Friday, May 12, 2023

MRADI WA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI KUTATUA CHANGAMOTO ZA UFUGAJI VIUMBEMAJI CHATO.

 


Imeelezwa kuwa Mradi wa kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unakwenda kutatua changamoto wanazokumbana nazo wafugaji VIUMBEMAJI katika kituo Cha Rubambagwe kilichopo Wilayani Chato,mkoani Geita.

Hayo yameelezwa Leo na Dkt. Nazaeli Madala, Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. amesema kituo Cha Rubambagwe kipo katika UJENZI ambapo, Nia na madhuni ya kituo hiki ni kuhamasisha, kuendeleza na kusimamia ukuzaji viumbe Maji,Kwa maana Ufugaji wa samaki kwa mabwawa na vizimba katika ukanda wa ziwa Victoria.

Alisema kuwa, kituo kitakwenda kutoa mafunzo ya utengenezaji wa chakula cha samaki,Ufugaji na ulishaji sahihi wa samaki, wafugaji watafundishwa pia namna ya kutengeneza chakula Cha samaki Kwa kutumia malighafi za asili, kutakuwa na majengo ambayo yatawezesha wafugaji wanaotoka mbali kukaa hapo wakati wa mafunzo, sambamba na hilo, kutakuwa na kiwanda kidogo Cha kutengeneza chakula cha samaki.

Aliongeza kusema kuwa kituo pia kitazalisha vifaranga vya samaki ili kuweza kutatua changamoto ambazo wafugaji wanakutana nazo "kutakuwa na kitotoleshi ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha vifaranga ambavyo vitakwenda kuwezesha vitotoleshi vya sekta binafsi kupata wazazi "Alifafanua

Akiongea na ujumbe huo, Bi. Sifa Buguni  mmoja wa wafugaji wa samaki Rubambagwe Chato alibainisha changamoto kubwa mbili  walizokumbana nazo kabla ya mradi huu kukamilika kuwa ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa mbegu na chakula cha kulisha samaki.

Awali, ujumbe huu wa IFAD ulifika ofisini Kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Prof. Godius Kahyarara ambapo alisema ni wakati sasa kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kujikita katika katika shughuli za kilimo na ufugaji wa viumbemaji na kwa uwekezaji wa uhakika kuweza kuwekeza katika sekta hizo kama wanavyowekeza katika sekta ya madini.

Ujumbe kutoka IFAD, wataalam na Mratibu wa Programu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salim Mwinjaka wapo katika ziara ya ukaguzi wa maeneo yanayotekelezwa mradi huo

 


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.