Thursday, May 25, 2023

SERIKALI KUZINGATIA MAFUNGU MAALUM YA FEDHA KWA WAVIU KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2023/24



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 pamoja na vipaombele vingine inazingatia pia mafungu ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika kila Wizara na Taasisi.

Ameyasema hayo mapema  katika Ukumbi wa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA).

Mhe. Mhagama, aliendelea kusema kuwa hii ni namna ambavyo Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kwa dhati kusaidia utekelezaji wa Afua za masuala ya UKIMWI nchini, kwa kuzingatia maeneo muhimu ikiwemo masuala ya lishe bora, dawa za kupunguza makali ya virusi na kuhakikisha mambo mengine yanayochangia ustawi wao kupatikana.

Akizungumzia suala la Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 Mhe. Mhagama alisema kuwa kuna kila Sababu ya Sera hiyo kufanyiwa mapitio na maboresho kwani ni ya muda mrefu na kuona, namna gani sekta zote zinaweza kushiriki katika suala hili ili kuweza kuyafikia malengo ya dunia ya kupunguza vifo, maambukizi na unyanyapaa ifikikapo 2030.” Niwahakikishie kwamba sisi kama Serikali tunaweza kusimamia kufikia malengo haya ya dunia”Alisisitiza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA Mwalimu Leticia Mourice alimpongeza Mhe. Waziri Jenista kwa uteuzi wake na pia kumshukuru kwa juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, aidha aligusia kuhusiana na maandalizi ya Mdahalo wa Kitaifa kuhusu uhimilivu wa mwitikio wa jamii katika mwitikio wa Taifa wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Sambamba na hilo alizungumzia kuhusu, uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Taifa, ambao unalenga utekelezaji wa NMSF5 (Mpango Mkakati wa Tano wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI) na alisisitizia umuhimu wa ushirikiano, katika kujenga mwitikio wa kijamii katika mapambano dhidi ya UKIMWI, akitolea mfano maeneo kadhaa muhimu ikiwemo Uhimilivu wa Kisera.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA Bw. Deogratius Rutatwa, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuipongeza Serikali ya watu wa Marekeni (PEPFAR/USAID) kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha shughuli za mwitikio wa UKIMWI za NACOPHA na wadau wote wanaotekeleza suala la UKIMWI na kusema kuwa kuna haja ya kuwepo kwa mkakati endelevu na uhimilivu.

Read More

Wednesday, May 17, 2023

WAZIRI MHAGAMA KATIKA KIKAO CHA BUNGE CHA 27


Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt Selemani Jafo wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.

Read More

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA KATIKA KIKAO CHA BUNGE CHA 27


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja Wakati wa Bunge la 12 Mkutano 11 wa Bunge la Bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.

Read More

Saturday, May 13, 2023

WILAYA YA IGUNGA KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI. AFDP



Halmashauri ya Wilaya ya IGUNGA iliyopo Mkoani Tabora imetajwa kuwa miongoni mwa Wilaya nchini itakayonufaika na programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) inayofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa kuendeleza Kilimo IFAD.

Hayo yameelezwa mapema leo na Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw. Salim Mwinjaka alipokuwa na mazungumzo na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya IGUNGA, wataalam pamoja na ujumbe kutoka AFDP ulipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yatakayoteleza programu hiyo.

Bw. Mwinjaka alisema kuwa Wilaya ya IGUNGA ni miongoni mwa Wilaya itakayopata fedha za utekelezaji wa  programu hiyo kupitia wizara ya Kilimo Kwa mwaka wa fedha 2324, "na Kwa mwaka wa fedha unaofuata Kwa kuzingatia maandali ya Mpango wa mapato na matumizi ya bajeti kuwekwa vizuri, fedha hizo zitakuja Moja Kwa Moja katika Wilaya husika."Alifafanua

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa ushirika wa umoja wa wafugaji wa samaki Igunga (UWASAI) uliopo katika kata ya Mwamapuli Bw. Francis Mgaragu, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Kwa kuwaletea mradi huo "mradi tumeupokea Kwa mikono miwili tunahaidi ushirikiano, na tunahaidi kuwa tutatekeleza mradi Kwa malengo yaliyokusudiwa." Alisema

Read More

Friday, May 12, 2023

MRADI WA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UFUGAJI VIUMBEMAJI CHATO.

 


Imeelezwa kuwa Mradi wa kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unakwenda kutatua changamoto wanazokumbana nazo wafugaji VIUMBEMAJI katika kituo Cha Rubambagwe kilichopo Wilayani Chato,mkoani Geita.

Hayo yameelezwa Leo na Dkt. Nazaeli Madala, Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. amesema kituo Cha Rubambagwe kipo katika UJENZI ambapo, Nia na madhuni ya kituo hiki ni kuhamasisha, kuendeleza na kusimamia ukuzaji viumbe Maji,Kwa maana Ufugaji wa samaki kwa mabwawa na vizimba katika ukanda wa ziwa Victoria.

Alisema kuwa, kituo kitakwenda kutoa mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha samaki,Ufugaji na ulishaji sahihi wa samaki, wafugaji watafundishwa pia namna ya kutengeneza chakula Cha samaki Kwa kutumia malighafi za asili, kutakuwa na majengo ambayo yatawezesha wafugaji wanaotoka mbali kukaa hapo wakati wa mafunzo, sambamba na hilo, kutakuwa na kiwanda kidogo Cha kutengeneza chakula cha samaki.

Aliongeza kusema kuwa kituo pia kitazalisha vifaranga vya samaki ili kuweza kutatua changamoto ambazo wafugaji wanakutana nazo "kutakuwa na kitotoleshi ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha vifaranga ambavyo vitakwenda kuwezesha vitotoleshi vya sekta binafsi kupata wazazi "Alifafanua

Akiongea na ujumbe huo, Bi. Sifa Buguni  mmoja wa wafugaji wa samaki Rubambagwe Chato alibainisha changamoto kubwa mbili  walizokumbana nazo kabla ya mradi huu kukamilika kuwa ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa mbegu na chakula cha kulisha samaki.

Awali, ujumbe huu wa IFAD ulifika ofisini Kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara ambapo alisema ni wakati sasa kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kujikita katika katika shughuli za kilimo na ufugaji wa viumbemaji na kwa uwekezaji wa uhakika kuweza kuwekeza katika sekta hizo kama wanavyowekeza katika sekta ya madini.

Ujumbe kutoka IFAD, wataalam na Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salim Mwinjaka wapo katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayotekelezwa mradi huo

 

Read More

Thursday, May 11, 2023

PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI ITACHANGIA KULETA UHAKIKA NA USALAMA WA CHAKULA NCHINI - DKT. BATILDA

 


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema, Programu ya AFDP itasaidia upatikanaji wa mbegu za mazao zinazoweza kuhimili na kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Aidha mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi nchini AFDP italeta uhakika wa usalama wa Chakula upatikanaji wa ajira katika maeneo inapotekelezwa programu hiyo, pamoja na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.

Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda ameyasema hayo mapema alipokutana na ujumbe kutoka IFAD walipokuwa katika ziara ya Usimamizi wa utekelezaji wa programu hiyo ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP).

Akielezea kuhusu sekta za kilimo na ufugaji Mheshimiwa Balozi Dkt Batilda ameelezakuwa mkoa wa Tabora ni maarufu kwa kilimo Cha zao la Tumbaku na Ufugaji wa nyuki.

Kwa Upande wake mtaalamu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa programu hiyo Bw. Bernard Ulaya  akielezea utekelezaji wa Programu hiyo mkoani Tabora, programu hiyo ameeleza kuwa programu hiyo inaendeleza kituo cha kuzalisha vifaranga vya samaki kilichopo Mwamapuli wilayani Igunga, shamba la kuzalisha mbegu za mazao ya kilimo la Wakala wa Mbegu (ASA) )lililoko Kilimi katika wilaya ya Nzega, na Wilaya ya  Uyui itapewa nafasi ya kuendeleza mnyororo ya Alizeti, Mahindi na maharage.

Read More

Thursday, May 4, 2023

VIONGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA KWA WELEDI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KILIMO NA UVUVI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewataka watendaji wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia vizuri utekelezaji wa Programu ya Kilimo na Uvuvi katika maeneo yao kwani ni sekta muhimu katika uchangiaji wa uchumi na usalama wa chakula nchini.

Ameyasema hayo mapema leo Jijini Dodoma, katika warsha ya  utambulisho na uelewa  wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri.

Dkt. Yonazi amesema kuwa Serikali imeona kuna ulazima wa kuwepo kwa usalama wa mbegu katika kilimo hivyo kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini ASA imeweza kuwekeza mbegu kwa wingi ili kuyafikia maono ya serikali.

“Serikali imeendelea kusimamia uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora ambapo hadi kufikia Aprili 2023, jumla ya tani 49,962.35 za mbegu bora zimepatikana sawa na asilimia 26.68 ya mahitaji ya tani 187,197 kwa mwaka,”alisema Dkt. Yonazi.

 

Aliongezea kuwa, serikali imejitahidi kuweka nguvu katika upatikanaji wa mbegu hizo ili  kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula nchini, na kwa upande wa sekta ya uvuvi imehakikisha kunakuwa na manufaa ya rasilimali zilizopo katika sekta hiyo kwani bado hazijatumika vizuri.

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ina mpango wa kununua meli zitakazotumika katika uvuvi wa kina kirefu cha bahari na hivyo kuweza kuongeza lishe na hatimaye nchi kunufaiika na rasilimali za uvuvi.

Aliendelea kufafanua kuwa, Programu hii pia, itahusisha ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu mingine ikiwa ni pamoja na upanuzi wa vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki cha Kingolwira Morogoro.

“Lazima tushirikishe wadau ili tupeleke elimu ya kuweza kuzalisha vifaranga na kujenga mabwawa, natoa msisitizo kwa viongozi wa mkoa kuwa kuna jukumu la usimamizi, tuhakikishe tunasimamia vizuri mradi huu, kushauri na kuutekeleza kwa wakati.” Alisisitiza Dkt. Yonazi

Awali, akiongea wakati wa Ufunguzi wa Warsha hiyo Bw. Paul Sangawe Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, alisema lengo la programu hii kwa upande wa sekta ya uvuvi, ni kuendeleza ufugaji wa viumbe maji pamoja na kuanza uvuvi wa bahari kuu.

“Tunatazamia katika program hii meli zitanunuliwa kwa matumizi ya pande zote mbili za Muungano na kuwezesha nchi yetu kwa mara ya kwanza kufanya uvuvi katika bahari kuu ili kuweza kutumia rasilimali tulizonazo kwa ufanisi, lakini vile vile uzalishaji wa mbegu pamoja na usambazaji, na kuhakikisha fedha ambazo za mkopo ambazo tumepewa kutoka shirika la IFAD takribani dola 58.8 milioni,zinatumika kwa ufanisi na kuleta tija katika utelezaji wa program hii.” Alisisitiza

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchumi na Uzalishaji toka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Afisa Kilimo Mkuu Dkt. Rehema Mdendemi amesema programu hii ya maendeleo ya kilimo na uvuvi itaenda kuboresha maisha ya wakulima na wavuvi , na kujitosheleza kwa usalama wa chakula na kuleta ajira hivyo program hii ni ya muhimu kwa serikali na wanachi kwa ujumla.

Read More

Wednesday, May 3, 2023

NEC YAANZA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2025


 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa kuzingatia utaratibu na vigezo.

Hayo  yamesemwa leo  Bungeni Jijini Dodoma na Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga wakati akijibu  maswali  ya baadhi ya  wabunge walioomba majimbo yao  yagawanywe.

Amesema muda utakapofika, Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba.

Mhe. Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa jimbo, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Read More