*Yadaiwa wazazi
Kahama wanatozwa sh. 20,000 kwa kaya
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna
michango yoyote itakayokusanywa kutoka kwa wazazi kwa ajili ya shule kama haina
kibali cha Mkurugenzi wa Halmashuri.
“Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe
Magufuli alishapiga marufuku michango ya aina hii na akatangaza mpango wa
elimumsingi bila malipo. Sasa hivi zinaletwa zaidi ya sh. bilioni 20 kila mwezi
kwa ajii ya kuboresha elimu ya msingi katika kila wilaya.”
Waziri Mkuu ametoa katazo hilo
jana (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati
akizungumza na maelfu
ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Kahama, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Kahama, Bw.
Jumanne Kishimba ambaye alisema kuna michango inatozwa bila kibali chochote na
kwamba kila kaya inatakiwa ilipe sh. 20,000. “Michango hii itolewe kwa kibali
ina iangalie uwezo wa familia kiuchumi,” alisema.
Akitoa mfano, Mbunge hiyo alisema kuna familia ina
madebe matatu tu ya mahindi ukiitoza hiyo hela, manake wauze mahindi yao yote
ndiyo walete ya michango ma hiyo wabaki na njaa kwa mwaka mzima. Ni vema
michango hiyo izingatie kipato halisi cha kaya,” alisema,
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu aliwaeleza wananchi hao juhudi mbalimbali ambazo Serikali imezichukua ili
kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma za maji, umeme, elimu na afya.
Alisema ameridhishwa na ujenzi wa viwanda unaoendelea
kwenye mkoa wa Shinyanga na kukiri kuwa ameguswa kuona kuna uzalishaji mkubwa
wa mafuta ya kula yanayotokana na mazao ya mbegu kama pamba na alizeti wakati
kuna watu wanaagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
“Nimetembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya
pamba cha Kahama Oil Mills, na mwenye kiwanda ameniambia kuwa miaka yote huwa anafanya
kazi kwa miezi mitatu tu lakini mwaka huu ana uhakika wa kufanya kazi kwa miezi
tisa, kutokana na jinsi ambavyo wakulima wameitikia wito wa kufufua zao la
pamba,” alisema.
“Jana pia nilitembelea kiwanda cha JIELONG
ambacho kiko kwenye Manispaa ya Shinyanga. Na kwenyewe nimeona uzalishaji
mkubwa wa mafuta ya kula ambao sijapata kuona,” alisema Waziri Mkuu.
Mapema, Waziri
Mkuu alizindua kituo cha afya cha Mwendakulima ambacho kilianza kujengwa mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2016 kwa ufadhili wa
kampuni ya kuchimba madini ya ACACIA kupitia mpango wake wa Corporate Social Responsibility.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.