Monday, September 10, 2018

WAZIRI MKUU BUNGENI LEO 10.09.2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mtwara vijijini, Hawa Ghasia, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.
 Naibu Waziri wa Fedha,Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jaku Hashim Ayoub, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.
Read More

MAJALIWA AREJEA DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma akitoka Dar es salaam Septemba 10, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrabas Kitambi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma akitoka Dar es salaam, Septemba 10, 2018.

Read More

Sunday, September 9, 2018

MAJALIWA AREJEA NCHINI

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitoka nchini China, Septemba 9, 2018 alikomwakilisha Rais  John Magufuli kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing hivi karibuni.

Read More

Wednesday, September 5, 2018

MAJALIWA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MEYA WA SHENZHEN NCHINI CHINA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meya wa Manispaa ya Shenzhen kwenye hoteli ya Wuzhou nchini China, Septemba 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Shenzhen, Bw. Wang Wanzhong kwenye ukumbi wa Hoteli ya Wuzhou nchini China, Septemba 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa piano ya Kichina na msan , Xing Man baada ya mazungumzo kati yake na Meya wa Manispaa ya Shenzhen nchini China. Bw. Wang Wanzhong, Septemba 5, 2018. 

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA OFISI KUU YA KAMPUNI YA HUAWEI TECHNOLOGIES ILIYOPO SHENZHEN NCHINI CHINA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maua wakati alipowasili kwenye makao mkuu ya kampuni ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen nchini China, Septemba 5, 2018. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo duniani, Li Da Feng.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya jengo la Makao Makuu ya Kampuni ya Huawei Techinologies  yaliyopo Shenzhen nchini China baada ya kutembelea  Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wa Kampuni hiyo, Septemba 5, 2018. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya jengo la Makao Makuu ya Kampuni ya Huawei Techinologies  yaliyopo Shenzhen nchini China baada ya kutembelea  Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wa Kampuni hiyo, Septemba 5, 2018.

Read More

TUMENUFAIKA NA MKUTANO WA FOCAC-MAJALIWA


WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa kutokana na kushiriki kwake katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Amesema kikao hicho kimekuwa na tija kwa Tanzania kutokana na maeneo ya vipaumbele yaliyojadiliwa katika mkutano huo hususani masuala ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Septemba 05, 2018) alipokutana na waandishi wa habari katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi China ambako alikwenda kumuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano wa FOCAC. 

Alisema maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mkutano huo ni masuala ya usalama wa nchi, maendeleo ya kiuchumi hususani uboreshaji wa sekta ya viwanda, elimu, kilimo, afya, elimu na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

“Kikao hiki kimekuwa na tija kwa Tanzania kwa sababu maeneo yote yaliyojadiliwa ni muhimu kwetu. Tumeanza kuona idadi nzuri ya wawekezaji kutoka China na ni matokeo ya mpango uliowekwa katika kikao cha kwanza cha FOCAC kilichofanyika Afrika Kusini.”

Waziri Mkuu alisema maeneo mengine yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya madini, mifugo na uvuvi, ambazo nazo zimewekewa mikakati ya namna ya kuziboresha ili ili ziweze kuchangia ukuzaji wa uchumi katika mataifa hayo.

Kadhalika, Waziri Mkuu alisema kikao hiko pia kilijadili namna ya kuboresha sekta ya utalii kwa kuvutia watalii kutoka za Afrika na nje ya bara hilo ikiwemo na China, hivyo Tanzania inatakiwa kutumia fursa fursa zilizopo kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali.

Alisema ushirikiano huo unaanza mara moja na China imetenga dola bilini 60 za Marekani kwa ajili ya kusaidia Afrika ili ziweze kuboresha maeneo hayo yaliyoainishwa. Tanzania inatakiwa kutumia vizuri fursa hiyo.

Pia Waziri Mkuualisema atakaporejea nchini ataitisha kikao cha kazi cha Mawaziri na kutoa maelekezo kwa mawaziri wote ambao sekta zao zimeguswa  kwenye mpango wa FOCAC ili waweze kuandaa utaratibu mzuri wa namna tukavyonufaika na fedha hizo.
“Watanzania tushirikiane kwa pamoja na watendaji katika wizara zote ili tuweze kujipanga vizuri. Wataalamu katika kila sekta waweke mpango kazi utakaokwenda kuhitaji fedha hizo kwa ajili ya kuimarisha sekta husika ili maeneo yote yapate tija.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amempongeza Rais wa China, Xi Jinpingkwa kuitambua Tanzania kama moja kati ya nchi rafiki wa muda mrefu wa China na kuipa kipaumbele kwenye mkakati wa kuwekeza kwenye viwanda.

Alisema wawekezaji wengi kutoka China wamedhamiria kuja Tanzania kujenga viwanda na kuviendesha kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi ili viweze kuzalisha kwa uhakika na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. 

Waziri Mkuu alisema tayari Tanzania ilishafanikiwa katika mkakati wa kuboresha mazao makuu matano ya biashara ambayo ni korosho, chai, kahawa, pamba na tumbaku na sasa imejipanga kuboresha mazao ya mbegu za kuzalisha mafuta na ameitaka mikoa husika ifuatilie mazao hao ambayo ni michikichi, alizeti na ufuta.

Mkutano huo wa FOCAC wa siku mbili ulifunguliwa Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing China na Rais wa China, Xi Jinping. Ulihudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi 53 kutoka Afrika.


Read More

Monday, September 3, 2018

MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA ULIOANZA JIJINI BEIJING

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi  Jinping katika Mkutano wa  Jukwaa la Ushirikiano  Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakuu wa Afrika na China baada ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kufungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Tanzania na China Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Great Hall of the  People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi  Jinping katika Mkutano wa  Jukwaa la Ushirikiano  Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI WA KILIMO WA CHINA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo wa China, Bw.  Han Changfu (kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo iliyopo Beijing, Septemba 3, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu  wakishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya Uvuvi kati ya China na Tanzania kwenye ukumbi wa Wizara ya Kilimo ya China katika jiji la  Beijing, Septemba 3, 2018. Wanaotia Saini ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na  Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu wakati alipotembelea Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo iliyopo Beijing Septemba 3, 2018.  Majaliwa yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Afrika na China - FOCAC.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu (wanne kulia)  na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa wizara hiyo jijini Beijing, Septemba 3, 2018. Wengine pichani ni  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi  wa Zanzibar,  Rashid Ali Juma. (wapili kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (watatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki na Naiba Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiagana na viongozi wa Wizara ya Kilimo ya China baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo, Beijing nchini China, Septemba 3, 2018.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA NAIBU GAVANA WA JIMBO LA JIANGSU NCHINI CHINA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Gavana  wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw.  Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania  uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Gavana wa Jimbo la  Jiangsu nchini China, Bw.  Guo Yuan Qiang  (kushoto) kwenye ubalozi wa Tanzania  uliopo Beijing nchini China, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC.   Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Gavana  wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw.  Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania  uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC.

Read More

Sunday, September 2, 2018

WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi  wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao  kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani uliopo jijini Beijing. 

Alisema nchi zote zilizoendelea  zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’

Waziri Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu  kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga  mkono juhudi za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje ya nchi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya  ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa. 

“Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga alisema mwelekeo  wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa nchi yao.

Alisema Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.

 (mwisho)
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHI CHINA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China Septemba 2, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mke wa Balozi wa Tanzania nchini China na  Waziri wa Madini, Angela Kairuki wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing China kuzungumza na Watanzania, Septemba 2, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ua kutoka kwa mtoto Johari Said Masoro wakati alipowasili kwenye Ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing kuzungumza na Watanzania  waishio nchini China, Septemba 2, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio nchini China Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 2, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio nchini China Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 2, 2018.


Baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 2, 2018.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing Septemba 2, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing Septemba 2, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing Septemba 2, 2018.
Read More

MAJALIWA AHUTUBIA KONGOMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA- BEIJING

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa hoteli ya  Westin jijini Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Makampuni yapatayo 80 yalishiriki katika Kongamano hilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa hoteli ya  Westin jijini Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Makampuni yapatayo 80 yalishiriki katika Kongamano hilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Biashara Kati ya Tanzania na China kwenye ukumbi wa hoteli ya  Westin jijini Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Makampuni yapatayo 80 yalishiriki katika Kongamano hilo.

Read More

TANZANIA INAONGOZA KWA UWEKEZAJI UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni  wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki. 

“Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubiaKongamano la Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya  Winstin jijini Beijing nchini China.

Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria  kwa dhati  kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.

Amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania  inaongoza kwa kupokea  uwekezaji  katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.

Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa  ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo  mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo  mkubwa katika  kujenga msingi imara wa viwanda.

“Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza  mkakakati wetu wa kukuza  uchumi wa viwanda na biashara.”

Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji  kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.

Kuhusu uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017,  Waziri Mkuu amesema  umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda na utalii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesemakuna fursa nyingi kwenye sekta ya huduma hususan katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa kwa haraka nchini Tanzania. 

Pia kumekuwa na ukuaji na mageuzi ya haraka katika soko la TEHAMA nchini kwa miaka 10 iliyopita. “Soko la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano limekuwa kwa ongezeko la watumiaji, aina ya huduma zinazotolewa pamoja na kupanuka kwa eneo ambalo huduma hizo hutolewa.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, “Tanzania kuna fursa zisizo na ukomo katika eneo hili huku kukiwa na matarajio ya kukuwa kwa soko la kikanda.” 

“Maeneo ya kuwekeza ni pamoja na utoaji wa huduma za simu hususan katika maeneo ya vijijini, utoaji na uendeshaji wa huduma za mtandao pamoja na ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mawasiliano. Tunawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo haya.”

Amesema kwa wale ambao nia yao ni kuwekeza katika kilimo, Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na takribani hekta milioni 29.4 kwa ajili ya umwagiliaji.

 “Ninawakalibisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo cha biashara kwa mazao kama miwa, mpunga, ngano, kahawa, chai na mahindi. Tuna fursa kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari.”

 (mwisho)
Read More

Friday, August 31, 2018

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA FOCAC


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Ijumaa, Oktoba 31, 2018) kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.
Read More

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM MKUTANO WA FOCAC NCHINI NCHINI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka nichini kwenda China kumwakilisha Rais John Magufuli  Katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

Read More

Wednesday, August 29, 2018

FLYOVER YA TAZARA IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 98-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.

Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam. 

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi huo inayoendelea kwenye hilo.

“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani  kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya  wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa barabara za juu (interchange) eneo la Ubungo, katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma, eneo la Ubungo jijini Dar Es Salaam.

Amesema ni vema wafanyabiashara hao wakaondolewa na kutafutiwa eneo lingine ili kulinda usalama wao kutokana na kazi za ujenzi zinazoendelea kwenye maeneo hayo. Pia amewataka viongozi hao wawaelekeze wananchi maeneo watakapowahamishia wafanyabiashara hao ili waweze kwenda kununua bidhaa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mradi huo nao unalengo la kupunguza msongamano wa magari kwa kutenganisha njia za barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma ili kuwa na ngazi mbili juu ya barabara za sasa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya juu katika eneo la Tanzara (Mfugale flyover) unagharimu sh. bilioni 100.52 na unajengwa na kampuni  ya Sumitomo Mitsui ya nchini Japan.

Amesema mradi huo umezingatia jinsi ya kuwezesha muunganiko wa mfumo wa usafiri jijini Dar Es Salaam na ule wa mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, tatu na ya nne. “Tumeacha eneo la mita 12 katikati ya barabara kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.”

Read More

DAWA YA KUUA VILUILUI ITUMIKE KUTOKOMEZA MARALIA-MAJALIWA

 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa yote nchini waendeleze kampeni ya kutokomeza ugonjwa malaria kwa kutumia dawa ya kuua viluilui vya mbu.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29, 2018) alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mbu kilichopo katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Amesema nchi inakabiliwa na matatizo makubwa ya ugojwa wa malaria, hivyo ni vema viongozi wa mikoa wakatokomeza viluilui vya mbu kwa kuwa dawa inatengenezwa nchini.

Waziri Mkuu amesema kiwanda hicho cha Labiofam ni cha pekee barani Afrika kwa kuwa na uwezo wa kutengeneza dawa za aina hiyo.”Tutumie fursa hii kutokomeza maralia nchini.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutumia vyombo vya habari  kwa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma kuhusu dawa wanayozitengeneza.

Amesema wananchi wanatakiwa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia dawa hiyo kwa ajili ya kuua viluilui katika maeneo ya makazi yao ili kuutokomeza ugonjwa wa maralia nchini.

Naye,Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Aggrey Ndunguru amesema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zina uwezo wa kuua viluilui vya mbu tu na haina madhara kwa binadamu.

Amesemma dawa hiyo ambayo ipo katika ujazo tofauti tofauti inaweza kuwekwa kwenye makaro ya vyoo, maji yaliyotuama pamoja na katika matanki ya maji ili kuua viluilui.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alifuatana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na maafisa wengine wa Serikali.

Read More

Monday, August 27, 2018

CAF YARIDHISHWA NA MAANDILIZI YA AFCON


RAIS wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 27, 2018) wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.
Kwa upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.mashindano 

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi.”

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.
Read More

Sunday, August 26, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJLIA HALI DR HAMISI KIGWANGALA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla,  leo Agosti 26.2018 akiwa anaendelea kupatiwa  matibabu katika Wodi aliyolazwa ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa,  Muhimbili (MOI).

Read More