Thursday, May 11, 2023

PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI ITACHANGIA KULETA UHAKIKA NA USALAMA WA CHAKULA NCHINI - DKT. BATILDA

 


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema, Programu ya AFDP itasaidia upatikanaji wa mbegu za mazao zinazoweza kuhimili na kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Aidha mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi nchini AFDP italeta uhakika wa usalama wa Chakula upatikanaji wa ajira katika maeneo inapotekelezwa programu hiyo, pamoja na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.

Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda ameyasema hayo mapema alipokutana na ujumbe kutoka IFAD walipokuwa katika ziara ya Usimamizi wa utekelezaji wa programu hiyo ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP).

Akielezea kuhusu sekta za kilimo na ufugaji Mheshimiwa Balozi Dkt Batilda ameelezakuwa mkoa wa Tabora ni maarufu kwa kilimo Cha zao la Tumbaku na Ufugaji wa nyuki.

Kwa Upande wake mtaalamu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa programu hiyo Bw. Bernard Ulaya  akielezea utekelezaji wa Programu hiyo mkoani Tabora, programu hiyo ameeleza kuwa programu hiyo inaendeleza kituo cha kuzalisha vifaranga vya samaki kilichopo Mwamapuli wilayani Igunga, shamba la kuzalisha mbegu za mazao ya kilimo la Wakala wa Mbegu (ASA) )lililoko Kilimi katika wilaya ya Nzega, na Wilaya ya  Uyui itapewa nafasi ya kuendeleza mnyororo ya Alizeti, Mahindi na maharage.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.