Sunday, July 16, 2017

KUHITIMISHWA KWA AWAMU YA PILI YA UREJESHAJI HALI YA MIUNDOMBINU YA SERIKALI MKOANI KAGERA BAADA YA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI SEPTEMBA, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, kama ishara ya kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, kama ishara ya kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimshuhudia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, wakati wa  kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi, Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo,  (katikati) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya.

Read More

Saturday, July 15, 2017

WATANZANIA KUACHANA NA NGUO ZA MITUMBA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.

Pia amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo  jana (Jumamosi, Julai 15, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.

Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.

“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya  sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.

Pia Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi. 

Read More

WATANZANIA KUACHANA NA NGUO ZA MITUMBA-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akingalia mitambo ya kutengeneza  Nguo katika Kiwanda cha NIDA kilichopo Jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu  alifanya ziara katika kiwanda hicho Jumamosi 15 july 2017 kushoto anaye toa maelezo ni Mkurugenzi  Mkuu wa  Kiwanda cha kutengeneza  Nguo cha NIDA   Bwana  Muhammadhamza  Rafiki na kushoto  ni  Meneja Mkuu wa Kiwanda cha NIDA  Bwana   Muhammad  Waseem

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  katikati  akionyeshwa   Ubora wa Kanga zinazo tengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha NIDA wakati alipofanya ziara Jumamosi 15 july 2017 katika kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es salaam    wanao muonyesha  kulia ni  Mkurugenzi  Mkuu wa  Kiwanda cha kutengeneza  Nguo cha NIDA  Bwana  Muhammadhamza  Rafiki na kushoto  ni  Meneja Mkuu wa Kiwanda cha NIDA  Bwana   Muhammad  Waseem.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  katikati  akionyeshwa   Ubora wa Kanga zinazo tengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha NIDA wakati alipofanya ziara Jumamosi 15 july 2017 katika kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es salaam,kulia ni  Mkurugenzi  Mkuu wa  Kiwanda  cha NIDA  Bwana  Muhammadhamza  Rafiki na kushoto  ni  Meneja Mkuu  NIDA  Bwana   Muhammad  Waseem.



Read More

Thursday, July 13, 2017

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA NHC KWA UTENDAJ


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.

Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza  huduma karibu kwa wananchi wake.

 “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5.

“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.”

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.

Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.


Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME LINDI

* Asema changamoto ya kukatika umeme Mkoa wa Lindi kuwa historia

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara-Lindi.
                             
Amesema hayo leo (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo uliogharimu sh. bilioni 16 kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Lindi.

Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

“Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme, kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika.”

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema kuimarika kwa upatikanaji wa umeme kutawezesha safari ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema atahakikisha anapambana na watu wote watakaokwamisha jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuwahudumia wananchi.

Pia ameahidi kusimamia shughuli za maendeleo ya wananchi wote Tanzania bila ya kujali maeneo wanakotoka wala itikadi zao za kisiasa na kidini.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Nanganga, Nyangao, Mtama na Nyengedi alipowasilisi wilayani Lindi, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

 “Tunataka fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi zitumike ipasavyo na hatutakubali kuona mtu napewa fedha na kuzitumia atakavyo.”

Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi hao kuweka pembeni  itikadi zao za kisiasa na badala yake washirikiane kwa pamoja katika kufanya shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

“Rais Dkt. Magufuli amesema Watanzania kwa sasa hatuhitaji kufanya siasa, sasa ni kazi tu, hivyo tutumie muda wetu mwingi kwa kufanya kazi za maendeleo. Tupunguze muda wa kubishana hakuna tija watu wanataka maji, afya.”


Awali Mbunge wa jimbo la Mtama Mheshimiwa Nape Nnauye kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo aliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma mbalimbali kwenye jimbo hilo.
Read More

Wednesday, July 12, 2017

MBUNGE WA CHADEMA AWAOMBA WANANCHI WALIOMBEE TAIFA AMANI

MBUNGE viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu  ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

“Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele,  tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”

Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

Kwa pamoja wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWA RUANGWA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.


Read More

WAZIRI MKUU AKIWA MKOANI LINDI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017.

Read More

WAZIRI MKUU AKABIDHI ‘AMBULANCE’ MBILI RUANGWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa.

Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.

Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

 “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

Waziri Mkuu amesema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa  wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa.

 Kabla ya kukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya  akina  mama na ya  watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji huduma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.

“Tunatambua na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla, nasi tutayatumia magari haya kama ilivyokusudiwa.”

Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Dkt. Regan Rajuu amesema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo umeongezeka kutoka asilimia 80 Desemba, 2016 na kufikia asilimia 90 Juni 2017.

Pia Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyoanza kujengwa Desemba, 23, 2016 kwa michango ya Halmashauri, fedha za mfuko wa jimbo pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Emmanuel Sechawe alisema msingi wa kuanzisha shule hiyo ulitokana na uwepo wa wanafunzi 319 waliofaulu darasa la saba mwaka 2016 kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika shule zilizopo.

Mbali na kutembelea shule hiyo, pia Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gereza la wilaya ya Ruangwa, ambalo litakapokamilika litapunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Nachingwea.


Read More

MAJALIWA: HAKUNA KIJIJI TANZANIA KITAKACHOACHWA BILA YA UMEME

*Asema vilivyo mbali na gridi kufungwa sola


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

Amesema Serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Julai 11, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa aliyasema hayo katika mikutano aliyoifanya kwenye vijiji vya Chiapi, Nandanga, Mbecha na Luchelegwa, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Pia Waziri Mkuu amesema  mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.
Waziri Mkuu alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumiwa majumbani lakini pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati,shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Lindi Mhandisi, Johnson Mwigune  alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu mkandarasi aliyepangiwa katika vijiji hivyo atakuwa tayari ameanza kazi ya kusambaza umeme.
Read More

Tuesday, July 11, 2017

WAZIRI MKUU ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA MTO LUKULEDI

*Asema watu wengi wamekufa wakikatiza katika eneo hilo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa kilomita 30.45 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara na na  kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema ujenzi wa daraja hilo unatakaogharimu sh. bilioni 5.4 ni mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo hasa wa wilaya za Ruangwa na Masasi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana  katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo na huduma za kijamii.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumanne, Julai 11, 2017) alipotembelea mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo katika kijiji cha Nandanga alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

“Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba walipokuwa wakikatiza katika eneo hilo. Ujenzi wa daraja hili ni muhimu, watu wengi wa Ruangwa wanavuka kufuata matibabu katika hospitali ya Ndanda, wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda wanavuka kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa.”

Pia Waziri Mkuu amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa mkandarasi anayejenga daraja hilo ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kumaliza mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ndanda, Mheshimiwa Cecil Mwambe ameipongeza na kuishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendele0 na kubadilisha maisha yao.

Amesema mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni faraja kwa wananchi wa mikoa hiyo kwa kuwa eneo hilo ni makazi ya mamba, hivyo kukamilika kwake kutaokoa maisha ya watu pamoja na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vijiji vya Litama, Luchelegwa, Nandanga, Ipingo na Chiapi kuwa historia baada kuungwanishwa na mradi wa maji wa Mbwinji.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Litama, Chiapi, Nandanga, Luchelegwa alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza  Kampeni yake ya  kumtua mama ndoo, hivyo itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini, hususan ni ya vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400.

Ameitoa kauli hiyo baada ya wananchi wa vijiji hivyo kumueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao zikiwemo za maji, barabara, umeme, ambapo aliwahakikishia kwamba Serikali imeshaanza kuboresha huduma hizo.


Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua Zahanati  ya Nandanga ambayo imejengwa kwa fedha kutoka mfuko wa jimbo umegaharimu kiasi cha sh. milioni 73.47 na kuwahakikishia kwamba  Serikali itawapelekea  wataalam wa kutosha ili kuwahudumia.
Read More

HABARI PICHA : WAZIRI MKUU AKIWA KIJIJI CHA LIKWACHU MKOANI LINDI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017.
Wananchi wa kijiji cha Likwachu, Wilaya ya Ruangwa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipo ongea nao, wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. 


Read More

Monday, July 10, 2017

HAKUNA MGONJWA ATAKAYEKOSA DAWA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba na kwamba hakuna mgonjwa atakayekwenda kutibiwa katika hospitali, vituo vya afya au zahanati  bila ya kupatiwa dawa.

Ameyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Wilaya.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, alisema Serikali haitaki kusikia wananchi wanakwenda hospitali, Vituo vya afya au zahanati na kukosa dawa.

Alisema moja kati ya ajenda muhimu ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake, ambapo kila mwezi halmashauri zote nchini zinapelekewa fedha za ununuzi wa dawa.

“Serikali hii ya Rais Dkt. John Magufuli inatoa fedha za kununulia dawa kila mwezi katika halmashauri zote nchini. Sasa kama hapa Liwale kuna malalamiko ya wananchi kukosa dawa katika hospitali yetu, Mkuu wa Wilaya kafuatilie huko Halmashauri ili kujua wanapeleka wapi fedha za dawa.”

Katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 236 zimetengwa kwenye ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 iliongezeka kwa asilimia 50 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2015/2016.

Bw. Zambi alisema katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka 2016 hadi Februari 2017 mkoa wa Lindi ulipokea sh milioni 538 kwa ajili ya ununuzi wa dawa kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Hospitali ya mkoa ilipokea sh. milioni 195,328,186 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na pia ilitumia sh.  Milioni 127,171,700 toka fedha za uchangiaji kwa ununuzi wa dawa.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wa Halmashauri kwenda vijijini na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.

Pia amewaagiza Maofisa Kilimo wote kuhakikisha wanaacha kushinda maofisini na badala yake waende mashambani kwa ajili ya kuwaelimisha wakulima namna bora ya kulima kwa kufuata njia za kisasa ili kupata tija.

Kila ofisa kilimo awe na shamba lake ambalo litatumika kama darasa kwa wananchi
Read More

WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA WATAZILIPA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa wilaya.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa waaminifu.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.

Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa Tengeneza, ambapo amewataka Watumishi wa Umma Nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Amesema Watumishi wanawajibu wa kuwahudumia Wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema Watumishi wa Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi jambo litakaloondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi.

“Lazima Wananchi waone na wanufaike na kazi inayofanywa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa Watumishi kuwatumikia Wananchi popote walipo na si kukaa maofisini.”

Pia amewataka Watumishi hao kupanga mipango itakayoleta tija kwa Wananchi na si vinginevyo.
Read More

UFUTA KUUZWA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akutane na Bodi ya mazao mchanganyiko kwa ajili ya kuliondoa zao la ufuta na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Pia amewaagiza wakuu wa mikoa yote inayolima zao la ufuta kukutana na Dkt. Tizeba kwa ajili ya kupanga mfumo mzuri wa uuzaji katika msimu wa mwaka 2016/2017 wakati Serikali ikijipanga kuliingiza zao hilo katika mfumo wa stakabadhi ghalani.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017) wakati akisalimiana na wananchi katika vijiji vya Nangano, Kibutuka na Kiangara alipowasili katika wilaya ya Liwale kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Lindi.

Ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa jimbo la Liwale, Mheshimiwa Kuchauka pamoja na wananchi kuiomba Serikali iwasaidie kuboresha bei ya zao la ufuta ambayo imekuwa ikiyumba.

Waziri Mkuu amesema “tatizo lipo kwenye mfumo wa  uuzaji zao la ufuta, unauzwa kwa bei ya rejareja, wanunuzi wako huru. Serikali imemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuliondoa zao katika bodi ya mazao mchanganyiko na kuliingiza katika mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuboresha bei yake.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Justine Monko kuhakikisha anamaliza tatizo la maji katika vijiji vya Nangano,Kibutuka na Kiangara.

Amesema  Serikali imedhamiria kuondoa tatizo la maji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400. “Ndio maana Serikali imekuja na Kampeni inayosema mtue mama ndoo kichwani.”

Pia amemtaka Mhandisi wa Maji Bw. Andrew Kilembe kuandika barua ya kufuatilia fedha za maji sh. milioni 76 kwa ajili ya kijiji cha Kiangara walizopangiwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa Waziri wa Maji ili waweze kukamilisha uchimbaji wa kisima.
Read More

WAZIRI MKUU AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaeleza   wananchi wa Kijiji cha Kiangala  jinsi serekali ya awamu ya tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao   walijitokeza July 10, 2017  ili waweze kumueleza kero  zinazo wasumbua  Waziri  yupo Wilayani Liwale Mkoa wa lindi Kwaziara ya Kikazi ya siku Nne
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akihutubia umati wa wananchi wa  wilaya ya liwale waliojitokeza kuja kumsikliza  Michezo wa  wilaya ya Liwale July 10, 2017 Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa  wa LINDI.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na Mkewe Mery Majaliwa Wametembelea Hospitali  ya Wilaya ya Liwale July 10, 2017 Kuwazawadi  Watoto Mapacha wenye Siku Mbili  walio zaliwa katika Hospital ya  Liwale Waziri Mkuu yupo wilayani Liwale Mkoani Lindi kwa ziara ya Kikazi katika Mkoa  wa LINDI



Read More

Sunday, July 9, 2017

MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA AGAKHAN

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9, 2017.

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea shada la maua wakati akikaribishwa kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017.
  
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017.


 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani, katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee, Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo, Julai 9, 2017.


Read More

WAZIRI MKUU AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAFANIKIO

*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
                                                                                  
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka  kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa  madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.

Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.


Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa  upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo. 
Read More