Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado amesema
elimu ya usimamizi wa Maafa itaendelea kutolewa kwa wananchi kwa maeneo yanaoathirika kwa matukio ya
tofauti tofauti ya maafa.
“Tunatoa elimu kwa wananchi
ili kujenga uelewa wanamna ya kukabiliana na maafa, kwa kueleza dhana ya maafa,
kueleza maana ya majanga ikiwa pamoja na kuangalia mzingo wa maafa kwa ujumla”
Hayo yamesemwa na Luteni
Kanali Selestine Masalamado Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya
Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na shirika la
kimataifa la uhamiaji (IOM) katika kikao cha mafunzo ya Udhibiti wa Maafa kwa
jamii yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhusisha wananchi wa kata
ya Mbuguni na Shambaray Bruka.
“Washiriki wameelewa mfumo mzima wa Kudhibiti
Maafa kwa kuanzia ngazi ya taifa hadi kufikia ngazi ya Kijiji, alisema Luteni
Kanali”
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameshukuru
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kufanya mafunzo hayo Halmashauri
ya wilaya ya Meru.
“Tunashukuru kwa
kutuongezea wataalamu wa maafa kupitia
mafunzo yaliyoyotolewa ili kutusaidia namna ya kukabiliana na Maafa.”
Mwl. Makwinya amefanunua kata
ya Shambaray Bruka na Mbuguni yamekuwa yakiathirika na mafuriko na ukame,
Ametoa wito kwa washiriki
kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza maarifa kwa kusaidia maeneo mengine yanayoyoathirika na maafa.
Naye Mshiriki Fanael Kaaya
Mshiriki kutoka kata ya Mbuguni amesema mafunzo ya kukabiliana na maafa
waliyopata imesaidia kuchukua tahadhari ya kujikinga na maafa kabla hajatokea
ikiwemo kutengeneza matuta ya kuzuia maji kwenye maeneo yanayoathirika na
mafuriko na pamoja kufukua mifereji iliyoziba pamoja na mito ili mafuriko ya
maji yanapokuja yaweze kupita.