Wednesday, July 4, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA MABANDA BAADA YA KUFUNGUA MAONYESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kutoka kwenye Banda la Fursa sawa kwa Wote (EOTF) kwenye Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Sarah Lutahya (kushoto) kuhusu bidhaa mbalimbali zilizofumwa kwa mikono wakati alipotembelea banda la mkoa wa Kagera katika  Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Miku Investment, Bw. Paul Lema  (kushoto) kuhusu vipodozi vya Shine and Lovely vinavyotengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabanda mabalimbali kwenye Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam, Julai 4, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara  Tanzania (Tan Trade), Edwin Rutaberuka (kushoto)  wakati akitoka kwenye Banda la Zanzibar baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha pambo lenye rangi za bendera ya taifa lililobuniwa na kutengenezwa nchini Kenya wakati alipotembelea banda la Kenya katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.