Wednesday, July 4, 2018

WAZIRI MKUU ATEMBELEA SABASABA, AKABIDHI MATREKTA 500


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi  matrekta 560 kwa wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini. 

Amekabidhi matrekta hayo leo (Jumatano, Juni 4, 2018) wakati akifungua Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. 

Waziri Mkuu amesema uchumi wa viwanda  ni pamoja  na kilimo, hivyo  ameagiza matrekta hayo yaende vijijini kutekeleza shughuli za kilimo ili kuwaongezea tija wakulima.

Wateja wa kwanza waliokabidhiwa matrekta hayo Ursus yaliyounganishwa nchini ni Wizara ya kilimo (500), Jeshi la Magereza (50) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) (10).

Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya kilimo ili itoe  mchango unaotegemewa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya viwanda. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua kitabu kinachotoa muongozo na taratibu za kufuata wakati wadau mbalimbali wanapotaka kujenga viwanda kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa. 

Waziri Mkuu mesema lengo la mwongozo huo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wa viwanda nchi nzima.

“Kijitabu hiki kidogo kina maelezo muhimu kuhusu taratibu za kufuata unapotaka kujenga kiwanda, kuanzia kutenga maeneo ya kuvutia uwekezaji na hata kuendesha makongamano ya biashara,”. 

Kadhalika, Waziri Mkuu, amewashuru na kuwapongeza washiriki wote wakiwemo wa sekta binafsi kwa ushiriki wao. Amesema kwamba Serikali inatambua kuwa sekta binafsi ndio muhimili mkuu wa kujenga uchumi wa viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu amegawa tuzo kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo, ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeibuka mshindi wa jumla.

Baada ya kufungua maonesho hayo, Waziri Mkuu alitembelea mambanda mbalimbali yakiwemo ya Zanzibar, Viwanda na Biashara, Asasi, Azam, TPA na EOTF.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.