Thursday, November 9, 2017

WAZIRI MKUU BUNGENI LEO TAREHE 09 NOVEMBA,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kabla ya kuanza kikao cha Bunge mjini Dodoma, Novemba 9, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu swali la papo kwa papo, leo bungeni mjini Dodoma, Novemba 9, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe, wakati akiuliza swali la papo kwa papo, bungeni mjini Dodoma, Novemba 9, 2017.

Read More

KATIBU MKUU MPYA APOKELEWA KWA SHANGWE DODOMA

Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola wakati wa kumpokea alipowasili katika  Ofisi yake  Mjini Dodoma  Novemba 9, 2017.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kumpokea rasmi katika Ofisi hiyo Novemba 9, 2017 Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo wakati alipowasili katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo wakati alipowasili katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi (kushoto) akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola katika ofisi yake mpya mara baada ya kuwasili Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika ofisi yake mpya Novemba 9, 2017 Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akiteta jambo na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo Ofisi hiyo walipokutana kumkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akiwatambulisha Wasaidizi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.

Read More

Wednesday, November 8, 2017

BUNGENI LEO TAREHE 08 NOVEMBA,2017

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri , Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8,2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahi jambo na Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8,2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Geita, Upendo Peneza, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 8,2017.

Read More

Tuesday, November 7, 2017

MAWAZIRI MSITOE MATAMKO YASIYOTEKELEZEKA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikali.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Novemba 7, 2017) wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ni vema  viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.

Pia amewataka viongozi hao wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili kuithibitishia jamii kuwa Rais Dkt. John Magufuli aliwateua kutokana na uadilifu na uwezo wao kiutendaji.

“Tunao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anafanya kazi kwa nguvu na bidii ili kutimiza matarajio ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na wananchi wote kwa ujumla.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wajiwekee utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za Wabunge na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Pia amewataka wafanye ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayohusu sekta zao kwa kuwa wao ni wasimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Waziri Mkuu amesema Mawaziri na Naibu Mawaziri wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. 

Pia wasimamie utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Read More

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma Novemba 7, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akisisitiza jambo kuhusu mkakati wa Serikali kuboresha mazingira ya Ajira hapa nchini walipokutana leo Mjini Dodoma katika kikao cha Wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.


Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw .Geodfrey Simbeye akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akichangia mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika programu zinazotekelezwa na Serikali katika masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ili kujikwamua kiuchumi.
Wajumbe wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kujadili Masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara na Huduma Bi Jane Gonsalves akichangia hoja kuhusu mikakati ya Serikali kuwawezesha Vijana kupata ajira na kujiajiri wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi leo Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akichangia hoja kuhusu namna bora ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi wakati wa kikao cha Kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Novembna 7, 2017 Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Dkt.Aggrey Mlimuka akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.


Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWASIKILIZA MAWAZIRI

Waziri MKuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Selemani Jaffo wakati wa Kikao cha Kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilicho anza leo Novemba 7/2017 Mjini Dodoma.
Waziri MKuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Umi Mwalimu, wakati wa Kikao cha Kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilicho anza leo Novemba 7/2017 Mjini Dodoma.

Read More

Monday, November 6, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA MAADALIZI YA BUNGE KINACHO ANZA KESHO

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Wabunge kwa ajali ya maandalizi ya Mkutano wa Tisa wa Bunge la Kumi na Moja unaotarajiwa kuanza kesho Novemba 7/2017 Mjini Dodma. Mkutano huo umefanyika leo Novemba 6/2017 katika Ukumbi wa Msekwa Dododma.kushoto kwake ni Spika wa Bunge,Mheshimiwa Job Ndugai na kulia kwa Waziri Mkuu ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai.

Read More

Sunday, November 5, 2017

WAZIRI MKUU AKIWA MKOANI LINDI KWA ZIARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kata ya Mbekenyera, Wilayani Ruangwa, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira miwili na jezi Meneja wa timu ya Namungo FC Fred Kimbi, katika Mkutano wa hadhara uliyofanyika katika kata ya Mbekenyera, Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi, mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, iliyopo kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya msingi Ng’au iliypo Wilayani Ruangwa, Daniel Chilemba kwa kusimamia ujenzi kikamilifu, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa shule, Novemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, iliyopo kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya msingi Ng’au, iliyopo kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2017.

Read More

‘RUANGWA INAHITAJI SEKONDARI YA WASICHANA’

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wilaya ya Ruangwa inahitaji kuwa na shule ya sekondari ya wasichana ambayo ni ya bweni ili kupunguza tatizo la wasichana kukosa elimu.

Ametoa wito huo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ng’au, kata ya Mnacho wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambako alienda kukagua ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo ujenzi wake ulianza wiki mbili zilizopita.

“Mpango wetu ni kujenga shule ya msingi mpya hapa kijijini Ng’au ili watoto wanaotoka ng’ambo hii wasome hapa hapa. Wakati wa masika nyote mnajua taabu wanayopata watoto wetu kukatisha kwenda ng’ambo ile,” alisema.

“Nimefurahi kukuta msingi wa vyumba tisa uko tayari na hii idadi inaweza kuongezeka. Wanakijiji tushirikiane kujaza kifusi ili kazi ya ujenzi iende haraka,” alisema.

Waziri Mkuu alisema ng’ambo ya pili kuna shule ya msingi Mnacho ambayo ina madarasa 11 na wanafunzi waliopo ni karibu 500, na ndoto yake ilikuwa ni kuona ile shule inabadilika na kuwa ya sekondari.

“Ile shule ina historia na wakazi wengi kutoka Nandagala, Namahema, Chimbila ‘A’ na Chiemeka wamesoma pale. Mimi mwenyewe nimesoma pale kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule ilishazeeka, ndipo tukatafuta fedha ili ifanyiwe ukarabati na sasa ina miundombinu mizuri ndiyo sababu inaonekana inafaa kuwa ya sekondari,” alisema.

“Kwa vile shule ina miundombinu ya kutosha, ni vema ikawa ya bweni ambayo ni mahsusi kwa wasichana wa wilaya hii kwani tunalo tatizo la watoto wa kike kupata elimu, na wanahangaika sana,” alisema.

“Ujenzi wa hii shule ukikamilika, watoto wale 500 watahamia hapa na walimu wao na ile pale itapokea wanafunzi sekondari za wilaya hii ili tuwe na kidato cha kwanza hadi cha nne na ianze mara moja,” alisema.

Alisema shule hiyo itaitwa Lucas Malia kwa heshima ya mwalimu mkuu wa zamani wa shule hiyo ambaye alisomesha watu wengi katika wilaya hiyo na wengine sasa hivi ni viongozi Serikalini na jeshini. Mwalimu Malia hivi sasa ni marehemu.

Waziri Mkuu amerejea Dodoma leo asubuhi kuendelea na vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza kesho (Jumanne, Novemba 7, 2017).
Read More

WATAKAOKWAMISHA MALIPO YA KOROSHO KUKIONA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote watakaokwamisha malipo ya wakulima wa zao la korosho.

“Hatutamuacha mtu yeyote atakayesababisha wakulima kuchelewa kulipwa fedha zao. Tutawakamata wote na kuwachukulia hatua stahiki.”

Ametoa kauli hiyo jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alisema wakulima hao ni lazima walipwe fedha zao kwa wakati na asitokee mtu wa kuzitamani fedha hizo.

“Mkulima amelima mikorosho mwenyewe, ameokotoa na kukodoa mwenyewe wao wamepewa dhamana ya kuziuza, hivyo wahakikishe wanawapelekea fedha zao na wala wasizitamani.”

Pia Waziri Mkuu amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi wahakikishe mkulima hakosi sh. 3,500 katika kilo moja ya korosho atakayoiuza baada ya kukatwa michango.

Alisema bei ya juu ya korosho katika minada ya mkoa wa Lindi sh. ni 3,970 na ya chini sh. 3,800. “Vyovyote itakavyokuwa mkulima hawezi kukosa sh. 3,500, viongozi wa AMCOS mnisikie.”

 Waziri Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa bei ya zao la korosho pamoja na kupungua kwa makato ya mkulima ambapo kwa sasa hayazidi sh. 300 katika kilo moja ya korosho.
Read More

WAZIRI MKUU AHIMIZA LINDI WAJIPANGE MAANDALIZI YA BARAZA LA MAULID KITAIFA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wana-Lindi na wana-Ruangwa watumie fursa zilizopo ili kufanikisha maandalizi ya sherehe za Maulid na Baraza la Maulid Kitaifa mwaka huu.

Ametoa wito huo leo (Jumapili, Novemba 5, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Lindi na wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja.

Waziri Mkuu amesema sherehe hizo zitafanyika Desemba mosi kwa mkesha wa Maulid na kufuatiwa na Baraza la Maulid litakalofanyika Desemba 2, saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Likangale.

Aliwataka wana-Ruangwa waharakishe kujenga nyumba za kulala wageni na sehemu za kula ili waweze kupokea ugeni huo mkubwa wa kitaifa. “Kila mmoja anayeona hapo kuna fursa, ni lazima aitumie vizuri,” alisisitiza.

“Kwa niaba ya wana-Ruangwa, tunamshukuru Mheshimiwa Mufti na Baraza la Maulamaa kwa kuridhia sherehe hizi zifanyike kitaifa hapa wilayani kwetu. Nitumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote tuungane katika sherehe hizi licha ya tofauti za madhehebu yetu tuliyonayo,” alisema.

Alisema uamuzi huo wa BAKWATA ulitangazwa kwenye Baraza la Maulid lililofanyika Singida, mwaka jana ya kwamba wameamua kuadhimisha sherehe hizo kwenye ngazi ya wilaya badala ya kuwa inafanyika makao makuu kila mwaka.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaarifu viongozi hao kwamba maandalizi yanaendelea na kwamba vifaa mbalimbali kama mchele, vitoweo, unga wa ngano, sukari, maji, juisi, mahema, mikeka na mazulia vimekwishapatikana.

“Ninaomba Kamati ya Uhamasishaji iifanye kazi hii kwa kutambua kuwa jambo hili si la kwenu peke yenu, bali linaungwa mkono na Serikali, na hii ni kwa sababu Serikali yenu inafanya kazi kwa karibu sana na viongozi wa dini,” alisema.

Alisema misingi ya amani katika nchi hii imejengwa na mahubiri ya viongozi wa dini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji, Sheikh Ali Mohammed Mtopa alisema Ruagwa iko tayari na imepokea wito huo wa kitaifa. “Tunakuhakikishia wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wawakilishi wa Mufti waliopo hapa kwamba tumepokea hiyo heshima,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Itifaki kutoka BAKWATA Makao Makuu na Msimamizi wa Malidi za Kitaifa, Sheikh Mohammad Nassir ambaye alisema wana Ruangwa an wana Lindi wanalo jukumu la kuhamasisha watu washiriki sherehe hizo.

“Hamasa haitatoka Morogoro au Dar es Salaam bali hapahapa Lindi. Tunataraji watu wasiopungua 10,000 watahudhuria sherehe hizi za Maulid kutoka wilaya zote za mkoa wa Lindi na hii ni mbali wawakilishi kutoka kila mkoa wapatao 100 -150,” alisema.

Waziri Mkuu anatembelea vijiji vya jimboni mwake ambako atahutubia wananchi.

Read More

Friday, November 3, 2017

WAZIRI MKUU AWASILI TOKEA NCHINI CANADA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017.


Read More

Wednesday, November 1, 2017

HABARI PICHA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watanzania waishio nchini Canada, kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watanzania waishio nchini Canada, kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.

 Watanzania waishio nchini Canada,wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipo kutana nao  kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.

 Watanzania waishio nchini Canada,wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipo kutana nao  kwenye hoteli ya The Ritz-Carlton Toronto Oktoba 31, 2017.


Read More

Tuesday, October 31, 2017

KUWENI WAZALENDO, WAZIRI MKUU AHIMIZA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao.

Ametoa wito huo jana (Jumanne, Oktoba 31, 2017) wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada.

Waziri Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake. “Tembea huku ukiringia nchi yako, wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine wanasemea vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.”

Aliwataka wakumbuke kuweka akiba na wanapopata fursa watume fedha zao nyumbani ili zisaidie kuleta maendeleo. “Ukipata kitu kidogo, rusha nyumbani; ukipata mtu anayeweza kuleta tija, mlete nyumbani, nasi tutawapokea wewe na yeye,” alisisitiza.  

“Tunawasisitiza muitangaze nchi yetu kwa mataifa mengine ili nao waone Tanzania ni mahali pa fursa, na akitaka kuwekeza ajue kuwa anawekeza mahali ambapo ni salama,” alisema.

Alisema Serikali inasisitiza wananchi waishio nje ya nchi, wawe wazalendo na washirikiane kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa za kimaendeleo kwa manufaa ya nchi yao.
  
Awali, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania waishio nchini humo wazingatie sheria za nchi hiyo.


“Wote sisi tunawatambua kama mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada. Tunawashauri muwe raia wema, na muishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii na msisahau mlipotoka, kwani hakuna mahali pazuri kama nyumbani,” alisisitiza.
Read More

Thursday, October 26, 2017

VITUO VYA KUTOA TAHADHARI YA MAAFA YA MAFURIKO NA UKAME VYAFUNGWA NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa vituo vya hali ya hewa vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutoa tahadhari ya uwepo wa maafa ya mafuriko na Ukame nchini, kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya, Meneja Kanda ya Kusini, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,  Daudi Amas na Mratibu Mradi wa mifumo ya Tahadhari za mapema, Alfei Daniel, wakati alipokuwa anakagua vituo hivyo mkoani Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa  Mhandisi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,  David CChilambo, juu ya jinsi vituo vya hali ya hewa vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutoa tahadhari ya uwepo wa maafa ya mafuriko na Ukame nchini, , wakati alipokuwa anakagua vituo hivyo mkoani Ruvuma, katikati ni Mkuu wa Wilaya Namtumbo, Luckness Amlima.


Moja ya Kituo cha hali ya hewa kati ya vituo 36  vilivyofungwa na Ofisi ya Waziri Mkuu nchi nzima kwa  usimamizi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ambapo kutokana na uwezo wa vituo hivyo taarifa zake zinatumika kutoa tahadhari ya uwepo wa maafa ya mafuriko na Ukame nchini, , kutokana na uwezo wa vituo hivyo vinavyopatikana  hapa nchini na Ethiopia kwa bara la Afrika, vimeongeza uwezo wa ufanisi wa utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kutoka asilimia 82 hadi asilimia 87 kwa sasa.

Read More

Wednesday, October 25, 2017

MHAGAMA : HAYATI ASKOFU CASTOR MSEMWA ALIKUWA KIUNGO MUHIMU KWA MIRADI YA KANISA KUWEZESHA HUDUMA ZA SERIKALI

Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha rambi rambi wakati alipofika kushiriki maziko ya aliyekuwa askofu wa jimbo la Katoliki Tunduru Masasi Hayati Castor Msemwa yaliyofanyika katika  jimbo hilo, mkoani Ruvuma, leo tarehe 25 Oktoba, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama  akiwa na spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Anna Makinda, wakati wa misa ya  maziko ya aliyekuwa askofu wa jimbo la katoliki Tunduru Masasi Hayati Castor Msemwa yaliyofanyika katika  jimbo hilo, mkoani Ruvuma, leo tarehe 25 Oktoba, 2017



Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa salaam za serikali wakati wa maziko ya aliyekuwa askofu wa jimbo la katoliki Tunduru Masasi Hayati Castor Msemwa yaliyofanyika katika  jimbo hilo, mkoani Ruvuma, leo tarehe 25 Oktoba, 2017.

Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Anna Makinda, akinena kuhusu kifo cha Hayati askofu wa jimbo la katoliki Tunduru Masasi Hayati Castor Msemwa wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika  jimbo hilo, mkoani Ruvuma, leo tarehe 25 Oktoba, 2017.

Read More