Thursday, July 12, 2018

WAZIRI MKUU ATAKA MAAFISA UGANI WAWEZESHWE


*Awataka wasimamie mifumo rasmi ya ununuzi wa mazao

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ofisi za maafisa ugani zinapaswa kuwepo walipo wakulima, wafugaji na wavuvi na kwamba maafisa ugani katika ngazi zote lazima wawezeshwe na wasimamiwe kikamilifu.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Julai 12, 2018) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa maafisa kilimo, mifugo na uvuvi kutoka Tanzania Bara ulioanza leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma. Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki 570.

“Maafisa ugani katika ngazi zote lazima wawezeshwe na wasimamiwe kikamilifu kutekeleza majukumu yao. Wataalam wa Wizara washuke hadi ngazi ya mikoa na Halmashauri kusaidiana na waliopo kwenye ngazi hizo.

“Walioko ngazi ya mkoa washuke mara kwa mara hadi ngazi ya Halmashauri na ngazi ya Halmashauri ishuke na kushirikiana na maafisa ugani wa kata na vijiji kuelekeza wakulima, wafugaji na wavuvi kuhusu utaalam na maarifa yanayohitajika katika kuendeleza sekta hizi kibiashara,” amesema.

Amesema wakulima, wafugaji, na wavuvi hawana budi kupatiwa mbinu bora kuanzia hatua ya uzalishaji hadi kupata masoko ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia sahihi zenye tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Amesisitiza kwamba maafisa ugani ni lazima wawe na orodha sahihi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wote kuanzia ngazi ya kitongoji na aina ya mazao wanayoshughulikia, malengo ya uzalishaji na utekelezaji.

“Maafisa ugani wawe na takwimu sahihi za aina na kiasi cha mahitaji ya teknolojia na  pembejeo za uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi katika maeneo yao lakini pia wasaidie kuunganisha vikundi vya wakulima, wafugaji, wavuvi na kuunda ushirika imara ili kuendeleza juhudi za kufufua ushirika kama mkombozi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.”

“Ukiwa na ushirika imara hata kama unataka kuwapatia taarifa ya haraka kuhusu ongezeko la bei, au tarehe ya mnada inakuwa rahisi kwa sababu wana Mwenyekiti wao au Katibu wao na kupitia kwake, wote wanaweza wakaitishwa na kupewa taarifa kwa haraka,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka maafisa ugani waende wakasimamie mifumo rasmi ya ununuzi wa mazao ili kuwasaidia wakulima kupata bei nzuri za mazao yao.

“Hatutaki kusikia watu wanatumia mifumo isiyo rasmi kama chomachoma (kwenye ufuta), butura (kahawa huko Karagwe), katakichwa (kahawa Moshi), kangomba (korosho) na vishada (tumbaku). Nenda kapambane nao, wewe ni afisa wa Serikali na hupaswi kuacha wananchi wanateseka,” alisema.

“Nenda kahimize mfumo wa kuuza mazo kwa ushirika badala kuruhusu wanunuzi kwenda kwa mkulima mmojammoja. Pia mtusaidie kufafanua dhana ya Stakabadhi za mazao Ghalani kwamba siyo malipo ya papo kwa papo. Muwaeleze wakulima kwamba wanapeleka mazao pake wakati wakisubiria bei iwe nzuri, siyo kwamba wanakopwa,” amesisitiza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. Selemani Jafo alisema Aprili mwaka huu, Serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji wa agizo la kuwa na viwanda 100 kwa kila mkoa na kubaini kuwa umefikia 49.4 ndani ya miezi mitatu tu.

“Tarehe 20 Aprili, 2018, tulifanya kikao cha kwanza cha utekelezaji wa wa agizo la kila mkoa uhakikishe unajenga viwanda 100 vidogo na vya kati. Kwenye agizo hilo, tulilenga malighafi za viwanda hivyo zitokane na mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo. Agizo hilo lilitaka wakuu wa mikoa wawe wamelitekeleza kati ya Desemba 2017 na Desemba 2018; na kufikia Aprili 2018, viwanda 1,280 vilikuwa vimeshajengwa sawa na asilimia 49.4 ya lengo tulilojiwekea,” alisema.
Read More

TAASISI ZA DINI ZIWEKEZE KWENYE VIWANDA - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini wasibaki nyuma katika suala zima la kuwekeza kwenye viwanda ili waweze kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi wa viwanda. Nawaomba msiwe nyuma katika suala hili, tumieni fursa ya ardhi tuliyonayo hasa katika ujenzi wa viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo (Alhamisi, Julai 12, 2018) wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 52 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Mkutano huo wa siku mbili, umehudhuriwa na maaskofu zaidi ya 80, wenyeviti wa makanisa na wawakilishi wa vyama vishiriki.

Amesema uwepo wa viwanda hivyo utachangia ukuaji wa sekta ya kilimo na kuongeza ukuaji wa mnyonyoro wa thamani ya mazao. Akitoa mfano fursa zilizopo hivi sasa, Waziri Mkuu aliwaeleza Maaskofu hao kwamba bei ya ufuta kwa mwaka huu imepanda na kufikia sh. 3,100/- ikilinganishwa na sh. 1,400/- ambayo ilikuwa ni bei ya mwaka jana.

Ametumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa dini kwa kwa kubwa wanayofanya ya kukemea maovu kama vile ujangili, ukatili wa kijinsia na matumizi ya dawa za kulevya.

"Serikali inaheshimu mahubiri yenu sababu tunajua yana nguvu sana. Kupitia mahubiri yenu, watu wakimjua Mungu, watakuwa na hofu ya Mungu, kwa hiyo watu watakuwa waadilifu na maovu mengine yatapungua," amesema.

"Nitumie fursa hii kuwajulisha kwamba Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa wa nchi zilizosimamia vizuri mapambano dhidi ya dawa za kulevya barani Afrika. Kwa hiyo tumepewa heshima ya kuandaa mkutano mkubwa wa kimataifa utakaofanyika hapa nchini Septemba, mwaka huu."

Amesema mshikamano uliopo baina ya viongozi wa Serikali na viongozi wa dini hauna budi kuendelea. "Natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wajenge mshikamano wa pamoja na viongozi wa dini katika maeneo yao husika. Viongozi wa Kitaifa nasi, tutaunga mkono katika ngazi ya kitaifa," amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na maaskofu hao, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo alisema Jumuiya hiyo inaendelea kusisitiza suala la umoja na mshikamano wa Kitaifa.

“Suala la umoja wa kitaifa na amani ya nchi yetu ni masuala mtambuka; tena ni nguzo ya utaifa wetu. Tunashukuru jinsi Serikali inavyosimamia masuala haya kwa hekima na uthabiti. Tunaahidi kuwa tutaendelea kuliombea Taifa letu pamoja na viongozi wake ili mzidi kuilinda amani ya Taifa letu pamoja na watu wake.”

“Hata wakati inapotokea masuala haya yanapoguswa au kuumizwa, Kanisa limeendelea kuhimiza mara zote kutafuta ufumbuzi wake kwa njia ya mazungumzo,” amesema.
Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA MAAFISA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kilichofanyika kwenye  ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Julai 12, 2018.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Julai 12, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  katika mkutano wa Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Julai 12, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi baada ya kuhutubia  Mkutano wa Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Julai 12, 2018.  Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge.

Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCT JIJINI DODOMA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo  Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo baada ya kuhutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo na wapili kulia ni  Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Jacob Chimeledya.

Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania  (CCT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Jukuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  jijini Dodoma, Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo, na wapili kushoto ni Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu, Dkt. Jacob Chimeledya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo  Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo baada ya kuhutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo na wapili kulia ni  Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Jacob Chimeledya.

Read More

Wednesday, July 11, 2018

MAJALIWA AKUTANA NA WATALAAMU WA UTAFITI WA MAZAO YA KILIMO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watafiti  wa Mazao ya Kilimo  kutoka Kituo cha Utafiti  cha Mikocheni jijini Dar es salaam, Wakala wa Mbegu za Kilimo  (ASA) na Taasisi ya Utafiti  wa Kilimo Tanzania, kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Julai 11, 2018.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo  Tanzania, Japhet Justine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watafiti  wa Mazao ya Kilimo  kutoka Kituo cha Utafiti  cha Mikocheni jijini Dar es salaam, Wakala wa Mbegu za Kilimo  (ASA) na Taasisi ya Utafiti  wa Kilimo Tanzania, kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Julai 11, 2018.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo  Tanzania, Japhet Justine.


Read More

Saturday, July 7, 2018

WAZIRI MKUU: SERIKALI HAITANUNUA MADENI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina mpango wa kununua madeni yaliyosababishwa na mikopo ya kibenki kwenye vyama vikuu vya ushirika nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

“Serikali ya awamu ya tano hatuna biashara ya kununua madeni ya vyama vikuu, kulikuwa na tabia ya watu wa ushirika kukopa na hali ikiwa mbaya wanakimbilia Serikalini. Serikali hii hatuna biashara hiyo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema anazo taarifa kwamba Chama Kikuu cha mkoa wa Kagera (KCU) kimekopa fedha Benki ili kiweze kulipa deni la mwaka 2014. “Nimeambiwa KCU wamekopa fedha benki ili kulipa deni la mwaka 2014, hii inaingia akilini kweli? Mnakopa fedha kulipa deni la zamani, ni kwa nini msiwatafute waliosababisha deni na kuwachukulia hatua?,” alihoji.

“Ninyi mlikuwa watu sita ambao mlikubaliana kama viongozi, mlienda kukopa kuzidi uwezo mlionao. Leo hii ni kwa nini serikali ije kulipa wakati mmetumia ninyi?,” aliuliza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya tatno inasisitiza masuala ya ushirika kwa sababu imeamua kuwahudumia wananchi kuanzia ngazi ya chini kuanzia pembejeo, dawa hadi masoko.

“Tunataka tuondoe utaratibu wa chama kikuu kukopa fedha benki ili kikanunue mazao. Vyama vingi vimetengeneza hasara, leo hii vyama vikuu vina madeni. Hii ni kwa sababu mlikopa fedha benki wakati hata hamjui mna kilo ngapi ambazo zimevunwa.

“Fedha mnachukua nyingi na hata ikibaki hamrudishi benki. Riba anadaiwa mkulima kupitia kilo anazouza, deni anapelekewa mkulima na kuanza kukatwa kwa kila kilo. Hatutaki tena utaratibu huu. Kuanzia sasa, AMCO ndiyo itaratibu na kukusanya mazao ya kila mwanachama kwa sababu yenyewe inajua ina wanachama wangapi, wana ekari ngapi na wanatarajia kuvuna kilo ngapi,” amesema.

Amesema ili kuondokana na utaratibu wa vyama vikuu kukopa benki, Serikali imepiga marufuku utaratibu huo na badala yake wanunuzi wataenda kununua mazao kwenye vyama vya msingi kupitia minada na watatakiwa kuwa wameingiza fedha kwenye vyama vya msingi (AMCOS) ndani ya siku tatu.

“Tulishasema mwisho uwe ni msimu huu, yasijirudie tena haya mambo ya kukopa benki.  Mnunuzi akipata mnada, ndani ya siku tatu, anatakiwa awe amehamisha fedha kwenda kwenye akaunti ya AMCOS husika,” alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema mfumo wa ushirika bado unakabiliwa na changamoto ya upotoshaji na maewagiza maafisa ushirika wakasimamie suala hilo kwa kutoa taarifa sahihi kwa wakulima.

“Leo hii tunakabiliwa na changamoto kubwa kupitia uuzaji wa mazao kwa mfumo wa stakabadhi za Mazao Ghalani, Kuna watu wanapita wakipotosha kwamba serikali inawakopa wakulima mazao yao.”

“Nendeni mkawaelimishe wakulima kwamba mtu akipeleka mazao yake ghalani siyo kwamba anakuwa tayari ameuza, bali anayaweka pale na kujua ana kilo ngapi, amapewa risiti na kusubiri bei iwe nzuri wakati wanunuzi wakibishana. Hela ikilipwa, anapewa hela yote kulingana na mzigo wake,” alisema.

Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.”

Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI- UWANJA WA FURAHISHA MWANZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa TANESCO wakati alipotembelea banda lao katika maonyesho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa furahisha jijini Mwanza  Julai 7, 2018.  Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kahawa iliyotengwa katika madaraja mbalimbali wakati alipotembelea banda la Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Kagera katika Maonyesho ya Siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018.  Kushoto ni Meneja wa Mauzo ya Nje wa Chama hicho, Joseph Katabalo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba  na mafuta yanayotokana na mbegu za pamba wakati alipotembelea banda la Ushirika wa wilaya ya Chato katika maonyesho ya Ushirika yaliyofanyika kitaifa  kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Ushirika nchini, Bibi Renata Mwageni (kushoto) Tuzo ya  Rais John Pombe Magufuli iliyotolewa na Wanaushirika nchini  ili kutambua mchango wa Rais  katika kuendeleza sekta ya ushirika na kuinua uchumi wa wananchi wa Tanzani ya 2018 . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye  uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Juni 7, 2018.  Wapili kushotoi ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab  Telack.

Msanii wa kikundi cha sanaa cha Buyegi, John Riziki akicheza ngoma ya nyoka katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Msanii wa kikundi cha sanaa cha Buyegi, John Riziki akicheza ngoma ya nyoka katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.  Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati alipomkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia katika Maadhimisho ya siku ya Ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa  Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya ushirika duniani yaliyofanyika kitaifa  kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, Julai 7, 2018.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika Maadhimisho ya  Siku ya Ushirika duniani  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Julai 7, 2018.

Read More

HIMIZENI WAKULIMA WAKULIMA KUFUNGUA AKAUNTI BENKI - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maafisa ushirika wawahimize wakulima wafungue akaunti benki ili kuepuka wizi wa fedha za vyama vya msingi (AMCOS).

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

Amesema kumekuwa na wizi wa kupanga unaofanywa na watu wachache wasio waaminifu. "Kuna AMCOS walienda kuchukua sh. milioni 50 benki, wakaja nazo kwenye pikipiki, wakati wanafungua mlango na boksi la hela liko hapo chini, ikaja pikipiki nyingine na watu wawili wakabeba boksi na kupotea nalo."

"Sasa ujiulize hao waliokuja na pikipiki ya pili walijuaje kama wale wa mbele walikuwa na fedha? Mtu anaporwa hela yote hiyo hata mchubuko hana, hiyo siyo sahihi, hizo ni hela za Chama cha msingi tunapaswa kuzilinda," alisisitiza.

Aliwataka maafisa ushirika wakasimamie jukumu hilo ili fedha ikilipwa na mnunuzi baada ya mnada, meneja wa AMCOS anaenda benki anaingiza hela kwenye akaunti za wanachama wake mara moja.

"Hii itaondoa shaka ya wanachama kuibiwa fedha zao, itaondoa hatari ya maafisa wa vyama vya msingi kutembea na fedha nyingi za Chama, na kuepusha wizi usio wa lazima. Hivi sasa wakulima wengi wana simu za mkononi. Ni rahisi kwao kupata ujumbe mfupi wa maandishi kwamba kuna fedha imetumwa katika akaunti yako," alisema. 

Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwepo wa mfumo jumuishi wa huduma za kifedha (financial inclusion) ambao umesaidia kuwepo kwa mawakala wa kibenki hadi vijijini.

"Mkulima akitaka kuichukua fedha yake hana haja ya kusafiri hadi wilayani, sasa hivi anapata huduma hizo pale alipo kupitia kwa mawakala au kwenye mtandao wa simu," alisema.


Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni:“Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.”

Read More

WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

Amesema kuna maafisa ushirika ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiriwa TAMISEMI na wengine wako chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

"Afisa Ushirika wa Wilaya yuko mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI, Mrajis Msaidizi wa Mkoa yuko Wizarani. Serikali ni moja, kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa," alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma yao maafisa ushirika wa wilaya na wahakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri zao.

"Msimpe kazi ya kufundisha Afisa Ushirika kwa sababu hakuna mtu mwingine. Afisa Ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapokutana kwenye Baraza, mpeni nafasi Afisa Ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu."

Alisema changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika waliopewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo.

Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa elimu ya kutosha ya ushirika miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika; kuporomoka kwa imani ya ushirika miongoni mwa jamii na kwa baadhi ya wanachama kutokana na vyama vya ushirika kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake.

Nyingine ni uwepo wa madeni makubwa katika baadhi ya vyama vya ushirika nchini na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara kuwa na mtazamo hasi kwenye ushirika kwa malengo ya upotoshaji kwa maslahi yao binafsi.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Mkuu aliitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika ihakikishe kwamba usimamizi, udhibiti,uhamasishaji wa vyama vya ushirika unafanyika kikamilifu na kwa wakati kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 na kanuni zake za mwaka 2015.

Pia aliiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika iwasaidie wanaushirika katika mchakato wa urasimishaji wa mali zao na utoaji wa hati miliki za kimila za kumiliki ardhi kwa wakulima wadogo wadogo vijijini ili waweze kuzitumia kama dhamana ya kukopa mikopo katika taasisi za kifedha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.

Aidha alizitaka mamlaka zote zinazohusika na maendeleo ya sekta ya ushirika nchini zijiwekee malengo yanayotekelezeka ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya ushirika na kujipima kila inapohitajika.

Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni:“Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.”
Read More

WAZIRI MKUU: AMCOS ZIAJIRI WATUMISHI WENYE SIFA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) waajiri mameneja wenye sifa ili kuepuka ubadhirifu ndani ya vyama hivyo.

Ametoa rai hiyo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.

Amesema watumishi ambao wamepata nafasi za juu katika AMCOS ni lazima wawe na elimu ya ushirika kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). "Utumishi katika hivi vyama mara nyingi unaenda na uaminifu. Kama Chama kikiona kina mtu wanayemwamini, ni lazima kimpeleke chuoni ili apate sifa stahiki," alisema.

Alisema anataka kuona huduma za ushirika kwa wananchi zikiwianishwa na kile wanachofundishwa wataalamu kwenye vyuo vya elimu ya juu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemwagiza Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi ahakikishe wanafunzi wanaopangiwa kufanya mafunzo kwa vitendo (field training) wanasambazwa kwenye AMCOS mbalimbali nchini.

"Wanafunzi wanaoenda field training kutoka kwenye Chuo chako, wapangiwe kwenda katika AMCOS. Hapa nchini tuna zaidi ya AMCOS 4,000 na wanafunzi wako 1,000 kwa hiyo kila mmoja akisimamia AMCOS nne, nne, watakuwa wamesaidia sana kupeleka elimu ya ushirika huko vijijini.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba na Naibu wake Dkt. Mary Mwanjelwa. Wengine ni Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula, Wakuu wa Mikoa ya Kagera, Mara, Simiyu, Wakuu wa Wilaya na viongozi wa CCM.

Siku ya Ushirika Duniani huadhimishwa Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni: “Ushirika kwa ulaji wa uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma.”

Read More

Wednesday, July 4, 2018

MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kitabu cha Mwongozo wa Taratibu za Kujenga Kiwanda Nchini Tanzania baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Edwin Rutaberuka. 

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe  ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.  Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) wakitazama trekta lenye uwezo wa kupanda mbegu mbalimbali lili tengenezwa na Kampuni ya CRMATEC ya  Arusha baada ya Waziri Mkuu, kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salam. Julai 4, 2018.

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA MABANDA BAADA YA KUFUNGUA MAONYESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kutoka kwenye Banda la Fursa sawa kwa Wote (EOTF) kwenye Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Sarah Lutahya (kushoto) kuhusu bidhaa mbalimbali zilizofumwa kwa mikono wakati alipotembelea banda la mkoa wa Kagera katika  Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Miku Investment, Bw. Paul Lema  (kushoto) kuhusu vipodozi vya Shine and Lovely vinavyotengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabanda mabalimbali kwenye Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam, Julai 4, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara  Tanzania (Tan Trade), Edwin Rutaberuka (kushoto)  wakati akitoka kwenye Banda la Zanzibar baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha pambo lenye rangi za bendera ya taifa lililobuniwa na kutengenezwa nchini Kenya wakati alipotembelea banda la Kenya katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. 


Read More

PROF.KAMUZORA AWAASA WATUMISHI WA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI KUZINGATIA UBORA NA UFANISI KATIKA UTENDAJI.


Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora moja ya mtambo unaotumika kuchapisha nyaraka za Serikali unaoitwa Original Heidelberg alipotembelea katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Julai4, 2018 Jijini Dodoma.
Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akikabidhi vitabu vya maandiko yanayoeleza juu ya Idara hiyo kuwa Wakala kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alipotembelea Idara ya Mpigachapa tarehe 4 Julai, 2018 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo na Watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) alipofanya ziara ofisini hapo kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.

Mhudumu Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Jackson Ainea akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati alipotembelea katika Ofisi hizo Jijini Dodoam Julai 4, 2018.
Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Severin Kapinga akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo Pichani) wakati wa kikao chake na Watumishi wa Idara hiyo alipowatembelea Julai 4, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali alipowatembelea Julai4, 2018.
NA.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora amewataka watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali kuzingatia ubora na ufanisi katika uchapaji wa nyaraka za Serikali.
Wito huo ameutoa hii leo Julai 4, 2018 alipotembelea katika Idara hiyo ili kuangalia namna wanavyoendesha shughuli zao za kila siku.
Prof.Kamuzora alieleza umuhimu wa kuendelea kuwa na ubunifu katika utendaji kwa kuzingatia unyeti wa nyaraka za Serikali wanazochapisha na kuongeza wigo wa uzalishaji kwa kuwa na machapisho yenye ubora na viwango vya kuendana na soko ili kuongeza mapato ya nchi.
“Niwaombe watumishi wote mzingatie uzalishaji wenye tija kwa kuchapisha nyaraka zenye ubora na ufanisi utakao saidia kuongeza mapato ya nchi hivyo ni vyema kuwa na ubunifu wa hali ya juu,”alisema Prof.Kamuzora
Pamoja na maagizo hayo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wa nchi yao kwa kuwa waadilifu katika kuitumikia kwa uaminifu bila kutoa siri za Serikali.
“Ni lazima mzingatie maadili ya utumishi wa umma kwani Idara hii ni nyeti inayoshughulika na uchapaji wa nyaraka za Serikali hivyo ni lazima kuwa na namna bora ya uendeshaji wa shughuli zenu kwa kuaminiana na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwingine,”alisisitiza Prof.Kamuzora
Kwa upande wake Kaimu Mpigachapa Mkuu  wa Serikali Bw.John Kaswalala alimpongeza Katibu Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Idara hiyo, na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo aliyotoa kwa lengo la kuboresha utendaji wa Idara ili kuwa na uzalishaji wenye tija na kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia.
“Kipekee nikushukuru kwa kuona umuhimu wa kuitembelea idara hii na kujua mazingira na changamoto za kiutendaji, nimefarijika kwa hatua hii hivyo tumeyazingatia maagizo yote tutayatekeleza ili kuendana na soko na mabadiliko ya kiteknolojia nchini,”alisisitiza Kaswalala.


Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA SABASABA, AKABIDHI MATREKTA 500


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi  matrekta 560 kwa wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini. 

Amekabidhi matrekta hayo leo (Jumatano, Juni 4, 2018) wakati akifungua Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. 

Waziri Mkuu amesema uchumi wa viwanda  ni pamoja  na kilimo, hivyo  ameagiza matrekta hayo yaende vijijini kutekeleza shughuli za kilimo ili kuwaongezea tija wakulima.

Wateja wa kwanza waliokabidhiwa matrekta hayo Ursus yaliyounganishwa nchini ni Wizara ya kilimo (500), Jeshi la Magereza (50) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) (10).

Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya kilimo ili itoe  mchango unaotegemewa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya viwanda. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua kitabu kinachotoa muongozo na taratibu za kufuata wakati wadau mbalimbali wanapotaka kujenga viwanda kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa. 

Waziri Mkuu mesema lengo la mwongozo huo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wa viwanda nchi nzima.

“Kijitabu hiki kidogo kina maelezo muhimu kuhusu taratibu za kufuata unapotaka kujenga kiwanda, kuanzia kutenga maeneo ya kuvutia uwekezaji na hata kuendesha makongamano ya biashara,”. 

Kadhalika, Waziri Mkuu, amewashuru na kuwapongeza washiriki wote wakiwemo wa sekta binafsi kwa ushiriki wao. Amesema kwamba Serikali inatambua kuwa sekta binafsi ndio muhimili mkuu wa kujenga uchumi wa viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu amegawa tuzo kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo, ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeibuka mshindi wa jumla.

Baada ya kufungua maonesho hayo, Waziri Mkuu alitembelea mambanda mbalimbali yakiwemo ya Zanzibar, Viwanda na Biashara, Asasi, Azam, TPA na EOTF.
Read More