Friday, July 28, 2017

MAJALIWA AANZA ZIARA YA MKOA WA MBEYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya Julai 28,2017
Baadhi ya watumishi wa umma wa wilaya ya Kyela wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza naokwenye ukumbi wa Halmahauri ya wilaya ya Kyela akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya julai 29, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa  wilaya ya Kyela  baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (kushoto) kwenye ukumbi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kyela Julai 29, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa skafu na vija wa CCM, Green Guard bade ya kuwasili kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kuanza ziara wilayani humo Julai 29, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mbeya baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya Julai 28, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya julai 28, 2017.


Read More

RAIS AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI KWA NAIBU KAMISHNA WA UHAMIAJI

 *Ni baada ya kutoa vibali vya uraia kwa Wasomali 50

RAIS Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo asimamishwe kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.
                  
Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”

Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi  kuivumilia.”

Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.

"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."

Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. " Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchungilzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.


Read More

TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA INDIA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
 “Ushirikiano wa Tanzania na India ni wa kihistoria, hivyo tutauendeleza na kuudumisha. India tunashrikiana nao katika sekta za uchumi, afya, elimu na ulinzi.”
Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili walioutoa kwa Tanzania  katika kuimarisha miradi ya maji kwenye mikoa mbalimbali nchini.
Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa India kuja kutembelea maeneo ya  utalii nchini ukiwemo mlima wa Kilimanjaro, mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Lanba ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya India hususan katika masuala ya ulinzi.
Amesema wamefanya kikao na Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo ambapo katika mazungumzo yao wameweka mikakati ya kushirikiana katika kuimarisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani pamoja na masuala ya mafunzo.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI WA INDIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance mabeyo (kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.


Read More

Thursday, July 27, 2017

UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAJADILIWA.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu cha Kujadili na kuupitisha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.

Kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Julai 27, 2017 ambapo kilihusisha Makatibu wakuu pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujadili mwongozo huo ili kuhakikisha utekelezaji wake unaanza mapema iwezekanavyo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Dkt. Mwinyimvua alieleza umuhimu wa mwongozo ikiwa ni nyenzo muhimu ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na watoto ambapo kabla ya kuandaliwa Mwongozo huo, Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Lengo la Mwongozo huu ni kupunguza masuala ya ukatili kwa watoto na wanawake hivyo ni vyema ukajadiliwa na kuanza utekelezaji wake mapema ili kutatua changamoto za wanawake na watoto katika jamii.”Alisema Dkt.Mwinyimvua

Aidha mwongozo huo umeainisha mambo ya msingi yanayohusu masuala ya wanawake na watoto kwa kuangalia sheria mbalimbali zinazowalinda katika maisha yao ya kila siku ili kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia haki na usawa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkingaamesema kuwa wanawake na watoto ndiyo wahanga wakubwa wa vitendo ya ukatili katika jamii hivyo Mwongozo huu ni nyenzo itakayoleta ufanisi katika kutatua vitendo vya ukatili dhidi yao na kuhakikisha haki na usawa vinakuwepo ndani ya jamii.

Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini utaleta ufanisi na kusaidia masuala ya ukatili wa wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vyema kila mdau alione hili na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na vita hii”.alisema Bi.Sihaba

Juhudi hizi zinafanyika ikiwa ni moja ya maadhimio ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi wanachama ambapo kwa pamoja waliadhimia kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.

“Uwepo wa mwongozo huu utasaidia kupunguza athari za matokeo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto angalau kwa asilimia 50 ili kundi hili liendelee kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu”.Alisisitiza Bi.Sihaba

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula alipongeza hatua zilizofikiwa na kuona kuwa ni mpango mzuri utakao fikia malengo yaliyokusudiwa ya kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

“Niipongeze Serikali kwa kuendelea na jitihada hizi ikiwemo kuwepo kwa mwongozo huu ambapo utatupa dira ya kuyafikia malengo yaliyokusudiwa juu mapambano ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto”.Alieleza Dkt. Zainabu.

AWALI:Mwongozo huo ulizinduliwa rasmi tarehe 13 Desemba, 2016 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es Salaam.

Read More

MWONGOZO WA URATIBU WA MPANGO KAZI WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WAJADILIWA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua  akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kilichofanyika tarehe 27 Julai, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) alipokuwa akielezea lengo la Mwongozo huo Julai 27, 2017 Mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Makatibu Wakuu cha Kupitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) alipokuwa akielezea lengo la Mwongozo huo Julai 27, 2017 Mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akionesha kitabu cha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwa wajumbe wa mkutano wa kupitia na kujadili mwongozo huo kilichofanyika Julai 27, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Atupele Mwambene akiwasilisha Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa wajumbe wa kikao cha kuujadili na kuupitisha mwongozo huo kilichofanyika tarehe 27 Julai, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

atibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akipitia Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuujadili kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Julai 27, 2017.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Obey Assery (wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuupitia na kuujadili mwongozo huo kilichofanyika Julai 27, 2017 Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainabu Chaula akichangia hoja wakati wa kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao cha Makatibu wakuu walipokutana kuujadili na kuupitisha mwongozo huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akichangia hoja wakati wa kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wakati wa kikao cha kuujadili mwongozo huo kilichjofanyika Julai 27, 2017 Dodoma.

Mkurugenzi wa Anuai za Jamii Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Anne Mazalla akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Kikao cha kujadili Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (hayupo pichani) Julai 27, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Read More

Wednesday, July 26, 2017

PROGRAMU ZA ELIMU YA JUU ZIWEZESHE WAHITIMU KUJIAJIRI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha kwamba programu zote zinazotolewa na taasisi za elimu ya juu zinawawezesha wahitimu kujiajiri na kuwa na sifa za ushindani katika soko la ajira kimataifa.

Amesema wakati umefika sasa kwa wasomi katika vyuo vyetu vikuu tujiridhisha kuwa mitaala inayotolewa kama inawaandaa wahitimu kupata taaluma na stadi za kuweza kujiajiri na kupambana na changamoto za kimaisha.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 26, 2017) wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya Elimu ya Juu, jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi za elimu ya juu nchini ziangalie mitaala yake na kuimarisha mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ili kwenda sambamba na dunia ya kazi inayoendana na agenda ya maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu amesema maonesho hayo ni jukwaa la kipekee ambalo litaibua mjadala sahihi kuhusu uhalali wa kozi zinazotolewa na vyuo husika vya elimu ya juu. “Hivyo mnayo nafasi ya kuonesha kwa vitendo uwezo wenu katika utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia zinazotumika katika maendeleo ya viwanda.”

Amesema ni vema mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ukaimarishwa ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada kwenye sekta ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.

Amesema taasisi za elimu ya juu ziweke mikakati ya kuinua na kuboresha taaluma  wanayoitoa ili ilete tija kwa maendeleo ya Taifa na Dunia. Pia kuanzisha program za mafunzo zenye kukidhi mahitaji na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi hizo kuendelea kuimarisha mfumo wa udahili na kujipanga kutumia fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya nchi kwa makundi yote ya jamii kwa usawa katika ngazi zote hususan ufundi, hisabati, sayansi na teknolojia.

Pia Waziri Mkuu amesema ni wakati muafaka kwa taasisi za elimu ya juu nchini kuandaa mikakati ya kuongeza udahili kwa kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu na ujuzi unaohitajika katika sketa zinazokua haraka mfano mafuta, gesi na madini.
Read More

MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA VYUO VIKUU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu mtambo wa kuamia ndege waharibifu wa mazao kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Tekinolojia ya Dar es salaam (Dar es salaam Insititute of Technology), Profesa  Preksedis Ndomba  (kulia) wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles  Mwijage.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage  (kulia kwake) pamoja na Viongozi wa TCU wakiimba wimbo wa taifa kabla ya Waziri Mkuu kufungua Maonyesho ya Vyuo Vikuu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea mabanda kabla ya kufungua Maonyesho ya Vyuo Vikuu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julai 26, 2017.
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya viongozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwenye viwanja vya  Mnazi Mmoja jijini Dr es salaam Julai 26, 2017.


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya viongozi na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika kwenye viwanja vya  Mnazi Mmoja jijini Dr es salaam Julai 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja  kufungua Monyesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es salaam Julai 26, 2017.


Read More

Monday, July 24, 2017

MAJALIWA AKUTANA NA MWALIMU WAKE WA SEKONDARI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwalimu  wake, Agrias Sichone ambaye alimfundisha katika Shule ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1977 hadi 1980. Alikuwa katika kikao cha  kuhitimisha ziara yake mkoani Songwe kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise mkoani humo Julai 24, 2017.  kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwalimu  wake, Agrias Sichone ambaye alimfundisha katika Shule ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1977 hadi 1980. Alikuwa katika kikao cha  kuhitimisha ziara yake mkoani Songwe kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise mkoani humo Julai 24, 2017.  kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.

Read More

WAZIRI MKUU AELEKEZA NAMNA YA KUMALIZA MGOGORO ARDHI KATI YA WANANCHI NA KIWANDA CHA SARUJI MBEYA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa maelekezo ya namna ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka sita, kati ya uongozi wa Kiwanda cha Saruji Mbeya na wananchi wa kijiji cha Nanyala, wilayani Mbozi.

Mgogoro huo, umetokana na Kiwanda cha Saruji Mbeya, kupewa  eneo la kijiji hicho chenye ekari 2,315 na uongozi wa mkoa wa Mbeya bila ya makubaliano na wanakijiji hali iliyosababisha wagome kuondoka.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa Mikoa ya Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  na wa Mbeya Bw. amos Makalla kukutana na kufanya mazungumzo ya kulirudisha eneo hilo mkoa wa Songwe.

Waziri Mkuu alitoa uamuzi huo leo (Jumatatu, Julai 24, 2017) baada ya wananchi wa kijiji hicho kuzuia msafara wake kwa lengo la kumuelezea changamoto yao ya kudhulumiwa ardhi yao na kukabidhiwa kwa muwekezaji bila ya kushirikishwa.

Amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ni sikivu na inawajali wanyonge ndio maana amesimama ili aweze kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi, hivyo amewaomba  waendelee kuiamini na watarudishiwa ardhi yao.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Kampuni ya Saruji Mbeya kuondoa kesi iliyoifungua mahakamani dhidi ya wananchi wa eneo hilo, ili waweze kukutana na Serikali pamoja na wananchi hao kwa ajili ya kujadili namna bora ya uwekezaji katika eneo hill.

Amesema kiwanda hicho kilipewa eneo hilo la mkoa wa Songwe kimakosa na mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kupata malighafi ya kutengenezea saruji, amesema Serikali haiwazuii kulitumia eneo hilo ila wakubaliane na wananchi kwanza.

“Hatuzuii kiwanda kufanya kazi ila tunataka mkubaliane na wananchi kwanza ili kuondoa migogoro. Wananchi wanahitaji viwanda ila si kwa migogoro. Wananchi nawaomba muendelee kuwa na amani na hakuna atakayechukua ardhi yao bila ya ridhaa yao.”

Eneo hilo lilikuwa mali ya Serikali toka mwaka 1987, ambapo wakati Kampuni ya Saruji Mbeya ilikuwa inamilikiwa na Serikali, kabla ya kubinafsishwa.

Wananchi hao wamesema wamefurahishwa na uamuzi huo wa Waziri Mkuu wa kutatua mgogoro huo ambapo wananchi hao walidai kwa muda mrefu ulikuwa ukiwasumbua kwa kutakiwa kuondoka katika eneo lao bila na kukabidhiwa kwa muwekezaji bila ya kushirikishwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe amemshukuru Waziri Mkuu kwa kulitolea tamkoa suala hilo na kwamba atakutaka na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hili ili wananchi waweze kuishi kwa amani katika ardhi yao.

Read More

LORI LAPINDUKA DARAJA MTO SONGWE NA KUZIBA BARABARA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipenya  ili kuvuka  katika daraja la mto Songwe kwenye mpaka wa  mikoa ya Mbeya na Songwa  baada ya Lori lililokuwa limebeba vinywaji baridi   kupinduka katika  daraja hilo na kuziba barabara.   Ajali hiyo ilisababisha msururu mrefu wa magari  yaliyokuwa yakitoka Tunduma na yale yaliyokuwa yakitoka Mbeya Julai 24, 2017.
Msururu wa magari uliosababishwa na  ajali ya lori lililopinduka  kwenye daraja la mto Songwe katika barabara Mbeya- Tunduma Julai 24, 2017. Lori hilo lilikuwa limebeba vinywaji baridi. 
Msururu wa magari uliosababishwa na  ajali ya lori lililopinduka  kwenye daraja la mto Songwe katika barabara Mbeya- Tunduma Julai 24, 2017. Lori hilo lilikuwa limebeba vinywaji baridi.


Read More

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA SONGWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu  Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto kwake ni mkewe Mary na watatu kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24, 2017.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi    katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi.

 Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao  katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017.

Read More

Sunday, July 23, 2017

MKE WA WAZIRI MKUU AWASIHI WANAFUNZI KUTOKATISHA MASOMO

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.

Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.

Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017) alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.

Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.

“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”

Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”

Alisema ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.

Mke wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya juu watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.

“Kilichonifurahisha zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa hiyo inavyoona wanafunzi wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba msome kwa bidii.”

Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.
Read More