Friday, September 11, 2020

WADAU WA UWEKEZAJI SEKTA YA UMMA WARIDHISHWA NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI SERA YA TAIFA YA UWEKEZAJI YA MWAKA 1996

 


OWM, DODOMA.

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji imekutana na wadau wa uwekezaji wa sekta ya Umma kwa lengo la kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996. Wadau hao ni kutoka Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Baada ya kupokea taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Sera hiyo,wameridhishwa kwa jinsi ilivyobainisha nchi inavyoweza kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.

 

Wakipongeza wakati wa kujadili taarifa hiyo, leo tarehe 11 Septemba, 2020 jijini Dodoma. Wadau hao wamesisitiza Tathmini hiyo iliyojikita kwenye masuala ya kisera, kisheria na kiutendaji inaendelea kutoa mapendekezo ya kuendelea kutatua changamoto za uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya Uratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Utangazaji wa Fursa za Uwekezaji, Uwezeshaji Uwekezaji, pamoja na Vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi.

 

Akiongea wakati akifungua kikao kazi hicho, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Bibi Dorothy Mwaluko amesisitiza kuwa upo umuhimu wa wadau hao kubainisha masuala ya kisera, kiutendaji na kisheria, ili kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya uwekezaji na Sheria ya Uwekezaji nchini haikinzani na sheria nyingine za kisekta kwenye masuala ya uwekezaji.

 

“Serikali imekuwa ikitunga Sera na Sheria kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini, tunahitaji kuwa na Sera madhubuti za kuvutia na kuwezesha uwekezaji katika sekta zote ili kutumia vilivyo fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.”Amesisitiza Mwaluko.

 

Akiongea kwenye kikao kazi hicho Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje, amefafanua kuwa kukutana kwa wadau hao kujadili taarifa ya tathmini hiyo kutawezesha kujua changamoto wanazozipata wakati wa utekelezaji wa sera hiyo na hatimaye utatuzi wake, utawezesha uwekezaji na kuleta tija kwa mwananchi wa kawaida.

 

Naye Mkurugenzi wa Uwezeshaji Uwekezaji, kutoka Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (EPZ), James Maziku amefafanua kuwa, sera hiyo imetungwa kwa muda mrefu hivyo tathmini hiyo itasaidia kuhuisha (Review) Sera na Sheria za uwekezaji za kisekta, kupunguza migongano ya kiutendaji na kuelewa namna ya kuboresha utendaji wa pamoja wa kisekta.


Sera ya Taifa ya Uwekezaji imebainisha malengo mahsusi sita (6) na malengo nane (8) ya kisekta. Baadhi ya malengo hayo ni kuhamasisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje; Kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi; Kuhimiza na kuvutia matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwekezaji; Kuweka mfumo mzuri na wa wazi wa kisheria; na kuondoa urasimu katika taratibu za upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.

 

Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997 iliyoanzisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), vinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali. Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimepewa jukumu la kuratibu, kuvutia, kutangaza na kuwezesha wawekezaji hapa nchini.

 

MWISHO.

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji),  Dorothy Mwaluko, akifungua warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, leo tarehe 11 Jijini Dodoma, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baadhi ya washiriki wa  warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi  kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  warsha  hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi akieleza umuhimu wa wadau kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  wakati wa  kikao kazi ikilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa  warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia kikao kazi  kilicholenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  warsha  hiyo imeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mratibu wa Masuala ya Uwekezaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jumanne Gomera, akiwasilisha wasilisho la taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  wakati wa warsha  ya wadau wa uwekezaji sekta ya Umma kujadili taarifa  hiyo, kikao kazi hicho kimeratibiwa  na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa  kikao kazi cha wadau wa uwekezaji sekta ya Umma wakifuatilia Warsha iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996,  kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Mkurugezi wa Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi  na Mtaalamu wa Utafiti wa masuala ya sheria ya uwekezaji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Saudin Mwakaje wakiteta jambo wakati wa kikao kazi cha  wadau wa uwekezaji sekta ya Umma iliyolenga kuidhinisha taarifa ya Tathmini ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 11 Jijini Dodoma.

Read More

Wednesday, September 2, 2020

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAGUGU

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magugu wilayani Babati waliojipanga  barabarani wakimtaka asimame  na kuzungumza nao, Agosti 2, 2020.  Alikuwa  akitoka Babati kwenda Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magugu wilayani Babati waliojipanga  barabarani wakimtaka asimame  na kuzungumza nao, Agosti 2, 2020.  Alikuwa  akitoka Babati kwenda Mto wa Mbu wilayani Monduli kuzindua Kampeni za CCM wilayani humo.

 

Read More

Tuesday, September 1, 2020

MAJALIWA AVUNJA MAKUNDI CCM BABATI

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa  na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul (katikati) na   Esther Mahawe (kushoto) wakati alipowaasa  wanaCCM wote waliotia nia ya kugombea ubunge wa Jimbo hilo  waondoe tofauti zao  na wamuunge mkono mgombea aliyeteuliwa na CCM . Alikuwa akizindua Kampeni za CCM katika Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul akikumbatiana na  Esther Mahawe, mmoja wa wanaCCM waliotia nia ya kuomba uteuzi wa Chama wa kuwania ubunge katika Jimbo hilo katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM mkoani Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020.

 

Read More

Friday, August 28, 2020

NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI AKUNWA NA MAFUNZO KAZINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

 

Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya mafunzo ya kujenga uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa maafisa 36 kutoka idara na vitengo vya ofisi hiyo. Mafunzo hayo ya wiki moja yamefanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Agosti 2020, Jijini Dodoma, ambapo Wakala wa Serikali ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) waliendesha mafunzo hayo kwa ufadhili wa Shirika la Chakula Duniani. 


Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kujenga uwezo kwa maafisa wake katika maeneo ya Uchambuzi wa Sera, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Uandishi wa taarifa. Mafunzo hayo pia yamewezesha maafisa hao kuongeza umahiri wa utekelezaji majukumu waliyokasimiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 52, ambapo jukumu la msingi la Ofisi hiyo ni kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali katika sekta zote na Bungeni pamoja na majukumu mengine yaliyoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 144 Aprili 2016, lililofanyiwa mabadiliko tarehe 7 Oktoba 2017.


Akiongea wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, leo tarehe 28 Agosti  jijini Dodoma,  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli hakusita kueleza furaha yake juu ya utaratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendesha mafunzo kwa watumishi yanayolenga kujenga uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa.


“Nimevutiwa sana na mbinu zilizotumika katika ufundishaji wa mafunzo haya. Nimeambiwa katika kuhakikisha mnapata mbinu na umahiri kwenye Tathmini na Ufuatiliaji wa Sera, mmepitia Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa masuala ya Lishe. Naelewa Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo mratibu wa mpango huu na sisi TAMISEMI tunatekeleza. Nakusudia na mimi Kufanya mafunzo kama haya kwa watumishi wa wizara yangu” amesisitiza Mweli.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko amelishukuru Shirika la Chakula Duniani kwa ufadhili wa mafunzo hayo, ambapo   matokeo ya mafunzo hayo  ni Ofisi hiyo kuwa na mfumo bora wa uratibu wa shughuli za serikali kutokana na mamlaka iliyonayo kikatiba ya kuratibu shughuli zote za Serikali pamoja na masuala mtambuka ikiwemo masuala ya lishe.


“Mafunzo haya yatakuwa ni mwendelezo kwa   maafisa wote na menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lengo ni kuongeza umahiri kwa uchambuzi bora wa sera, ufuatiliaji na tathmini ya sera pamoja na kuwa na  mfumo bora wa mawasiliano ya utekelezaji wa majukumu kwa idara zote ndani ya Ofisi, pia na mfumo bora wa uratibu wa shughuli za serikali” amesisitiza Mwaluko.


Awali akiongea kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika amefafanua kuwa mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa utaratibu wa mijadala washiriki walipata fursa ya kufahamu mbinu za kimkakati za uchambuzi wa Sera na kanuni za uratibu wa Sera, njia za kufanya ufutiliaji na tathmini, vigezo vya kuzingatia katika kufanya tathmini na ufuatiliaji pamoja na  namna ya kuandika taarifa na muundo wa taarifa.


Wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye mafunzo hayo, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, Frank Mwega na Elilanga Kaaya  wamebainisha kuwa mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa washiriki katika kuwajengea uwezo. Aidha, wameshauri uendelevu wa mafunzo ya namna hiyo yenye kuwajengea uwezo watumishi kwenye maeneo ya utendaji.

MWISHO.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti, 2020.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, akimshukuru Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani, Neema Shosho, kwa ufadhali wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti, 2020.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli akisisitiza umuhimu wa ubora wa Uratibu wa shughuli za serikali wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko na kulia ni  Kaimu mkurugenzi mkuu  wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) Dickson Mwanyika,  


Baadhi Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).

Mchumi Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu. Frank Mwenga, akieleza umuhimu wa  mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo wakati wa kufunga mafunzo hayo  leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).

Mchumi Ofisi ya Waziri Mkuu. Elilanga Kaaya, akieleza umuhimu wa  mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo wakati wa kufunga mafunzo hayo  leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Gerald Mweli,   akimkabidhi cheti Afisa Habari Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Isabela Katondo,  baada ya kuhitimu mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji  na Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Gerald Mweli,   akimkabidhi cheti Afisa Utumishi Ofisi ya Waziri Mkuu Herman Chando, baada ya kuhitimu mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji  na Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).

Washiriki wa mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji  na Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu,  Gerald Mweli (mwenye tai),  kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti  2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).


Read More

Tuesday, August 25, 2020

MAJALIWA AREJESHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA RUANGWA

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Ruangwa, Frank Chonya ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, fomu za kuwania Ubunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia CCM,,wakati aliporejesha fomu hizo kwenye Ofisi ya Mukurugenzi huyo, Agosti 25,2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Ruangwa, Frank Chonya ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, fomu za kuwania Ubunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia CCM,,wakati aliporejesha fomu hizo kwenye Ofisi ya Mukurugenzi huyo, Agosti 25,2020.

Read More

Monday, August 24, 2020

MAAFISA OFISI YA WAZIRI MKUU WAPIGWA MSASA UTEKELEZAJI MAJUKUMU


Baadhi ya maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao(TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.

Mtaalamu wa masuala ya Sera kutoka Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) Apronius Mbilinyi akiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mafunzo hayo ya siku tano yanajikita katika namna ya kufanya Uchambuzi wa sera, Tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera hizo, utaalamu katika Uandishi wa Ripoti pamoja na namna bora ya  kutekeleza shughuli za Uratibu.  Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri  Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.

Baadhi ya maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo likiwa ni kutekeleza kwa ufanisi na weledi majukumu waliyokasimiwa. Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao, jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika akisisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kupata mafunzo ya kujenga uwezo kwa watumishi wa umma  lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo, jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.

Mchumi mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu, Happiness Mugyabuso akipitia makabrasha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa maafisa wa Ofisi hiyo, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri  Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa shughuli za serikali Paul Sangawe akisisitiza umuhimu wa ufanisi na weledi katika kutekeleza uratibu wa shughuli za serikali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa maafisa wa Ofisi hiyo, Mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri  Mkuu na kuendeshwa na Wakala hiyo jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Afisa Tawala Mwandamizi  ofisi ya Waziri Mkuu Stephen Magoha akichangia juu ya masuala ya Uratibu wa Ofisi hiyo wakati wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko wakati akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi hiyo na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2020.
Read More

Friday, August 21, 2020

MAJALIWA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE WA RUANGWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Ruangwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)  kutoka kwa Frank Chonya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa, Agosti 21, 2020.

Read More

Tuesday, August 18, 2020

WAZIRI MKUU: WATANZANIA TUBADILIKE, TUJIVUNIE VYETU

         *Akagua mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Bagamoyo


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wabadilike na wajifunze kujivunia kilicho chao. "Lazima tubadilike Watanzania, tuwe wazalendo, tukisemee kitu chetu, tujivunie kitu chetu na tujivunie ujuzi tulionao," amesema.

 

Ametoa wito huo leo (Jumanne Agosti 18, 2020) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Bagamoyo (BSL), katika kata ya Makurunge, wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.

 

Waziri Mkuu ambaye alifika kiwandani hapo na kukagua ujenzi wa kiwanda unaoendelea, pia alikagua miundombinu ya mradi wa shamba la miwa ikiwemo vitalu vya mbegu, miche, maabara ya kupima maji na udongo na miundombinu ya umwagiliaji.

 

"Ninasema tubadilike sababu nimeenda kwenye maabara yao na kukuta wataalamu wetu wako vizuri, wanafanya utafiti wa udongo, maji na mbegu. Wameelezea vizuri utafiti wao na matokeo tumeyaona ni mazuri.”

 

“Rais wetu alisema Watanzania tunaweza, na leo nimethibitisha kwamba Watanzania tunao uwezo wa kazi lakini tatizo letu hatuwezi kujisemea wenyewe. Lazima tujisifu, tujisemee kuhusu umahiri tulionao. Ni kwa nini tujidharau?", alihoji.

 

"Nataka tubadilike sababu Watanzania tunaweza. Baadhi yao wanatoka hapa hapa Bagamoyo. Nimemuuliza ulisoma wapi, akajibu Chuo cha Kilimo Kaole, na hiki kiko Bagamoyo. Wengine wanatoka SUA (Chuo cha Kilimo cha Sokoine). Lazima turingie nchi yetu, lazima tuitangaze nchi yetu na ni lazima tuisemee nchi yetu," amesisitiza.

 

Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa eneo hilo lenye hekta 10,000 ili lilimwe miwa na kujenga kiwanda cha sukari, ulilenga kuongeza uzalishaji wa sukari nchini. "Tunahitaji kupata mashamba mengi ya miwa ili tuongeze uzalishaji wa sukari nchini".

 

“Hivi sasa mahitaji ya suakri nchini yamefikia tani 450,000 kwa sukari ya mezani. Ile sukari ya viwandani ambayo inatumika kutengeneza soda, biskuti na pipi mahitaji yake ni tani 165,000 ambayo hapa nchini hatuizalishi, kwa hiyo inabidi tuiagize kutoka nje ya nchi.”

 

Amesema uzalishaji wa sukari ya mezani kwa sasa unafikia tani 380,000 kwa viwanda vyote vilivyopo na kwamba bado kuna bakaa ya tani 70,000. Amesema mbali ya viwanda vilivyopo vya TPC, Kagera, Mtibwa, Kilombero, Manyara na Bagamoyo bado kuna maeneo ya kulima miwa huko Tarime na Kigoma. “Tunawaalika wawekezaji walime miwa na kuzalisha sukari zaidi.”

 

Akielezea kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kazi inayofanyika na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutahakikisha sukari inapatikana kulekule na pia itatoa fursa ya kilimo cha miwa kwa wakazi wa maeneo jirani.

 

Amewataka maafisa kilimo waende wakatoe elimu kwa wananchi kuhusu kilimo cha miwa. “Wapeni uhakika wa soko ili wasisite kushiriki kwenye hiki kilimo. Wananchi watavutiwa wakijua kuna faida kwenye kilimo hicho lakini pia kiwanda kitapata tani za ziada na kuongeza uzalishaji wake,” amesisitiza.

 

Mapema, Mkurugenzi wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Abubakar Bakhresa alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia shamba hilo na kuahidi kuendana na dhamira ya Serikali ya kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari nchini.

 

Akielezea hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Hussein Sufian alisema gharama ya mradi huo ni dola za Marekani milioni 100 na kwamba hadi sasa wameshapata asilimia 70 ya mtaji.

 

“Benki ya Kilimo (TADB) imetukopesha dola za Marekani milioni 6.5, Benki ya CRDB wametukopesha dola za Marekani milioni 25, makampuni ya Bakhresa tumetoa dola za Marekani milioni 30 na benki ya Standard Chartered imetukopesha dola za Marekani milioni 10. Tunayashukuru mabenki za ndani kwa kukubali kutuunga mkono,” alisema.

 

Alisema kampuni yao mpaka sasa imetoa ajira kwa watu 600 ambapo 500 kati yao wanatoka kwenye vijiji jirani vinavyozunguka eneo la mradi na kwamba mara baada ya awamu ya kwanza kukamilika, uzalishaji utakapoanza wataweza kuajiri watu 1,500. “Awamu ya pili inatarajiwa kuwahusisha wakulima wa nje (outgrowers scheme) kwani mradi utawapa fursa ya kushiriki kilimo cha miwa na kupata soko la uhakika kutoka kiwandani,” alisema.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justin alisema mbali ya kiwanda hicho cha sukari, wamelenga pia kuwanufaisha wakulima wadogo wa miwa. “Kwa kawaida wenye mabenki wanaamini ili aweze kumkopesha mkulima ni lazima aone eneo lake analomiliki.”

 

“Sisi tumeona fursa, na tumeamua wakulima watakaopata mikataba baina yao na kiwanda cha sukari Bagamoyo, tutachukua mikataba hiyo iwe dhamana ya kupata mikopo ya kuendeleza mashamba yao. Hii ni kwa sababu kuna vijiji vitano tayari vimefanyiwa upimaji na kuna uwezekano wa hekta 3,600 zitakazotumika kulima miwa.”

 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kutoa eneo hilo ili BSL ianzishe kilimo cha miwa. “Tunamshukuru kwa sababu ametuongezea zao jingine la biashara.”

 

“Kabla ya hapo, tulikuwa na zao la korosho ambalo mwaka jana limewaingizia wakulima shilingi bilioni 60. Pia zao la ufuta liliwaingizia shilingi bilioni 19. Mwaka huu umetuita Tanga na kutuelekeza tuanzishe zao la mkonge, kwa hiyo kilimo cha miwa kimekuwa zao la nne mkoani kwetu na hivi sasa kuna kata tano ambazo ziko tayari kulima miwa.”

 

Read More

Monday, August 17, 2020

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA DINI

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Viongozi wa Dini Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kuunga Mkono Juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Ustawi wa Amani, Uzalendo na Kumtanguliza Mungu uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full  Gospal Bibble Fellowship, Zakary Kakobe akizungumza katika  Mkutano wa Viongozi wa Dini Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kuunga Mkono Juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Ustawi wa Amani, Uzalendo na Kumtanguliza Mungu uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020.

Mufti  na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir  Ally  akizungumza katika  Mkutano wa Viongozi wa Dini Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kuunga Mkono Juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Ustawi wa Amani, Uzalendo na Kumtanguliza Mungu uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Viongozi wa Dini Kuelekea Uchaguzi Mkuu na Kuunga Mkono Juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Ustawi wa Amani, Uzalendo na Kumtanguliza Mungu uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020.  Wa pili kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum.

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA MAHAFALI YA VYUO NA VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mic Mdegela ambaye ni Mwanachuo wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anayesoma kozi ya Menejimenti ya  Rasilimaliwatu baada ya kuzungumza  na kutoa vyeti katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu vya jijini Dar es salaam yaliyofanyika  kwenye kumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Kheri James.
MAJALIWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mic Mdegela ambaye ni Mwanachuo wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anayesoma kozi ya Menejimenti ya  Rasilimaliwatu baada ya kuzungumza  na kutoa vyeti katika Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu vya jijini Dar es salaam yaliyofanyika  kwenye kumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Kheri James.

Wanavyuo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika  Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu vya  jijini Dar es salaam yaliyofanyika  kwenye kumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu jijini vya Dar es salaam yaliyofanyika  kwenye kumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2020. 

Read More