Tuesday, March 10, 2020

“ TUNATAKA SHUGHULI ZA UCHAGUZI MKUU 2020 ZIFANYIKE JENGO JIPYA LA NEC” MHAGAMA


Na. OWM, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, amekagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma na kusema kuwa serikali imedhamiria shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka huu kufanyika kwenye jengo hilo jipya la Tume hiyo.

Amebainisha hayo wakati alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya Tume hiyo, leo tarehe 10 Machi, 2020, ambapo amekagua hatua za ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa kukagua  Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.

Kukamilika kwa majengo hayo itakuwa ni  utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambaye aliitaka tume hiyo kuhakikisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo unakamilika   kwa wakati,  ili shughuli za uchaguzi Mkuu wa  mwaka huu zifanyike kwenye majengo hayo.

Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL ndio wanaohusika na shughuli za ukandarasi wa majengo hayo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga jingo lake.
MWISHO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akikagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiwaeleza Watendaji wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wakandarasi wa Jengo la Tume hiyo juu ya umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi huo unaofanyika  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020, wakati alipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo.

Muonekano wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi linaloendelea kujengwa  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020,  ujenzi wa ofisi za Tume hiyo utakuwa ni Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, akiwaeleza Watendaji wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wakandarasi wa Jengo la Tume hiyo juu ya umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi huo unaofanyika  Njedengwa Jijini Dodoma, leo Machi 10, 2020, wakati alipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo.




EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.