Saturday, May 13, 2023

WILAYA YA IGUNGA KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI. AFDPHalmashauri ya Wilaya ya IGUNGA iliyopo Mkoani Tabora imetajwa kuwa miongoni mwa Wilaya nchini itakayonufaika na programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) inayofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa kuendeleza Kilimo IFAD.

Hayo yameelezwa mapema leo na Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw. Salim Mwinjaka alipokuwa na mazungumzo na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya IGUNGA, wataalam pamoja na ujumbe kutoka AFDP ulipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yatakayoteleza programu hiyo.

Bw. Mwinjaka alisema kuwa Wilaya ya IGUNGA ni miongoni mwa Wilaya itakayopata fedha za utekelezaji wa  programu hiyo kupitia wizara ya Kilimo Kwa mwaka wa fedha 2324, "na Kwa mwaka wa fedha unaofuata Kwa kuzingatia maandali ya Mpango wa mapato na matumizi ya bajeti kuwekwa vizuri, fedha hizo zitakuja Moja Kwa Moja katika Wilaya husika."Alifafanua

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa ushirika wa umoja wa wafugaji wa samaki Igunga (UWASAI) uliopo katika kata ya Mwamapuli Bw. Francis Mgaragu, ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Kwa kuwaletea mradi huo "mradi tumeupokea Kwa mikono miwili tunahaidi ushirikiano, na tunahaidi kuwa tutatekeleza mradi Kwa malengo yaliyokusudiwa." Alisema


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.