Wednesday, December 18, 2019

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu baada ya  kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam.

Akiongea mara baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF leo Desemba 18, 2019 baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo wilayani Kigamboni, Jijini Dar es salaam, Mhe. Mhagama amesema kuwa Mhe. Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF Kuharakisha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kutumiwa na watanzania.

Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF kuwasiliana na vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati, Taasisi za Umma ili kuangalia uwezekano wa wanafunzi wa  elimu ya juu na watumishi wa umma pamoja na watanzania wenye nia ya kutaka kupanga nyumba hizo waweze waweze kupangishwa kwenye nyumba za hizo 161 zilizoko  Tuangoma, 720 zilizoko Mtoni Kijichi.

“Nimefurahishwa katika taarifa yenu kuwa mmewasiliana na vyuo kadhaa ikiwemo DUCE ambao wameonesha nia ya kuomba nafasi za wanafunzi 3000, lakini pia DIT wanahitaji nafasi za wanafunzi 300, tunawasubiri IFM na taasisi nyingine za elimu ya juu na Umma,kwa kuwa kwa Mradi wa Kijichi unazo nyumba 720 ambazo zinaweza kupangishwa na wananfunzi 7,200 kwa mantiki hii inaonesha tunao uwezo wa kukidhi mahitaji ya vyuo vikuu ” Amesema Mhe.Mhagama.

Mhe. Mhagama, ameongeza kuwa katika kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa mkombozi wa malazi kwa wanafunzi wa vyuo, hivyo ameishauri menejimenti ya NSSF kuwapa kipaumbele wanafunzi wa kike kwa kuzingatia kuwa takwimu za hivi karibuni zimebainisha kuwa maabukizi mapya ya virusi vya UKIMWI asilimia 40 ni kwenda kwa vijana ambapo asilimia 80 ya vijana ni watoto wa kike wa vyuo vikuu, amabapo mojawapo ya kichocheo cha maabukizi hayo ni  kutokana na kutokuwa na malazi salama.

Waziri Mkuu, alielekeza TARURA kuhakiksha wannatengeneza  miundombinu ya barabara katika miradi ya nyumba za NSSF, ambapo tayari wamekamilisha taratibu za  awali za ujenzi wa barabara hizo na wataalamu wa NSSF tayari wamehakiki gharama za ujenzi wa barabara hizo ili kuona kama zinaendana na uhalisia wa ujenzi utakaofanyika kupitia SUMA JKT. Zahanati

“Katika kuboresha barabara za mitaa za hizi nyumba nimeonakazi inayoendelea  na wameniambia DIT wanafanya kazi yao ya kuweka  taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi na watafanya kazi kwa wakati kama tulivyokubaliana” amesema Mhagama.

Aidha, agizo jingine kwa menejimenti ya NSSF ilikuwa ni kuboresha miundo mbinu ya Umeme, maji taka na maji safi, ambapo tayari taasisi zinazohusika na miundo mbinu hiyo ikiwemo TANESCO na DAWASA wamekamilisha taratibu za awali za utekelezaji na wameahidi kukamilisha shughuli zake kwa wakati ili nyumba ziweze kutumika.

Waziri Mhagama amefafanua kuwa agizo lingine ambalo NSSF wamelitekeleza ni  Mthamini Mkuu wa Serikali kutathimini nyumba hizo na kutoa   bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.

“Nimefurahishwa na taarifa mliyonipatia kuwa mthamini mkuu wa serikali atakabidhi ripoti yake leo kwa NSSF na naamini sasa watu wengi ambao wameonesha nia ya kupanga au kununua tutawapatia huduma kwa kuwa tunalo kundi la wanafunzi, watumishi wa umma na watu binafsi wenye uwezo wa kununua nyumba hizo”, Amesisitiza Mhagama.

Pia, Waziri Mkuu aliagiza  Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kupewa kipaumbele kwa nyumba 439 za Nungu ambapo Mkuu wa wilaya  na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni walielekezwa kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo  kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi  hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo mara ukarabati utakapo kamilika.

“Nimeridhishwa na utekelezaji wa shughuli za miundo mbinu kwa hapa Nungu na hivyo menejimenti ya NSSF wasilianane na Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwa uboreshaji wa majengo unaenda vizuri ili watumishi tunaowalenga waweze kutumia nyumba hizo, ” Amesema Mhagama.

Pia Mheshimiwa Mhagama amefurahishwa  na hatua ya LATRA kuanza kutekeleza agizo la kuanzisha njia za mabasi ya daladala   kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua na kupanga  nyumba hizo kupata usafiri wa umma, kama ilivyokuwa imeelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu.

Aidha, Mhe. Waziri pamoja na kuwapongeza NSSF kuanza kutekeleza maagizo hayo, pia amewataka wazingatie muda uliowekwa wa kukamilisha kazi hiyo, hivyo amewataka kufanya kazi usiku na mchana kwa kuzingatia ubora wa kazi.

“Zingatieni uhalisia wa gharama zinazotumika katika ujenzi wa mradi huu ili fedha za wanachama zitumike vyema kwa kuonekana fedha zimewekezwa kwenye miradi yenye tija ” Amesema Mhe. mhagama
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, amesema NSSF imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mhagama  na kwamba watafanya kwa weledi na ubora ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Balozi Ali Idd Siwa amemhakikishia Mhe. Waziri Kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha kuwa maagizo aliyoyatoa yanatekelezwa kwa wakati ili kuhakikisha nyumba hizo zinawanufaisha watanzania.

 Miradi ya nyumba za NSSF, wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, ipo katika maeneo ya Tuangoma   jumla ya nyumba 161, Dungu nyumba 439 na Mtoni Kijichi   jumla ya nyumba 720.
MWISHO
Read More

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA TANZANIA BARA APONGEZA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KUKUZA UJUZI

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula (kulia) akieleza jambo alipokuwa kwenye Kitalu nyumba kilichopo Ihemi, Mkoani Iringa. (Wenye shati ya Bluu) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Na; Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa utekelezaji wa programu ya taifa ya kukuza ujuzi ambayo imekuwa ni chanzo cha kuwajengea uwezo vijana nchini.
Pongezi hizo zimetolewa jana Disemba 18, 2019 na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula wakati alipokuwa  akizindua Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ihemi, Mkoani Iringa.
Alieleza kuwa utekelezaji wa programu hiyo umeleta mabadiliko makubwa sana kwa vijana ambapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa mustakabali wa taifa lao.
“Serikali ya awamu ya tano inatambua umuhimu wa vijana na ndio maana inatekeleza programu hii kwa kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yatayowasaidia vijana wa kitanzania kuondokana na changamoto ya ajira,” alisema Mangula
Aliendelea kuelezea kuwa Mafunzo ambayo yatakuwa yakitolewa katika chuo hiko yatahamasisha vijana kushiriki kwa wingi kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na pia kuinua ari ya vijana katika utendaji kazi wao.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde alifafanua kuwa Ofisi hiyo inatekeleza Programu hiyo ya kukuza ujuzi kwa njia mbalimbali ikiwemo uanagenzi, mafunzo ya vitendo mahali pa kazi, mafunzo ya urasimishaji ujuzi uliyopatikana nje ya mfumo rasmi na mafunzo ya kukuza ujuzi kwa walio makazini.
“Programu hii imekusudia kuwezesha vijana ambao kwa asilimia kubwa ndio nguvukazi ya taifa, hivyo kuwapatia ujuzi na stadi za kazi stahiki kutawasaidia kujiajiri au kuajiriwa katika soko la ajira,” alieleza Mavunde
Akitolea mfano Mafunzo ya Kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Greenhouse) yaliyokuwa yakitolewa kwa vijana waliopo kituoni hapo yametoa fursa kwa vijina kutambua kuwa kilimo kinaweza kuwapatia ajira na kipato.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde amesisitiza vijana kuchangamkia fursa ya mafunzo yatakayokuwa yanatolewa katika chuo hiko ili waweze kupata ujuzi wa fani mbalimbali zitakazowafanya waweze kujiajiri na kupata kipato.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Bw. Raymond Mwangwala (wenye kofia nyeusi) akifafanua jambo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula (wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ufundi Stadi wa Ushonaji kilichopo katika Chuo cha Ihemi, Mkoani Iringa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (wenye shati la bluu) akipanda mche wa mti pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi katika eneo la Chuo hiko. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bi. Venerose Mtenga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akielezea jambo kuhusu Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ihemi, Mkoani Iringa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula (wenye miwani) akitazama Nyanya zilizopo katika Kitalu nyumba (Greenhouse) alipotembelea mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kujionea Mafunzo ya kilimo wanayopatiwa vijana. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally.
Agronomia kutoka Kampuni ya HolyGreen Bi. Veronica Rusagira (kushoto) akitoa maelezo kuhusu kilimo cha Matango kwa  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula (wa pili mstari wa kulia) alipotembelea Kitalu Nyumba kilichopo katika Kituo hiko cha Ihemi, Mkoani Iringa.

Read More

Monday, December 16, 2019

KATIBU MKUU MWALUKO ATAKA MIPANGO KABLA YA MAAFA NA SIO WAKATI WA MAAFA





Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Dorothy Mwaluko amelielekeza Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini kutoa ushauri wa kitaalamu unaojikita katika hatua ya kabla ya maafa kutokea na sio kujikita wakati wa maafa yanapotokea kama ilivyozoeleka, kwa kuwa ushauri wa namna ya kuzuia na kujiandaa na maafa kabla ya maafa kutokea huweza  kupunguza madhara ya maafa na rasilimali zinazohitajika katika upunguzaji wa madhara hayo.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma tarehe 16 Desemba, 2019, wakati akifungua kikao cha Jukwaa hilo ambapo amebainisha kuwa wakati wa kukabili majanga na maafa kunakuwepo na mipango mingi ambayo hutekelezwa na wadau wa Usimamizi wa maafa na kwa uchache wakati wa urejeshaji hali wa maafa,  lakini mipango ya kujiandaa na  kuzuia maafa ambayo hufanyika kabla ya maafa kutokea  kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara ya  maafa yatakapotokea huwa haitekelezwi.

“Tumekuwa na maafa hapa nchini ambayo yameleta madhara nchini,  itakumbukwa ajali ya moto mjini Morogoro hivi karibuni, tujiulize kuna mipango inayoendelea katika kuzuia majanga hayo, yapo maafa ya mvua yanaendelea kutokea,  lakini je ipo mipango ya kabla ya maafa kutokea, lakini pindi maafa yakitokea wadau wa usimamizi wa  maafa hujitokeza na kuanza kukabili maafa, sasa nataka nguvu nyingi ielekezeni kwenye mipango ya kabla ya maafa kutokea na hata ikibidi ainisheni majanga yanayoweza kutokea kwenye maeneo husika ili jamii iweze kujiandaa na kuyazuia maafa husika kabla yakutokea“ Amesisitiza Mwaluko.

Aidha, amelielekeza Jukwaa hilo kuupitia Mkakati wa Taifa wa Kupunguza athari za maafa na kuhakikisha kuwa unaendana na uhalisia wa hali ya majanga yanayotokea katika jamii ili uweze kutekelezeka kwa kuweka malengo yenye uhalisia, huku akisisitiza kuwa ni vyema mkakati huo ukatafsiriwa kwa Kiswahili ili uweze kutumiwa vyema na walengwa kuanzia ngazi ya msingi ya maafa ambayo ni kamati za vijiji.

Katika hatua nyingine  Katibu Mkuu, Mwaluko  amelielekeza Jukwaa hilo kuwa na ushirikiano miongoni mwa wadau wa jukwaa hilo kwa kila mdau kuainisha majukumu yake na namna anavyoyatekeleza majukumu yake, ili kuweza kujua jukumu la kila mdau na anafanya nini  na kwa wakati gani na hatimaye mipango ya kuimarisha Usimamizi wa maafa iwe inayotekelezeka.

“Kupunguza madhara ya maafa ni suala mtambuka lenye mchango mkubwa katika shughuli za maendeleo.Wakati mwingine wananchi wamekuwa wakipata madhara kwa kukosa uelewa hivyo ni vyema kila mdau kuwajibika katika majukumu yake kwa kutoa fursa ya uratibu wa usimamizi wa maafa kwa ushirikiano  wa wataalamu wa  fani mbalimbali” Amesema,  Mwaluko

Awali akiongea katika kikao hicho, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ameeleza kuwa Jukwaa hilo ni chombo cha kisheria ambacho kipo kwa ajili ya kutathmini na kutoa ushauri wa kitaalam kwa serikali kuhusu majanga ya aina zote, ambapo Jukwa hilo  linaundwa kwa kuzingatia Kifungu cha 40 cha Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na.7 ya mwaka 2015.

Kikao hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana  na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kupitia ufadhili wa Awamu ya Pili ya Programu ya Kidunia ya Utoaji wa Huduma za Hali ya Hewa ya GFCS (Global Framework for Climate Services Adaptation Programme in Africa (APA) II). 

Jukwaa hilo ambalo linajumuisha wataalamu wa fani mbali mbalimbali  kwa kujumuisha sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na umoja wa mataifa na asasi za kiraia jukumu lake la  msingi ni kutoa ushauri maeneo ya kipaumbele katika usimamizi wa maafa kwa uratibu na ushirikishawaji wa wadau ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya taifa na katika misaada ya kibinadamu.  

MWISHO.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019.kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja, Selestine Masalamando
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe,akieleza umuhimu wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakati wa kikao cha Jukwaa hilo, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019.kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Dorothy Mwaluko na Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja, Selestine Masalamando.
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019. Jukwaa hilo hutathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa serikali kuhusu majanga ya aina zote.
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019., Jukwaa hilo ni muhimu kwa ajili ya ushauri wa maeneo ya kipaumbele katika usimamaizi wa maafa.
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019,  Jukwaa hilo linajumiisha wataalamu kutoka katika sekta za umma, binafsi, asasi za kiraia na kimataifa.
Mratibu wa masuala ya Maafa Ofisi  ya Waziri Mkuu, Charles Msangi akifafanua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika usimamizi wa maafa wakati wa  kikao cha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo linajumiisha wataalamu kutoka katika sekta za umma, binafsi, asasi za kiraia na kimataifa
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo linalojukumu la kufuatilia utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Madhara ya maafa wa Sendai, 2015-2030.
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakifuatilia kikao cha Jukwaa hilo leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo limekutana kwa mara ya kwanza tangu Sheria ya maafa Na. 7  ya mwaka 2015 ianze kutumika.
Wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakiwa katika kikao cha Jukwaa hilo,  leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.
Wajumbe wa Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Maafa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko leo jijini Dodoma, tarehe 16 Desemba, 2019, Jukwaa hilo linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.
Read More

Thursday, December 12, 2019

SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU WA TANZANIA BARA PAMOJA NA MIAKA 57 YA JAMHURI ZILIZOFANYIKA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri: Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri: Uzalendo, Uwajibikaji ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiwa na viongozi wengine wa Itifaki  katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,  tayari kwa kuwapokea viongozi wa Kitaifa na wageni waalikwa wa sherehe  za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri Desemba 9,  2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri. Desemba 9, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  katika Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.  Desemba 9, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, mara baada ya kukagua gwaride la heshima katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  na akiwa tayari  kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.  Desemba 9, 2019
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa  (kulia) pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Mhe, Zubeir Ali Maulid (kushoto kwake) na Jaji Mkuu Zanzibar Omar Othman Makungu wakiwa wamesimama kwa ajili ya wimbo wa Taifa katika Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.  Desemba 9, 2019, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.


Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Desemba, 9, 2019.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Desemba 9,  2019.
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Baadhi ya Mawaziri, Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa wakifuatilia shughuli za Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri katika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Desemba 9, 2019.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shughuli za Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri katika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Desemba 9, 2019.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na viongozi wa Taasisi za serikali wakifuatilia shughuli za Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri katika  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Desemba 9, 2019.
Gwaride la Heshma lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Polisi, Magereza na JWTZ yakipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika,  katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza, Desemba 9, 2019.
Kikosi cha Makomando wa JWTZ wakionesha umahiri wao wa kufanya zoezi la uokozi katika mfano wa Tukio la Utekaji, tarehe 9 Desemba, 2019, kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.

Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza wakiimba wimbo wa AMANI walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza, Desemba 9, 2019.
Kikundi cha Sungusungu cha kutoka Kwimba mkoani Mwanza kikitumbuiza katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza, tarehe 9 Desemba, 2019.


Kikundi cha Sungusungu cha kutoka Kwimba mkoani Mwanza kikitumbuiza katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza, tarehe 9 Desemba, 2019.


Wacheza ngoma ya Litungu ya kabila la Wakurya  wakitumbuiza kunogesha Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Desemba 9, 2019.
Msanii Rajabu Abduli maarufu kama “Harmonize” akitumbuiza katika  Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Desemba 9, 2019.


Read More