Wednesday, April 25, 2018

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZIKO YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaleo (Jumatano, Aprili, 25, 2018) ameshiriki maziko ya aliyekuwa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege Mwakasege yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma.

Bw. Mwakasege ambaye alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016 akitokea Ofisi ya Rais-TAMISEMI amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema kifo hicho kimeiachia pengo kubwa  kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na familia.

“Natumia fursa hii kutoa pole kwa wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu ameacha pengo ndani ya familia, hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili pengo hilo.”

Marehemu Bw. Mwakasege ambaye alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na Kelvin Mwakasege.

Maziko hayo pia yamehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi, Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Read More

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakiweka shada la  maua kwenye kaburi la mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma, Aprili 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege, nyumbani kwa marehemu eneo la Kikuyu mjini Dodoma Aprili 25, 2018.

Read More

MAJALIWA AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kwa matibabu, Aprili 25, 2018.

Read More

Tuesday, April 24, 2018

NIMERIDHISHWA NA MAADHALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akitazama onesho lahalaiki, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr Florens Turuka, naMkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.
Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja  wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.


Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja  wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki  ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.

“Nimeridhika na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.”
Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.



Read More

WAZIRI MHAGAMA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUCHUKUA HATUA KWA VYAMA VINAVYOKIUKA SHERIA NA MIONGOZO ILIYOPO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari juu ya Ufafanuzi wa Hoja za ofisi yake zilizoainishwa katika Ripoti ya  Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 Bungeni Dodoma.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo, Kwa Mawaziri walipokutana kutoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dodoma Aprili 23, 2018.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Na.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.
Ametoa kauli hiyo leo (Aprili 23, 2018) alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana na  waandishi wa habari Bungeni Dodoma.
Waziri Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.
“Namtaka Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri Mhagama
Aidha amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache mara moja kwa mujibu wa sheria.
Waziri Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi
Pamoja na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista ya mali za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.
“Msajili wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kuwa na regista ya mali zake ndani ya wiki tatu kuanzia leo kwani kukosa daftari la mali za kudumu ni kinyume na kifungu Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya mwaka 1992.”alisisitiza Waziri.
Sambamba na hilo Waziri alimtaka Msajili wa Vyama vya siasa kuhakikisha vyama vyote  vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili kuondokana na mapungufu ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama vitatu kati ya tisa vina nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.
“Msajili wa vyama ahakikishe vyama vya siasa vinatekeleza miongozo yote kihasibu pamoja na kanuni za fedha, ambazo zinaelekeza nyaraka ziwe na viambatisho sahihi kwani ripoti ilibainisha vyama vitatu vilikuwa na malipo yenye nyaraka pungufu zenye thamani ya shilingi 735,978,559 ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa uhalali wa malipo hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.
AWALI:
Kifungu cha 14(1)(a) na (b)(i) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kinaelekeza kuwa, kila chama cha siasa kinapaswa kutunza taarifa za mapato na matumizi, ikiwamo taarifa za mali zake. Vile vile, kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, taarifa ya hesabu zake zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja taarifa ya mali zake.
Hivyo, Kifungu hicho kinampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa hesabu za kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Katika mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2017, CAG amefanya ukaguzi wa hesabu za Vyama vya Siasa kumi ikiwemo; CCM, CHADEMA, NLD, TLP, Demokrasia Makini (MAKINI), TLP, DP, SAU, AFP, CCK na ADC kati ya vyama vya siasa kumi na tisa vyenye usajili wa kudumu. Vyama vya Siasa tisa (9) havikuwasilisha hesabu zake kwake kwa wakati kwa ajili ya ukaguzi, hivyo hakukaguliwa.








Read More

Monday, April 23, 2018

BUNGENI LEO 23.04.2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) akiteta na Naibu Waziri , Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Bungeni mjini Dodoma, Aprili23, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Bungeni mjini Dodoma  Aprili 23, 2018.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akijibu swali  bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018.

Read More

SPIKA EALA AIPONGEZA TANZANIA KWA MAENDELEO

SPIKA wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dkt. Martin Ngoga ameishukuru na kuipongeza Serikari ya Tanzania kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa reli kwa sababu inaleta manufaa hata kwa nchi jirani.

"Miradi hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa kwa kasi si kwamba inachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, bali hata wa nchi nyingi za jirani kwa kuwa nazo zitanufaika na miradi hiyo kwani si nchi zote zina bandari".

Dkt. Ngoga ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 23, 2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Bungeni mjini Dodoma. 

Amesema tayari wamejadili ripoti iliyotokana na ziara iliyofanywa na wabunge hao katika upande wa korido ya kuishi na korido ya kaskazini ambapo wametoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na baraza la mawaziri.
"Tayari tumeshajadili miswada miwili inayohusu Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na  mswada wa Takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  ya mwaka 2017."
Pia Spika huyo amesema wamefurahia uwepo wao nchini, ambapo mbali na shughuli zao za kibunge pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wameshiriki kampeni ya kukijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1,000 kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema amefarijika na uamuzi wa Bunge la EALA kufanya vikao vyake katika nchi wanachama kwa sababu unatoa fursa ya kujua mazingira ya nchi hizo pamoja na maendeleo yake.

Amesema nchi wanachama wanamatumaini makubwa na bunge hilo katika kuimarisha na kuboresha maendeleo ya mataifa yao,  hivyo amewatakia mjadala mwema.

Katika hata nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wabunge hao na marafiki zao kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanja, utalii, kilimo na madini.

Kwa mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) vinafanyika Dodoma katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa ulipo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vilianza Aprili 17, 2018 na vinatarajiwa kumalizika Aprili 29, 2018.
Read More

MAJALIWA AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe.  Martin Ngoga, Bungeni mjini Dodoma Aprili 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katikia picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Martin Ngoga (watatu kushoto) baada ya mazungumzo, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. Wengine pichani ni  Wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, kutoka kushoto  ni Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki,  Mhe.Martin Ngoga kabla ya mazungumzo yao, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA WABUNGE WA AFRIKA YA MASHARIKI WANAOIWAKILISHA TANZANIA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge wa Bunge la  Afrika ya Mashariki wanaoiwakilisha  Tanzania, Ofisini kwake mjini Dodoma Aprili 23, 2018.  Kutoka kushoto ni Josephine Lemoyan,  Happiness Lugiko, Mhandisi Habibu Mnyaa, Mariam Ussi Yahya, Alhaj Adam Kimbisa, Fancy Nkuhi na Dkt. Abdullah Hasnuu Makame. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge wa Bunge la  Afrika ya Mashariki wanaoiwakilisha  Tanzania, Ofisini kwake mjini Dodoma Aprili 23, 2018.  Kutoka kushoto ni Josephine Lemoyan,  Happiness Lugiko, Mhandisi Habibu Mnyaa, Mariam Ussi Yahya, Alhaj Adam Kimbisa, Fancy Nkuhi na Dkt. Abdullah Hasnuu Makame. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki wanaoiwakilisha Tanzania baada ya kuzungumza nao, Ofisini kwake mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. Kutoka kushoto ni Mhandisi Habibu Mnyaa, Josephine Lemoyan, Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Alhaj Adam Kimbisa,  Mariam Ussi Yahya, Happiness Lugiko na  Fancy Nkuhi.







Read More

Saturday, April 21, 2018

UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI UMEIMARIKA-MAJALIWAWAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.

Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota  mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.

Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mradi huo mkubwa na baada ya kukamilika utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, hivyo amewataka viongozi wa NFRA wahakikishe kwamba hakuna mahindi yatayoharibika katika maghala yao.

”Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha NFRA inakuwa na uwezo wa kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya dharula lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bila vikwazo”.

Hata hivyp, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakuu wa Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanatimiza wajibu wao ili mradi ukamilike kwa wakati.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bibi Vumilia Zikankuba alisema mradi huo unatekelezwa katika maeneo manane ya Kanda za Wakala huo ambayo ni Dodoma (Dodoma), Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga (Shinyanga), Babati (Manyara).

Bibi Vumilia alisema katika Kanda ya Dodoma wanajenga vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na kufanya kanda hiyo kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,000 kutoka uwezo wa sasa wa tani 39,000.

Alisema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

“Utekelezaji wa mikataba kati ya NFRA na wakandarasi ulianza Desemba 2017 ambapo muda wa utekelezaji ni miezi 18 tangu tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji wa mikataba ya wakandarasi, hivyo kabla ya 2020 utakuwa umekamilika”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira  na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama.

Wengine ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na  Ajira, Anthon Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na
Balozi wa Poland nchini Tanzania, Balozi Krzysztof Buzalski.

Read More

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MJINI DODOMA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski wakati alipowasili kwenye viwanja vya magahla ya Wakala wa Hifadhi yaTaifa ya Chakula chino (NFRA) kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala  na vihenge vya kisasa, eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba , kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na kulia ni Mjumbe wa bodi ya kampuni ya Freerum ya Poland, Bw. Piotr Wielesik.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na balozi wa Poland nchini, Mhe Krzysztof Buzalski wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala  na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. 

 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wabunge na Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliopozungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.


Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai akizungumza Katika sherehe  ya uwekaji jiwe la msingi la maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018. Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala  na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala  na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzystof Buzalski na kulia Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye sherehe ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na balozi wa Poland nchini, Mhe Krzysztof Buzalski baada ya  kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala  na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba , kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bilinith Mahenge.

Read More

Friday, April 20, 2018

BUNGENI LEO 20.04.2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Wenyeulemavu, Antony Mavundebungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.

 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akijadili jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Wenyeulemavu, Antony Mavunde, Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa kitu na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2018, kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo.

Read More

BUNGENI LEO 19.04.2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2018.

 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia  Muungano na Mazingira, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi  Isack Kamwelwe, bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Nyasa,  Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Naibu Waziri wa  Viwanda, Biashara na Uwekezaji (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum, Zaynab Vullu kwenye viwanja via Bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

Read More

Thursday, April 19, 2018

MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepushe na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabondeni  kwa kuwa jambo hilo linafanywa kwa maslahi ya wananchi wenyewe.

Amesema wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na mali zao kila yanapotokea mafuriko, hivyo ni vizuri kwa viongozi wakiwemo wabunge washirikiane na Serikali kuwahamasisha wakazi wote wa mabondeni wahame.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Aprili  19, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Temeke, Bw. Abdallah Mtolea katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

 “Mara nyingi Serikali imekuwa ikiwataka wakazi ya maeneo ya mabondeni kuhama  ila suala hilo limekuwa likikwamishwa na masuala ya kisiasa. “Wabunge ni mashahidi jambo hili linapoamuliwa, zinaingizwa siasa.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wananchi walioathiriwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko zikiwemo familia za watu 12 waliofariki mkoani Dar es Salaam.

Katika swali lake, Bw Mtolea alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.

Mapema akijibu swali la Mbunge wa Nyang’hwale , Bw. Hussein Nassoro Waziri Mkuu alisema suala la kurejesha miundombinu iliyoharibika linashughulikiwa na kamati za maafa za mikoa na wilaya ambazo kwa sasa zinafanya tathmini ili kujua kiwango cha uharibifu na hatua gani zichukuliwe.

Bw. Nassoro alitaka kujua Serikali imejipangaje katika kurejesha miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito wa wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali ya biashara na chakula. Kuhusu mazao ya biashara amesema Serikali itawasaidia kutafuta masoko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bi. Aida Khenani (Viti Maalumu), aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuandaa masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima.

Read More

UKAGUZI BANDARINI HAULENGI KUWABAGUA WAZANZIBARI - WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ukaguzi unaofanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa wasafiri wanaokwenda Zanzibar, hauna lengo la kuwabagua bali ni kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi.

“Hatulengi kuzuia biashara za wafanyabiashara ndogondogo, bali tunaimarisha ukaguzi ili kuzuia wasafirishaji wa dawa za kulevya, wasambazaji na wauzaji,” amesema. 

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Aprili 19, 2018) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Bw. Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya kuwapunguzia makali wafanyabiashara wanaotoka Zanzibar.

Waziri Mkuu amesema: “Wanaofanya ukaguzi pale bandarini siyo watu wa TRA peke yao kama Mheshimiwa Jaku alivyosema, bali tukumbuke kuwa Tanzania imeingia katika vita ya dawa za kulevya, kwa hiyo tunaimarisha ulinzi wa mipaka yetu.”

“Tanzania inapambana na matumizi ya dawa za kulevya, kwa hiyo ukaguzi huu umelenga kuzuia watumiaji, wasambazaji na wasafirishaji wa dawa hizo. Upekuzi huu umelenga kupunguza hili tatizo, umelenga abiria wote na siyo Wazanzibari peke yao,” amesisitiza.

Amesema Serikali inaendelea na mipango ya kutafuta mitambo ya kisasa ya kukagua mizigo ya wasafiri wanaotumia bandari za Tanzania bara.

Mapema, akiuliza swali lake, Mhe. Jaku alisema: “Kilio cha wabunge wengi wanaotoka Zanzibar hapa Bungeni ni bandari ya Dar es Salaam kutoza kodi wafanyabiashara wadogo wanaosafirisha TV au vyerehani. Ni lini utakaa nao au kufanya ziara ya kushtukiza ili ujionee hali halisi?”
Read More

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WANUNUZI WA PAMBA NCHINI NA WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chama Wanunuzi wa Zao la Pamba Tanzania pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Morogoro, Manyara, Mwanza, Singida, Simiyu, Shinyanga na Tabora, Ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chama Wanunuzi wa Zao la Pamba Tanzania pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Morogoro, Manyara, Mwanza, Singida, Simiyu, Shinyanga na Tabora, Ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2018. 



Read More

BUNGENI DODOMA LEO TAREHE 19.04.2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  akizungumza na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, bungeni  mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza, bungeni Mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2018.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda (kulia)  kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 19, 2018. Wengine pichani ni watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani.

Read More