Na. OWM, DAR ES SALAAM.
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo
ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta Binafsi kwa lengo la
kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya
Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao kupitia Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Baada ya kupokea rasimu ya taarifa
hiyo,wameridhishwa kwa jinsi serikali imekuwa ikiishirikisha sekta binafsi
katika masuala ya uwekezaji nchini.
Akiongea wakati wa kufungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Uwekezaji) Dorothy Mwaluko, Mkurugenzi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya
Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa amewahakikishia wadau wa Sekta Binafsi kuwa Serikali
itaendelea kushirikiana nao katika kukuza uwekezaji na biashara nchini.
“Serikali imekuwa ikitekeleza sera za mageuzi ya uchumi
kuanzia miaka ya 1980 kwa lengo la kuimarisha na kuiwezesha sekta binafsi kuwa
mhimili wa ukuaji wa uchumi. Ili kutimiza azma hii, Serikali imekuwa
ikitunga Sera na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya kukuza
uwekezaji na biashara nchini. Kwa mantiki hii tunakutana na nyie sekta binafsi ili muweze kutoa maoni yenu kuhusu rasimu
ya taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka
1996”
Amesisitiza Mkongwa.
Ameongeza kuwa ili kuiwezesha Sekta Binafsi kuwa yenye nguvu na
ushindani nchini amewataka wadau hao kuendelea kushirikiana na serikali katika
kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kwenye nyanja za Uratibu
wa Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji na Uwezeshaji
Uwekezaji. Moja ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Sera hiyo ni pamoja na Tanzania kufikia lengo la kuwa na
Uchumi wa kipato cha Kati, Ukuaji wa Uchumi usioteteleka na kudhibiti mfumuko
wa bei.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna akielezea
maoni ya wadau na amefafanua kuwa mkutano huo wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya
Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 ni muendelezo wa juhudi za serikali katika kuweka mazingira bora
na wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini.
“Sisi wadau wa sekta Binafsi
tungependa Sera ya Taifa ya Uwekezaji iwe kwenye mtazamo wa Kuhamasisha
uwekezaji, kwa maneno, utekelezaji wake pamoja na sheria zinazo husiana na
masuala ya uwekezaji zioneshe zinalenga kuhamasisha uwekezaji wa hapa nchini,
kikanda na kimataifa. Sawa tunatengeneza Sera ya Uwekezaji ya Tanzania lakini
lazima iwe imezingatia masuala yanayohusu uwekezaji ya kikanda na kimataifa”
Ameeleza Mbenna.
Aidha, ameeleza kuwa Sera ya Uwekezaji
haina budi kuangalia namna ya kutoa mwongozo wa kuwafanya wawekezaji wa ndani
na nje wanao wekeza nchini juu ya namna wanaweza kuhimili majanga endapo
yanatokea na kuweza kuathiri shughuli za uwekezaji. Mfano mzuri wa ugonjwa wa
homa ya COVID-19 ulivyo athiri shughuli zao za uwekezaji. Amesisitiza pia kuwa
ni vyema kuwa sera ikazingatia kuwa inawezesha kutumika kuchagiza maendeleo ya ukuaji
wa uchumi nchini.
Mbenna amefafanua kuwa
wangependa sheria za kisekta kwenye masuala ya uwekezaji na Biashara ioneshe namna
zinavyounga mkono sheria mama ya uwekezaji. Pia tusiruhusu jitihada zinazo
kinzana katika kuendeleza uwekezaji bali ziwe na uwiano mzuri, vile vile
amesema katika uwiano huo, Sera za Zanzibar na Tanzania bara hazina budi
kuzingatia hilo. Pia amebainisha kuwa Sera ni vyema itambue makundi yanayoibuka
kama vijana yanaweza kuchukua nafasi katika masula ya uwekezaji.
Sera ya Taifa
ya Uwekezaji imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya
kisekta. Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa
kwa ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na
kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo mzuri
na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za upatikanaji wa vibali
vya uwekezaji.
Mkutano huo
uliowashirikisha wadau wa sekta binafsi
ni wa pili baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 11 Septemba, 2020 jijini
Dodoma ambao ulihusisha wadau wa sekta ya umma kwa maana ya Wizara na Taasisi
za Serikali. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo
ya Uwekezaji kwa kushirikiana na Taasisi ya
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
(MWISHO).
Mkurugenzi
Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa akiwahakikishia
wadau wa sekta Binafsi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika kukuza
uwekezaji na biashara nchini wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa
Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020
Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta Binafsi wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna akisisitiza jinsi
serikali inavyowapa ushirikiano wa kutosha kwenye masuala ya uwekezaji na
biashara wakati wa mkutano wa
kuijadili rasimu ya taarifa ya
Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo
tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa sekta Binafsi wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Dkt. Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa ya Tathmini ya
sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, wakati wa Mkutano wa kuijadili
rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es
Salaam, mkutano huo
umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mshiriki wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini
ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, akichangia wakati
wa mkutano huo leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam. Mkutano
huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi
kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Biveline Mushumbusi, akichangia wakati wa mkutano wa kuijadili
rasimu ya taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020 Dar es
Salaam, mkutano huo
umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau wa Sekta Binafsi kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya
Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo
tarehe 21 Septemba 2020, Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF). Mkurugenzi
Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu, Packshard Mkongwa (wa pili
kutoka kushoto), Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga (wa pili
kutoka kulia), Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi (wa kwanza kulia) na Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakifuatilia mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini
ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo tarehe 21 Septemba 2020, Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF). Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya
uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje akisisitiza umuhimu wa wadau wa Sekta Binafsi kuijadili rasimu ya taarifa ya Tathmini ya
Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo
tarehe 21 Septemba 2020, Dar es Salaam, mkutano huo umeratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF).
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga akifafanua jinsi Baraza hilo
linavyshirikiana na Sekta Binafsi wakati wa mkutano wa kuijadili rasimu ya taarifa
ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996, leo
tarehe 21 Septemba 2020 Dar es Salaam, mkutano
huo umeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya maendeleo ya Sekta
Binafsi kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Read More