WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lina
jukumu kubwa la kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuwafikia watu wa
kipato cha chini.
Amesema
ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli
inahimiza uchumi wa viwanda, hivyo sekta ya nyumba ina mchango mkubwa
sana katika kuchochea ukuaji wa viwanda.
Ameyasema
hayo leo (Jumamosi, Juni 30,2018) wakati akizindua mradi wa Singidani
Commecial Complex, mjini Singida. Jengo hilo la biashara na ofisi
limejengwa na NHC kwa ajili ya kupangisha wafanyabiashara na taasisi
mbalimbali.
Waziri
Mkuu amesema sekta ya nyumba ni mtambuka kwa kuwa huchochea ukuaji wa
uchumi, kutoa ajira na kukuza uwekezaji wa viwanda vya vifaa vya ujenzi
kama saruji, mabati, nondo, marumaru na vinginevyo, ambavyo vinafungua
fursa kubwa ya ukuaji wa viwanda.
Hivyo,
Waziri Mkuu amesema wadau mbalimbali wanapaswa kuitazama sekta ya
nyumba kama sekta mtambuka katika kuleta maendeleo endelevu ya uchumi na
jamii kwa ujumla.
“Napenda
kutoa pongezi kwa Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga jengo hili
zuri na la kisasa kabisa hapa mjini Singida. Vilevile, jengo hili
limeboresha na kupendezesha mandhari ya mji wa Singida kwa kiwango
kikubwa kabisa,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema amefurahi kusikia jengo hilo limesanifiwa na ujenzi wake
kusimamiwa na Watanzania wenyewe, wakandarasi washauri wakiwa ni NHC
wenyewe na kwamba Watanzania zaidi ya 600 walipata ajira wakati wa
ujenzi.
Awali,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi alisema mradi wa jengo
hilo la ofisi na biashara la Singidani lililogharimu sh. bilioni 3.4
ulianza Januari 26, 2015 na kukamilika Februari 17, 2018 na linatarajia
kuliingizia shirika pango ya sh. milioni 420 kwa mwaka. Tayari asilimia
50 ya jengo hilo limepangishwa.
Mkurugenzi
huyo alisema mbali na mradi huo wa Singidani, pia shirika limeendelea
kukua na kuimarika katika utendaji wake ambapo thamani ya mali zote
imeongozeka kutoka sh. trilioni 1.7 mwaka 2011 mpaka kufikia sh.
trilioni 4.8 mwaka 2018.
Bw.
Maagi alisema mapato ya shirika yamekua kutoka sh. bilioni 40 kwa mwaka
2011 hadi kufikia sh. bilioni 154 mwaka 2018.” Pia shirika linalipa
gawio la Serikali kila mwaka na gawio hilo limekua kutoka sh. milioni
250 mwaka 2011 hadi sh. bilioni 1.2 kwa mwaka 2018,”
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, wabunge wa
mkoa wa Singida, viongozi wa dini na maafisa wa Serikali.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.