Friday, February 21, 2020

MAJALIWA: HAKUNA MTANZANIA ATAKAYEKOSA KITAMBULISHO CHA TAIFA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kila raia wa Tanzania aliyeomba kitambulisho cha Taifa atakipata, hivyo amewataka waombaji ambao bado hawajapata waendelee kuwa na subira.

Amesema waombaji hao watapatiwa vitambulisho hivyo baada ya wahusika kupitia maombi yao na kujiridhisha kwamba wote ni raia wa Tanzania na Serikali inafanya hivyo ili kulinda usalama wa nchi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 21, 2020) wakati akizungumza katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma. Waziri Mkuu ni mlezi wa CCM wa mkoa wa Kigoma.

“Watu wote wanaotaka kuingia nchini ni lazima wafuate taratibu zilizowekwa pia Uhamiaji na vyombo vingine vya dola vijiridhishe kwamba hata hao wanaopitia njia sahihi kama kweli ni watu wema.”

Waziri Mkuu amesema katika mikoa ya mipakani ina tatizo la watu kuingia bila ya kufuata taratibu, hivyo kabla ya kutoa kitambulisho ni lazima Serikali ijiridhishe kama kweli aliyeomba ni raia. “Pale wahusika watakapohitaji kujiridhisha waombaji watoe ushirikiano.”

Waziri Mkuu amesema lazima zoezi hilo lifanyike vizuri na wataharakisha ili wananchi waweze kupata vitambulisho. Tayari Serikali imeshaongeza vifaa na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Akizungumzia kuhusu taarifa baadhi ya wananchi wakuombwa rushwa ili waweze kupata vitambulisho, Waziri Mkuu amewataka watu wote walioombwa rushwa wakaripoti katika vyombo vya sheria. Amesema marufuku mtu kuomba wala kupokea rushwa.

Waziri Mkuu amesema kuwa suala la kuimarisha ulinzi na usalama katika mikoa ya mipakani ukiwemo na mkoa wa Kigoma ni jambo muhimu kwa sababu bila ya kuimarisha ulinzi mikoa hiyo haitakweza kupata maendeleo. Amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM washirikiane na wabunge na madiwani waliopo sasa na wasiwavuruge wawaache watekeleze majukumu yao hadi pale muda wao utakapomalizika.

Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM wajiepushe na suala la ukabila na udini katika kuteua mtu wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na badala yake wateue mtu ambaye anauzika ndani na nje ya chama.

(mwisho)

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA MKOA WA KIGOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga  (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa CCM wa  Mkoa wa Kigoma,  Amandus Nzamba  (wa pili kushoto) na Mjumbe wa  Halmashauri Kuu  ya Taifa ya CCM, Kirumbe Ngenda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Februari  21, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Februari 21, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Februari 21, 2020. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa Halmashuri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Kigoma wakati alipozungumza katika mkutano huo, Februari 21, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya  CCM ya Mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kigoma, Februari 21, 2020.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu  ya CCM ya  Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu na  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Februari21, 2020.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu  ya CCM ya  Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu na  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Februari21, 2020.


Read More

MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IJUMAA MJINI KIGOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushiriki katika Swala ya Ijumaa Kwenye Msikiti wa Mujahidina  eneo Buzebazeba mjini Kigoma, Februari 21, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi  baada ya kushiriki Swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Mujahidina, eneo la Buzebazeba mjini Kigoma, Februari  21, 2020.


Read More

KATIBU MKUU MWALUKO AZITAKA SEKTA ZISHIRIKIANE KUKABILI MAAFA.


Na. OWM, ZANZIBAR

“Tatizo la athari za maafa yanayotokana na majanga ya asili linahitaji ushiriki wa sekta zote ili kukabiliana nalo ipasavyo, katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)” Mwaluko.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko wakati alipokuwa anafungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye yeye ni mwenyekiti.

 Mwaluko amesema nchi zote za SADC zina uzoefu wa masuala ya maafa, hivyo ni matarajio yake kuwa kazi waliyopewa ya kuandaa nyaraka kwa ajili ya mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya maafa utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Februari 2020,  uweze kufikia malengo yake.

Katika kikao hicho, Makatibu Wakuu wataandaa nyaraka itakayo ainisha mikakati na programu za kukabiliana na maafa na mpango unaobainisha namna nchi za SADC zilivyojipanga kukabiliana na maafa yanapotokea katika ukanda huo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo  alieleza kuwa athari za maafa zikiwemo vifo, uharibifu wa mali na miundombinu zimezikumba takribani nchi zote za SADC. Hivyo amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kushirikiana kwa pamoja kuandaa mikakati ya menejimenti ya maafa.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi amewaeleza  wajumbe wa kikao hicho kuwa nchi za SADC zimelipa umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na athari za maafa na hilo linadhihirishwa na ushiriki wa nchi 15 kati ya 16 wanachama wa SADC katika mkutano huo.

Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Madinat AL Bahir iliyopo Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar unatarajiwa kuhitimishwa kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri tarehe 21 Februari 2020 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

“Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
MWISHO.


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akifafanua umuhimu wa ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa, wakati akifungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo yeye ni mwenyekiti wa kikao hicho, leo tarehe 18 Februari 2020, Zanzibar.

Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo akifafanua umuhimu wa Nchi  za SADC kuwa na mikakati ya kukabili maafa yanayo zikabili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifafanua namna ya nchi za SADC zinavyoathirika na maafa ya asili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar


Baadhi ya makatibu wakuu kutoka Tanzania, wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18, Februari, 2020, Zanzibar, (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,anayeshughulikia Mifugo,  Profesa Olesante Ole Gabriel (kulia kwake), Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Faraij Mnyepe,  na Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar.


Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe,(kulia), Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Zanzibar , Makame Khatibu Makame na Naibu Mkurugenzi wa Kamisheni hiyo, Muhidin Ali Muhidin
Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
Makatibu Wakuu na maafisa waandamizi wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, Februari, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”


Read More

MAJALIWA: UZALISHAJI MBEGU ZA MICHIKICHI UNARIDHISHA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika uzalishaji wa mbegu bora za zao la michikichiki katika kituo cha Tari Kihinga mkoani Kigoma.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Frbruari 21, 2020) alipotembelea kituo cha utafiti wa zao la michikichi cha Tari Kihinga kilichopo wilayani Kigoma alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Kigoma.

Akiwa kituoni hapo, Waziri Mkuu alipokea taarifa ya utafiti juu ya uendelezaji wa zao la michikichi uliliyofanywa na TARI kuanzia mwaka 2018, ambapo hadi kufikia Februari 15, 2020 taasisi hiyo ilikuwa imezalisha mbegu 1,525,017 ambazo zinaweza kupandwa katika shamba lenye ukubwa wa ekari 30,500.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kulipa kipaumbele zao la michikichi kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, hivyo ufufuaji zao hilo utaliwezesha Taifa kuzalisha mafuta ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya ndani na ziada itakayobakia itauzwa nje ya nchi.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi hasa vijana kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa wingi kwa kuwa upo uhakika wa kupata mbegu bora na pia zao hilo litawakwamua kiuchumi na kuwaondolea umasikini wa kipato.

Pia, amewaagiza Maofisa Ugani kuwafuata wakulima katika maeneo yao na kuwaelekeza namna ya kulima zao hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji mashamba, matumizi bora ya pembejeo ili waweze kulima kisasa na kujiongezea tija.

Baada kutembelea kituo hicho Waziri Mkuu alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre uliopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watumishi wa umma watenge muda ya kusikiliza kero za wananchi.

“Watumishi mnatakiwa kwenda kwa wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi. …hamuendi na kama mngekuwa mnaenda kusingekuwepo na mabango kwani kitendo cha kuwepo mabango ni ishara tosha kwamba hamuendi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imepeleka fedha nyingi mkoani Kigoma za kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh bilioni 4.6 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, ambapo Manispaa ya Kigoma Ujiji inapata sh milioni 50 kila mwezi hivyo hakuna sababu ya wananchi kukosa dawa.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa kujenga vituo vya afya karibu na makazi ya wananchi zikiwemo za afya ili kuwapunguzia kutembea umbali mrefu hadi hospitali za wilaya au mkoa.

Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Baraza lake la Madiwani wahakikishe wanasimamia vizuri matumizi ya fedha mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kugharamia miradi ya maendeleo.

 Waziri Mkuu alikemea tabia ya baadhi ya wananchi katika maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma kudai fidia kwenye maeneo  hata ya mapori na kukwamisha baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya kanda, aliwataka wabadilike.

Awali, Waziri Mkuu alishiriki swala ya Ijumaa katika msikiti wa Mujahidina uliopo eneo la Buzebazeba mijini Kigoma, ambapo alitumia fursa hiyo kuwaasa waumini wa dini ya kiislam na wananchi kwa ujumla kuendelea kushikama na kulinda amani.

Pia, Waziri Mkuu aliwahamasisha walime zao la michikichi kwani Serikali imeamua kulifufua zao hilo ili waweze kuondokana na umasikini. Wanaotamani kulima michikichi wajiandae wakati utakapofika watasambaziwa miche.

 (mwisho)

Read More

MAJALIWA AFUNGA MKUTANO WA KIMATAIFA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI TANZANIA WA MWAKA 2020.







Read More

MAJALIWA AFUNGA MKUTANO WA KIMATAIFA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI TANZANIA WA MWAKA 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya michikichi wakati alipotembelea kitalu cha mbegu bora zinazooteshwa katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya michikichi wakati alipotembelea kitalu cha mbegu bora zinazooteshwa katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya michikichi wakati alipotembelea kitalu cha mbegu bora zinazooteshwa katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Filson Kagimbo kuhusu uoteshaji wa mbegu bora za michikichi wakati alipotembelea kitalu cha miche ya michikichi cha kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichpo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya michikichi wakati alipotembelea kitalu cha mbegu bora zinazooteshwa katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya michikichi wakati alipotembelea kitalu cha mbegu bora zinazooteshwa katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga kilichopo wilayani Kigoma, Februari 21, 2020.


Read More

Thursday, February 20, 2020

MAJALIWA: SERIKALI HAINA LENGO LA KUMKOMOA MTU


 *Ni kuhusu maelekezo ya utoaji wa vutambulisho vya Taifa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeagiza umakini ufanyike katika utoaji wa vitambulisho vya Taifa hususani katika mikoa ya mipakani si kwa lengo la kutaka kumkomoa mtu bali ni kwa ajili ya kuimarisha usalama wa nchi.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 20, 2020) baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wabunge wa mkoa wa Kagera kuhusu usumbufu wanaoupata baadhi ya wananchi wanapofuatilia vitambulisho vya Taifa kwani wengine wanadaiwa kuwa si raia.

Malalamiko hayo yametolewa wakati Waziri Mkuu akizungumza katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera. Waziri Mkuu ni mlezi wa CCM wa mkoa wa Kagera.

“Watu fuate taratibu katika suala ugawaji wa vitambulisho, Idara ya Uhamiaji wafuatilie kwa umakini kwa sababu lazima usalama wa nchi usimamiwe ipasavyo hususani katika mikoa ya mipakani. Watanzania mnatakiwa muwe makini msiruhusu watu kuingia kwa njia za panya kwani watu hao hawana nia njema.”

Waziri Mkuu amesema lazima zoezi hilo lifanyike vizuri na wataharakisha ili wananchi waweze kupata vitambulisho. Tayari Serikali imeshaongeza vifaa na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM waimarishe mshikamano miongoni mwao na pale kwenye dosari zirekebishwe kwa sababu hakuna jambo lisiloweza kutatuliwa.

“Tunahitaji kuwa na umoja na mshikamano ndani ya chama ili sote kwa pamoja tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea….Hata katiba yetu ya chama inatuhimiza tushikamane kwani wote tunajenga nyumba moja hivyo hatuna sababu ya kugombea fito.”

Waziri Mkuu amesema lazima wahakikishe kuwa chama cha CCM kinabaki salama na kinaendelea kushika dola. “Ni wajibu wa kila kiongozi na mwanachama kuwezesha malengo hayo kutimia na ni lazima kila tawi litafakari namna ya kukiwezesha chama kujitegemea kiuchumi.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM wajiepushe na suala la ukabila na udini katika kuteua mtu wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na badala yake wateue mtu ambaye anauzika ndani na nje ya chama.

(mwisho)

Read More

Sunday, February 16, 2020

MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MENEJIMENTI YA MAAFA KWA NCHI ZA SADC KUKUTANA ZANZIBAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Zanzibar, Makame Khatibu Makame akitoa Ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa kuhusu  Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya menejimenti ya Maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika tarehe 16 Februari, 2020, Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja.

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Menejimenti ya  Maafa kwa Nchi Wanachama  Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika, tarehe 16 Februari, 2020, Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed (hayupo pichani) wakati wa akifafanua kuhusu Mkutano wa  kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Menejimenti ya  Maafa kwa Nchi Wanachama  Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika, tarehe 16 Februari 2020, Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja.

Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed (hayupo pichani) wakati wa akifafanua kuhusu Mkutano wa  kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Menejimenti ya  Maafa kwa Nchi Wanachama  Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika, tarehe 16 Februari 2020, Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu Wananchi,
Kama tunavyoelewa kuwa kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika mwezi Agosti 2019 ambapo, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokea rasmi uenyekiti wa jumuiya hiyo, hali hiyo imepelekea mkutano mbalimbali ya  Kisekta kufanyika hapa Tanzania.
Ndugu Wananchi,
Mkutano huu unafanyika kutokana na umuhimu mkubwa wa Mawaziri wa nchi wanachama wa SADC wanaohusika na masuala ya maafa kukutana kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kukabiliana na matukio ya  maafa yanayoukabili ukanda huu yakiwemo vimbunga, mafuriko, ukame, na hata ajali za baharini ambayo yamekuwa yakisababisha athari kubwa kwa maisha ya watu na mali.

Sote ni mashuhuda athari za Kimbunga Idai na Keneth vilivyotokea katika nchi za Madagascar, Malawi, Msumbiji na Zimbabwe vilipelekea vifo vya maelefu ya watu na wengine kutoonekana kabisa na kupelekea  mahitaji ya kiasi cha dola bilioni 10 za Kimarekani kwa ajili ya kurejesha hali.

Ndugu Wananchi,
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wanaohusika na Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahri Mbweni, tarehe 18 – 21 Februari, 2020,  hapa Zanzibar. ambapo Kaulimbiu ya Mkutano huu: “Ushiriki wa Kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa ni njia bora ya kujenga uhimili katika ukanda wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika” (SADC)

Ndugu Wananchi,
Mkutano huu unakuja kipindi ambacho nchi nyingi wanachama katika ukanda huu zimekuwa zikiathiriwa na majanga ya asili mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa. Hali iliyoonesha wazi umuhimu wa mashirikiano ya kikanda katika kukabiliana na maafa  ili kupunguza athari za maafa, kukuza uwezo wa kujiandaa  na kukabiliana kwani mara nyingi athari zinazotokana na majanga ya kimaumbile yakiwemo ukame, mafuriko, maradhi ya mlipuko na mengineyo, hupelekea vifo kuharibu miundombinu muhimu ikiwemo barabara na hudumaza msingi za jamii kama vile afya na elimu na kupelekea gharama kubwa  katika kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Ndugu Wananchi,
Katika hatua ya kujenga mataifa yenye uhimili katika kukabiliana na maafa, SADC imefanikiwa katika kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema inayoendana na majanga ya Hali ya  hewa, kuandaa vikao vya mwaka kwa nchi wananchama  kwa ajili  ya kujikinga, kujiandaa na kukabiliana na maafa pamoja  na kuandaa mipango ya dharura na kutoa mafunzo ya utafutaji na uokozi kwa majanga ya baharini kwa nchi wananchama.
Ndugu Wananchi,
SADC imetekeleza program ya ufanyaji wa tathmini na uchambuzi wa usalama wa chakula kwa nchi wananchama 14 zilizoathiriwa na majanga yanayoendana na hali ya hewa yakiwemo ukame, imeandaa mpango na mkakati wa pamoja kwa ajili ya kujikinga na kukabili maafa. Mikakati yote hiyo ni kwa ajili ya kupunguza athari za maafa katika kanda hii. Mnamo mwaka 2017-2018 takribani watu wapatao milioni 7 waliathiriwa na maafa idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na watu milioni 17 walioathirika katika miaka ya 2015-2016.
Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekamilisha kuandaa nyaraka zote muhimu katika masuala ya kukabiliana na maafa ikiwemo sheria ya Usimamizi wa Maafa ya Kitaifa Na. 7 ya 2015, Sheria ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar No. 1 ya mwaka 2015, Sera za Kukabiliana na Maafa, Mipango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa na Mkakati wa Mawasiliano Wakati wa Maafa na rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Maafa pamoja kuanzisha vituo vya mawasiliano na operesheni za dharura na vituo vya uokozi hasa kwa majanga ya baharini.
Mkutano huu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unalenga katika kushajihisha juhudi zilizopo katika kukabiliana na maafa kwa kuziwezesha nchi wanachama kuandaa mikakati ya uhimili kutokana na athari za maafa, kuandaa mkakati wa kujiandaa na kukabiliana na maafa. Aidha, mikakati hii itaisaidia sana juhudi za ukanda huu katika kupunguza athari za maafa na kuimarisha uwezo wa nchi husika katika kukabiliana na maafa pamoja na kurejesha hali baada ya maafa kutokea.

Ndugu Wananchi,
Nachukua fursa hii kuwakaribisha waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kufuatilia juu ya Mkutano huu ambao utakuwa ni fursa tosha ya kutangaza utalii wetu na kukuza uchumi wan chi pamoja na kupunguza athari za maafa.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mhe. Mohamed Aboud Mohamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa wa Pili wa  Rais Zanzibar



Read More

Friday, February 14, 2020

MAJALIWA: MUUNDO WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA UKAMILISHWE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais–TAMISEMI ishirikiane na mamlaka nyingine, zihakikishe zinakamilisha mchakato wa muundo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Pia, Waziri Mkuu ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma iongeze kasi ya upimaji wa viwanja pamoja na kusimamia kikamilifu udhibiti wa uendelezaji holela wa makazi. “Hatuhitaji kuona Jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na holela.” 

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi, Februari 13, 2020) wakati akizindua mpango kabambe wa jiji la Dodoma katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali haitaki kuona jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na holela kwani kasi ndogo ya upimaji wa viwanja kwa halmashauri ya jiji ndiyo itakayosababisha wananchi kujenga makazi holela yasiyopimwa.

Amesema wananchi hawawezi kuisubiri halmashauri bali halmashauri ndiyo inapaswa kuendana na kasi ya mahitaji ya wananchi. “Tayari katika baadhi ya maeneo wananchi wameanza na wanaendelea kujenga bila kufuata taratibu zinazotawala masuala ya ujenzi mijini.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa upimaji wa maeneo uende sambamba na uendelezaji wa miundombinu na huduma muhimu katika maeneo, ikiwemo maji na barabara. “Kasi ya uboreshaji barabara za mitaa iongezwe.”

Pia, Waziri Mkuu amesema halmashauri ya Jiji la Dodoma iweke utaratibu mzuri wa ufuatiliaji, utekelezaji na tathmini ya Mpango Kabambe ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kikamilifu. 

“Hili ni takwa la kisheria kwa mujibu wa kifungu namba 14(3) cha Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 ambacho kinaitaka kila mamlaka ya upangaji kutoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kabambe kila mwaka katika maeneo yao ya upangaji kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza halmashauri ya Jiji la Dodoma ianzishe mchakato wa kutambua nyumba zote zilizojengwa kwenye barabara kwa lengo la kujua idadi kamili, uhalali wao kuwepo au kama ni wavamizi na baadaye kuandaa utaratibu wa fidia kwa wananchi wanaostahili.

Kadharika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Wizara, Halmashauri, Taasisi, sekta binafsi, Jumuiya za Kimataifa, wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango Kabambe ili kufikia malengo ya kuwa na jiji bora, lenye mandhari ya kuvutia na litakalokidhi mahitaji ya kijamii na kiuchumi ya sasa na ya baadae.

Uamuzi wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Read More

Thursday, February 13, 2020

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA KWANZA KWA KAMATI YA MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MENEJIMENTI YA MAAFA KWA NCHI ZA SADC

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira,  Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira,  Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Kulia kwake ni, Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, KanalI, Jimmy Matamwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira,  Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika tarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. Mgeni Rasmi, atakayefungua mkutano huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



NduguWananchi,
Serikaliya Tanzania itakuwamwenyejiwaMkutanowa Kwanza waKamatiyaMawaziriwenyedhamanayaMenejimentiyaMaafakwaNchiWanachamawaJumuiyayaMaendeleoKusinimwaAfrikautakaofanyikatarehe 18 – 21 Februari, 2020, Zanzibar. MgeniRasmi, atakayefunguamkutanohuoniRaiswa Zanzibar naMwenyekitiwaBaraza la Mapinduzi.Mhe Dk. Ally Mohamed Shein.
KaulimbiuyaMkutanohuu: “UshirikiwaKisektakwenyeKupunguzamadharayamaafaninjia bora yakuimarishaustahimilivukatikaukanda wan chi WanachamawaJumuiyayaMaendeleoKusinimwaAfrika” (SADC).
Itakumbukwakuwa Tanzania ilichukuarasminafasiyaMwenyekitiwajumuiyakuanziamweziAgosti, 2019 kwakipindi cha mwakammojahadimweziAgosti, 2020
Mkutanohuuunafanyikakwamaraya kwanza visiwani Zanzibar tanguMhe. Dkt. John Joseph PombeMagufuli,RaiswaJamhuriyaMuunganowaTanzania akabidhiweuenyekitiwajumuiya. Kufanyikakwamkutanohuunifursakubwakwawananchiwa Tanzania kwaniutasaidiakukuzabiasharanautaliikatikanchiyetuhasavisiwavya Zanzibar nakuendeleakujitangazakimataifa.
NduguWananchi,
KamatiyaMawaziriwenyedhamanayamenejimentiyaMaafaimeanzishwakwalengo la kulishauriBaraza la Mawaziriwanchizajumuiyaya SADC kuhusumasualayaupunguzajiwamadharayamaafakikanda. Lengomahususi pia ni,  kuwanajukwaa la kubadilishanataarifanauzoefuwakiutendajimiongonimwanchiwanachamailikutekelezakwaufanisishughulizausimamiziwamaafa.
NduguWananchi,
Mkutanohuuunakujakipindiambachonchinyingiwanachamakatikaukandahuuzimekuwazikiathiriwanamajangayaasilimarakwamaranakusababishamadharamakubwa. Sotetunakumbukaukamewamwaka 2016 ambaouliathiritakribaniwatumilioni 40 katikaukandahuunakusababishaukosefuwachakula. Idadihiiiliongezekahadiwatumilioni 41.6 katikanchi 13 Wanachamakipindi cha msimuwa 2018/2019.
NduguWananchi,
Baadhiyanchiwanachamaikiwemo; (Komoro, Malawi, Msumbijina Zimbabwe) kwamwaka 2019 zilipatamafurikoyaliyosababishwanaVimbungaIdaina Kenneth. Kutokanamadharayamafurikohayo, Gharamazamisaadakukabilianamadharanikubwa (zinakadiriwakuwadolamilioni 323)wakatigharamazakurejeshahalizilikadiriwakuwadolabilioni 10.
Ili kuwezakupunguzagharamakubwakatikaurejesahiwahalindiomaanakatikamkutanohuuwa SADC tutajadiliananamnayakuwekezakatikapunguzamadharayamaafa, kwakuwaGharamazausimamiziwamaafakamayaukamaenamafurikohuzilazimuNchiWanachamakuelekezarasilimalizilizotengwakwaajiliyashughulizazamaendeleonabadalayakekuelekezwakatikashughulikurejeshahali.
Sotetunakumbuka, matukioyaVimbungavyaIdainaKeneth, vilivyosababishaatharikubwakatikanchizaMsumbiji, Malawi na Zimbabwe.KutokananamadharayaVimbungahivyo,  Nchiyetuilishirikiipasavyokatikahatuazakurejeshahalikwenyenchihizotatu  .
NduguWananchi,
Kwa uzoefuwaainayamajangaambayohutokeakatikanchiza SADC, inadhihirishaumuhimuwaushirikianowakikandauliothabitikatikakukabiliananayo. Majangahayakwakiasikikubwayanatokananamabadilikoyatabianchinahaliyahewa, Pia yamekuwayakitokeamagonjwayamilipukoyawanyamanamazao, katikaukandahuuambaoasilimiakubwayawananchi wake hutegemeasanashughulizakilimokwaustawiwauchumi.
Hali hiiimekuwaikichangiakudumazaukuajiwauchumiwakikanda, hivyohatunabudikuchukuahatuakwapamojazakupunguzamadhara, kuimarishautayariwakikandanauwezowakukabiliananamaafa.
Aidha, katikakuchukuahatuazakuimarishaustahimilivuwakikandadhidiyamaafa, SekretarietiyaJumuiyakwakushirikianananchiwanachamaimekuwaikifanyajuhudimbalimbalizakuimarishaustahimilivukwakuandaaMpangowaDharurawaKujiandaanaKukabiliananaMaafa,  kushirikianakuandaataarifazautabiriwamsimunakutoatahadhariyaawalikuhusuhatarizitokanazohaliyahewapamojanakutoamafunzokwawataalamwanchiwanachamakatikafanimbalimbaliikiwemotathmini, utafutajinauokoaji.
Aidha, baadhiyanchiwanachamaikiwemo Tanzania zimefaidikakwakupatavifaanamifumoyakufuatiliamajangayamafuriko, ukamena moto wamisitunikwaajiliyakutoatahadhariyaawalikupitiaushirikianohuo.
Ili kwendasambambanajuhudizakikandanakimataifa, serikaliyaawamuyatanoinayoongozwanaDkt. John PombeMagufuli,  itaendeleakuimarishauwezo wake wausimamiziwamaafakatikanyanjazote. TayariserikaliyaawamuyaTanoimetungaSheriayaUsimamiziwaMaafayaKitaifa Na. 7 ya 2015 nakanunizake, TunaoWasifuwaJanga la MafurikonaUkamewaKitaifanaMkakatiwaTaifaKupunguzaMadharayaMaafa;
Lengokubwa la serikalinikuhakikishakilasektainazingatiahatuazaupunguzajiwamadharayamaafakatikamipangoyamaendeleonauandaajiwabajetiilikupunguzamadharakwajamiinahasarazakiuchumi.
NduguWananchi,
 MkutanowaKwanzawaKamatiyaMawaziriwanaohusikanaMenejimentiyaMaafakwaNchiWanachamawaJumuiyayaMaendeleoKusinimwaAfrikautakaofanyikamweziFebruari, 2020 visiwaniZanzibar unakusudiakuchocheajuhudizilizopokatikakupunguzamadharayamaafakwakutelelezayafuatayo:
  1. KujadilinakupitishaMkakatiwaKujiandaanaKukabiliananaMaafawaKikanda 2016 – 2030;
  2. KujadilinakuridhiaMfumoMkakatiwaUstahimilivuwaKikanda 2020 – 2025;
  3. Kupokeataarifazamaendeleojuuyautekelezajiwamkakatiwamabadilikoyatabianchinampangokazi wake;
  4. Mpangowapamojawamazoeziyanadhariayakukabiliananadharura, utafitinanjiambadalazakukabiliananamajangakatikakutoahudumazakibinadamu, urejeshajiwamiundombinukutokananamajangayaasili.
Asantenikwakunisiliza.

Mhe. JenistaMhagama (MB)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, URATIBU, BUNGE, UWEKEZAJI, AJIRA, VIJANA NA WENYE WALEMAVU)


13 FEBRUARI, 2020
Read More