Friday, June 8, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA OFISI ZA MPIGA CHAPA WA SERIKALI JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mitambo ya kwanza ya Mpiga  Chapa wa Serikali uitwao  Original Heidelberg wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Bw. Mohammed  S. Mohammed (kulia) ambaye ni Mtalaam na mwendeshaji  mkongwe wa mitambo ya uchapaji kuhusu jarada lililochapwa na mtambo uitwao Original Heidelberg wenye umri wa zaidi ya miaka 100 wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kuhusu mtambo unaochapa majarada ya serikali kutoka kwa Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, Bw. John Kaswalala (kushoto) wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Der es salaam, Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri . Kulia ni mwendeshaji wa mtambo huo, Dismas Shayo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akikagua moja ya karatasi zenye nembo na maadishi yalisioonekana kwa macho ya kawaida  kwenye  Kitengo cha Digitali wakati  alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018.  Katikati ni Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, John Kaswalala na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Ali Machupa.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.