Monday, July 8, 2019

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MJI WA SERIKALI(ACUDO),MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali (ACUDO),Ahmed Zaki (kulia), wakati alipotembelea mji huo, mjini CairoJulai 8.2019. Kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mji mpya wa Serikali, wakati alipotembelea mji huo, mjini Cairo,Julai 8.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kjushoto), wakati alipotembelea kanisa jipya la Katoliki, katika mji Mpya wa Serikali, mjini Cairo MisriJulai 8.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kjushoto), wakati alipotembelea kanisa jipya la Katoliki, katika mji Mpya wa Serikali, mjini Cairo Misri,Julai 8.2019.

Read More

UDHIBITI MAPATO, NIDHAMU KWA WATUMISHI VIMEPAISHA UCHUMI-MAJALIWA

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hatua ya kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali, uboreshwaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma kumesababisha kukua kwa uchumi.

Amesema Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu na Serikali imeendelea kuongeza nguvu katika kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yote nchini, hali inayotoa fursa kwa wananchi wake kuendeleza shughuli zao za maendeleo. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 8, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi nchini Misri.

Hivyo, amemuhakikishia Waziri Mkuu wa Misri kwamba Serikali ya Tanzanzia na wananchi wake wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya nchi hiyo na wananchi wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili.

Amesema nchi za Tanzania na Misri zinahitaji kutumia nafasi ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika ukuzaji wa uchumi, hivyo Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Amesema Serikali ya Tanzania imefanikiwa kiuchumi na kwa sasa ni nchi pili ambayo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika, ikitanguliwa na nchi ya Ivory Coast. Uchumi wa Tanzania ulitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka jana kutoka asilimia saba.

“Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea vizuri, tumeendelea kushuhudia kushuka kwa mfumuko wa bei ambapo kwa sasa tumefikia asilimia 3.2, kiwango hiki ni matokeo ya kukuza sekta za madini, ujenzi, mawasiliano, utalii pamoja na kushuka kwa bidhaa za chakula na mafuta. Tunatarajia kiwango hiki kitashuka zaidi kwa sababu ya uwekezaji.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda.

 (mwisho)
Read More

ZIARA YA WAZIRI MKUU NCHINI MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji, Dkt. Sahar Nasr, kabla ya kukutana na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo MisriJulai 8.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo MisriJulai 8.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo MisriJulai 8.2019.
Wawekezaji kutoka Misri, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipozungumza nao, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo MisriJulai 8.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo MisriJulai 8.2019.

Read More

WAZIRI MKUU AKIWA ZIARANI NCHINI MISRI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu ya Jamhuri ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly katika mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Misri, katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, mjini CairoJulai 8.2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu ya Jamhuri ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Misri, nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, mjini CairoJulai 8.2019.

Read More

WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI MISRI KWENYE ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya kuwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatuJulai 8.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, wakati akiwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 8.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya kuwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatuJulai 8.2019.

Read More

Friday, July 5, 2019

VIONGOZI WA DINI IMARISHENI MALEZI KWA VIJANA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa dini waendelee kuimarisha malezi na mafundisho ya kiroho kwa vijana na kuepusha mmomonyoko wa maadili ili Taifa liendelee kung’ara, kuheshimika na kusifika duniani kwa utulivu, amani na umoja. 

Amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini ikiwemo CCT katika kutengeneza mustakabali mwema na ustawi wa familia kupitia mahubiri ya injili na malezi ya kiroho kwa waamini. “Mtakubaliana nami kuwa siku zote Taifa imara msingi wake hujengwa na familia imara.” 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 5, 2019) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.

Amesema Serikali inatambua mchango wa malezi ya kiroho katika ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla na mafundisho yake kwani yamesaidia kujenga watumishi wa umma ambao wamelelewa katika misingi bora ya kumcha Mwenyezi Mungu.    

Waziri Mkuu amesema Serikali inaamini kwamba watumishi wa namna hiyo watachapa kazi kwa bidii, uadilifu, uaminifu na kupiga vita vitendo vyote vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini kwa ajili ya ustawi wa Taifa na watu wake.

Akizungumzia kuhusu harambee hiyo ambayo jumla ya sh. milioni 357.35 zilipatikana, Waziri Mkuu amesema ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa CCT wa miaka mitano (2017 – 2022) wenye lengo la kuiwezesha CCT kujitegemea kwa kuwa na vitega uchumi vyake ambavyo vitawawezesha kujiendesha kwa asilimia 80.

Waziri Mkuu ameipongeza CCT kwa kuanza kuchukua hatua za kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kiuchumi kwani zinahitajika nguvu za pamoja katika kuhakikisha wanawahudumia Watanzania na kuwaletea maendeleo. 

“Kujizatiti kwa CCT katika kufikia malengo yake ya kujitegemea kiuchumi ni muhimu katika kutimiza kusudio na agizo la Mungu la kuwahudumia wahitaji ambao ni Watanzania lakini pia mtakuwa mnajaliza juhudi za Serikali katika wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.”

Waziri Mkuu amesema kwa msingi huo, Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za CCT na madhehebu mengine ya dini katika kuwahudumia Watanzania kupitia sekta za elimu, maji, afya na shughuli za ujasiriamali.

Amesema suala la kujitegemea ndiyo msingi wa uongozi wa Rais Dkt. Magufuli wa kujenga uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025 na katika kufanikisha hilo, Serikali imeendelea kupunguza kiwango cha utegemezi.

Amesema kiwango cha utegemezi kutoka kwa Washirika wa Maendeleo katika bajeti kimepungua kutoka asilimia 12.5 mwaka 2017/2018 hadi asilimia nane 2019/2020. “Kuimarika huko kwa bajeti yetu kunakwenda sambamba na kuimarika kwa huduma za kijamii kama vile elimu, maji na kupungua kwa umaskini wa mahitaji muhimu.”

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCT, Mchungaji Canon Moses Matonya, amesema jumuiya hiyo imeanzisha mkakati wa kuwa na vitegauchumu vyake kwa lengo kuondokana na utegemezi wa fedha za ufadhili ambazo zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka.

(mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN MAGUFULI, KATIKA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA 53 YA JUMUIYA YA KIKRISTO(CCT)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu, Alinikisa Cheyo, wakati akiwasili katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5.2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu, Alinikisa Cheyo, kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5.2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na waumini wa Kikristo, kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulioambatana na harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha jumuiya hiyo, uliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Julai 5.2019. Waziri Mkuu, amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, katika mkutano huo.

Thursday, July 4, 2019

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DR JOHN MAGUFULI NCHINI RWANDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda  Paul Kagame mjini Kigali aliko mwakilisha Rais Dkt . John Pombe  Magufuli  katika sherehe za miaka 25 ya Ukombozi wa Nchi hiyo .Julai 4/2019 anayeshudia ni Rais wa Sierra  leon Mh Mada Bio.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amejumuika na Viongozi wenzake katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Ukombozi wa Rwanda
Askari wa JWTZ wakiwa katika sherehe ya miaka 25 ya Ukombozi wa Rwanda

Read More

Wednesday, July 3, 2019

UKAGUZI WA MIKATABA YA AJIRA KWA MADEREVA

1.            Katika kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali inaendelea, pamoja na mambo mengine, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara katika sekta mbali mbali hapa nchini, ikiwemo sekta ya usafirishaji. Sekta hii ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, sekta hii imekuwa ikichangia pia kuzalisha ajira kwa vijana wetu katika nafasi mbali mbali kama vile Madereva, Mafundi na kada nyingine nyingi.

2.            Pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na sekta hii, zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na Serikali kwa kushirikiana na wadau.  Kwa upande wa utekelezaji wa Sheria za Kazi, changamoto zimeendelea kujitokeza katika masuala ya Mikataba ya Ajira, Malipo ya Mishahara na Posho mbali mbali, ambapo imebainika yapo Makampuni machache yanayolenga kuchafua kazi nzuri inayofanywa na sekta hii, ambapo makampuni hayo machache yamekuwa yakifanya udanganyifu kwenye Mikataba ya Ajira za Madereva wao pindi yanapofanya maombi ya Leseni za Usafirishaji.

3.            Aidha, katika jitihada za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani na LATRA inatarajia kufanya Zoezi Maalum la Ukaguzi kwa lengo la kukagua Mikataba hiyo na kuangalia utekelezaji wa Sheria kwa ujumla.

4.            Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa namna mbili tofauti ambapo; (i) Maafisa Kazi waliopo katika Ofisi za Kazi watapita katika Kampuni zote za Usafirishaji na (ii) Timu maalum ya Maafisa Kazi wa kushirikiana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva, LATRA na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani watafanya Ukaguzi wa Mikataba kwenye Vituo Vikuu vya Ukaguzi kama vile Kituo cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Kuegesha Malori cha Misugusugu na vituo vingine vinavyofanana na hivyo hapa nchini.

5.            Aidha, sambamba na ukaguzi huo, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Vyama vya Waajiri watapatiwa elimu kuhusu haki na wajibu wao katika kutekeleza Sheria za Kazi.

Hivyo, ninapenda kuwaarifu Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Wafanyakazi Madereva na Umma kwa ujumla kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatarajia kuanza rasmi Zoezi  la Ukaguzi wa Mikataba ya Ajira ya Madereva na Utekelezaji wa Sheria za Kazi kwa ujumla ifikapo tarehe 15 Julai, 2019.

6.            Ili kulifanya zoezi hili kuwa lenye ufanisi, ni vema Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji kuhakikisha kuwa Mikataba ya Madereva wenu inakuwepo katika maeneo yenu ya kazi, na kwa upande wa Madereva, kuhakikisha mnakuwa na nakala za Mikataba yenu mnapokuwa katika kazi zenu ili iwe rahisi kwa Wakaguzi kuiona.

7.            Aidha, ninapenda kuwaarifu kuwa Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba ya ajira na Utekelezaji wa Sheria kwa ujumla litakuwa endelevu na litaendelea pia katika Sekta nyingine hapa nchini.

8.            Mwisho, ninapenda kutoa wito kwa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva pamoja na Madereva wote nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakaguzi wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hili ili kutoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi kwa namna yoyote ile.

IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
3/7/2019
Read More

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA VIETNAM

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vitemam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza na Balozi wa Vitemam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao yao. 

“Serikali imeendelea kuondoa  vikwazo vya  kuanzisha na kuendesha  biashara  kwa kupitia upya   sheria, kanuni na taratibu za biashara  na kuzifuta zile  ambazo zimethibitika  kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kuwa magumu.”

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi hiyo.

Amesema kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua. Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote kuwasaidia. 

Kwa upande wake, Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu. 

Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.

Nchi za Vietnam na Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1965. Mwaka 1984, Vietnam ilifungua ofisi ya Ubalozi  wake hapa nchini kwa muda na kuufungua upya mwaka 2003.
Read More

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA VIETNAM

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao yao. 

“Serikali imeendelea kuondoa  vikwazo vya  kuanzisha na kuendesha  biashara  kwa kupitia upya   sheria, kanuni na taratibu za biashara  na kuzifuta zile  ambazo zimethibitika  kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kuwa magumu.”

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi hiyo.

Amesema kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua. Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote kuwasaidia. 

Kwa upande wake, Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu. 

Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.

Nchi za Vietnam na Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1965. Mwaka 1984, Vietnam ilifungua ofisi ya Ubalozi  wake hapa nchini kwa muda na kuufungua upya mwaka 2003.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen   Doanh, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 3, 2019.

Read More

Tuesday, July 2, 2019

RAIS KENYATTA AMTUMIA UJUMBE RAIS DKT. MAGUFULI

*Ni kuhusu kuchukizwa kwake na kauli ya Jaguar 
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemtumia ujumbe maalumu Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli unaoelezea msimamo wa Serikali yake kuhusu kukerwa na matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa jimbo la Starehe, Charles  Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar.

 Ujumbe huo wa maandishi umewasilishwa leo (Jumanne, Julai 02, 2019) na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dany Kazungu na kupokelewa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar Es Salaam. 

Akipokea taarifa hiyo Waziri Mkuu amesema Watanzania wamefurahishwa na hatua mbalimbali zilizochukulia na Serikali ya Kenya dhidi ya mbunge huyo zinazodhihirisha kwamba matamshi hayo hayakuwa msimamo wa Serikali ya Kenya wala wananchi wake bali  ulikuwa ni msimamo  binafsi wa mbunge huyo.

Amesema siku zote Watanzania na Wakenya wamekuwa huru kuishi na kufanya kazi au biashara katika nchi za Afrika ya Mashariki na pale yalipotokea matatizo au kutokukubaliana serikali husika zilikaa mezani na kumaliza tofauti hizo.

"Uhusiano kati ya Kenya na Tanzania ni wa karibu mno na wa kidugu kwani kuna baadhi ya makabila yapo katika nchi mbili hizi kama vile Wamasai na Wakurya na  Wajaluo  hivyo ushirkiano katika masuala ya mbalimbali yakiwemo ya  kabiashara na ya kijamii haukwepeki."

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi na wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kujiepusha na kauli zenye viashiria vya  kujenga chuki, uhasama na migongano miongoni mwa wananchi kwani  kauli hizo zisipodhibitiwa mapema zinaweza kusabisha hofu na kutokuelewana miongoni mwao.

Waziri Mkuu  ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo na ndugu zao wa Kenya na wageni wote kutoka nchi za Afrika ya Mashariki na duniani kwa ujumla ambao wapo nchini wakifanya shughuli mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi. 

“Mambo yetu yote katika nchi za Afrika ya Mashariki  hasa ya biashara na ya  kiuchumi kwa ujumla yataenda vizuri endapo  tutalinda na kudumisha amani, bila amani tutaogopana na tutashindwa kabisa  kushirikiana”, amesisitiza Mheshimiwa Majaliwa.

Waziri Mkuu  ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania kamwe ahaitaruhusu wala kufumbia macho kauli au vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uchochezi  dhidi ya nchi jirani  ili na kulinda na kuunga mkono juhudi mbalimbali za ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi zinazofanywa na viongozi  wakuu wa Mataifa ya Afrika.

Kwa upande wake Balozi Kazungu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni jijini Dodoma iliyowataka Watanzania kuwa watulivu na wayachukulie matamshi ya Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya, Njagua kuwa ni msimamo wake binafsi na siyo  msimamo wa Wakenya na Serikali yao.

Balozi Njagua mesema Msimamo wa Rais Kenyatta siku zote umekuwa ni kuwapokea na kuwakubali ndugu zao  wote wanaotoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioamua kuishi au kufanya biashara nchini Kenya.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya Njagua alitoa matamshi ya kichochezi akiwataka raia wa kigeni kutoka Mataifa mbalimbali wanaofanya shughuli za kibiashara nchini Kenya wakiwemo Watanzania waondoke ndani ya muda wa saa 24.

Read More

Monday, July 1, 2019

TTCL YASAMBAZA HUDUMA YA MAWASILIANO KWA VIONGOZI

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa. Akabidhiwa Simu ya TTCL na Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba, leo Julai 1,2019 Jijini Dar es salaam ,wanao shuhudia kushoto kwa Waziri Mkuu ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Kinondoni Bibi Janeth Maeda na kulia mwisho ni Meneja Huduma wa TTCL Kinondoni Bwana Salim Msalilwa.

Read More