Wednesday, July 4, 2018

PROF.KAMUZORA AWAASA WATUMISHI WA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI KUZINGATIA UBORA NA UFANISI KATIKA UTENDAJI.


Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora moja ya mtambo unaotumika kuchapisha nyaraka za Serikali unaoitwa Original Heidelberg alipotembelea katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Julai4, 2018 Jijini Dodoma.
Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akikabidhi vitabu vya maandiko yanayoeleza juu ya Idara hiyo kuwa Wakala kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alipotembelea Idara ya Mpigachapa tarehe 4 Julai, 2018 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo na Watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) alipofanya ziara ofisini hapo kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.

Mhudumu Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Jackson Ainea akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati alipotembelea katika Ofisi hizo Jijini Dodoam Julai 4, 2018.
Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Severin Kapinga akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo Pichani) wakati wa kikao chake na Watumishi wa Idara hiyo alipowatembelea Julai 4, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali alipowatembelea Julai4, 2018.
NA.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora amewataka watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali kuzingatia ubora na ufanisi katika uchapaji wa nyaraka za Serikali.
Wito huo ameutoa hii leo Julai 4, 2018 alipotembelea katika Idara hiyo ili kuangalia namna wanavyoendesha shughuli zao za kila siku.
Prof.Kamuzora alieleza umuhimu wa kuendelea kuwa na ubunifu katika utendaji kwa kuzingatia unyeti wa nyaraka za Serikali wanazochapisha na kuongeza wigo wa uzalishaji kwa kuwa na machapisho yenye ubora na viwango vya kuendana na soko ili kuongeza mapato ya nchi.
“Niwaombe watumishi wote mzingatie uzalishaji wenye tija kwa kuchapisha nyaraka zenye ubora na ufanisi utakao saidia kuongeza mapato ya nchi hivyo ni vyema kuwa na ubunifu wa hali ya juu,”alisema Prof.Kamuzora
Pamoja na maagizo hayo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wa nchi yao kwa kuwa waadilifu katika kuitumikia kwa uaminifu bila kutoa siri za Serikali.
“Ni lazima mzingatie maadili ya utumishi wa umma kwani Idara hii ni nyeti inayoshughulika na uchapaji wa nyaraka za Serikali hivyo ni lazima kuwa na namna bora ya uendeshaji wa shughuli zenu kwa kuaminiana na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwingine,”alisisitiza Prof.Kamuzora
Kwa upande wake Kaimu Mpigachapa Mkuu  wa Serikali Bw.John Kaswalala alimpongeza Katibu Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Idara hiyo, na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo aliyotoa kwa lengo la kuboresha utendaji wa Idara ili kuwa na uzalishaji wenye tija na kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia.
“Kipekee nikushukuru kwa kuona umuhimu wa kuitembelea idara hii na kujua mazingira na changamoto za kiutendaji, nimefarijika kwa hatua hii hivyo tumeyazingatia maagizo yote tutayatekeleza ili kuendana na soko na mabadiliko ya kiteknolojia nchini,”alisisitiza Kaswalala.



EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.