Tuesday, March 10, 2020

“ TUNATAKA SHUGHULI ZA UCHAGUZI MKUU 2020 ZIFANYIKE JENGO JIPYA LA NEC” MHAGAMA


Na. OWM, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, amekagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma na kusema kuwa serikali imedhamiria shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka huu kufanyika kwenye jengo hilo jipya la Tume hiyo.

Amebainisha hayo wakati alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya Tume hiyo, leo tarehe 10 Machi, 2020, ambapo amekagua hatua za ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa kukagua  Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.

Kukamilika kwa majengo hayo itakuwa ni  utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambaye aliitaka tume hiyo kuhakikisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo unakamilika   kwa wakati,  ili shughuli za uchaguzi Mkuu wa  mwaka huu zifanyike kwenye majengo hayo.

Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL ndio wanaohusika na shughuli za ukandarasi wa majengo hayo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga jingo lake.
MWISHO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akikagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiwaeleza Watendaji wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wakandarasi wa Jengo la Tume hiyo juu ya umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi huo unaofanyika  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020, wakati alipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo.

Muonekano wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi linaloendelea kujengwa  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020,  ujenzi wa ofisi za Tume hiyo utakuwa ni Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiwaeleza Watendaji wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wakandarasi wa Jengo la Tume hiyo juu ya umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi huo unaofanyika  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020, wakati alipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo.



Read More

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA VIONGOZI WA DINI NA BUNGE YA KUPUNGUZA UNYANYAPAA KWA VVU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma, Machi 10, 2020 kuzindua Kampeni ya Kitaifa  ya Viongozi wa Dini  na Bunge  katika  kuongeza jitihada za kupunguza unyanyapaa dhidi ya Ukimwi. Kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai, wa tatu kushoto  ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,Watano kushoto ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai na wa sita kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni ya Kitaifa  ya Viongozi wa Dini  na Bunge  katika  kuongeza jitihada za kupunguza unyanyapaa dhidi ya Ukimwi kwenye ukumbi wa Msekwa jijini   Dodoma, Machi 10, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni ya Kitaifa  ya Viongozi wa Dini  na Bunge  katika  kuongeza jitihada za kupunguza unyanyapaa dhidi ya Ukimwi kwenye ukumbi wa Msekwa jijini   Dodoma, Machi 10, 2020. 


Read More

Friday, March 6, 2020

WAFICHUENI WAFANYABIASHARA WA MAGENDO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi washirikiane na Serikali katika kuwafichua wafanyabiashara wa magendo wanaoingiza bidhaa kwa kupitia bandari bubu.

Pia ameiagiza Idara ya  Uvuvi wilaya ya Pangani ihakikishe inadhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu na nyavu zisizo stahili kwa kuwa unahatarisha mazalia ya samaki.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 6, 2020) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Bomani, wilayani Pangani.

Amesema uwepo wa bandari bubu katika wilaya hiyo unasababisha kuingizwa kwa bidhaa ambazo viwango vyake havijathibitishwa na mamlaka husika hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.

“Wananchi shirikianeni na Serikali katika kuwataja wanaoingiza bidhaa kupitia bandari bubu kwani licha ya bidhaa hizo kutokuwa na uhakika wa ubora, pia hata wakwepakodi nao wanapitia huko.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu malalamiko ya wafanyakazi wa mkonge ambapo amesema atamuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aende kushughulikia suala hilo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, maji na umeme kwani kati ya vijiji 33 vya jimbo hilo vitatu tu ndio havina umeme.

Pia mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani yenye urefu wa kilometa 50 pamoja na ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha mradi huo.

Awali, Waziri Mkuu alizindua mradi wa ujenzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kwa upande wa kaskazini wenye urefu wa mita 950 uliogharimu sh. Bilioni 2.9. Pia alizindua kituo cha polisi cha wilaya ya Pangani pamoja.

Mwisho

Read More

ZIARA YA MAJALIWA WILAYANI PANGANI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Machi 6, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga, Machi 6, 2020.
Wananchi wa Pangani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bomani Pangani akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga Machi 6, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa  ukuta wa mto Pangani kabla ya kuuzindua ukuta huo, Machi 6, 2020. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zaibab Abdallah  Issa .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa  ukuta wa mto Pangani kabla ya kuuzindua ukuta huo, Machi 6, 2020. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zaibab Abdallah  Issa .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa ujenzi wa  ukuta wa mto Pangani kabla ya kuuzindua ukuta huo, Machi 6, 2020. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Sima na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zaibab Abdallah  Issa .
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitia saini kitabu cha wageni akiwa  kwenye Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya ya Pangani, Georgina Matagi (kulia) wakati alipozindua kituo kipya cha  Polisi cha wilaya ya Pangani, Machi 6, 2020. Kituo hicho kimejengwa uhamasishaji uliofanywa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo. 


Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA UWANJA WA JITEGEMEE MUHEZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Jitegemee Muheza, Machi 6, 2020.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Jitegemee, Muheza Machi 6, 2020. 

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Jitegemee, Muheza Machi 6, 2020. 


Read More

WAFICHUENI WAFANYABIASHARA WA MAGENDO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi washirikiane na Serikali katika kuwafichua wafanyabiashara wa magendo wanaoingiza bidhaa kwa kupitia bandari bubu.

Pia ameiagiza Idara ya  Uvuvi wilaya ya Pangani ihakikishe inadhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu na nyavu zisizo stahili kwa kuwa unahatarisha mazalia ya samaki.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 6, 2020) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Bomani, wilayani Pangani.

Amesema uwepo wa bandari bubu katika wilaya hiyo unasababisha kuingizwa kwa bidhaa ambazo viwango vyake havijathibitishwa na mamlaka husika hivyo kuhatarisha afya za watumiaji.

“Wananchi shirikianeni na Serikali katika kuwataja wanaoingiza bidhaa kupitia bandari bubu kwani licha ya bidhaa hizo kutokuwa na uhakika wa ubora, pia hata wakwepakodi nao wanapitia huko.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu malalamiko ya wafanyakazi wa mkonge ambapo amesema atamuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aende kushughulikia suala hilo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, maji na umeme kwani kati ya vijiji 33 vya jimbo hilo vitatu tu ndio havina umeme.

Pia mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani yenye urefu wa kilometa 50 pamoja na ulipaji fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha mradi huo.

Awali, Waziri Mkuu alizindua mradi wa ujenzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kwa upande wa kaskazini wenye urefu wa mita 950 uliogharimu sh. Bilioni 2.9. Pia alizindua kituo cha polisi cha wilaya ya Pangani pamoja.

Mwisho

Read More

MAJALIWA: MKURUGENZI WA BODI YA MKONGE ARUDISHWE ALIKOTOKA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania, Yunus Mssika arudishwe katika wizara aliyotoka na nafasi itakaimiwa na Katibu wa Timu ya Uchunguzi wa Tuhuma mbalimbali katika Tasnia ya Kilimo cha Mkonge mkoani Tanga Bw. Saddy Kambona.

Pia, Waziri Mkuu amewasimamisha wajumbe wote wa Bodi ya Mkonge hadi hapo watakapotaarifiwa, lengo ni kuhakikisha zoezi la urejeshaji wa mali linafanyika kwa ufanisi.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Ijumaa, Machi 6, 2020) wakati alipokutana na Bodi ya Mkonge katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, jijini Tanga.

Katika kikao hicho ambacho kilitanguliwa na Katibu wa Timu ya Uchunguzi wa Tuhuma mbalimbali katika Tasnia ya Kilimo cha Mkonge mkoani Tanga kuwasilisha taarifa ya mali za iliyokuwa Mamlaka ya Mkonge ambazo zilizwa kinyume na taratibu na zinatakiwa zirejeshwe Serikalini.

Baada ya taarifa hiyo, Waziri Mkuu amesema ili utaratibu wa kurejesha mali hizo utekelezeke kwa ufanisi ni Mkurugenzi akarudishwa katika wizara aliyotoka na wajumbe wa Bodi ya Mkonge wakasubiri hadi hao watakapotaarifiwa.

Amesema Bw. Kambona anaanza zoezi la kuratibu na kuishauri timu katika shughuli ya urejeshwaji wa mali na ndiye atakayesimamia shughuli za bodi. Waziri Mkuu ameongeza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mkonge Tanzania Bibi  Mariam  Nkumbi ataendelea na majukumu yake.

“…Watachukua hatua kwa watu wote waliohusika na upotevu wa mali zote na kwamba maamuzi hayo yamefanyika ili kuzua uvurugwaji wa muundo wa uchunguzi wa kwa sababu mali ni nyingi n azote zinatakiwa zirejeshwe Serikalini.” Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona jambo hilo linaenda bila ya kusimama na mali zote zinarudi mikononi mwa bodi.

Machi Mosi mwaka huu, Waziri Mkuu aliapokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali katika tasnia ya kilimo cha mkonge mkoani Tangana kuagiza mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yakiwemo ya kurejeshwa Serikalini kwa nyumba na. 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Bw. Salum Shamte yafanyiwe kazi.

Nyumba nyingine zilizopendekezwa kurejeshwa Serikalini ni pamoja na nyumba kumi zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone, Bombo, Nguvumali na Market street ambazo zilinunuliwa na watumishi hao kwa udanganyifu.

Timu hiyo maalum ya uchunguzi iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani Tanga kuanzia tarehe 29/11/2019 hadi tarehe 07/02/2020. Timu hiyo iliyokuwa na  wajumbe 13 ilihusisha maafisa kutoka ofisi mbalimbali za Serikali.

Uchunguzi huo maalum ulihusu masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge mkoani Tanga ambayo ni pamoja na uzalishaji wa mkonge, bei ya zao la mkonge katika soko la ndani na nje ya nchi.

Pia, ilichunguza kuhusu mali za iliyokuwa Mamlaka ya mkonge nchini, ubia kati ya Kampuni ya Katani Limited na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Utendaji kazi wa Kampuni ya Katani Ltd na pia Utendaji kazi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB). 

(mwisho)
Read More

Thursday, March 5, 2020

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI KOROGWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Korogwe, Machi 5, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi  wakati  alipowasili kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Korogwe kuhutubia  mkutano wa hadhara Machi 5, 2020. 
Wasanii wa kikundi cha Selo  wakicheza ngoma wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Korogwe, Machi5, 2020.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Korogwe, Machi 5, 2020.

Read More

MAKAMU WA RAIS MHESHIMIWA SAMIA SULUHU AMEWATAKA MAWAZIRI NA WADAU WA UTATU WA SADC SEKTA YA KAZI NA AJIRA KUWA NA MIKAKATI YA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri na Wadau wa Utatu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya Kazi na Ajira kuweka Mazingira wezeshi yatakayowajengea vijana uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri.
Hayo yameelezwa wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu  wa SADC wa Sekta ya Kazi na Ajira pamoja na uzinduzi wa Programu ya Taifa ya Mafunzo kwa Vitendo Mahala pa Kazi (Internship) iliyofanyika katika Kitio cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ikiwa ni “Kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mema Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu”.
Makamu wa Rais alieleza kuwa ni muhimu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakawa na mikakati ya kuiwezesha nguvukazi ya Jumuiya hiyo na hasa vijana kupata ujuzi stahiki utakaowawezesha kufanya kazi zenye staha.
Alifafanua kuwa taarifa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu mwenendo wa soko la ajira kwa mwaka 2020, zaidi ya watu milioni 187.7 ikiwa sawa na asilimia 5.5 duniani hawana kazi na takribani wafanyakazi bilioni 2 ikiwa sawa na 61.2% wanafanyakazi kwenye sekta isiyo rasmi na zaidi ya watu milioni 267 ikiwa ni sawa na asilimia 22 ambao kati yao wana umri wa miaka 15 hadi 24 na hawapo kwenye mafunzo wala ajira.
“Sisi kama Jumuiya ya SADC tunalazimika kuwa na mikakati itakayowezesha nguvukazi ambao kwa idadi kubwa ni vijana na wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 60 katika jumuiya yetu, hivyo kama Jumuiya hatuna budi kuwekeza katika kuwajengea uwezo vijana ili waweze kushiriki kikamilifu katika ukuzaji wa uchumi wa nchi za ukanda huo,” alisema   
Alisema kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto ya ajira kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu nchini iliamua kuanzisha programu ya taifa ya kukuza ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa.
“Niwasihi wenzetu katika nchi za SADC ambao bado hawajaanzisha utaratibu huu, wajifunze kutoka Tanzania na wakiona utaratibu huo unafaa wautelekeze kwa manufaa ya vijana wa jumuiya hiyo,” alisema
Sambamba na hayo Makamu wa Rais amewapongeza waajiri katika sekta binafsi na sekta ya umma kwa kushirikiana na Serikali katika kuwajengea uwezo vijana kujifunza maadili, mtazamo chanya kuhusu kazi pamoja na tamaduni za kuishi mahali pa kazi na Kuwapatia uzoefu wa kazi unaohitajika na waajiri.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi nchini kwa vijana wa kitanzania imewasaidia vijana wengi kujiandaa na kuingia katika soko la ajira ikiwemo sekta muhimu za kipaumbele kama vile Ujenzi, Ukarimu, teknolojia ya habari, mawasiliano na utalii.
Aliongeza kuwa Programu ya Mafunzo kwa Vitendo Mahali pa Kazi kwa wahitimu imewanufaisha vijana zaidi ya 5,967 ambapo vijana 3,967 wamehitimu mafunzo na kati yao vijana 1,827 wamepata ajira moja kwa moja na vijana 2,000 bado wanaendelea na mafunzo hayo.
Naye, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax alieleza kuwa Serikali ya Tanzania imeonesha nia thabiti ya kutatua changamoto ya ajira kwa kuanzisha programu ya kukuza ujuzi kwa vijana lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo vijana.
“Nichukue fursa hii kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi inazozifanya katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, kwa kuwapatia mafunzo yatakayowajengea uzoefu katika soko la ajira,” alisema Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Tax
Mkutano huo wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeshirikisha pia Wadau wa Utatu wa Jumuiya hiyo ikiwemo Jukwaa la Vyama vya Waajiri Kusini mwa Afrika (SPSF), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Kusini mwa Afrika (SATUCC), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji kanda ya Kusini mwa Afrika (IOM).
Read More

MAJALIWA AKABIDHI MIKOPO YA MATREKTA KWA WAKULIMA WA MKONGE ILIYOTOLEWA NA BENKI ZA NMB NA CRDB

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa kwa mkopo na Benki ya NMB wa matrekta  11 na matrela  yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni  moja, kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge mkoani Tanga, Greyson Nyari (wa pili kulia) akionyesha ufunguo wa moja ya matrekta aliyokabidhiwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa na Benki ya NMB wa matrekta  11 na matrela  yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni  moja, kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya matrekta hayo  Greyson  Nyari , Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge  Mkoa wa Tanga kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la  Mwelya Sisal Estate la Korogwe. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua matrekta  manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh. Milioni 65 yaliyotolewa kwa mkopo na Benki ya CRDB kwa kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Mheshimiwa Majaliwa aliyakabidhi matrekta hayo kwa wakulima kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate  la Korogwe Tanga, Machi 5, 2020.  
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolea na Benki ya CRDB  wa matrekta  manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh. Milioni 65 kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya matrekta hayo  Emmanuel Urio ambaye ni mkulima. Makabidhiano hayo  yalifanyika  kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la  Mwelya Sisal Estate la Korogwe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua matrekta  manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh. Milioni 65 yaliyotolewa kwa mkopo na Benki ya CRDB kwa kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Mheshimiwa Majaliwa aliyakabidhi matrekta hayo kwa wakulima kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate  la Korogwe Tanga, Machi 5, 2020.

Read More

SUDANI WAJIFUNZA URATIBU WA URUTUBISHAJI WA VYAKULA TANZANIA



Na. OWM, DODOMA
Ujumbe wa maafisa waandamizi wa serikali kutoka nchini Sudani umekuja hapa nchini kujifunza masuala ya Uratibu wa Vuguvugu la Lishe  na urutubishaji wa Vyakula. Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiratibu masuala ya lishe nchini kutokana na mamlaka iliyonayo kikatiba ya kuratibu shughuli zote za Serikali pamoja na masuala mtambuka. Uratibu huo unafanywa kupitia Kamati ya kitaifa ya Lishe chini ya Uongozi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko.

Tanzania kupitia Ofisi hiyo imefanikiwa kuandaa Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe ambao hutoa mwongozo wa utekelezaji wa masuala ya Lishe nchini, ikiwemo kupambana na upungufu wa ukosefu wa virutubishi kwa kuongeza virutubishi hivyo kwenye vyakula,  pamoja na    uanzishwaji wa majukwaa mengine ya lishe katika ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya mkoa na wilaya likiwemo jukwaa la sekta binafsi linalojikita sana kwenye masuala ya urutubishaji wa vyakula.

Akiongea mara baada ya kikao cha  kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Urutubishaji wa vyakula,  mjini Dodoma,  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,  ambaye pia ni Mratibu wa Vuguvugu la lishe nchini,  amefafanua kuwa Tanzania ilikuwa  miongoni mwa nchi za awali duniani kujiunga na Vuguvugu la Lishe, ambalo linahimiza ushiriki wa sekta zingine na wadau wa lishe kupambana na utapiamlo wa watoto wa chini ya miaka mitano hasa aina ya udumavu, ambapo kwa sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza udumavu kutoka 42% mwaka 2010 hadi 32% mwaka 2018.

“Kutokana na utekelezaji mzuri wa Vuguvugu la Lishe tumefanikiwa kuwa na mtandao mzuri  wa Lishe wa kisekta kwa sekta binafsi, lakini pia utashi wa kisiasa umeongezeka hapa nchini ambapo tayari takribani wabunge 55 wamejitanabaisha kujihusisha na masuala ya lishe. Masuala ya lishe tayari yameingizwa kwenye Mpango wa Pili wa  Taifa wa Maendeleo  wa miaka mitano (2016-2021) na Mwongozo wa Mpango na Bajeti ambao umesaidia masuala ya lishe kuingizwa kwenye mipango ya kisekta  ya nchi ” amesisitiza Sangawe.

Aidha, Sangawe amebainisha kuwa tayari Tanzania imefanikiwa kuwa na Kanuni za Urutubishaji wa Vyakula za mwaka 2011, ambapo kanuni hizo zinavihusu viwanda vikubwa vya uzalishaji wa vyakula hususan unga wa ngano na mafuta ya kupikia.

Amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John  Pombe Magufuli, imeendelea kulipa kipaumbele suala la lishe kwa kutoa muongozo kwa Halmashauri zote nchini  kutenga  fedha za lishe kwa kila mtoto, ambapo awali ilikuwa  Shilingi 550/=,  kwa kila mtoto na kwa sasa ni shilingi 1,000/=  kwa kila mtoto.

 “Kwa sasa serikali imefanikiwa kuajiri wataalamu wa masuala ya lishe katika ngazi ya Wizara na Halmashauri ambapo kwa sasa 57% ya Halmashauri 185 zote nchini zimeajiri wataalamu wa masuala ya lishe huku Halmashauri zilizobaki zina maafisa viungo tu wa masuala ya lishe ” Amesisitiza Sangwe.

Amebainisha kuwa serikali imeamua suala la lishe kuwa agenda ya Kitaifa ambapo kwa sasa imeandaa makubaliano maalum (mikataba ya lishe) kwenye ngazi za serikali za mitaa ambayo ni kati ya ngazi hizo na  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), lengo ni kuongeza uwajibikaji kwenye masuala ya lishe.

Kwa upande wake, Kiongozi wa ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani, Kutoka Wizara ya Afya nchini Sudani, Huda Kambal, amefafanua kuwa wamechagua kuja Tanzania kujifunza uratibu wa kisekta wa masuala ya lishe na Urutubishaji wa vyakula hususani kwenye unga wa ngano na mafuta ya kupikia.
“Sisi katika nchi ya Sudani hatuna huu Uratibu wa kisekta katika masuala ya lishe na Urutubishaji wa vyakula. Lengo la kuja hapa ni kujifunza na kutaka kupata uzoefu wa namna ya kuratibu na kutekeleza shughuli za Urutubishaji wa Vyakula hasa kwa wazalishaji wakubwa wa vyakula ili twende tukaboreshe nchini kwetu shughuli hizo” Amesisitiza Kambal
 Amebainisha kuwa katika kuhakikisha wanafanikiwa kwenye kuanzisha Utaratibu huo wanatarajia kujifunza na kupata uzoefu katika maeneo ya Udhibiti na Usimamizi wa vyakula vilivyorutubishwa, ushiriki wa sekta binafsi kwenye masuala ya lishe, ufuatiliaji wa mara kwa mara na mawasiliano kwa umma juu ya masuala ya lishe.
Kikao  hicho kilihudhuriwa na maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali, Taasisi ya Lishe Tanzania, Shirika la Viwango Tanzania pamoja na maafisa waaandamizi kutoka nchini Sudani ambao wametoka Wizara ya Afya,  Shirika la Chakula Duniani, Shirika la Afya Duniani, Mamlaka ya Viwango na Ubora Sudani, Mamlaka ya utafiti na Viwanda, Wizara ya Viwanda na Shirika la Biashara Sudani
Mnamo mwaka 2012 Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi za kwanza Duniani kujiunga kwenye Vuguvugu la Lishe Duniani, ambapo mnamo mwaka 2011 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipindi hicho , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza kuingia kwenye kikundi cha viongozi wa Vuguvugu la Lishe Duniani. Kuanzia Kipindi hicho Agenda ya kitaifa ya masuala ya lishe ilianza kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kama Ofisi yenye dhamana ya kuratibu shuguli za Serikali kwa mujibu wa sheria.

MWISHO.


Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,(Mwenye tai)  na Kiongozi wa ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani, Kutoka Wizara ya Afya nchini Sudani, Huda Kambal (mwenye Ushungi), wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, maafisa hao wamekuja kujifunz hapa nchini kuhusu masuala hayo, tarehe 3 Machi 2020 Jijini Dodoma.

Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na maafisa waandamizi kutoka nchini Sudani, wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, tarehe 3 Machi 2020 Jijini Dodoma.
Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka nchini Sudani, wakifuatilia kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini,yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Machi 2020 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe (Mwenye tai), akiwa katika picha  ya pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka nchini Sudani  mara baada ya kumaliza kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu uratibu wa masuala ya Urutubishaji wa vyakula nchini, Machi 2020 Jijini Dodoma.

Read More

MAJALIWA AFUNGUA MAKTABA YA CHUO CHA UALIMU KOROGWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitabu baada ya  kufungua  maktaba ya Chuo cha Ualimu Korogwe, Machi 5, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe wakati alipofungua Maktaba ya Chuo cha Ualimu Korogwe, Machi 5, 2020.  Wa tano kushoto ni Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.  Leonard Akwilapo.  Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa pili kushoto ni Mbunge wa Korogwe Mjini , Mary Chatanda, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wa sita kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika maktaba ya  Chuo cha Ualimu Korogwe baada ya kuifungua Machi 5, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Ualimu Korogwe baada ya kufungua maktaba ya chuo hicho, Machi 5, 2020.


Read More

MAJALIWA: TUMESITISHA UCHIMAJI MADINI MAGAMBA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha uchumbaji wa madini ya boxite katika mlima wa Magamba wilayani Lushoto baada ya wananchi kuulalamikia mradi huo unasababisha uharibifu wa mazingira.
Hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa Serikali wahakikishe wanaimarisha ulinzi katika eneo hilo mtu yeyote asiendeshe shughuli za uchumbaji wa madini hata Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) nao wasichimbe eneo hilo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Alhamisi, Machi 5, 2020) baada ya kutembelea eneo hilo na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mabughai kata ya Magamba wilayani Lushoto, Tanga.
Amesema alipokea taarifa kwamba yapo malalamiko kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini zinazoendelea kwenye mgodi huo kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa pamoja na mbunge wa Lushoto, Shabn Shekilindi. 
“Hatuwezi kuendelea na shughuli za uchumbaji wa madini kwenye eneo hili wakati wananchi wanalalamikia uharibifu wa mazingira unaosababisha na shughuli hii. Serikali yenu ni sikivu hivyo nawaomba muendelee kuiamini na kushirikiana nayo.”
Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza watu wote waliopewa leseni za kuchimba madini katika eneo hilo wazirudishe Serikalini na amemuelekeza Waziri wa Madini, Doto Biteko asimamie zoezi hilo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Lushoto amesema wananchi hawataki shughuli za uchimbaji wa madini ya boxite ziendelee kufanyika kwenye mlima Magamba kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa mazingira.
Amesema katika mlima huo ndiko kwenye chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi pia mlima huo umezungukwa na miundombinu mbalimbali ya shughuli za kijamii, hivyo kuendelea kwa uchimbaji wa madini kutasababisha athari kubwa ikiwemo ukosefu wa maji.
Awali,Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema eneo hilo la Magamba lina leseni 22 za uchimbani lakini kutokana na mvutano wa wenye leseni na wananchi, wizara iliamua kusitisha shughuli za uchimbaji hadi watakapokubaliana.
Baada ya kuzungumza na wananchi, Waziri Mkuu alimtembelea Bi Miriam Shemndolwa ambaye ni mlemavu mkazi wa Mombo aliyemfahamu kupitia TBC alipohojiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Wape Nafasi, Tuma Dandi.
Apohojiwa katika kipindi hicho Bi Miriam aliomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi ambapo alimtaja Waziri Mkuu. 
Waziri Mkuu ametoa msaada wa sh. milioni tano ili pamoja na michango mingine zimuwezesha kujenga nyumba ya kuishi yeye na bibi yake Eonica Hiza ambaye ndiye anayemlea. Kwa sasa Miriam na mlezi wake wanaishi kwenye nyumba ya mjomba wake.
 (mwisho)

Read More