Friday, October 26, 2018

WATANZANIA TUENDELEZE UTAMADUNI WETU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuuheshimu na kuuendeleza utamaduni ambao ndio urithi wao ili kulifanya Taifa liendelee kuwa hai.

Amesema suala la kuuenzi utamadini ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine hususan wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.

Waziri Mkuu aliyasema yao jana jioni (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) alipotembelea shughuli za tamasha la utamadini wa Mtanzania kwa jamii ya watu wa Lindi.

Katika tamasha hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania waendelee kuupenda utamaduni wao.

“Nimefurahi kuona nyumba zikiwa na zana mbalimbali za kitamaduni ambazo zilikuwa zikitumiwa na wazee wetu pamoja na namba ya utayarishaji wa vyakula vyetu vya asili.”

“Sikutarajia kuona haya ninayoyaona, nawashukuru wote walioshiriki katika kandaa tamasha hili pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Kijiji cha Makumbusho.”

Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ambalo limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda katika Kijiji cha Makumbusho kwa ajili ya kujifunza historia ya mkoa wa Lindi pamoja na fursa zilizoko.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za uwekezaji.


 (mwisho)
Read More

Thursday, October 25, 2018

MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Ripoti ya Kamati iiyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara (kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera na Uratibu, Profesa Faustin Kamuzora na  wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera  na Uratibu) Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Kamati  iliyoundwa na Serikali  Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali, George Waitara  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. 

Read More

WAZIRI MKUU APOKEA RIPOTI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa  ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.

Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.

Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.

“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi.

MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa.

Septemba 24 mwaka huu Waziri Mkuu alitangaza kamati ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo iliyoongozwa na Jenerali mstaafu, Waitara.

Akitangaza majina hayo kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Waziri Mkuu alisema wajumbe hao wanapaswa kuikamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Aliwataja wajumbe wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe, Bw. Joseph Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Wakili Julius Kalolo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Queen Mlozi.

Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uratibu Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu Hussein.



 (mwisho)
Read More

Wednesday, October 24, 2018

TANZANIA HAKUNA UBANAJI WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI-MAJALIWA

*Asisitiza kwa  atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.

Amesema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 24, 2018) katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Tunapenda kuwahakikishia kuwa, Serikali ya Tanzania inaongozwa na katiba na sheria za nchi ambazo zinatoa uhuru wa kujieleza na kupata habari,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba mwananchi yeyote atakayeenda kinyume na sheria, Serikali itamuwajibisha kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Amesema Serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na ule wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. 

Sambamba na kusimamia haki hizo, Serikali imeendelea kutekeleza wajibu wake katika kuiwezesha jamii kuishi salama kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.

Amesema kukuza, kuimarisha na kulinda haki za binadamu ni wajibu wa Serikali na kwa kuzingatia umuhimu huo mwaka 1984 iliingiza sheria ya haki za binadamu katika katiba.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwa zoezi la kuwarejesha wakimbizi wa Burundi nchini kwao lilikuwa ni la hiari na limetekelezwa baada ya hali ya amani kurejea.

Amesema hakuna sababu ya kuendelea kuwahifadhi wakimbizi ambao kwa hiari yao wameamua kurejea nchini kwao ili wakaendelee na shughuli za kulijenga Taifa lao.

“Nasisitiza kuwa zoezi hili ni la hiari. Tangu mwezi Septemba mwaka jana, Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Burundi na UNHCR imekuwa ikiwarejesha wakimbizi hao kwao.”

Amesema zoezi hilo limekuwa likifanyika kwa kuzingatia usalama na utu wa wakimbizi hao. Wakimbizi 52,283  wa Burundi wamerejea nchini kwao kati 81,281 waliokwisha jiandikisha.
Waziri Mkuu ameyasema hayo baada Serikali kupokea shutuma katika siku za hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya jamuiya ya kimataifa kuhusu uendeshaji wa zoezi hilo.

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa na washirika wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa mujibu wa mkataba wa UN wa mwaka 1967 wa kuwahudumia wakimbizi ili kufanikisha zoezi hilo la kuwarejesha makwao kwa hiari na kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu.

Maadhimisho hayo ya siku ya Umoja wa Mataifa ambao umetimiza miaka 73 tangu uanzishwe yalihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro.

Wengine ni Mratibu wa Mkaazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodrigues pamoja na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini.


Read More

Tuesday, October 23, 2018

MAJALIWA AFUNGUA MAONESHO YA SIDO MKOANI SIMIYU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye  uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonesho ya Shirika la  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018.

Badhi ya wananchi wa  mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)  kwenye uwanja wa Nyakabindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea jembe la asili kutoka mhunzi,  Mashaka Daniel wa  Bukoba katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO)  aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018.




Read More

WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)lijielekezekatika kubuni teknolojia na mitambo rafiki inayolenga kutatua changamoto za wajasiriamali kulingana na mazingira yao. 

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za SIDO lakini bado kuna  changamoto za wajasiriamali wadogo ambazo lazima zishughulikiwe kwa kasi kubwa ili kufungamanisha shughuli za SIDO na uchumi wa Viwanda

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 23, 2018) wakati akifungua Maonesho ya SIDO kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi vilivyoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na wajasiriamali 500.

Amesema ili kufikia uchumi wa kati inambidi kila Mtanzania mahali alipo afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Tusipoteze wakati kwa kufanya mambo yasiyo na tija. Tuzingatie falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu.”

“Mfano kwa hapa Bariadi, tunatarajia SIDO watuletee teknolojia na mitambo inayoweza kurahisisha ukamuaji wa mafuta yanayotokana na mbegu za alizeti na pamba, kwa Dodoma taknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata zabibu.”

“Kigoma pelekeni teknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata mbegu za michikichi na kwenye maeneo yanayolimwa korosho teknolojia na mitambo  ya kubangua korosho na maeneo kama Ilula ambayo yanazalisha nyanya kwa wingi wapate teknolojia na mitambo ya kusindika na kuhifadhi nyanya na mbogamboga.” 

Waziri Mkuu amesema ili nchi iweze kupata mafanikio, SIDO inatakiwa iwaunganishe wajasiriamali na taasisi mbalimbali za fedha ili wapate mikopo yenye masharti nafuu. “Mahitaji ni makubwa hivyo lazima SIDO ishirikiane na taasisi nyingine ikiwemo Baraza la uwezehaji Wananchi Kiuchumi. (NEEC).”

Pia, Waziri Mkuu amewasihi wajasiriamali wanaoshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo kujifunza namna nzuri ya kuboresha viwango vya bidhaa zao na kubadilishana ujuzi na uzoefu, kupanua masoko na kubaini teknolojia zitakazorahisisha uzalishaji wa bidhaa. 
‘’Kumbukeni kuwa Serikali ina matarajio makubwa katika sekta ya viwaanda hususan katika kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.’’ 

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mabanda mbalimbali ya washirii wa maonesho hayo yakiwemo ya taasisi za Serikali zinazotoa huduma katika sekta ya viwanda na biashara zikiwemo Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO); Shirika la Viwango Tanzania  (TBS) 

Mamlaka ya Vyakula na Dawa (TFDA), Wakala wa Vipimo (WMA); Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan-Trade); Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Balaza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). 

Waziri Mkuu ametoa wito kwa taasisi hizo zikikishe zinafanya kazi kwa kushirikiana, ujuzi na weledi mkubwa katika kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuendesha shughuli zao kwa viwango vinavyotakiwa. 

“Jukumu la mamlaka za Serikali ni kufundisha, kuwalea na kuwaelekeza wajasiriamali wa kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”


Read More

Monday, October 22, 2018

USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.

“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya  Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na   Serikali ni muhimu.”

Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza inawajibu wa kuhakikisha kwamba maeneo ya mkoa huu yanaendelea kuwa salama.

Pia, Waziri Mkuu amempongeza Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Bin Mussa Kabeke kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

“Nakupongeza kaimu sheikh wa mkoa kwa kuteuliwa na ninakutakia kila la heri katika kazi yako na kwamba dhamana yako kubwa ni kuwaunganisha waislamu na waumini wa dini zote.”



 (mwisho)
Read More

MAJALIWA AWASILI JIJINI MWANZA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hasani Bin Mussa Kabeke wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  Oktoba 22, 2018 akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.   Sheikh huyo amechaguliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  (katikati) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.

Read More

Sunday, October 21, 2018

WAZIRI MKUU AAGIZA KUBOMOLEWA KWA UZIO NA KUSITISHA UJENZI

*Ni baada ya kujengwa kwenye eneo la wazi na kuziba barabara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo.

Uzio huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia umeziba barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 21, 2018) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini Dodoma, ambapo alitembelea eneo hilo na kuagiza libomolewe na lisalie kama inavyoonekana katika ramani na aliyeuziwa atafutiwe eneo lingine.

“Huu mji umejengwa kwa ramani, hamuwezi kubadili ramani kwa lengo la kumpa mtu eneo. Kwa nini mmeziba barabara ya tisa na huu mji unatambulika kwa barabara, sasa bomoeni hapa nataka barabara iendelee kutumika na eneo la kuchezea watoto libaki wazi,”

Waziri Mkuu amemuagiza mkurugenzi wa jiji ahakikishe wanayatumia maeneo ya wazi kwa ajili ya kujenga sehemu za mapumziko ili kuwawezesha wananchi kupata maeneo ya kupumzika mara wanapomaliza kufanya shughuli zao za kikazi.

Amesema ni vema jiji likatenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko. “Msifanye makosa kama yaliyofanyika Dar es Salaam.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipangomiji wa jiji la Dodoma, Bw. Joseph Mafulu alimuonyesha Waziri Mkuu ramani ambayo iliyotolewa na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ambayo ilibadilisha matumizi ya eneo hilo na kumpa muwekezaji.

Baada ya Bw. Mafulu kuonesha ramani hiyo Waziri Mkuu alitoa ramani halisi ya jiji la Dodoma ambayo inaonesha eneo hilo ni la wazi na ni mahususi kwa ajili ya michezo ya watoto, hivyo alisisitiza kuwa litumike kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu aliwaonya watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kutorudia makosa yaliyofanywa na CDA na kwamba jukumu lao ni kuhakikisha wanayasahihisha makosa yaliyofanywa na mamlaka hiyo ili jiji liweze kupangika vizuri.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Kunambi aliahidi kuyafanyia kazi kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kesho (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) ataandika barua kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi kwa ajili ya kufuta hati ya eneo hilo na muwekezaji watampa eneo lingine.

Awali,Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wabadilike na wasimamie vizuri rasirimali za umma pamoja na kuwahamasisha na kuwasisitiza wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu alisema mtumishi asiyeweza kufanya kazi kwa bidii anaweza kupata matatizo kwa sababu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini pamoja na mameneja wasimamie vizuri utendaji kazi wa watumishi mbalimbali katika maeneo yao. Alisisitiza kuwa lazima watumishi wafanye kazi na matokeo yaonekane.

Pia Waziri Mkuu alifungua ofisi kuu ya kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makutupora na kisha alitembelea kiwanda cha kusindika zabibu cha Alko Vintage na kukagua uzalishaji wa mvinyo katika kiwanda hicho kilicho jijini Dodoma.


 (mwisho)
Read More

Saturday, October 20, 2018

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO

*Ni wale washio nje ya kituo, wawe wamehamia ifikapo Desemba 15 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametoa siku 25 kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

Pia amemkabidhi Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chamwino.

“Ifikapo Desemba 15 mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi.”

Waziri Mkuu amesema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa kwenye utumishi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato.

Amesema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielekroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

Pia Waziri Mkuu amekagua barabara za mitaa katika mji wa Chamwino zenye urefu wa kilomita 3.5 zinazojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.

Baada ya kukagua barabara hizo, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa miundombinu ya majengo ya kituo cha Chamwino na kisha kuzungumza na wananchi waliofika  kituoni hapo. 




 (mwisho)
Read More

Friday, October 19, 2018

WAZIRI MKUU AMKABIDHI WAZIRI JAFO ORODHA YA WATUMISHI WALIOGOMA KUHAMIA KITUO CHA KAZI

*Ni wa halmashauri ya wilaya ya Bahi waliogoma kuhamia kituo cha kazi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ili awachukulie hatua baada ya kugoma kuhamia katika kituo chao cha kazi na kuendelea kuishi jijini Dodoma.

Amemkabidhi orodha hiyo leo (Ijumaa, Oktoba 19, 2018) baada ya mkuu wa wilaya hiyo Bibi Mwanahamisi Mukunda kusoma taarifa ya wilaya, ambayo pamoja na mambo mengine alieleza kuwa watumishi wote wameshamia kwenye kituo chao cha kazi na wanaishi. Waziri Mkuu alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo.

“Mkuu wa wilaya umedanganywa watumishi bado wanaishi jijini Dodoma, walichokifanya baadhi wamejiunga watatu na wamekodi chumba kimoja. Namkabidhi Waziri wa TAMISEMI orodha ya watumishi hawa ambao wamegoma kuishi kwenye kituo chao cha kazi ili uwashughulikie”

Waziri Mkuu amesema watumishi hao wamegoma kuhamia katika kituo chao cha kazi licha ya Serikali kuwataka kufanya hivyo.”Maelekezo hatuyatoi kwa ajili ya kujifurahisha, bali tunataka utekelezaji ufanyike ili wananchi waweze kuhudumiwa ipasavyo.”

Jumatano, Juni 27, mwaka huu, Waziri Mkuu wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, aliwaagiza watumishi wa Halmashauri hiyo wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wahamie kituoni kwao.

Waziri Mkuu alisema Serikali inataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. “Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi jijini Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo Julai 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi wakiwemo madiwani na wakuu wa idara wahakikishe wanamaliza tofauti zao na washirikiane katika kufanyakazi kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.

Awali, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Mpalanga yenye uwezo wa kukaliwa na walimu sita, ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi huo. Mradi huo unagharimu zaidi ya sh. milioni 140.

Pia Waziri Mkuu amezindua daraja la Chipanga ambalo ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 2.18 na kisha alitembelea kituo cha Afya cha Bahi ambako alikagua wodi ya wazazi na kuzungumza na akinamama ambao waliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya.



(mwisho)
Read More

ZIARA YA MAJALIWA WILAYANI BAHI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka  katika moja kati ya nyumba sita za walimu alizozikagua katika Shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi  Athumani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa nyumba sita za walimu katika shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua  daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na wapili kushoto ni Mbunge wa Bahi,   Omary Badwel. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Bahi, Kassim Kolowa  (kushoto) kuhusu vifaa vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji cha Kituo hicho  wakati alipokitembelea, Oktoba 19, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Bibi Subi Mchome, ambaye ni mmoja wa wazazi waliojifungua salama katika wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya cha Bahi  mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim Kolowa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mtalaam wa Maabara, Petronila Olomi  (kushoto) wakati alipotembealea Maabara ya Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Selemani Jafo na Wapili kushoto ni Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Kassim  Kolowa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ambao bado hawajahamia Bahi na wananishi mjini  Dodoma licha ya serikali kuwataka wahame, ili awachukulie hatua. Alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo, Oktoba 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa  wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa  wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wagonjwa wa nje wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bahi mkoani Dodoma, Oktoba 19, 2018.



Read More

Thursday, October 18, 2018

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO ZA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

NA.MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria kumaliza changamoto za ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kushirikia na wadau wanaohusika na masuala ya wanawake na watoto nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Patrick Golwike alipokuwa akifungua kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Taifa ya ulinzi wa wanawake na watoto kilichofanyika Oktoba 17, 2018 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya makundi hayo.
Kamati hiyo imekutana kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi huo unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) na changamoto zinazotokana na vitendo hivyo.
Aidha, Miongoni mwa maeneo muhimu yaliyojadiliwa katika mpango kazi huo ni pamoja na kuhakikisha maeneo nane ya kimkakati yanafikiwa ili kufukia malengo ya kupunguza aina zote  za ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020, na kuwataka wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na vita ya ukatili kwa wanawake na watoto.
Maeneo ya utekelezaji yaliyoainishwa ni pamoja na; uimarishaji wa uchumi wa Kaya, kupinga mila na desturi zinazomkandamiza  mwanamke na mtoto, kuhakikisha mazingira salama sehemu za umma, kuimarisha mahusiano mema na kuziwezesha familia katika malezi bora, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji huduma kwa waathirika wa ukatili pamoja na mazingira salama shuleni na stadi za maisha.
“Wajibu wa wadau wote wenye kutekeleza afua za kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutumia mwongozo huu katika maeneo mnayosimamia kwani utarahisisha katika utekelezaji wa majukumu yetu na kuhakikisha maeneo nane yaliyoainishwa yanafikiwa kikamilifu”.Alisisitiza Golwike
Aliongezea kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili nchini kupitia Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Mipango ya Kisekta ikiwemo uanzishwaji wa madawati ya Jinsia na watoto katika kila Wizara na katika vituo vya polisi 417, kuandaliwa kwa sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) na Sera ya Mtoto ya mwaka 2008.
Jitihada nyingine ni pamoja na uanzishwaji wa mifumo ya ulinzi wa mtoto katika Halmashauri 63 nchini pamoja na uanzishwaji wa Mahakama za kusimamia kesi za watoto katika Halmashauri 131.
Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa Dawati la Jinsia na Watoto Bi.Happiness Mugyabuso aliongezea kuwa ili kufikia malengo ya kutokomeza ukatili kwa makundi hayo ni vyema mpango kazi huo ukatekelezwa kwa vitendo ili kutorudisha nyuma jitihada za Serikali.
“Ni vyema sasa mpango kazi huu ukajadiliwa kwa kina ili kufikia malengo na kuwa miongozo mizuri itayotoa utaratibu wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji”.alisistiza Mugyabuso
Aidha, alieleza kuwa wadau wanaotekeleza mpango huu ni pamoja na  Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaoshughulikia masuala ya wanawake  na watoto, Mashirika ya Kimataifa , Asasi zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi, Taasisi za Dini na Wanawake kwa pamoja wamekuwa ni chachu katika vita dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto nchini.
=MWISHOI=
Read More

Monday, October 15, 2018

SUKOS YAKABIDHI VIFAA VYA ZIMAMOTO IDARA YA URATIBU WA MAAFA NCHINI



Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akizungumza jambo wakati wa kukabidhi vifaa vya zima moto pamoja na hati ya shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Utafiti) Idara hiyo  Bw.Bashiru Taratibu walipotembelea Oktoba 15, 2018.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji - SUKOS, Suleiman Kova akimkabidhi vifaa vya zima moto Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto katika maeneo ya kazi.

Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Utafiti Idara ya Uratibu wa Maafa Bw.Bashiru Taratibu akiangalia vifaa vya zima moto vilivyokabidhiwa na Taasisi ya Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji –SUKOS Oktoba 15, 2018 kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Oparesheni Bi.Rahma Kova wakati wa kukabidhi cheti cha Shukrani ya ushirikiano uliopo kati ya SUKOS  na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akikabidhi Hati ya Shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe walipomtembelea kukabidhi vifaa vya zima moto Ofisini kwake Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa SUKOS Foundation walipotembelea Idara hiyo ili kukabidhi Vifaa vya Zima Moto pamoja na hati ya shukrani kwa namna Taasisi yake inavyoshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Suleiman Kova.




Read More