Sunday, April 7, 2019

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DR. JOHN MAGUFULI KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA MAUJI YA KIMBARI RWANDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya Nje wa Rwanda Balozi Richard Sezibera .aliye mpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali alipo wasili leo Aprili 7/2019 alipo fika kumuwakilisha  Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 Kkulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Ernest Mangu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo na Rais Mstaafu wa Naigeria Olusegun Obasanjo walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,mwenye Tai nyekundu akiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 katika wakitoa heshima katika eneo la kumbumbu ya mauji ya kimbari Waziri Mkuu yupo Kigali Rwanda akimuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994.

Read More

Saturday, April 6, 2019

TUTAENDELEA KUMUENZI MAREHEMU SOKOINE-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wote wataendelea kumuenzi shujaa wao, Marehemu Edward Moringe Sokoine.

Amesema Marehemu Sokoine wakati wa uhai wake alijitoa kuchapa kazi kwa bidii na amelitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 6, 2019) katika mbio za marathon kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine. Mbio hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kwa makusudi kukiita Chuo Kikuu cha Kilimo jina la Sokoine  ili kumuenzi  shujaa huyo.

Amesema Taifana Watanzania kwa ujumla wataendelea kufuata nyayo za Marehemu Sokoine katika mema mengi aliyolitendea Taifa la Tanzania na siku zote watandelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Waziri Mkuu amesema kufanyika mbio hizo za Marathon ni ushahidi kwamba Marehemu Sokoine bado anakumbukwa na kuheshimiwa  na Watanzania kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika ustawi wa Taifa. 

Alisema katika uhai wake, Marehemu Sokoine alikuwa ni mfano bora wa kiongozi wa juu  wa nchi  aliyedhamiria kwa dhati  kupambana na vitendo vya rushwa, uonevu, ubadhirifu na ufisadi.

“Leo hii tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inayoendeleza kwa vitendo  utendaji, uandilifu na mtazamo aliokuwa nao marehemu Sokoine.” 

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Sokoine, mtoto wa Marehemu, Namelok Sokoine alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa Taifa la Tanzania.

Alisema anafarijika kuona kwamba yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia Marehemu Sokoine hivi sasa yanatekelezwa kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu na Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Magufuli. 

Amesisitiza kwamba   familia ya Marehemu Sokoine  inaunga mkono kwa dhati  juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na inaamini kwamba Tanzania yenye neema inakuja.

Katika Marathon hiyo, washindi kwa uapnde wa wanaume waliokimbia kilomita 21 ni Joseph Panga, mshindi wa kwanza, na wa pili alikuwa ni Aliphonce Felix Simbu na mshindi wa tatu alikuwa Lazaro Damasi.

Upande wa wanawake kilomita 21, mshindi wa kwanza alikuwa ni Faulina Abdi Matanga, mshindi wa pili alikuwa ni Magdalena Shauri na mshindi wa tatu alikuwa ni Nathalia Elisante.

Waliohudhuria katika mashindano hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Wabunge na viongizi pamoja na wengine wa Serikali.

 (mwisho)
Read More

VIJANA WAPONGEZA SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO KUHUSU KILIMO CHA KITALU NYUMBA


NA.MWANDISHI WETU
Wanufaika wa programu ya kukuza ujuzi eneo la kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba “green house” wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwawezesha katika masuala ya kilimo hicho na kujikwamua kiuchumi.
Pongezi hizo wamezitoa hii leo Aprili 06, 2019 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea kukagua utekelezaji wa Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.
Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio ikiwemo, kupata ujuzi wa kilimo cha mazao mbalimbali, kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kujipatia vipato halali pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaowezeshwa elimu hiyo.
Mtaalam kutoka kampuni ya Holly green Bw. Octovian Lasway alieleza kuwa, zaidi ya vijana 100 wamenufaika na elimu ya kilimo cha kitalu nyumba katika Wilaya hiyo na kusaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira nchini.
“Programu hii imekuja wakati sahihi na imesaidia kundi kubwa la vijana kwa kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija kwa kuwa na mazao bora na kuongeza kipato kwa wananchi,”alisisitiza Octovian.
Akitoa maelezo kwa wanufaika hao, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde alieleza jitihada za Serikali katika kufikia kundi kubwa la vijana katika kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili kuendelea kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia falsafa ya uchumi wa viwanda.
“Mradi umekusudiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania Bara ambapo awamu ya kwanza itafikiwa mikoa 12 na Halmashauri 83 kwa lengo la kuwezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za maisha  ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama Serikali,”alieleza Mavunde
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira wa ofisi hiyo Bw.Ally Msaki alieleza kuwa, mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na kuboresha kipato kwa watanzania.
“Mpango huu unalenga kufikia vijana 18800 nchi nzima ambapo kila Halmashauri itafikia vijana 100 na hadi sasa tumefikia halmashauri za mkoa 10, ikiwemo;Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera,”alieleza Msaki
Naye Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nagma Giga alifurahishwa na utendaji na bidii ya vijana hao na kuwaasa kuendelea kutumia  ujuzi huo kwa vijana wengine nchini.
Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa aliwataka vijana kutodharau kilimo kwa kuzingatia mchango wake katika kujikwamua kimaisha.
“Maisha hayapo kwenye karamu peke yake bali jembe linauwezo wa kuwatoa na kuwakwamua kiuchumi endapo kutakuwa na umakini na kujitoa kwa bidii,”alisisitiza Ikupa.
Kwa upande wake mwanagenzi Bw.Festo Ezikiel aliendelea kuipongeza serikali kuendelea kuwaamii na kuwajengea uwezo wa kilio cha kisasa cha kutumia kitalu nyumba.
“Tunaipongeza Serikali kutuamii na kutupa ujuzi kuhusu kilimo hiki nasi tunaahidi kushirikisha vijana wengine waliopo katika maeneo yetu ili kujikwamua kiuchumi,”alisema Ezekiel
=MWISHO=
Read More

VIJANA WAPONGEZA SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO KUHUSU KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Moja ya Kitalu Nyumba cha mafano katika Wilaya ya Chamwino kama Kinavyoonekana ikiwa ni moja ya mikakati ya kuwainua vijana kupitia  programu ya uwezeshaji inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella  IKupa akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Dodoma kujionea utekelezaji wa   Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti   wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga wakiwa ndani ya moja ya vitalu nyumba hivyo.
Mtendaji  Mkuu wa Kampuni ya Holly Green Agric Mhandisi Octavian Lasway akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati  ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu namna walivyoweza kutekeleza Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino pamoja na kuwajengea uwezo vijana ili kufanya mpango huo unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma Aprili 06, 2019.
Sehemu ya Vijana zaidi ya 100 wa Wilaya ya Chamwino walionufaika na Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.
Sehemu ya miche ya nyanya katika kitalu nyumba kama inavyoonekana katika picha ikiwa tayari kumika katika kitalu nyumba.
Muonekano  nyanya katika moja ya vitalu nyumba vilivyotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini.
Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu  Bw. Ally Msaki akiwa kwenye moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria  katika Wilaya ya Dodoma mjini na Chamwino.
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA MARATHON YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 35 YA KIFO CHA MAREHEMU EDWARD MORINGE SOKOINE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Mamelok Sokoine akitoa salamu za familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. 
Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
Wasanii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipoozungumza katika Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21 wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha Aprili 6, 2019.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Read More

TANZANIA YAONGOZA KWA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI – MAJALIWA

* Miradi mipya ya kisekta yatarajiwa kuzalisha ajira mpya 15,491

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa uwekezaji katika Afrika Mashariki na imeweza kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.18, ikifuatiwa na Uganda dola za Marekani bilioni 0.7 na Kenya dola za Marekani bilioni 0.67.

“Kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuvutia uwekezaji nchini, hali ya uwekezaji imeimarika ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha kuwa Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 4, 2019) Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 kwenye mkutano wa 15 wa Bunge.

Amesema Taarifa ya Uwekezaji ya Dunia (World Investment Report) ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imebainisha kiasi hicho kikubwa cha uwekezaji.

“Taarifa nyingine ya“The Africa Investment Index (AII) 2018” inaonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 13 kati ya nchi 54 za Afrika katika kutoa fursa za masoko na vivutio vya uwekezaji.”

Vilevile, Waziri Mkuu amesema kuwa taarifa ya “Where to Invest in Africa” ya mwaka 2018, nayo imeonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya saba kati ya nchi 52 zinazovutia zaidi kwa uwekezaji barani Afrika.

Kutokana na uwekezaji huo mkubwa, Waziri Mkuu amewataka Watanzania wachangamkie fursa zinazojitokeza kutokana na ukuaji wa uchumi, maendeleo ya kijamii na pia uwekezaji wa sekta ya umma kwenye miundombinu kwa kuthubutu kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwemo kutekeleza mapendekezo ya Mpango Kazi Jumuishi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini. Pia itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema uhamasishaji wa miradi ya kisekta ndani na nje ya nchi, umefanikisha kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za kimkakati na unatarajia kuwekeza mitaji ya jumla ya dola za Marekani bilioni 1.84 na kuzalisha ajira mpya 15,491.

“Hadi kufikia Februari, 2019 jumla ya miradi mipya 145 ilisajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Kati ya miradi hiyo, miradi 104 sawa na asilimia 72 inamilikiwa na wawekezaji wa ndani; miradi 38 sawa na asilimia 26 inamilikiwa na wawekezaji kutoka nje na miradi mitatu sawa na asilimia 2.01 ni ya ubia,” amesema.

Akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali imekusanya shilingi bilioni 9.9 tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo Desemba, 2018.

“Hadi tarehe 10 Machi 2019, jumla ya vitambulisho 496,221 sawa na asilimia 74 vilikuwa vimegawiwa kwa wajasiriamali wadogo katika mikoa yote nchini.” Amesema hatua hiyo ilichukuliwa ikiwa ni kutambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo nchini katika kuchangia pato la Taifa na kukuza uchumi

“Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa vitambulisho 670,000 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo ambao mitaji yao haizidi shilingi milioni nne. Lengo la kutoa vitambulisho hivyo vyenye kugharimu shilingi 20,000 kwa kila kimoja ni kuwatambua, kuwaandalia maeneo ya kufanya biashara bila usumbufu wowote na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza mapato ya ndani,” amesema.



(mwisho)
                               BONYEZA HAPA KUSOMA HOTUBA YA BAJETI
Read More

SERIKALI YAONGEZA NGUVU UZALISHAJI WA MAFUTA-MAJALIWA

UZALISHAJI mdogo wa zao la Michikichi ni miongoni mwa sababu za kushindwa kujitosheleza kwa mahitaji ya mafuta ya kula nchini na Serikali imekuwa ikilazimika kutumia fedha nyingi za kigeni kwa ajili ya kununua mafuta  hayo kutoka nje ya nchi.

Kutokana na changamoto hiyo, Serikali imeamua kuweka nguvu kubwa kwenye uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta ili kuondokana na utegemezi na kuokoa matumizi ya fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa leo (Alhamisi, Aprili 4, 2019) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha hotuba ya Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020.

Waziri Mkuu amesema katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imeanza kuimarisha kilimo cha zao la michikichi hususan katika mkoa wa Kigoma ili kusaidia upatikanaji wa mbegu bora za chikichi.

Amesema lengo ni kuzalisha na kusambaza kwa wakulima miche ipatayo milioni 20 katika kipindi cha miaka minne (2018/2019 hadi 2021/2022), pia Serikali imeamua kukifanya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kihinga, mkoani Kigoma kuwa Kituo cha Utafiti wa Mbegu Bora za michikichi.

“Maamuzi haya ya Serikali yameanza kuzaa matunda, hadi kufikia Februari 2019, Kituo cha Kihinga kimezalisha mbegu 4,747 ambazo zimefanyiwa uoteshwaji wa awali. Katika mwaka 2019/2020, Serikali imepanga kuzalisha miche ya michikichi milioni tano.”

Waziri Mkuu amesema matarajio ya Serikali ni kuhakikisha kwamba usimamizi mzuri wa mkakati huo wa miaka minne utalisaidia Taifa kuondokana na uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje, kutengeneza fursa mbalimbali za ajira na kuwaongezea kipato wakulima wa michikichi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2017/2018 na upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2018/2019, imeendelea kuimarika.

Waziri Mkuu amesema hatua hiyo imetokana na hali nzuri ya mvua katika maeneo mengi ya nchi, kuongezeka kwa tija na uzalishaji. “Uzalishaji wa mazao ya chakula umefikia tani milioni 16.89 ikilinganishwa na mahitaji ya chakula ya tani milioni 13.57 na kufanya nchi kuwa na ziada ya chakula ya tani milioni 3.32.”

Amesema uzalishaji wa mazao makuu ya kimkakati yakiwemo chai, kahawa, korosho, pamba na tumbaku umeimarika kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ikiwemo kuimarisha ushirika.

“Kwa mfano, uzalishaji wa zao la pamba uliongezeka kutoka tani 132,934 mwaka 2017/2018 hadi kufikia tani 222,039 mwaka 2018/2019 wakati uzalishaji wa zao la Kahawa uliongezeka kutoka tani 45,245 hadi kufikia tani 65,000.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa mazao hayo na mengine kwa kuwa ndiyo mhimili wa kutoa malighafi za kuendesha viwanda na yana mnyororo mpana wenye fursa ya kutoa ajira nyingi na kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

(mwisho)
                       BONYEZA HAPA KUSOMA HOTUBA YA BAJETI
Read More

Thursday, April 4, 2019

MAJALIWA AWASILISHA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA WAZIRI MKUU Bonyeza hapa kusoma bajeti


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma Makadirio  ya Mapato na Matumizi  ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 4, 2019.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma Makadirio  ya Mapato na Matumizi  ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma Makadirio  ya Mapato na Matumizi  ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.
     BOFYA HAPA KUSOMA BAJETI ILIYOWASILISHWA LEO TAREHE 04.04.2019
Read More

BUNGENI LEO 04.04.2019

 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 4, 2019.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 4, 2019.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 4, 2019.
     BONYEZA HAPA KUSOMA HOTUBA KAMILI
Read More

Monday, April 1, 2019

MASHAURIANO KATI YA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE NA KAMATI YA BAJETI YA BUNGE


Waziri Mkuu akihudhuria kikao cha mashauriano kati ya kamati ya uongozi ya Bunge na kamati ya bajeti ya Bunge leo tarehe 1 Januari,2019.
Waziri Mkuu akihudhuria kikao cha mashauriano kati ya kamati ya uongozi ya Bunge na kamati ya bajeti ya Bunge leo tarehe 1 Januari,2019.


Read More

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

Na; OWM (KVAU), SONGWE
Wananchi waaswa kutunza rasimali mbalimbali katika mazingira yao na kuyapenda ili kuepuka kuathiri na kuharibu mazigira yaliyopo.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Ichenjeziya alipotembelea eneo hilo lenye chanzo cha maji ya asili na kupanda mche wa mti ikiwa ni siku ya Kitaifa ya upandaji miti.
Waziri Mhagama alieleza kuwa Nchi yetu imeamua kutumia uchumi wa viwanda ili kutekeleza azma ya Serikali kuelekea uchumi wa pato la kati, hivyo hata upandaji miti na maliasili ya misitu inaendana na uchumi wa viwanda,” alieleza Mhagama.
Aliongeza kuwa kuelekea kwenye Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, ni vyema wananchi wakashiriki kauli mbiu ya upandaji miti ambayo inaendana na kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru isemayo“Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.
“Wanaichenjeziya mnatakiwa kuweka historia kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji ili kupata maji safi na salama,” alisema Mhagama
Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa kila mwananchi kuhakikisha anakuwa msimamzi wa mazingira na anatunza vyanzo vya maji kwa kufuata sheria na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na maji safi na salama kama haki ya msingi.
Hata hivyo Mhe. Mhagama alitumia pia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Songwe na Mikoa ya jirani kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa Aprili 2, 2019 katika Uwanja wa Kimondo uliopo Kata ya Forest, Wilayani Mbozi.
“Hii ni nafasi ya kipekee kwa wananchi na ni siku ya kuhamasishana kwa vijana kwa kujitathimini na kutambua mchango wa Baba wa Taifa na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibari katika kujenga Taifa,” alisema mhagama
Naye Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume alisema kuwa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni siku muhimu sana kwa wananchi kutambua historia ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyopelekea Taifa katika mwanga.
MWISHO
Read More