Wednesday, November 7, 2018

BUNGENI LEO TAREHE 07.11.2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mbunge wa viti maalum Salma Kikwete, Bungeni jijini Dodoma. Novemba 7, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma Novemba 7, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Malindi Ally Saleh, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Novemba 7, 2018.


Read More

Tuesday, November 6, 2018

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA WABUNGE WALIO KULA KIAPO BUNGENI LEO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara baada ya kula kuapo Bungeni jijini Dodoma .leo .Novemba 6/2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Korogwe Mjini baada ya kula kuapo Bungeni jijini Dodoma leo. Novemba 6/2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Liwale, Mohamed Kuchauka baada ya kula kiapo Bungeni jijini Dodoma leo .Novemba 6/2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Viajana na Ajira Anthony Mavunde. wakati wa picha ya pamoja katika Viwanja vya Bunge na  Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa  Dodoma . leo Novemba 6/2018. 



Read More

WATANZANIA KUFAIDI MATUNDA YA RELI YA KISASA MWAKANI

*Waziri Mkuu alidhishwa na kasi ya ujenzi
*Asilimia 96 ya walioajiriwa ni Watanzania


MIUNDOMBINU ni muhimu katika maendeleo ya Taifa lolote ambalo linalohitaji kusonga mbele kiuchumi, kijamii kwa sababu husaidia Serikali katika kufanikisha malengo iliyojiwekea.

Miundombinu hiyo ambayo inalenga kuboresha na kuimarisha uchumi inajumuisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya uchukuzi na usafirishaji kama reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, ununuzi wa ndege na meli.

Kukosekana kwa miundombinu ya uhakika kunachangia kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kuongezeka gharama za uchukuzi.

Katika kutambua umuhimu wa miundombinu kwenye kukuza uchumi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujikita katika kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ili kuhakikisha Taifa linasonga mbele kiuchumi.

Mradi huo wa ujenzi wa mfumo wa reli mpya ya kisasa (SGR) unaojengwa na Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), unatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Mwanza ina urefu wa km. 1,219.

Jumamosi, Novemba 3 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa reli hiyo kuanzia eneo la Shaurimoyo (Dar es Salaam) hadi Soga (Pwani) ambapo alisema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi huo.

Alisema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 kinatarajiwa kukamilika Novemba 2019 na kipande wa cha kutoka Shaurimoyo hadi  eneo la Pugu chenye urefu wa km. 20 ambacho kilipangwa kukamilika Julai 2019, lakini kwa kasi ya mkandarasi kitakamilika Machi 2019.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii na kiwango hikihiki. Kazi mnayoifanya inavutia,” alieleza.

Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. Magufuli ya kutaka kuona SGR  inakamilika kwa wakati na kuanza kutumika nchini yanatimia kwani wananchi nao watakuwa wamerahisishiwa usafiri.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo kutaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani hususani ambazo hazijapakana bahari pamoja na kupunguza muda wa safari katika maeneo ambayo mradi huo unapita.
Pia  itasaidia katika kutunza barabara na kupunguza gharama za ukarabati wa mara kwa mara kwa sababu mizigo mingi itakuwa inasafirishwa kwa njia ya reli na maroli yatapungua barabarani, hivyo kuzifanya ziwe imara na kudumu.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa SGR inakwenda kukuza sekta zingine za kiuchumi nchini kwa sababu nazo zinategemea uimara wa miundombinu ya usafiri wa uhakika.
Katika  sekta ya viwanda reli hiyo itasaidia kusafirisha bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda mbalimbali na kuwafikia watumia kwa wakati na kwa gharama nafuu.
Akizungumzia kuhusu suala la ajira katika ujenzi wa mradi wa SGR, Waziri Mkuu alisema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.
“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu, hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uadilifu na muwe mabalozi wazuri ili wananchi wengine waweze kupata ajira kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa nchini ikiwemo ya ujenzi.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli  kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.

Alisema awamu hiyo ya mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na njia kuu 205 ambazo km 95 zitakuwa zinapisha kitagharimu sh. trilioni 2.7.

“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422  na njia kuu 336 ambazo km 86 zitakuwa zinapishana kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5 chenye njia kuu 294 na km 73.5 zitakuwa zinapishana.

Kipande kingine ni cha kutoka Tabora hadi Isaka km 162.5 chenye njia kuu 130 na km 32.5 zitakuwa za kupishana na Isaka hadi Mwanza km. 311.25 njia kuu 249 huku km 62.5 zitakuwa za kupishana.”

Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa itachochea mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Mkurugenzi huyo alisema reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na uhakika.

“Kuchangia katika pato la Taifa na sera ya viwanda kwani mradi huo umeongeza mahitaji ya saruji, kokoto, nondo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi, hivyo kuvifanya viwanda vyetu vya ndani kupata soko la bidhaa zake.”

Akizungumzia mradi huo kwa ujumla, Mkurugenzi huyo alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha Morogoro-Makutupora.

Alisema jumla ya km. 722 za ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa kwa sasa zinatekelezwa katika vipande viwili, kipande cha Dar Es Salaam-Morogoro km. 300 kinajengwa kwa ubia wa kampuni ya YAPI MERKEZI ya Uturuki na MOTA-ENGIL ya Ureno na kipande wa Morogoro-Makutupora km. 422 kinajengwa na kampuni ya YAPI MERKEZI.

Kadogosa alisema katika mradi huo wa reli za kisasa mfumo wa uendeshaji wa treni utatumia nishati ya umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na tayari taratibu za kumpata mkandarasi za kujenga njia za umeme upo katika hatia za mwisho.

Kuhusu ujenzi wa madaraja Kadogosa alisema kazi ya ujenzi wa madaraja na makaravati unaendelea ambapo daraja refu katikati ya jiji la Dar es Salaam ina jumla ya urefu wa km. 2.56 na ujenzi wake umefikia asilimia 46.

 “Kuna madaraja ya kati 26 na makaravati 243, madaraja ya treni kupita juu yapo 17, madaraja ya treni kupita chini yapo 15 na madaraja reli juu ya reli yapo matano, pia jumla ya stesheni sita zitajengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, kati ya hizo kubwa zitakuwa mbili na nne zitakuwa ndogo.”

Alisema usanifu wa stesheni hizo umezingatia mazingira na asili ya Tanzania ambapo stesheni ya Dar es Salaam ina sura ya madini adimu ya Tanzanite wakati stesheni za kati usanifu wake umezingatia utamaduni na nyumba za asili na stesheni ya Morogoro itaonesha uhalisia wa milima ya Uruguru.

Kadhalika, Mkurugenzi huyo alizungumzia kuhusu ajira katika mradi huo ambapo alisema una jumla ya wafanyakazi 5,440, vibarua 4,743 ambapo jumla ya asilimia 96 ni Watanzania na asilimia nne ni wageni, wataalamu 189 wa Kitanzania na 258 wa kigeni kwa uwiano wa asilimia 42 Watanzania na wageni asilimia 58.

Pia jumla ya ajira 626 za Watanzania wasio na utaalamu na 19 za wenye utaalamu zimepatikana kupitia kampuni za wazawa (sub-contractors) wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huo.

Akizungumzia kuhusu ardhi na mali nyingine, Kadogosa alisema mali za wananchi wapatao 6,514 zenye thamani ya kiasi cha sh. bilioni 83.099 zitakiwa kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa reli kwa kipande wa Dar es Salaam-Morogoro.

(mwisho)
Read More

Sunday, November 4, 2018

SHERIA KUTUMIKA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi Jijini Dares salaam.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi Jijini Dares salaam.

Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika majadiliano  wakati wa  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika kutoa maoni ya kuandaa sheria ya ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Dares salaam.


Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika  picha ya pamoja mara baada ya  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Dares salaam.

Na. Mwandishi Maalum
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori, mifugo, mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo, wameanza mchakato wa kuandaa sheria ya kudhibiti athari za vimelea hatarishi kwa jamii, sheria hiyo itasimamia ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati  wa mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Usalama wa Afya na Ulinzi dhidi ya vimelea hatarishi vya magonjwa Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha kuwa serikali kupitia Dawati  la uratibu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inategemea sana utaalamu wa kamati hiyo kutoa maoni yatakayojumuishwa katika sheria zitakazo simamia udhibiti wa vimelea hatarishi.  
 “Serikali itaendelea kuilinda jamii ya watanzania dhidi ya majanga yanayoweza kusababishwa na vimelea hatarishi ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii, kwa kulitambua hilo Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuwakutanisha wataalamu husika ili watoe maoni yao juu ya udhibiti wenye nguvu ya kisheria” Amesema kanali Matamwe.
Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa udhibiti wa vimelea hatarishi ni muhimu kuwa na nguvu ya sheraia kwani kumekuwepo  na muingilianao mkubwa baina ya nchi mbalimbali,  ambapo muingiliano huo  hungeza milipuko ya magonjwa  kwa afya ya binadamu,     wanyama na mimea.
Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu, wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana Wizara ya Afya wameratibu mkutano huo kwa kupata wataalamu kutoka  Shirika la DTRA na Ufadhili wa CDC.

MWISHO.
Read More

Saturday, November 3, 2018

WIZARA, MIKOA ONDOENI VIKWAZO UJENZI WA VIWANDA-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na masuala ya viwanda, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na sekta binafsi watambue na waondoe vikwazo na urasimu dhidi ya ujenzi na ustawi wa viwanda nchini.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ampelekee taarifa ya hatua iliyofikiwa juu ya kampuni ya Budget Motors walioomba kibali cha kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi tangu mwaka jana na hawajajibiwa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) wakati akifunga wiki ya maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba katika kata ya Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani. Amesena uwepo wa viwanda nchini unatoa ajira nyingi.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujenga uchumi wa viwanda utakaokuwa mhimili mkuu wa maendeleo ya Taifa na wananchi, hivyo itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha ajenda ya ujenzi wa viwanda inafanikiwa.”

Amesema katika kupunguza vikwazo na kuboresha sera nchini, Rais Dkt. Magufuli ameweka msukumo wa kutosha ili kurahisisha na kuondoa ukiritimba kwenye shughuli zote za kibiashara, lakini pia katika kuboresha sera za Taifa za kodi ili kulinda viwanda vya ndani

Waziri Mkuu amesema umuhimu wa viwanda umetokana na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ambayo inaielekeza Serikali kuweka nguvu katika ujenzi wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Amesema kwa msingi huo, Rais Dkt. Magufuli alitoa msukumo wa sekta binafsi nchini kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini kutokana na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili, vikiwemo viwanda vya nguo, sabuni, korosho na matunda.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa uwepo wa viwanda nchini utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. “Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano unaolenga kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.”

Kuhusu suala la kampuni ya Budget Motors, Wiziri Mkuu amesema ifikapo Ijimaa (Novemba 9, 2018) Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji awasilishe taarifa kuhusu suala hilo la kibali. “Huu ni urasimu, ni bora apewe atengeneze na akikosea arekebishwe.”

Kampuni ya Budget Motors inadai kuwa iliomba kibali cha kuwa na uthibitisho wa kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa takribani mwaka mmoja bila ya kujibiwa. Walitoa malalamiko hayo kwa Waziri Mkuu alipotembelea banda lao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zenye miradi mbalimbali nchini pamoja na wananchi kuthamini na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini zikiwemo na za viwanda vya mkoa wa Pwani kwani zina viwango vya ubora.

“Wakati natembelea mabanda kwenye maonesho haya nimeshuhudia bidhaa nyingi nzuri na zenye ubora. Nimeona wazalishaji wa saruji, mabati, nondo, marumaru, mabomba ya plastiki, chuma, zana za kilimo, vyakula, vinywaji na vifungashio.”

Waziri Mkuu amesema kupitia maonesho hayo ya viwanda vilivyopo katika mkoa wa Pwani vimeudhihirishia umma kuwa vina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na hata kuzidi zile zinazoingizwa kutoka nje, amewahamasisha wananchi kutumia bidhaa za ndani.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo ameiagiza mikoa yote nchini kuhakikisha inatumia bidhaa zinatengenezwa na viwanda vya ndani katika miradi mbalimbali ya ujenzi wanayoitekeleza kama ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya.

Amesema Wakuu wa Mikoa ni lazima wahakikishe bidhaa kama saruji, nondo, marumaru, mabati zinavyotumika katika ujenzi ziwe vimezalishwa na viwanda vya ndani kwa sababu vina viwango vya ubora unaotakiwa na pia itasaidia kuondoa tatizo la soko la bidhaa hizo.

Naye,Waziri Mwijage amewataka watendaji wanaohusika na masuala ya viwanda kutoweka vikwazo kwa wawekezaji ambao wanakwenda katika ofisi zao kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kuwekeza kwenye viwanda au wanaohitaji vibali kwani jambo hilo halina tija.


(mwisho)
Read More

NIMERIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA SGR-MAJALIWA


*Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019 badala ya Julai

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.

Amesema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi Soga,  Pwani.

“Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona SGR  inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.

Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.

“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”

Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli  kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.

Alisema mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni 2.7.

“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422 ambacho kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5, Tabora hadi Isaka km 162.5 na Isaka hadi Mwanza km. 311.25.”


Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa kutachochea mipango ya Serikali katika kutekeleza sera ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na uhakika.

Akizungumzia mradi huo kwa ujumla, Kadogosa alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha Morogoro-Makutupora.


(mwisho)
Read More

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA RELI YA KISASA YA SGR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania  (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya SGR wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Markezi inayojenga Reli hiyo,  katika eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam, Novemba 3, 3018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua maandalizi ya  ujenzi wa madaraja  ya  kupitisha treni  juu  wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya Kisasa ya SGR   Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo ipo eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya SGR wakati alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa  reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018.  Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa ya SGR kati ya Dar es slaam na Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa reli hiyo katika eneo la Soga mkoani Pwani,  Oktoba 3, 2018.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa.

Read More

Thursday, November 1, 2018

WAZIRI MKUU: TUTAHAKIKISHA WANANCHI WOTE WANAPATA MAJI


*Aagiza vijiji vyenye shida ya maji Bumbuli vibainishwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha wananchi katika vijiji vyote nchini wanapata huduma ya safi na salama wakiwemo na wa jimbo la Bumbuli.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Halmashauri  ya Bumbuli, wilayani Lushoto, Charles  Boy afanye utafiti na kubainisha vijiji vyenye shida ya maji Bumbuli.
Amesema baada ya kuvibaini vijiji hivyo, anatakiwa aweke mpango wa kuhakikisha navyo vinapata huduma ya maji safi ili kuwaondolea wananchi tatizo hilo la ukosefu wa  maji.
Alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 1, 2018) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mponde jimbo la Bumbuli, Lushoto.

Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wakazi wa wilaya ya Lushoto kwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto hiyo nchini.

“Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali, hivyo aliwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao.
Awali,Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi, ukarabati wa miradi ya maji, ambapo mkoa wa Tanga umetengewa sh. bilioni 13.
Aweso alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa wakandarasi wanajenga miradi ya maji wazingatie viwango vya ubora kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi katika kugharamia miradi hiyo.
“Serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maji alafu mnazitumia kujengea majumba na kununua magari, safari hii mtazitapika tunataka miradi itekelezwe kwa kuzingatia viwango.”
Waziri huyo aliahidi kufuatilia kwa kina ujenzi wa miradi yote ya maji nchini ili kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa katika miradi hiyo.

(mwisho)
Read More

NIMEFARIJIKA NA MAENDELEO YA VIWANDA-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa viwanda kwenye mkoa wa Tanga kwa sababu vitasaidia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.

Aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Novemba 1, 2018) alipotembelea kiwanda cha saruji cha Rhino na kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh, vyote vya jijini Tanga.

Waziri Mkuu ambaye jana alihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga, aliwapongeza wawekezaji wa viwanda hivyo kwa kuunga mkono mkakati wa Serikali. 

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda.

Akizungumzia kuhusu kiwanda cha Rhino, Waziri Mkuu alisema kiwanda hicho na vingine vya saruji nchini vitasadia kupunguza gharama ya saruji nchini na kurahisisha ujenzi.

“Serikali inaamini kwamba uwepo wa viwanda mbalimbali nchini si tu utawezesha ukuaji wa uchumi wa Taifa, pia utasaidia katika kumaliza changamoto ya ajira hususani kwa vijana.”

Akiwa katika kiwanda cha Tanga Fresh, Waziri Mkuu aliwataka wafugaji mkoani Tanga wabadili mfumo wa ufugaji na wafuge kwa kutumia njia za kisasa ili waongeze uzalishaji.

“Wafugaji lazima wakubali kubadilika watumie fursa ya uwepo wa kiwanda hiki kwa kufuga kisasa ili wapate maziwa mengi kwa sababu wana uhakika wa kuyauza kiwandani hapa”.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka wananchi walioajiriwa kiwandani hapo wafanye kazi kwa bidii, uaminifu na wawe waadilifu na wasijihusishe na vitendo vya wizi kwa kuwa havina tija.


 (mwisho)
Read More

AJALIWA ATEMBELEA VIWANDA JIJINI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Soni wilayani  Lushoto akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa saruji  kutoka kwa Bw. Pradeep Punlana  (katikati) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha  Rhino kilichopo eneo la Maweni jijini Tanga  wakati alipotembelea kiwanda hicho  Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa maziwa wakati alipotembelea kwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga, Novemba 1, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, watatu kushoto ni Meneja Ufundi wa kiwanda hicho, Adam Gamba na wanne kukhoto ni Meneja Mkuu wa kiwanda, Michael Karata.

Read More

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

*Yaagiza mashine zichunguzwe, mitambo yenye hitilafu ikarabatiwe kazi ianze

SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.

“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.”

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho .

Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho  kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.

Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.

“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa na  wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”

Amesema wakulima hao walikosea kwa kuunda Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA) ambapo katika kusajili badala ya kuanzisha ushirika wao walisajili NGO ambayo ilikuwa na wanachama wake, huku kiwanda kikiwa kimeanzishwa kwa ajili ya wakulima wote, jambo ambalo lilisababisha mgogoro baina ya wakulima na viongozi wa UTEGA.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa wakati mgogoro huo ukiendelea kati ya UTEGA na wakulima wa chai wasiokuwa wanachama wa NGO hiyo, uliibuka mgogoro mwingine baina ya wakulima wote pamoja na muwekezaji ambaye ni kampuni ya Mponde Tea Estate baada ya kukabidhiwa kiwanda hicho  na uongozi wa UTEGA bila ya wao kushirikishwa.

Amewasisitiza wakulima wafufue mashamba yao kiwanda ni cha  Serikali  hivyo watakuwa wamepata sehemu ya uhakikika ya kupeleka chai ambayo itachakatwa. Pia ameagiza Mrajisi wa Ushirika aende kwa wakulima na kutambua idadi yao pamoja na kujua                               ukubwa wa mashamba yao.

Amesema baada ya kubaini idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba yao awasaidie katika kuunda vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kisha kuunda ushirikia wao ambao watautumia katika kusimamia zao lao la chai na kuhakikisha mkulima ananufaika.

Waziri Mkuu amesema zao la chai ni miongoni mwa mazao makuu sita ya kimkakati, mengine ni korosho, kahawa, tumbaku, pamba na chikichi, hivyo amewataka wafufue mashamba yao na waendelee kuiamini Serikali yao ambayo imejidhatiti kuwahudumia.

Awali,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makam wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alisma Mgogoro huo wa kiwanda cha Mponde ulianza tangu mwaka 1999 na ilipofika mwezi Mei 2013, wananchi walimlalamikia kwa kushindwa kutatua tatizo hilo.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli aliwaomba wananchi hao waendelee kuwa na subira wakati suala lao likiwa linaendelea kushughuliwa na Serikali. “Mgogoro huo umesababaisha kudhorota kwa uchumi kwa sababu wananchi wengi waliacha kulima chai baada ya kiwanda hicho kufungwa miaka mitano iliyopita.”

HIvyo Makamba ameiomba Serikali iwasaidie wakulima wa zao la chai kuwapa miche mipya pamoja na pembe jeo kwa ajili ya kufufua zao hilo na kukiwezesha kiwanda cha chai MPonde kupata malighafi kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kuwa  tayari amekuja na wataalam kwa ajili ya kukagua mashine zote zilizopo kiwandani hapo ili mchakato wa kukiwasha uanze  mara moja.

Mwijage alisema “mimi kama Waziri mwenye dhamana ya viwanda nawaambia wananchi muondoe wasiwasi tayari kiwanda kimeshafunguliwa maana sitaondoka hapa Bumbuli mpaka kieleweke.”

(mwisho)
Read More

ZIARA YA MAJALIWA KATIKA JIMBO LA BUMBULI WILAYANI LUSHOTO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati alipowasili kwenye kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa  katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto Novemba 1, 2018.  Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wanne kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.

Wananchi wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipowasili kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde na kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika mkutano aliouhutubia kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mponde wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo kukagua kiwanda cha chai cha mponde na kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018.

Read More