Thursday, December 5, 2019

KATIBU MKUU MWALUKO ATETA NA MKUU WA MKOA MWANZA MAANDALIZI SHEREHE ZA UHURU

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) . Dorothy Mwaluko akimueleza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella,   juu ya umuhimu wa kukamilisha  kwa wakati  shughuli zitakazo fanyika siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 9 Desemba, mwaka huu, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe hizo leo, tarehe 5 Desemba, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Mkuu mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher Kadio, leo, tarehe 5 Desemba, 2019,  wakiwa katika viwanja vya CCM Kirumba, wakati alipofika uwanjani hapo kukagua maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo, tarehe  9 Desemba mwaka huu.
Kikundi cha Kwaya cha MVC cha mkoani Mwanza,  kikifanya  mazoezi kwa ajili ya siku ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko,  leo, tarehe 5 Desemba, 2019,  akishuka  katika jukwaa la Uwanja wa CCM  Kirumba, mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba mwaka huu.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo  leo, tarehe 5 Desemba, 2019 akishuka  katika jukwaa la Uwanja wa CCM  Kirumba, mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi za  Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”


Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyoakisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella,  leo, tarehe 5 Desemba, mara baada ya kukagua shughuli za maandalizi za  Majeshi ya Ulinzi kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya  miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri zitakayofanyika mkoani humo tarehe 9 Desemba 2019, katika viwanja vya CCM Kirumba. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa letu”.EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.