunga, kughushi na namna kada yao inavyoweza kusaidia kukidhibiti kichochoro hicho haramu katika habari. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wote wa taasisi za umma, kuanzia sasa washirikiane na maafisa wa habari kwenye maeneo yao kuhakikisha kuwa habari muhimu kwa wananchi hazizuiwi kwa urasimu kama hazijazuiwa kisheria. Habari zitolewe kwa haraka na kwa njia anuai za kisasa.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe afuatilie kuhusu uzinduzi wa tovuti za Halmashauri walioufanya jijini Dodoma tarehe 27 Machi 2017, kama zinafanya kazi ipasavyo. 

Amesema lengo la tovuti hizo ni kuiongezea Serikali uwezo wa kuwapatia wananchi habari na taarifa kwa haraka kwa kuzingatia kwamba wako katika kipindi muhimu cha mageuzi katika historia ya nchi, ambapo mambo mengi yanafanyika Serikalini ya kiuchumi na kijamii lakini hayafikishwi kwa wananchi. 

“Kuhusu hili, naiagiza Wizara ya Habari kufanya tathmini ya mara kwa mara na kuniletea taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu yenu na matakwa haya ya kisheria miongoni mwa wizara, taasisi za umma na sekretarieti za mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini”.

Waziri Mkuu amesema maafisa hao wanapaswa kufahamu kikao chao kimekuja wakati muafaka kwani Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, ipo katika mwaka wake wa nne wa kutekeleza mageuzi makubwa katika kila sekta zikiwemo za kiuchumi na kijamii nchini. 

Amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kazi kubwa tena ya kihistoria imefanywa na Serikali ya awamu ya tano na wao ni mashahidi wa hayo yanayofanywa. “Ni jukumu lenu sasa kuuhabarisha umma wa Watanzania kama ambavyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka katika Ibara ya 18(d).

Waziri Mkuu ametaja mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwenye kila sekta nchini ikiwemo elimu; afya; nishati; mifugo; viwanda; barabara; viwanja vya ndege; uchukuzi wa anga; uchukuzi wa reli; uchukuzi wa majini; madini; sanaa za filamu na muziki; utalii na michezo mbalimbali. Amesema maafisa hao wanapaswa kuyatangaza mageuzi hayo.


(mwisho)
Read More