Tuesday, June 25, 2019

BUNGENI LEO 25.06.2019

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akijibu  hoja za Wabunge kuhusu Bajeti ya Serikali, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Anne Kilango, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Naibu wake, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) baada ya Waziri wa Fedha na Naibu wake kujibu hoja za wabunge kuhusu Bajeti ya Serikali, Bungeni jijini Dodoma, Juni 25, 2019.

Read More

SERIKALI YA KENYA YAMKANA JAGUAR

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Kenya imesema kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar si kauli ya Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Juni 25, 2019) wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kauli iliyotolewa na mbunge huyo ya kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania waondoke nchini Kenya ndani ya saa 24.

Amesema baada ya mbunge huyo kutoa kauli hiyo, Serikali ilianza kulifanyiakazi jambo hilo ambapo ilimuita Balozi wa Kenya nchini Tanzania ili kujua kama huo ni msimamo wa Serikali yao ama la, ambapo balozi huyo alimesema ile si kauli ya Serikali ya Kenya wala wananchi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mbali na kuwasiliana na Balozi huyo, pia Serikali imewasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya ili afuatilie kuhusu kauli ya Mbunge huyo, hivyo amewataka Watanzania waendelee kushirikiana na Wakenya.

“Si kauli nzuri na kauli hii iliyotolewa na mtu mmoja linajenga chuki baina ya mtu na mtu, nchi na nchi na tayari Serikali ya Kenya inalifanyia kazi suala hili na imetuomba Watanzania tuendelee kuwa wavumilivu.”

Waziri Mkuu amesema tamko lile linaweza kuibua chuki na vurugu miongoni mwa nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki na tayari Wabunge wa Bunge Afrika Mashariki wanaoendelea na kikao cha Bunge hilo jijini Arusha wamepinga na kulaani kauli hiyo.
Wamesema hawatoa nafasi kwa mtu yeyote kuvuruga nchi hizo.

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania popote walipo waendelee kuishi vizuri na Wakenya kwa kuwa wao hawana chuki na Watanzania bali ni mtu binafsi. Pia amewatahadharisha wananchi wa Afrika Mashariki wawe makini na kauli zao ili kuepusha vurugu.

 (mwisho)
Read More

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KITAIFA YATAKAYOFANYIKA JIJINI TANGA



Tanzania ikiwa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya kwa lengo la kuikumbusha jamii juu ya tatizo kubwa lilipo katika jamii yetu juu ya Biashara na Matumizi ya Dawa za hizo.

Kitaifa Maadhimisho haya kwa mwaka huu yatafanyika jijini Tanga siku ya Jumatano tarehe 26 mwezi Juni, 2019 katika viwanja vya Tangamano na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa George H. Mkuchika (Mb).

Kauli mbiu ya Kimataifa ya maadhimisho haya kwa mwaka huu inasema Waathirika wa Dawa za Kulevya Wana Haki ya Kupata Huduma za Afya. Kwa kuzingatia Kauli mbiu hii inakumbusha kuwa mapambano dhidi ya Tatizo la Dawa za Kulevya yanahitaji mikakati mtambuka na jumuishi ikiwemo suala la tiba kwa waathirika. Ni muhimu kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya kupata tiba stahiki na zilizothibitishwa kisayansi (evidence based practices) ili kuweza kupunguza madhara ya dawa hizo kwa waraibu na jamii inayowazunguka. 

Baada ya tiba hizo, huduma endelevu za Stadi za Kazi pamoja na Ushauri Nasaha kuzingatiwa ili kuwasaidia waathirika wasirudi kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, mkakati huu unaenda sambamba na mkakati wa utoaji wa elimu kwa vijana ili wasiingie kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya pamoja na Udhibiti wa wafanyabiashara wa Dawa hizo.

Maadhimisho haya ni fursa kwa umma wa Watanzania kwa vile  Tatizo la Dawa za Kulevya linaathiri nchi yetu katika nyanja za kiafya, kijamii, kiuchumi pamoja na kutishia ulinzi na usalama wa nchi yetu.  Katika maadhimisho haya Watanzania  wataweza kupata elimu na kukumbushwa kuwa matumizi na biashara ya dawa za kulevya yana athari kubwa kwa mtumiaji, kwa jamii na kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.

Tatizo la dawa za kulevya husababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja na kuchochea kuenea kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI, virusi vya homa ya ini aina ya B na C, Kifua Kikuu, magonjwa ya akili, pamoja na usugu wa tiba ya kifua kikuu na UKIMWI. Aidha, baadhi ya dawa za kulevya husababisha matatizo ya uzazi ikiwemo upungufu wa nguvu za kiume, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa kwa watoto wenye matatizo ya akili pamoja na kuenea kwa kansa mbalimbali kama vile kansa ya koo, mapafu na mara nyingine husababisha vifo ghafla vya  kutokana na dozi kuwa kubwa “overdose”. 

 Aidha Serikali imeendelea kusimamia utoaji tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo, na kufanikiwa kuongeza idadi ya waathirika wa dawa za kulevya katika vituo vya tiba kutoka wagonjwa 2,400 mwaka 2015 hadi wagonjwa 7000 mwaka 2018. Hali hii imeasaidia kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa waraibu wa dawa za kulevya wanaojidunga kutoka 35% mwaka 2015 hadi 18.5%.

Pia, Serikali inamtaka kila mwananchi kwa nafasi yake katika jamii kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa endapo kutabainika kuwepo kwa matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Pamoja na hilo Serikali inatoa wito kwa viongozi wa dini kulikemea suala la matumizi ya dawa za kulevya misikitikini na makanisani. Sambamba na hilo, Serikali inawakumbusha  Viongozi wa dini zote kuwa  wana nafasi kubwa katika jamii ya  kuhakikisha watoto,  vijana pamoja na jamii yote kwa ujumla wanapata mafunzo ya kuwajenga kiroho, kimwili na kisaikolojia ili wawe na tabia njema katika jamii na mfano wa kuigwa kwa matendo mema.

Serikali inaikumbusha jamii kushiriki kikamilifu katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya, kujenga malezi bora kwa watoto katika ngazi ya familia, na kuwapeleka kwenye matibabu watumiaji wa dawa za kulevya. Vilevile, Serikali inasisitiza Jamii kuzitambua, kuzienzi na kuziendeleza tamaduni zetu nzuri ili kuinusuru Wananchi wote hasa vijana ambao ndo nguvu kazi ya taifa na matumizi ya dawa za kulevya.

Read More

Monday, June 24, 2019

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MKUU WA WILAYA YA CHEMBA SIMON ODUNGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiakimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, aliyelazwa, katika Hospitali ya Mkoa, jijini DodomaJuni 24.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiakimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, aliyelazwa, katika Hospitali ya Mkoa, jijini DodomaJuni 24.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliyofika kupata huduma, katika Hospitali ya Mkoa, jijini DodomaJuni 24.2019, baada ya kumjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, aliyelazwa hospitalini hapo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliyofika kupata huduma, katika Hospitali ya Mkoa, jijini DodomaJuni 24.2019, baada ya kumjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, aliyelazwa hospitalini hapo.


Read More

WAZIRI MKUU AFUNGUA TAWI LA BENKI YA UKEZAJI TANZANIA (TIB )

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, wakati  wa ufunguzi wa Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati akifungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua akaunti katika Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki, katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019. Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja Elizabeth Mkondya.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihifadhi fedha baada ya kufungua akaunti katika Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki ya Benki hiyo, iliyopo katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019. Kushoto ni mtoa huduma wa fedha, Nasra Namkudai.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua Ofisi na Tawi la Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), katika jengo la PSSSF jijini DodomaJuni 24.2019 


Read More

SERIKALI YAITAKA SEKTA YA FEDHA IWE IMARA

*Ihakikishe huduma zake zinawafikia wananchi wa mijini na vijijini
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema sekta ya fedha inapaswa kuwa imara na kuhakikisha huduma zake zinawafikia wananchi wengi katika maeneo ya mijini na vijijini ili iweze kutoa mchango unaokusudiwa katika kuinua uchumi wa nchi na ustawi wa jamii. 

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Juni 24, 2019) wakati alipofungua Ofisi Ndogo na Tawi la Benki ya Biashara ya TIB jijini Dodoma. Amesema ukuaji wa sekta ya huduma za kifedha ni muhimu sana katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Waziri Mkuu amesema benki ndicho chombo kikuu cha kutolea huduma za kifedha kwa wananchi, hivyo, benki zinatakiwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, kuwahamasisha na kuwaelimisha umuhimu wa kutumia benki. 

“Wananchi nao pia wana wajibu wa kuzitumia benki hizi kwa kutunza akiba zao na kukopa wakati wanapohitaji kuwekeza kwa malengo yaliyokusudiwa. Suala la msingi ni kuwa mnapokopa mkumbuke pia kurejesha kulingana na makubaliano.”

“Sifurahishwi sana na takwimu zinazoonesha kwamba ni asilimia 16.7 tu ya Watanzania wote ndiyo wanaopata huduma za kifedha kupitia mifumo halali ya kibenki, huku asilimia 48.6 wakipata huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu na asilimia 35 ya waliosalia kutopata kabisa huduma rasmi za kibenki.”

Waziri amesema hali hiyo haikubaliki kwenye nchi kama Tanzania ambayo inakabiliana na ujenzi wa uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ametoa wito kuwa benki zote ziendelee kubuni mikakati na mbinu zitakazowawezesha Watanzania wengi zaidi kupata huduma rasmi za kibenki tena kwa gharama nafuu ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua kutoka kwenye umaskini. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema tozo za mabenki kwa wateja bado ni kubwa na haziwasaidii wananchi wa kawaida, kwa hiyo, zipunguzwe. “Riba kwa wakopaji nazo ziko juu sana ukilinganisha na mfumuko wa bei, pia nazo zipunguzwe.”

Kuhusu changamoto ya riba kubwa inayotozwa kwa mikopo ya benki, Mheshimiwa Majaliwa amesema tayari Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania imefanikiwa kupunguza riba ya hati fungani za Serikali, pamoja na ile inayotozwa kwa mabenki yanayokopa Benki Kuu. Moja ya lengo la kufanya hivyo ni kutaka riba za mabenki zipungue. 

“Naomba mabenki yaunge mkono jitihada hizo za Serikali kwa kupunguza riba zinazotozwa hasa kwenye mikopo ya watu binafsi na biashara ndogo ndogo kwani hawa wakipata unafuu wataweza kukuza biashara zao na hivyo kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji.”

Akizungumzia suala la baadhi ya benki kuwa na  tawi moja au mawili jijini Dar-es-Salaam tu, Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imeshaiagiza Benki Kuu ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kuzitathimini upya benki za aina hiyo.

“Leo narudia tena kuiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuzisimamia benki zetu ili zifungue matawi yake hadi vijijini waliko wenye uhitaji.! Kwanini? benki nyingi zimejikita katika kutafuta faida pekee bila kuwekeza kwa faida ya nchi yetu? Hadi sasa tuna benki ambazo zimekuwa siku zote na tawi moja tu tena liko Dar-es-Salaam. Benki Kuu ya Tanzania isisite kuchukua hatua za kisheria kurekebisha hali hiyo.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya TIB, Frank Nyabundege amesema kwa kipindi cha miaka minne benki hiyo imeweza kukuza mtaji kutoka sh. bilioni 206 wakati inagawanywa mwaka 2015 mpaka kufikia sh. bilioni 409 mwishoni mwa mwaka 2018 sawa na ukuajia wa aslimia 98.5.

Mkurugenzi huyo amesema mbali na kufanikiwa katika kukuza mtaji, pia benki hiyo imeweza kukuza amana za wateja kutoka sh. bilioni 110 mwaka 2015 mpaka sh. bilioni 338 mwezi Disemba 2018, sawa na ukuaji wa asilimia 207.

Mafanikio mengine yabenki ya TIB katika kipindi cha miaka minne ni pamoja na kuanza kutengeza faida angalau ya sh. bilioni 1.3 mwaka jana (2018), kutoa mchango stahiki katika Mfuko Mkuu wa Serikali kiasi cha sh. milioni 250.”

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa benki hiyo imetoa mikopo na dhamana kwa taasisi za umma hadi kufikia shilingi bilioni 224.35 kwa kipindi kilichoishia Machi 2019, kulipa kodi Serikalini kiasi cha sh. bilioni 19.2 tangu benki ianzishwe na kutoa mikopo kwenye sekta ya viwanda jumla ya sh. bilioni 65.12.

(mwisho)

Read More

Sunday, June 23, 2019

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA DKT. BADRIYA, MKE WA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR

 Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa Dkt. Badriya Abubakar Gurnah, mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi  katika  mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam  Juni 23, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Dkt. Badriya Abubakar  Gurnah, mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam Juni 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi ambaye amefiwa na Mkewe, Dkt. Badriya Abubakar Gurnah wakati alipokwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam Juni 23, 2019 kutoa pole kwa familia. Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na ndugu na jamaa wa marehemu Dkt.  Badriya Abdallah Gurnah, mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar, Abdallah Juma Mabodi  katika mazishi  ya  Daktari huyo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Upanga jijini Dar es salaam, Juni 23, 2019.


Read More

Saturday, June 22, 2019

KATIBU MKUU MASSAWE AHIMIZA USHIRIKIANO KWA WATUMISHI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na Watumishi wa ofisi hiyo (hawapo pichani) alipokutana nao kujadili utendaji kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi hiyo, Bw. Peter Kalonga akieleza jambo kwa watumishi wa Ofisi hiyo (hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi hiyo wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (hayupo pichani) walipokutana Jijini Dodoma.
Mmoja wa Watumishi wa Ofisi hiyo Bi. Grace Kigula akielezea baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji walipokutana na Katibu Mkuu wa ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) akifafanua jambo kwa wadau (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo la kujadiliana pamoja na kusikiliza maoni, ushauri na changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2019. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura na kulia ni Mwanasheria kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba.
Mmoja wa wadau kutoka Kampuni ya RECO Engineering Ltd, Bw. Abubakar Mukadam akichangia mada kuhusu masuala ya vibali vya kazi walipokutana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe alipokutana nao kusikiliza maoni na changamoto wazokabiliana nazo katika utendaji kazi wao.
Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura (kushoto) akifafanua jambo kuhusu masuala ya vyama vya wafanyakazi wakati wa mkutano huo uliofanyika ghorofa la PSSSF, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.
Mwanasheria kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzan Ndomba akielezea kuhusu baadhi ya Sheria zinazowaongoza Waajiri nchini wakati wa kikao na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (katikati) alipokutana na wadau mbalimbali wa ofisi hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Johanes Majura

Baadhi ya wadau wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.
Sehemu ya ya wadau wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe (haupo pichani) walipokutana kujadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira, Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na masuala ya Vyama vya Wafanyakazi.



Read More

MAJALIWA ASHIRIKI BONANZA NA BENKI YA NMB NA WABUNGE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua timu ya Mpira wa kikapu  ya Benki ya NMB ambayo ilipambana na timu ya Bunge katika mechi la Bonanza la Benki ya NMB na Bunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha  mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya  Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha  mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya  Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha  mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya  Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha  mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya  Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019.

Read More

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAASWA KUZINGATIA MAADILI


NA MWANDISHI WETU
Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu Waaswa Kuzingatia Maadili ya  Utumishi  wa Umma katika kutekeleza majukumu yao ili kuiwezesha Serikali  kufikia malengo  ya Serikali ya Awamu ya Tano  kutoa huduma Bora kwa wananchi.

Akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo leo (22 Juni, 2019) Jijini Dodoma , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza uwajibikaji, uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika utumishi wa umma ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

“Kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma katika Ofisi yetu kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kuwa jambo hilo halikubaliki kamwe kwani vitendo hivyo vinazorotesha juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo “ Alisisitiza Mhe. Mhagama

Akifafanua amesema kuwa mafunzo yaliyotolewa  na Serikali  kwa watumishi hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma yalijikita katika mada mbalimbali ikiwemo  Rushwa mahala pa kazi , haki na wajibu wa watumishi wa umma.

Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali  inaweka mkazo katika kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale wanapohitaji huduma hivyo ni wajibu wa kila mtumshi katika Ofisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wale wote wanaofika katika Ofisi hiyo na katika Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

Kwa upande wake Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi amesema kuwa watumishi wa Ofisi hiyo watazingatia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mhagama ili kuongeza tija katika kutoa huduma  kwa wananchi.

Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma  kwa kushiriki mafunzo ya kuwakumbusha taratibu na kanuni za utumishi wa umma, mafunzo kwa watumishi wanaotarajia kustaafu hivi karibuni.

Ofisi ya Waziri Mkuu imeadhimisha wiki ya Utumishi ya Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali na kuhitimisha kwa mafunzo ya siku moja kwa watumishi wote yakilenga kuwakumbusha wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili hatimaye kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu inasema;  "Uhusiano kati ya uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji; kujenga utamaduni wa utawala bora., Matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi"
=MWISHO=
Read More

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAASWA KUZINGATIA MAADILI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akihutubia watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea ambayo iliambatana na mafunzo kuhusu masuala ya utumishi wa umma kwa watumishi hao.Mkutano huo ulifanyika Juni 22, 2019 Ukumbi wa mikutano wa PSSSF Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na watumsihi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma inayoendelea.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma inayoendelea.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akikata keki kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, keki aliyoandaliwa na watumishi wa ofisi yake kumpongeza wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma kwa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimlisha keki Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini cha ofisi hiyo Bw. Agustino Tendwa kwa niaba ya watumishi wa ofisi yake, wakati wa mkutano wa kuhitimisha mafunzo ya masuala ya utumishi wa umma Juni 22, 2019.


Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Mazoea Mwera akifafanua jambo wakati mkutano huo.

Read More

WATUMISHI NI MUHIMU KUSHIRIKI MICHEZO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 22, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.

Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu. 

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.

(mwisho)
Read More