Wednesday, March 22, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SAMAKI CHA MAURITIUS

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa samaki katika kiwanda cha MER  Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama usindikaji wa samaki katika kiwanda cha MER  Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitazama makasha yenye minofu ya samaki wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha MER  Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha samaki cha MER  Des Mascareignes nchini Mauritius Machi 21, 2017.

Read More

VIONGOZI WA AFRIKA WAKUBALIANA KUFUNGUA FURSA ZA KIBIASHARA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wa mataifa ya Afrika wamekubaliana kufungua fursa za kiuchumi baina ya nchi hizo pamoja na kuweka utaratibu wa kutumia hati moja ya kusafiria.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumatano, Machi 22, 2017) wakati akingumzia makubaliano yaliyofikiwa katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP) uliofanyika nchini Mauritius Machi 20 hadi 21, 2017. Waziri Mkuu alimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri Mkuu alisema viongozi hao wamekubaliana kwamba mataifa ya Afrika yawe na hati moja ya kusafiria, ambayo itawawezesha wananchi kuingia nchi yoyote ndani ya bara hilo bila ya vikwazo kwa lengo la kurahisisha muingiliano wa watu na bidhaa.

Alisema jambo jingine walilokubaliana ni kuimarisha Jumuiya zao ikiwemo ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kuzishawishi nchi nyingine ambazo hazijajiunga kujiunga jumuia hizo.

Alisema viongozi hao walijadili namna watakavyoweza kuinua uchumi na kuweka mikakati ya kuimarisha viwanda, ambapo Tanzania ipo katika nafasi nzuri kwa kuwa tayari inatekeleza mpango wa kukuza uchumi wake kwa kupitia sekta ya viwanda.

Viwanda ndiyo mkombozi wa changamoto mbalimbali barani Afrika ikiwemo ya ajira, hivyo Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake,” alisema.

Jukwaa hilo lilizinduliwa Machi 20, 2017 na Waziri Mkuu wa Swazland Bw. Barnabas Sibusiso Dlamini kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Chad, Idriss Deby. Pia Bw. Dlamini alimuwakilisha Mfalme Muwsati wa III.

Bw. Dlamini alisema nchi za Afrika zinatakiwa kuboresha mitaa yake na kujikita katika kutoa elimu ya masuala ya sayansi na viwanda ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa masuala hayo angu wakiwa na umri mdogo.

Alisema iwapo wanafunzi wataanza kujifunza masuala ya viwanda kuanzia shule watakuwa na uelewa wa kutosha wa masuala hayo jambo ambalo litawarahisishia kupata ajira katika viwanda mbalimbali, hivyo kuondokana na tatizo la ajira linalozibakili nchi nyingi za Afrika.

Uzinduzi wa jukwaa hilo ulikuwa na ajenda nne ambazo zilihusu sekta ya viwanda, kukuza biashara miongoni mwa nchi za Afrika, kukuza ujuzi katika taaluma mbalimbali na kurahisisha muingiliano wa watu na bidhaa baina ya mataifa hayo.

Jukwaa hilo lilifanyika kwa siku mbili lilihudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.

Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA NGUO NCHINI MAURITIUS

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.

Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini Tanzania na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi pamoja na nguo kwa kuwa kuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.

Waziri Mkuu alitembelea kiwanda hicho kilichoko katika mji wa Latour Koenig jana (Jumatano, Machi 22, 2017) na kujionea namna wanavyotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kuamua kuwakaribisha waje kuwekeza nchini.

“Tumefarijika na uwekezaji wenu na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nvingi na yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.

Waziri Mkuu alisema madhumuni  ya kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika  viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na kuwawezesha wakulima kupata tija.

“Tunalima pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi ”  alisema.

Alisema viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato.

Mbali na kuwakaribisha wawekezaji hao, pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya kuiuza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho Bw. David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.

Bw. David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200. “Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka makubwa barani Ulaya,”
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NGO MAURITIUS

 Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha kuengeneza nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee kilichopo nje kidogo ya mji wa Port  Louis nchini Mauritious.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo zilizoshonwa  kwa vitambaa vilivyotengenezwa na kwanda cha nguo cha Compagne Mauricienne De Textile Ltee cha Mauritius wakati alipotembelea kiwanda hicho, nje kidogo ya mji wa Port Louis nchini Mauritius, Machi 22, 2017.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza viongozi wa kiwanda cha  nguo cha Mauritius cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo nje kidogo ya mji wa Port Louis Machi 22, 2017.

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAURITIU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watanzania waishio na wale wanaosoma nchini Mauritius kwenye hoteli ya Meridien,nje kidogo ya Mji wa Port Louis Machi 22, 2017.Kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed.
 Baadhi ya watanzania waishio nchini Mauritius na maofisa wa serikali ya Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji Port Louis Machi 22, 2017.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watanzania wanaosoma na wale wanaoishi nchini  Mauritius kwenye hoteli ya Meridien, nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi  22, 2017.  Kulia ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed na kushoto ni Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Mauritius, Merday Venkatasamy.

Tuesday, March 21, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NA KUKARABATI MELI CHA MAURITIUS

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kwanda cha kutengeneza na kukarabati meli, boti cha pantoni cha Contier Naval Del' Oceaniindien Limited (CNO 1 Company Limited) cha Mauritius Machi 21, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bibi Veroniqu Gorrioch kuhusu utengeneza na ukarabatiwa meli, pantoni na boti wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza na kukarabati meli, pantoni na boti cha Contier Naval Del' Oceaniindien Limited (CNO 1 Company Limited) cha Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kwanda cha kutengeneza na kukarabati meli, boti cha pantoni cha Contier Naval Del' Oceaniindien Limited (CNO 1 Company Limited) cha Mauritius Machi 21, 2017.

Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA ALTEO NCHINI MAURITIUS

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha sukari cha Kampuni ya Alteo ya Nchini Mauritius chenye uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani 170,000 za sukari kwa mwaka.

Kampuni ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro  kwa ubia na Serikali ya Tanzania na  kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.

Waziri Mkuu ametembelea kiwanda hicho leo (Jumanne, Machi 21, 2017) na kujionea namna wanavyozalisha sukari kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.

“Tekonolojia wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi mahitaji,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera  vinavyozalisha tani 320,000 kwa mwaka huku mahitaji ni tani 420,000.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na
uhaba wa malighafi.

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Khalid ameikaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye viwanda vya sukari. 

Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo ya uwekezani wa mashamba ya miwa nchini.

Pia ameomba Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro. “ Kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro,”.

Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu.

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA ALITEL NCHINI MAURITIU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mfumo wa kompyuta wa kiwanda cha sukari cha Alitel nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alitel nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha sukari cha Alitel nchini Mauritius Machi 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la miwa wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Alitel nchini Mauritius Machi 21, 2017.

Read More

Monday, March 20, 2017

MAJALIWA AWASILI MAURITIUS KUMWAKILISHA JPM KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini  Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini  Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiogozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo  wakati alipopokelewa  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini  Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.

Read More

MAJALIWA ASHIRIKI UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRICA MJINI PORT LOUIS- MAURITIUS.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa nchi za Afrika walioshiriki katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye Hoteli ya Westin mjini Port Louis nchini Mauritius Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Swaziland , Barnabas Sibusiso Dlamini katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika kwenye hoteli ya Westin mjini Port Louis, Mauritius, Machi 20, 2017.

Read More

Sunday, March 19, 2017

WAZIRI MKUU AMUWALIKISHA RAIS UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI AFRIKA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).

Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo.

Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.

Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017.

Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo.

Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.
Read More

Saturday, March 18, 2017

WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA JITIHADA ZA KUREJESHA MIUNDOMBINU MKOANI KAGERA

Mkuu wa Wilaya ya Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo akichangia hoja wakati wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji ya Kukabili na Kurejesha hali baada ya athari za tetemeko mkoani Kagera.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akinukuu hoja za wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko Mkoani Kagera kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkoa Machi 18, 2017 kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Miradi ya Kukabili na Kurejesha hali kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kujadili na kupokea taarifa hiyo mkoani Kagera.

Read More

WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA JITIHADA ZA KUREJESHA MIUNDOMBINU MKOANI KAGERA

Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kagera kwa hatua iliyofikiwa katika kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba10 mwaka 2016 katika Mkoa wa Kagera linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter.

Mhe. Mhagama alionesha kuridhishwa kwake baada ya kufanya ziara  Mkoani hapo mapema wiki hii kwa lengo la kutathimini utekelezaji unaoendelea katika kurejesha miundombinu ili wananchi waendelee kutumia huduma hizo kama kawaida.

Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama alitembelea Shule ya Sekondari Nyakato, Ihumo na Omumwani, Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi na Kituo cha Kulelea Wazee cha Kiilima na kubaini kuwa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kabyaile-Ishozi ambacho kimefikia asilimi 80 ambapo kimetumia kiasi cha shilingi 381, 506, 079.00.

“Nikiri kwamba ukiacha baadhi ya mapungufu kwa watendaji wachache, wengi mmetupa ushirikiano mzuri kwa kulinganisha hali ilivyokuwa kwa kuangalia tukio lilivyotokea na hadi hatua za kukabili hatimaye kurejesha hali.”Alisema Waziri

Aliendelea kushukuru ushirikiano mzuri uliopo katika kutekeleza majukumu hatimaye kufikia lengo “Kama sio ushirikiano wa pamoja kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkoa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania huwenda tusingefika hapa hivyo tuna kila sababu ya kupongeza juhudi hizi kwa niaba ya Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu tumefarijika kwa ushirikiano wenu”

Pamoja na pongezi hizo, Waziri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Kamishna Diwani Athuman kuendelea kuzingatia taratibu za manunuzi na kila eneo linalofanyiwa kazi kufuata taratibu, kanunuzi zilizopo kwani kwa atakaye kiuka sheria na taratibu hakutakuwa na msamaha.”Hakutakuwa na msamaha kwa yeyote atakayefanya uzembe lazima sheria zichukue mkondo wake hakuna kuoneana aibu” Alisisitiza waziri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Deogratius Kinawilo alipongeza kwa kukiri kuwa kazi inayoendelea ya kurejesha hali imefanyika kwa umakini mkubwa. “Tumefanya kazi kwa umakini mkubwa na kila mmoja alikaa kwenye nafasi yake hivyo niendelee kuwaomba watendaji wote kufuata sheria na kutekeleza yote yanayotupasa ili kuokoa mazingira ya wanakagera kwa ujumla”

Waziri mhagama alieleza pia pamoja na jitihada zote ifike mahali kile kilichokusudiwa kitimie na miradi yote ifikapo mwezi Mei mwaka huu imekamilika” Tuendelee kutekeleza majukumu yetu katika zoezi la kurejesha hali ili ifikapo mwezi Mei angalau asilimia 80 iwe imekamiliza” Alisema waziri

Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Januari mwaka huu na kuiagiza  Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya tathimini za shughuli zote wakati wa kukabili na urejesha hali baada ya kutokea kwa Tetemeko hilo.

Read More