Monday, February 26, 2018

WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI

Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi mjiniMorogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea,  Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizo chukuliwa na serikali  katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja mjiniMorogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Na. Mwandishi Maalum

Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo .


Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.


Akiongea wakati  wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati  la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na pia  kamati maalum ya wataalam hao imeundwa ili kuufatilia na kusimamia mpango huo.


“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye dhamana ya kuratibu maafa kama  ya magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali  za kuwakutanisha wataalam hawa ili  kuweza  kuijenga jamii salama  ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa wanyama kwenda  kwa  binadamu  kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.


Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa kati ya binadam na. wanyama.


Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.

Read More

Thursday, February 22, 2018

TANZANIA YAIPONGEZA FIFA KWA KUPAMBANA NA RUSHWA

SERIKALI ya Tanzania inalipongeza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na shirikisho hilo katika mapambano dhidi ya rushwa.
Kauli hiyo imetolewa leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa katika kikao chake na Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino kilichofanyika jijini Dae es Salaam.
“Serikali  tunaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo pamoja na matumizi mabaya ya fedha na ya madaraka yanayofanywa na FIFA”.
Waziri Mkuu amesema wanaunga mkono mapambano hayo ili Taifa liweze kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye maono ya mbali katika kuendeleza mchezo huo.
Amesema FIFA ambayo ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo , hivyo Tanzania inaiunga mkono kwa kuhakikisha sekta ya michezo inatumia vizuri fedha zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo.
Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inasimamia matumizi sahihi ya madaraka katika sekta ya michezo nchini ili kuleta maendeleo kwenye mpira wa miguu.
Serikali inaipongeza FIFA kwa jitihada za dhati za kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kuwa mipango mbalimbali ya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana wadogo wa kike na wa kiume nchini.
“Tunatambua msukumo wa FIFA wa kuendelea mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na kuboresha viwanja vya michezo pamoja na maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta hiyo.

Pia ameishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani jijini Dar es Salaam na kwamba Serikali itayasimamia vizuri na inajiandaa kwa kushinda.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa FIFA Bw. Infantino kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendesha mkutano mkubwa wa viongozi wa mpira wa miguu duniani Tanzania. Mkutano huo ulihusisha Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 21.
Pia alimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Bw. Ahmad Ahmad kwa jitihada zake za anazozifanya katika kuendeleza mpira barani Afrika na kwamba Serikali  ya Tanzania inamuunga mkono.
Rais wa FIFA Bw. Infantino ambaye ameahidi kuisaidia Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo aliwasili nchini leo alfajiri akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Bw. Ahmad Ahmad kwa ajili ya mkutano wa FIFA uliofanyika nchini Tanzania February 22, 2018.

Bw. Infantino amewasili kwa mara ya kwanza Tanzania toka awe Rais wa  FIFA na alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dtk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leodger Tenga na Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia.

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA FIFA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Kinyango Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA) Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Bandera ya FIFA kutoka kwa Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Jezi namba Tisa kutoka kwa Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania

Read More

Monday, February 19, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI YA MITINDO INAYOLEA NA KUSOMESHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI

 Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto Januari  wa Shule ya Msingi ya Mitindo wilayani Misungwi ambayo pia inawalea na kuwasomesha watoto wenye ulemavu wa ngozi , Februari 19, 2018. Mtoto huyo siku zote amesisitiza kwamba baada ya kumaliza masomo yake akiwa mtu mzima angependa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania .

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua madawati katika madarasa ya shule ya msingi ya Mitindo wilayani Misungwi baada ya kufungua bweni la wavulana shuleni hapo Februari 19, 2018. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hyo, S. Mafie.


Read More

MAJALIWA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ua Misungwi katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Mitindo Februari 19, 2018.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Read More

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA WILAYANI MISUNGWI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba lenye ukubwa w hekari 6 la  Bw. Muhoja Ngole (kulia kwa Waziri Mkuu) katika kijiji cha Mondo wilayani Misungwi, Februari 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Nyamanyinza wilayani Misungwi wakati alipowasili kwenye uwanja wa michezo kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo, Februari 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika – Misasi katika  kijiji cha Manawa  wilayani Misungwi, Februari 19, 2018. Wa pili kulia  ni mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa  wa Mwanza, John Mongella.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika- Misasi katika kijiji cha Manawa wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na wa pili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kiwanga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wa pili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi, Februari 19, 2018.


Read More

Saturday, February 17, 2018

WAZIRI MKUU AKIWA UKEREWE NA BUNDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakizungumza na Noella Tekela, mwanafunzi wa darasa la sita katika  shule ya msingi ya Masaunga wilayani Bunda baada ya kuwahutubia wavuvi, wafanyabiashara wa samaki na wananchi  kwenye kijiji cha Kisorya  Februari 17, 2018. Mtoto huyo alionekana akiandika kwa usahihi katika daftari hotuba yote ya Waziri Mkuu katika mkutano huo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmiliki wa Pantoni ya MV Nyehunge, Said Mohammed  kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri  na chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe Februari 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Pantoni ya MV Nyehunge  kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri na chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe Februari 18, 2018.

Read More

WAZIRI MKUU AAGIZA KUFUNGULIWA KWA ZAHANATI YA BUGABU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Magu, Dkt. Nindwa Maduhu ahakikishe zahanati Bugabu inafunguliwa leo.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Februari 17, 2018) wakati akiongea na watumishi na wananchi wa wilaya ya Magu katika kituo cha Afya cha Kahangara.

Alisema kama zahanati imekamilika na inavifaa vyote vinavyotakiwa katika utoaji wa huduma kwa nini watumishi wasipelekwe ili wananchi wahudumiwe.

Alitoa hilo baada ya wananchi kumuomba awasaidie kufunguliwa kwa zahanati ya kijiji chao ili waweze kupata huduma za afya karibu na makazi yao.

Wananchi hao walidai kuwa kwa sasa wanalazimika kutembea umbali wa kilomita tisa kufuata huduma za afya katika kituo cha Afya cha Kihangara.

Dkt. Maduhu alisema tayari watumishi walishahamishiwa katika zahanati ya kijiji hicho na leo watakwenda na kuanza kuwahudumia wananchi.

Pia Waziri Mkuu amemtaka mganga huyo kuhakikisha dawa zinazonunuliwa wilayani humo kulingana na magonjwa yanayopatikana ndani ya maeneo yao.

Kabla ya kuzungumza na wananchi na watumishi, Waziri Mkuu alikagua na kuweka jiwe la msingi la uboreshaji wa kituo cha Afya Kahangara.

Mradi wa kuboresha kituo hicho chenye uwezo wa kuhudumia watu 26,321 ulianza Oktoba 30, 2017 na umegharimu sh. milioni 500.
Read More

WAZIRI MKUU AKEMEA UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya uvuvi haramu wa kutumia sumu kali ndani ya ziwa Victoria kwa sababu vinaharibu soko la samaki.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Februari 17, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya wilayani Bunda mkoani Mara.

Alisema kitendo cha kuvua kwa kutumia sumu kinaharibu soko la samaki la ndani na nje ya nchi kwa sababu sumu hiyo inabaki hivyo kumuathiri mlaji.

Waziri Mkuu aliwaagiza Maofisa Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kutoa elimu kwa wavuvi wa eneo hilo juu ya madhara ya zana haramu za uvuvi.

Alisema baadhi ya wavuvi wanavua kwa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku, kokoro pamoja na mabomu jambo ambalo haliwezi kuvumilika kwa sababu zana hizo zinaharibu uhai wa viumbe hai ndani ya ziwa Victoria.

Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali tayari imeshaagiza nyavu zinazofaa kwa ajili ya uvuvi endelevu kutoka nje ya nchi ambazo zitauzwa kwa wavuvi mbalimbali.

Waziri Mkuu alisema wavuvi wote wanatakiwa kufuata sheria ikiwemo kuwa na leseni za uvuvi kwa vyombo vyao, hivyo  alimuagiza Afisa Uvuvi afanye ukaguzi.

Alisema Serikali inafanya uhakiki wa vyombo na wavuvi wote ili kubaini nani anavua wapi na kwa utaratibu upi. “Kamati ya Ulinzi na Usalama simamieni suala hili.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. Amos Kusaja kuhakikisha gari la kuhudumia wagonjwa la Kituo cha Afya cha Kasahunga linakuwa na mafuta wakati wote.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliodai kuchangishwa fedha za mafuta ya gari hilo mara wagonjwa wao wanapopewa rufaa kwenda katika hospitali ya wilaya.
Read More