Saturday, July 8, 2017

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA KINYEREZI II

*Asema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 08, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia unaojengwa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

“Tunataka tupate umeme wa kutosha ili viwanda vitakavyojengwa viwe na nishati ya uhakika na ya gharama nafuu. Ni wajibu wetu kuendelea kuimarisha utekelezaji wa miradi hii.” Amesema.

Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda amesema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Meneja huyo amesema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

“Pia tunaendelea na ujenzi wa nguzo za kupokelea laini ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, ambapo mtambo wa kwanza wa megawati 30 utawashwa ifikapo Desemba 2017 na kila mwezi tutaingiza megawati 30 katika gridi ya Taifa.”

Amesema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

Mhandisi Manda ameongeza kuwa mradi wa Kinyerezi 1 (150MW) ulikamilika Machi 2015 na miradi mwili ya Kinyerezi 1-extension na Kinyerezi II inatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

Mhandisi Manda amesema miradi mingine inayotarajiwa kujengwa katika eneo hilo ni wa Kinyerezi III (600 MW) na Kinyerezi IV utakaozalisha (450 MW).

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda alisema mradi huo umewanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo.

Alisema hadi sasa wananchi 100 wa eneo la Kinyerezi wameajiriwa katika miradi hiyo ambapo ni sawa na asilimia 40 ya watumishi wote.


Bi. Sophia alisema mbali na ajira pia wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kuboreshewa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo zikiwemo za maji na elimu ambapo wameahidiwa kupewa madawati ya shule tano.*Asema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi ya kuzalisha umeme wa Kinyerezi II na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 08, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia unaojengwa eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha Taifa kuwa na umeme wa uhakika, utakaowezesha kuendesha viwanda.

Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

“Tunataka tupate umeme wa kutosha ili viwanda vitakavyojengwa viwe na nishati ya uhakika na ya gharama nafuu. Ni wajibu wetu kuendelea kuimarisha utekelezaji wa miradi hii.” Amesema.

Naye, Meneja wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda amesema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Meneja huyo amesema tayari mradi huo umefikia asilimia 66.32 ya ujenzi wake na sasa wako katika hatua mbalimbali za kukamilisha, ikiwemo ujenzi wa misingi ya mitambo na jengo la kuendeshea mitambo.

“Pia tunaendelea na ujenzi wa nguzo za kupokelea laini ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Kinyerezi I hadi Kinyerezi II, ambapo mtambo wa kwanza wa megawati 30 utawashwa ifikapo Desemba 2017 na kila mwezi tutaingiza megawati 30 katika gridi ya Taifa.”

Amesema miradi iliyoko katika eneo hilo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni Kinyerezi 1 (150MW), Kinyerezi I Extension (185MW ) na Kinyerezi II (240MW).

Mhandisi Manda ameongeza kuwa mradi wa Kinyerezi 1 (150MW) ulikamilika Machi 2015 na miradi mwili ya Kinyerezi 1-extension na Kinyerezi II inatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

Mhandisi Manda amesema miradi mingine inayotarajiwa kujengwa katika eneo hilo ni wa Kinyerezi III (600 MW) na Kinyerezi IV utakaozalisha (450 MW).

Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda alisema mradi huo umewanufaisha wananchi wengi wa eneo hilo.

Alisema hadi sasa wananchi 100 wa eneo la Kinyerezi wameajiriwa katika miradi hiyo ambapo ni sawa na asilimia 40 ya watumishi wote.

Bi. Sophia alisema mbali na ajira pia wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kuboreshewa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo zikiwemo za maji na elimu ambapo wameahidiwa kupewa madawati ya shule tano.
Read More

Friday, July 7, 2017

ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI AAGWA DAR

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge.

Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.

Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa  mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi.

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”

Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.

Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.


Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Read More

ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI AAGWA DAR

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge.

Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.

Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa  mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi.

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”

Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.

Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.


Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Read More

Wednesday, July 5, 2017

WALIOPATA UJAUZITO KUFUKUZWA SHULE SI JAMBO JIPYA -MAJALIWA

*Asema ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za mwaka 2002
                                                              
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kutoruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu umetolewa kwa mujibu wa Sheria na sio utaratibu mpya kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanaharakati.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo leo (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema msimamo huo wa kisheria unalenga kuwafanya watoto wa kike wajishughulishe na masomo yao zaidi badala ya kushiriki kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015, jumla ya wanafunzi 3,637 waliacha masomo kutokana na kupata ujauzito.

“Kuwaachisha masomo wanafunzi waliopata ujauzito ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za mwaka 2002, zinazoruhusu kufukuza na kuondoa wanafunzi shuleni kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo uasherati, wizi, ulevi, kutumia dawa za kulevya pamoja na utoro.”

“Lengo hili lina nia ya kuwahimiza wazazi wawafundishe watoto wao mambo mema ndani ya familia na wawakataze kushiriki vitendo vya ngono katika umri dhamira ya Serikali ni kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu kwa ajili ya manufaa yake na Taifa kwa ujumla.”

Waziri Mkuu amesema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu. Hivyo ni lazima tuhakikishe mtoto wa kike anapata elimu stahiki na masomo yake hayakatizwi kwa kupata ujauzito.”

Amesema Serikali imewekeza kwenye mtoto wa kike, ambapo kifungu Na. 60 (b) cha Sheria ya Elimu Sura ya 353, kinatoa adhabu ya miaka 30 jela kwa yeyote atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi.

Pia, sheria inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni tano, au vyote kwa pamoja kwa anayeshiriki kumuozesha mtoto wa shule. 

“Natoa wito kwa Wakuu wa Wilaya kusimamia utekelezaji wa Sheria za nchi zenye lengo la kumlinda mtoto wa kike. Aidha, nawashauri Waheshimiwa Wabunge, mshirikiane na Halmashauri zenu kuweka mikakati ya kudhibiti ujauzito kwa watoto wa shule.”

 Wahamasisheni wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili wanaowapa wanafunzi ujauzito au kuwakatisha masomo ili waozeshwe wapate adhabu stahiki.


Read More

WATUHUMIWA 4,809 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA

*Heroine, Cocaine, bangi, mirungi na kemikali bashirifu vyakamatwa
* Mashamba ya bangi ekari 569.25 na mirungi ekari 64.5 yateketezwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miezi minne, Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 4,809 na kufungua majalada ya kesi 3,222.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

“Katika kipindi kifupi tangu Februari, 2017 Mamlaka hii ilipozinduliwa, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 4,809 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroine (gramu 327.173); cocaine (kilo 26.977); bangi (kilo 18,334.83); mirungi (kilo 11,306.67) na lita 6,338 za kemikali bashirifu zilikamatwa bandarini,” amesema.

Amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi za Mikoa imefanya operesheni za kuteketeza ekari 569.25 za mashamba ya bangi na ekari 64.5 za mashamba ya mirungi na kazi hiyo inaendelea. Kutokana na hatua hizo, jumla ya majalada ya kesi 3,222 yamefunguliwa.

“Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa ustawi wa familia zetu na Taifa kwa ujumla. Hivyo, napenda kurejea wito wangu kwa Watanzania wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano haya kwa kuendelea kutoa taarifa kuhusu watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.


Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kutokomeza kabisa mtandao wa dawa za kulevya nchini kwa kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanakuwa endelevu, yanafanyika kisayansi na yanaleta mafanikio. “Tuungeni mkono kwenye mapambano haya, ili tutokomeze kabisa mtandao huo,” amesisitiza.
Read More

SERIKALI YAPUNGUZA TOZO YA ARDHI KWA ASILIMIA 5

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia mwaka huu wa fedha, Serikali imepunguza gharama za malipo ya awali ya thamani ya ardhi iliyopimwa kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 2.5.

“Serikali inaendelea kupunguza gharama za umilikaji wa ardhi nchini na katika mwaka wa fedha 2017/2018, imepunguza tozo ya awali ya ardhi iliyopimwa (premium) kutoka asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi hadi asilimia 2.5 tu. Natoa wito kwa wananchi kuchangamkia punguzo hili na kujitokeza kupimiwa na kumilikishwa ardhi,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

Amesema Serikali itahakikisha kuwa kila kipande cha ardhi ya Tanzania kinapimwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. “Serikali imeweka mkakati na mpango kazi wa kuwezesha kufikia lengo la kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji 1,500 na wilaya tano kila mwaka.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha Ofisi za Ardhi za Kanda kwa kupeleka wataalam wa kada mbalimbali na kuwawezesha kwa kuwapatia vitendea kazi stahiki. “Kazi ya upimaji wa ardhi haiwezi kufanikiwa bila ya rasilmali watu. Lengo letu ni kuwawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za ardhi katika kanda badala ya kufuata huduma hizo makao makuu ya wizara,” amesema.


Amewasihi watumishi watakaohamishiwa katika ofisi za kanda pamoja na wale waliopo katika Halmashauri, wafanye kazi kwa ushirikiano na watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya ardhi na kutoa huduma kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote.
Read More

WAZIRI MKUU AMUAGIZA MWAKYEMBE AICHUNGUZE BMT

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alifanyie mapitio Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na iwapo hatoridhika na utendaji wake alivunje.

“Ninamuagiza Waziri mwenye dhamana kufanya mapitio na kutathmnini upya utendaji kazi wa Baraza la Michezo Tanzania juu ya usimamizi wake wa  michezo nchini na kama hataridhika, anayo mamlaka ya kulivunja Baraza hilo.”  

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa. Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki na kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika.

Amesema licha ya timu hiyo kumaliza ikiwa na jumla ya pointi 4 sawa na timu iliyoshika nafasi ya pili, ila Vijana hao wameonesha vipaji na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao.

Msisitizo wangu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kuendelea kuwatunza vijana hao, na kusimamia vilabu vya michezo nchini kuwekeza kwenye soka la vijana ili tujenge timu imara kwa miaka michache ijayo.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua umuhimu wa michezo kwa afya, umoja wa kitaifa na kama fursa ya ajira kwa vijana nchini.

“Wiki iliyopita, mkoani Mwanza yamehitimishwa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA. Wananchi wa Mwanza na Watanzania kwa ujumla wamejionea uwezo wa kimichezo, vipaji na hamasa kubwa iliyopo miongoni mwa vijana wetu kutumia vipaji vyao. “
Amesema Serikali itaendelea kuratibu michezo shuleni, ikiwa ni pamoja na kusimamia  ufundishaji wa michezo kama somo.  “Maelekezo yetu ni kwamba kila Mkoa uwe na shule angalau mbili zenye mchepuo wa michezo na walimu wenye sifa stahiki za kufundisha michezo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, wahakikishe kwamba kila shule inakuwa na viwanja vya michezo mbalimbali ili kuwapa fursa wanafunzi kushiriki michezo ili kupandisha na kuinua vipaji vyao.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za michezo nchini kwa dhamira yake ya kujenga uwanja mkubwa wa michezo mjini Dodoma kwa kushawishi mataifa rafiki kama vile Morocco ambao wanajenga uwanja huo.


Read More

“HATUNA MPANGO WA KUANZISHA MAENEO MAPYA YA UTAWALA”


*Asema Serikali yatenga sh. bilioni 412 kwa miradi ya maendeleo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kuanzisha maeneo mapya ya utawala hadi ikamilishe kuboresha miundombinu kwenye maeneo iliyoyaanzisha.

“Ili kutimiza azma hiyo, Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 412.38 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Serikali imetenga shilingi bilioni 16.985 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya majengo ya ofisi na makazi ya viongozi katika mikoa yote mipya,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

“Katika mgawo huo, mkoa wa Njombe umetengewa jumla ya shilingi bilioni 3.34; mkoa wa Katavi umetengewa jumla ya shilingi bilioni 3.080; mkoa wa Simiyu umetengewa jumla ya shilingi bilioni 3.775, mkoa wa Geita umetengewa jumla ya shilingi bilioni 2.978 na mkoa wa Songwe umetengewa jumla shilingi bilioni 3.812,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 61.7 kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri 64 ambapo kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 28.7 ni kwa ajili ya kukamilisha majengo ya ofisi katika Halmashauri 44 na shilingi bilioni 33 ni kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri mpya 20.

Sambamba na hatua hizo, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imetoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 pamoja na kununua magari ya kubebea wagonjwa katika Halmashauri 67.

Waziri Mkuu amesema miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na kuendeleza juhudi za ugatuaji wa madaraka kwenda katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na kuongeza mgawo wa fedha za ruzuku ya maendeleo inayopelekwa kwenye vyombo hivyo.


Amesema Serikali inachukua hatua hizo ili kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini zinatimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwa mujibu wa Ibara ya 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Read More

BUNGENI LEO 5.7.2017

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kufunga Bunge, Bungeni mjini Dodoma Julai 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Singida United, kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 5, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahi jambo na Kocha wa Singida United Hans van der Pluijm, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni, 5, 2017 katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba, katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 5, 2017. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Sadiq Murad wa Mvomero (kushoto) na Salim Turky wa Jimbo la Mpendae (kulia) katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Kazi Vijana na Ajira na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 5, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 5, 2017 katikati ni Mbunge wa Lushoto Shaaban Shekilindi.


Read More

Tuesday, July 4, 2017

MHE. WAZIRI MKUU NA MSHINDI WA TUZO YA UINGEREZA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel.

Samuel Mwanyika (19) akiwa ameshika tuzo wakati anatambulishwa kwa Wabunge mjini Dodoma. Samuel alishinda tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingereza bada ya kutuma picha ya pundamilia wawili wakiota jua kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Watoto kutoka nchi 18 walishiriki shindano la picha kwa mwaka 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samuel Mwanyika, mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Katikati ni Mama wa mtoto huyo Sophie Mshangama

Read More

BUNGENI LEO JULAI 4,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni, 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mufindi Kusini, Medard Kigola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Faida Bakari kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige (kulia) na Mbunge wa Bukene,  Selemani Zedi kwenye Jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Abdallah Ulega wa Mkuranga  (kushoto) na Stephen Masele kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.


Read More

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA NYANGAO WATEMBELEA BUNGE NA KUKUTANA NA MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye  wakisalimiana na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Julai 4, 2017.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na kulia ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.


Read More

Monday, July 3, 2017

MIVARF YAWAONGEZEA KIPATO WAKULIMA 56,637 MKOANI KAGERA

Program ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) imewajengea uwezo wakulima 56,637 mkoani Kagera kwa kuwawezesha kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Mhasibu Mkuu wa Benki ya Wakulima ya Ushiriki Kagera (KFCB) Bi. Adelina Kilaja tarehe 17 Mei, 2017 mkoani Kagera, wakati wataalamu wa MIVARF walipotembelea Benki hiyo na kujionea maendeleo yaliyofikiwa na benki hiyo kupitia uwezeshaji kutoka Programu ya MIVARF.

MIVARF imekwamua shughuli za Benki ya (KFCB) na kuwaongezea wigo mpana wa kuwahudumia wananchi kwa wingi zaidi ambapo awali haikuwa rahisi. “Program ya MIVARF umetuwezesha kuhamia katika mfumo wa Tehama ambao umerahisisha utendaji wetu wa kazi kwa kiwango kikubwa Zaidi, alieleza Kilaja”.

Benki yetu wateja wake wengi ni wavijijini, ambao ni Wakulima na Wafugaji hivyo benki imefanikiwa kuwajengea uwezo katika masuala ya Akiba na Mikopo, elimu ya kilimo bora, hii isingewezekana bila uwezeshaji kutoka MIVARF uliowawezesha wakulima hao kujikwamua katika maisha yao na kuwaongezea kipato, alisema Kilaja.  

Aidha, alifafanua kuwa kabla ya program ya MIVARF, benki ya KFCB ilikuwa na wateja wa moja kwa moja 7132 kwa  Desemba 2016 na wateja wa vyama vya Akiba na Mikopo walikuwa 26,874 kutokana na uwezeshaji wa MIVARF idadi ya wateja hao imefikia 56,637 Desemba 2016.

“Asilimia 70 ya wateja wetu tunaowahudumia ni wakulima wadogowadogo ambao hujishughulisha na kilimo cha Maharage na Mahindi kwa wingi. Ili kuhakikisha huduma inakuwa bora MIVARF imewajengea uwezo wafanyakazi wa benki hii na kutuboreshea mfumo wa uendeshaji wa kibenki ambapo benki imeweza kuanzisha huduma za Uwakala za kibenki pamoja na sim banking” Alisisitiza Kilaja.

Akifafanua Meneja wa IBUGA SACCOS Brighton Ferdinand alikiri kuboreshwa kwa huduma za utoaji mikopo katika SACCOS yao na kushukuru Benki ya KFCB kwa mkopo walio wapatia wa milioni 101 ambao umewasaidia kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa wakulima Mkoani Kagera katika Wilaya ya Muleba.

Aidha, baadhi ya wanufaika wa Mikopo hiyo wameeleza kuwa kutokana na mikopo waliyoipata kutoka katika vyama vya Akiba na Mikopo wameweza kuendeleza kilimo chao kwa tija na kuongeza kipato hali iliyowezesha kumudu gharama kilimo, biashara na elimu.


Programu ya Mundombinu ya Masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) inagharamiwa na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Lengo likiwa ni kuongeza kipato kwa wakulima na kuchangia katika kuboresha uhakika wa chakula kwa kaya zenye kipato cha chini hasa maeneo ya vijijini.
Read More

Sunday, July 2, 2017

MAJALIWA: CHANGAMOTO YA USAFIRI VIJIJINI KUWA HISTORIA



               *Azindua Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini  
                *Asema utashusha bei ya vyakula mijini

CHANGAMOTO ya usafiri nchini, hususan maeneo ya vijijini kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili,  Julai 02, 2017) wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.

“Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,”

“Utashusha bei ya vyakula mijini na bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua,”

Aidha, Waziri Mkuu amesema manufaa mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.

Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.

Amesema jambo hilo halikubaliki hivyo, amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.

Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza isimamiwe vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.

Akizungumzia vitendo vya baadhi ya viongozi wa Halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara, ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara zitumike kama ilivyopangwa.

Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa  Taifa wenye msingi imara.

“Barabara hizi zinachochea kilimo katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na jamii imara kiafya, kiakili na kiuchumi,”.

Kutokana na umuhimu wa mtandao wa barabara za Vijijini na Mijini, Mheshimiwa Simbachawene ameomba mgawanyo wa mapato ya Mfuko wa Barabara wa asilimia 70 kwa TANROADS  na asilimia 30 kwa Halmashauri uangaliwe upya, ambapo Waziri Mkuu ameridhia. 

Waziri Mkuu alisema “Naamini kwa kuanzishwa TARURA sasa hoja hii inajadilika, tumieni taratibu zilizopo ili maamuzi yaweze kufanyika,”.

Mtandao wa barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kilomita 108,942.2 ambao ni Zaidi ya nusu ya barabara za Kitaifa.
Read More

Saturday, July 1, 2017

MAJALIWA:HAKUNA MSAMAHA KWA WANAOUIBIA USHIRIKA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za fedha za Ushirika nchini.

“Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.

 Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai Mosi, 2017), katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD), iliyoadhimishwa kitaifa mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Amesema miongoni mwa changamoto zinazoukabili Ushirika nchini ni pamoja na wizi na ubadhilifu wa rasilimali za Ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na wanachama wasiokuwa waaminifu.

 Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine ni baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na kujifanyia mambo kwa maslahi yao binafsi.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya Ushirika kushamiri na kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao.

“Haikubaliki hata kidogo kuona sekta hii inayosadifu maisha ya Mwafrika hamnufaishi ipasavyo , hivyo naelekeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ihakikishe kuwa vyama vya Ushirika vinaendeshwa kisayansi na kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Pia amezielekeza Kamati za Ushauri za Mikoa na Wilaya nchini, ziingize agenda ya Maendeleo ya Ushirika kama moja ya agenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji. Pia wawe na takwimu za vyama vya Ushirika na Wanaushirika.

Hata hivyo Waziri Mkuu amezielekeza mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini zijiwekee malengo yanayopimika ya namna ya kuboresha sekta ya Ushirika.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameelekeza kwamba masuala yote yanayohusu Ushirika wa kilimo nchini lazima yaratibiwe na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Aidha, Waziri Mkuu amezielekeza Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Rais-TAMISEMI zifanye mapitio kubaini elimu na ujuzi katika ngazi zote za Ushirika kwa ajili ya kuwaandalia kozi za muda mfupi za kuongeza ujuzi au kubainisha aina ya watumishi wanaohitajika kwenye sekta hiyo.

Pia amewaagiza Maofisa Ushirika nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri uchanguzi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) na kuwaondoa wagombea wote waliowahi kuwa viongozi, ambao waliondolewa madarakani kutokana na ubadhilifu wa mali na fedha za Ushirika.

Awali, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alisema wizara itaendelea kusima na kuchukua hatua kwa viongozi wote wa vyama vya Ushirika watakaobainika kufuja mali na fedha za Ushirika.

Read More