Wednesday, December 18, 2019

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri  Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi Novemba, mwaka huu baada ya  kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es Salaam.

Akiongea mara baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF leo Desemba 18, 2019 baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo wilayani Kigamboni, Jijini Dar es salaam, Mhe. Mhagama amesema kuwa Mhe. Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF Kuharakisha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo ili ziweze kutumiwa na watanzania.

Waziri Mkuu alielekeza menejimenti ya NSSF kuwasiliana na vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati, Taasisi za Umma ili kuangalia uwezekano wa wanafunzi wa  elimu ya juu na watumishi wa umma pamoja na watanzania wenye nia ya kutaka kupanga nyumba hizo waweze waweze kupangishwa kwenye nyumba za hizo 161 zilizoko  Tuangoma, 720 zilizoko Mtoni Kijichi.

“Nimefurahishwa katika taarifa yenu kuwa mmewasiliana na vyuo kadhaa ikiwemo DUCE ambao wameonesha nia ya kuomba nafasi za wanafunzi 3000, lakini pia DIT wanahitaji nafasi za wanafunzi 300, tunawasubiri IFM na taasisi nyingine za elimu ya juu na Umma,kwa kuwa kwa Mradi wa Kijichi unazo nyumba 720 ambazo zinaweza kupangishwa na wananfunzi 7,200 kwa mantiki hii inaonesha tunao uwezo wa kukidhi mahitaji ya vyuo vikuu ” Amesema Mhe.Mhagama.

Mhe. Mhagama, ameongeza kuwa katika kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa mkombozi wa malazi kwa wanafunzi wa vyuo, hivyo ameishauri menejimenti ya NSSF kuwapa kipaumbele wanafunzi wa kike kwa kuzingatia kuwa takwimu za hivi karibuni zimebainisha kuwa maabukizi mapya ya virusi vya UKIMWI asilimia 40 ni kwenda kwa vijana ambapo asilimia 80 ya vijana ni watoto wa kike wa vyuo vikuu, amabapo mojawapo ya kichocheo cha maabukizi hayo ni  kutokana na kutokuwa na malazi salama.

Waziri Mkuu, alielekeza TARURA kuhakiksha wannatengeneza  miundombinu ya barabara katika miradi ya nyumba za NSSF, ambapo tayari wamekamilisha taratibu za  awali za ujenzi wa barabara hizo na wataalamu wa NSSF tayari wamehakiki gharama za ujenzi wa barabara hizo ili kuona kama zinaendana na uhalisia wa ujenzi utakaofanyika kupitia SUMA JKT. Zahanati

“Katika kuboresha barabara za mitaa za hizi nyumba nimeonakazi inayoendelea  na wameniambia DIT wanafanya kazi yao ya kuweka  taa za sola kwenye barabara za mitaa yote ya nyumba hizi na watafanya kazi kwa wakati kama tulivyokubaliana” amesema Mhagama.

Aidha, agizo jingine kwa menejimenti ya NSSF ilikuwa ni kuboresha miundo mbinu ya Umeme, maji taka na maji safi, ambapo tayari taasisi zinazohusika na miundo mbinu hiyo ikiwemo TANESCO na DAWASA wamekamilisha taratibu za awali za utekelezaji na wameahidi kukamilisha shughuli zake kwa wakati ili nyumba ziweze kutumika.

Waziri Mhagama amefafanua kuwa agizo lingine ambalo NSSF wamelitekeleza ni  Mthamini Mkuu wa Serikali kutathimini nyumba hizo na kutoa   bei halisi ya soko kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma kununua na kupanga katika nyumba hizo.

“Nimefurahishwa na taarifa mliyonipatia kuwa mthamini mkuu wa serikali atakabidhi ripoti yake leo kwa NSSF na naamini sasa watu wengi ambao wameonesha nia ya kupanga au kununua tutawapatia huduma kwa kuwa tunalo kundi la wanafunzi, watumishi wa umma na watu binafsi wenye uwezo wa kununua nyumba hizo”, Amesisitiza Mhagama.

Pia, Waziri Mkuu aliagiza  Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kupewa kipaumbele kwa nyumba 439 za Nungu ambapo Mkuu wa wilaya  na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni walielekezwa kuwasaidia watumishi wa wilaya na Halmashauri hiyo  kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha watumishi  hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba hizo mara ukarabati utakapo kamilika.

“Nimeridhishwa na utekelezaji wa shughuli za miundo mbinu kwa hapa Nungu na hivyo menejimenti ya NSSF wasilianane na Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kuwa uboreshaji wa majengo unaenda vizuri ili watumishi tunaowalenga waweze kutumia nyumba hizo, ” Amesema Mhagama.

Pia Mheshimiwa Mhagama amefurahishwa  na hatua ya LATRA kuanza kutekeleza agizo la kuanzisha njia za mabasi ya daladala   kupitia kwenye nyumba za NSSF Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua na kupanga  nyumba hizo kupata usafiri wa umma, kama ilivyokuwa imeelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu.

Aidha, Mhe. Waziri pamoja na kuwapongeza NSSF kuanza kutekeleza maagizo hayo, pia amewataka wazingatie muda uliowekwa wa kukamilisha kazi hiyo, hivyo amewataka kufanya kazi usiku na mchana kwa kuzingatia ubora wa kazi.

“Zingatieni uhalisia wa gharama zinazotumika katika ujenzi wa mradi huu ili fedha za wanachama zitumike vyema kwa kuonekana fedha zimewekezwa kwenye miradi yenye tija ” Amesema Mhe. mhagama
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio, amesema NSSF imeyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mhagama  na kwamba watafanya kwa weledi na ubora ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa au kupangishwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Balozi Ali Idd Siwa amemhakikishia Mhe. Waziri Kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha kuwa maagizo aliyoyatoa yanatekelezwa kwa wakati ili kuhakikisha nyumba hizo zinawanufaisha watanzania.

 Miradi ya nyumba za NSSF, wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, ipo katika maeneo ya Tuangoma   jumla ya nyumba 161, Dungu nyumba 439 na Mtoni Kijichi   jumla ya nyumba 720.
MWISHO


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.