Friday, June 8, 2018

KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MPANGO WA SERIKALI KUHAMIA DODOMA CHATEMBELEA ENEO LILILOTENGWA KWA AJILI YA MJI WA SERIKALI.

Makamu Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Joseph Kiraiya (watatu kutoka kushoto) akieleza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo linalotarajiwa kujenga Mji wa Serikali Juni 7, 2018 Ihumwa Dodoma.

Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiweka nguzo ya umeme katika eneo la Ihumwa ambalo limetengwa kwa ajili ya mji wa serikali Dodoma.

Afisa Mipango Miji Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw.William Alfayo akiwaonesha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Mji wa Serikali kwa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea eneo hilo Juni 7, 2018.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakiangalia maeneo mbalimbali yaliyotengwa kulingana na ramani ya Mji mpya wa Serikali Ihuma Dodoma.

Eneo la Ihumwa ambapo Mji wa kiserikali unatarajia kujengwa hapo Jijini Dodoma.

Katibu wa Kikosi kazi cha kitaifa cha Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi kutoka TANROADS walipotembelea kukagua eneo hilo la Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.