Thursday, March 5, 2020

MAJALIWA: MTUMISHI ASIYEFUATA MAADILI HATUFAI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mtumishi wa umma asiyetaka kufuata maadili ya utumishi pamoja na maelekezo ya viongozi wake hafai kufanyakazi katika Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Machi 5, 2020) wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Korogwe na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa TTC Korogwe akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Tanga.

Waziri Mkuu alisema uaminifu na uadilifu ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na watumishi wa umma nchini, hivyo aliwataka watumishi hao wasijiingize kwenye mambo ambayo hayana tija katika utumishi wao.
Alisema Serikali inataka kila mtumishi wa umma nchini awajibike kwa kufanya kazi kwa bidii na kufuata maadili ya kiutumishi na kwamba haitomvumilia mtumishi ambaye ni mwizi, mbadhilifu, mvivu na haitosita kumchukulia hatua.

“Watumishi mnatakiwa muwahudumie wananchi bila ya ubaguzi wa aliyenacho na asiyekuwa nacho kwa sababu wananchi wote wana haki sawa ya kuhudumiwa, hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.” 

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa ahakikishe anawasimaia wakuu wa idara katika kupanga ratiba za kwenda vijijini kuwasikiliza wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero zinazowakabili.

Akizungumzia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo hilo na kuwataka wananchi waendelee kuwa na subra wakati suala hilo linashughulikiwa.
Waziri Mkuu alisemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. 

Kuhusu suala la upatikanaji wa umeme, Waziri Mkuu alisemamaeneo yote nchini yakiwemo ya wilaya ya Korogwe yatasambaziwa umeme kupitia Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

Alisema wakati wa usambazaji wa huduma hiyo wananchi hawatowajibika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwani tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali. “Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama ya sh. 27,000 tu.”

Kwa upande wao, Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava na Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda waliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, elimu na pia waliiomba iwasaidie katika kutatua changamoto ya barabara, maji na umeme.

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi kwenye mradi wa shamba la ufuta Mkomazi na kujionea miundombinu ya umwagiliaji. Pia Waziri Mkuu alizindua miradi ya ghala la kuhifadhia nafaka Mombo na alifungua maktaba ya chuo cha Ualimu Korogwe.

(mwisho)
Read More

Wednesday, March 4, 2020

MAJALIWA AZINDUA MRADI WA MAJI WA BOKWA WILAYANI KILINDI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa Maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi 4, 2020. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kushoto ni Mbunge wa Kilindi, Omar Kigua.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijaza maji katika ndoo wakati alipozindua mradi wa Maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi  4, 2020. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na kulia ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Mariam Mgaza Hassan.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba ndoo ya maji, Mariam Mgaza Hassan wakati alipozindua mradi wa maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi 4, 2020. 


Read More

Tuesday, March 3, 2020

KATIBU MKUU MWALUKO AITAKA IDARA YA MPIGA CHAPA MKUU WA SERIKALI YA KIDIGITALI



Na. OWM, ZANZIBAR

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko ameeleza kuwa Katika kuhakikisha  Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali inakidhi mahitaji ya wateja wake kwa kuzingatia ubora wa huduma, ameitaka idara hiyo kuwekeza kwenye  matumizi ya mashine za kidigitali ambazo zina uwezo wa uchapaji kwa kasi kubwa, viwango bora na kwa idadi kubwa ndani ya  muda mfupi.

Akiongea mara baada kutembelea Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar kwa lengo la kujionea namna Wakala inavyotekeleza majukumu yake, Katibu Mkuu Mwaluko amefafanua kuwa amevutiwa na utekelezaji wa majukumu ya Wakala kwa kuwa inaendesha shughuli za uchapaji kibiashara, inao usimamizi mzuri wa ubora unaozingatia teknolojia ya kisasa ya uchapaji, hivyo Idara ya Mpiga chapa Mkuu wa serikali ya Tanzania bara,  hainabudi kutekeleza majukumu yake kama ilivyo kwa Wakala.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Khalfan Sheikh Saleh, amefafanua kuwa Wakala umewekeza kwenye mashine za kidigitali na wamewajengea uwezo wafanyakazi wake, ambapo kutokana na uwezo huo wamefanikiwa kukidhi mahitaji ya wateja wake kwa wakati na kwa ubora husika.

Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Wakala wamefanikiwa kutekeleza Mpango wao wa biashara kwa kupata soko la uhakika la uchapaji hususani kwa Taasisi na idara za serikali pamoja na sekta binafsi, hivyo wamefanikiwa kuongeza mapato ya Serikali kupitia fedha zinazopatikana kupitia kazi za uchapaji na ununuzi wa vifaa vya ofisi na kuandikia.

Tangu mwaka 2018, Zanzibar imeanzisha rasmi Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, chini ya Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ambapo Wakala hiyo imepewa uwezo kisheria wa kutoa huduma za uchapaji. Kwa upande wa Tanzania bara, Idara ya Mpiga chapa Mkuu wa serikali ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa na jukumu la  kutoa huduma ya uchapaji.

Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa serikali imeabainisha lengo lake kuu kuwa,  ni Kutoa huduma za Uchapaji kwa wakati zenye ubora na  kwa gharama nafuu. Idara hiyo inaongozwa na  Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali ambaye husimamia vitengo vya Udhibiti wa Ubora, Uzalishaji, Ufundi, Masoko na Maduka ya Vitabu ya Serikali.
MWISHO


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu wa mashine za kidigitali wakati alipotembelea Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, , wakati alipotembelea Wakala huo, Maruhubi, Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Khalfan Sheikh Saleh akimueleza namna Wakala unavyotekeleza majukumu yake, wakati alipotembelea Wakala huo, Maruhubi, Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akiangalia namna mashine za kidigitali zinavyofanya kazi ya uchapaji wakati alipotembelea Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, Maruhubi, Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uchapaji wa Serikali Zanzibar, , wakati alipotembelea Wakala huo, Maruhubi, Zanzibar.

Read More

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA KIWANDA CHA KUCHAKATA NAFAKA , MKATA WILAYANI HANDENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo baada ya  kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kuchakata nafaka katika kijiji cha Mkata wilayani Handeni Machi 3, 2020.

Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKATA WILAYANI HANDENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mkata wilayani Handeni, machi 3, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mkata wilayani Handeni, machi 3, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mkata wilayani Handeni, machi 3, 2020.

Read More

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA HALMASHAURI HANDENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Machi 3, 2020.

Read More

MAJALIWA AVUTIWA NA UBUNIFU WA MKUU WA WILAYA YA HANDENI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefurahishwa na ubunifu wa Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe wa kupanda mhogo kwenye eneo lote linalozunguka makazi yake  badala ya kupanda maua na nyasi. Alisema ubunifu huo licha ya kumpatia mboga za majani na mhogo wa kula, ziada atauza  na kujipatia fedha. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akitazama mhogo huo, Machi 3, 2020. Wa pili Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela na kulia ni Mkuu huyo wa wilaya.

Read More

WALIOFUJA MALI ZA MKONGE KUCHUKULIWA HATUA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawachukulia hatua watu wote waliohusika na ubadhilifu wa mali zikiwemo nyumba za Mamlaka ya Mkonge Tanzania.
Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itafanya uchunguzi katika  mashamba yote ya mkonge ili kubaini yameendelezwa kwa kiasi gani na sehemu ambazo hazijaendelezwa zitachukuliwa na kugawiwa kwa wananchi ili walime  mkonge.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Jumanne, Machi 3, 2020) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Segera na Kabuku akiwa katika ziara yake ya kikazi wilaya ya Handeni, Tanga.
Machi 1, mwaka huu Waziri Mkuu alipokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali katika tasnia ya kilimo cha mkonge mkoani Tangana kuagiza mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yakiwemo ya kurejeshwa Serikalini kwa nyumba na. 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Bw. Salum Shamte yafanyiwe kazi.

Nyumba nyingine zilizopendekezwa kurejeshwa Serikalini ni pamoja na nyumba kumi zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone, Bombo, Nguvumali na Market street ambazo zilinunuliwa na watumishi hao kwa udanganyifu.

Timu hiyo maalum ya uchunguzi iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani Tanga kuanzia tarehe 29/11/2019 hadi tarehe 07/02/2020. Timu hiyo iliyokuwa na  wajumbe 13 ilihusisha maafisa kutoka ofisi mbalimbali za Serikali.

Waziri Mkuu amesema kwa kuwa katani ndio zao la biashara mkoani Tanga Serikali itahakisha watu wote wenye mashamba makubwa ya mkonge ambayo wameshindwa kuyaendeleza itayachukua na kuyarejesha kwa wananchi.
Wakati huo huo,Waziri Mkuu amesema Serikali imejenga vituo 352 vya afya nchi nzima vikiwemo viwili vilivyojengwa Handeni, kutokana na mahitaji makubwa ya huduma hiyo kata ya Segera itapewa kipaumbele katika awamu ya pili ya ujenzi.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ahakikishe wananchi wanaokwenda kufuata huduma za matibabu katika vituo vya afya na zahanati wanapatiwa dawa badala ya kuelekezwa kwenda kununua kwenye maduka ya watu binafsi.
Alisema Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka sh. bilioni 37 hadi sh bilioni 269, hivyo hakuna sababu ya mwananchi kwenda kwenda eneo la kutolea huduma ya afya na kukosa dawa. 
Pia, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Handeni ahakikishe kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama kwa kusimamia uchimbaji wa visima kupitia fedha za makusanyo ya ndani.
Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. 
Kuhusu suala la umeme, Waziri Mkuu amesemamaeneo ya wilaya hiyo ambayo bado hayajapata umeme yote yatasambaziwa umeme kupitia Mradi wa Nishati Vijijini (REA) na wananchi hawatowajibika kulipia gharama za nguzo.

Amesema Rais Dkt. Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inawaka umeme tena kwa gharama nafuu ya sh. 27,000, hivyo amewataka waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

 (mwisho)
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CHA JIJINI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Simba cha jijini Tanga wakati alipokitembelea Februari 3, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Simba cha jijini Tanga wakati alipokitembelea, Februari 3, 2020. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Marten  Shigela na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart. 

Read More

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wawekezaji katika sekta mbalimbali nchini wakiwemo wenye viwanda vya kuzalisha saruji.
Amesema katika kuhakikisha inalinda viwanda vya ndani vya kuzalisha saruji Serikali imeamua kuzuia uingizwaji wa saruji kutoka nje ya nchi.
Waziri Mkuu aliyasema hayo leo(Jumanne, Machi 3, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa kiwanda cha saruji cha Simba alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Amesema licha ya Serikali kupata kodi kutokana na uwepo wa kiwanda hicho, pia kimesaidia katika kutatua changamoto ya ajira hususani kwa vijana.
Naye, Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa wanazingatia sheria zote za madini ukilinganisha na viwanda vingine.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Reinhardt Swart alisema kiwanda hicho kinauwezo wa kuzalisha tani milioni 1.25 kwa mwaka lakini kutokana na mahitaji ya soko kinazalisha tani milioni 1.075 kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kiwanda hicho kimeajiri jumla ya wafanyakazi 319 kati yao wazawa ni 316 na watumishi watatu ni raia ya kigeni.
Pia, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.
Read More

Monday, March 2, 2020

MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA PAMOJA CHA FORODHA CHA HOROHORO MKOANI TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa  Mkinga, Danstan Kitandula wakati alipofungua jengo la Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mkinga na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri  hiyo, Machi 2, 2020. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma za Fordha cha Horohoro mkoani Tanga wakati alipokitembelea kituo hicho, Machi 2, 2020. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kituo cha dharura cha kuwapokea na kuwafanyia uchunguzi  watu  wanaoingia nchini  kupitia mpaka wa Horohoro mkoani Tanga ambao wataonyesha kuwa na dalili za kuumwa magonjwa ya kuambukiza. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu   na wa pili kushoto ni Naibu Waziri Nchi, Ofisi y Rais TAMISEMI, Mwita Waitara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka kwenye jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma za Fordha cha Horohoro mkoani Tanga wakati alipokitembelea kituo hicho, Machi 2, 2020. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. 
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kufungua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Machi 2, 2020. 




Read More

MAJALIWA: SIJARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA HOROHORO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ujenzi wa jengo la kituo cha pamoja cha huduma ya forodha kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro, Tanga ambacho ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 7.6.
“Jengo hili kuta tayari zimeshaanza kuvimba, kwa nini majengo ya TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) yanajengwa kwa kiwango cha chini na kwa nini mmeruhusu majengo haya yatumike,” amehoji Waziri Mkuu.
Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amemtaka Afisa Miliki wa TRA, Bw. Haruna Sumwa, mkandarasi aliyejenga jengo hilo pamoja na wote waliohusika na ujenzi huo wafike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma Machi 11, 2020.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo  (Jumatatu, Machi 2, 2020) wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilaya ya Mkinga mkoani Tanga. Amesema ni lazima majengo hayo yakidhi viwango.
“Hapa ni sura ya nchi ni lazima majengo yawe katika hali nzuri, haiwezekani mgeni anaingia na kuhudumiwa katika jengo chakavu, tutachukua hatua kwa yeyote aliyehusika, hizi ni fedha za umma lazima zitumike vizuri.”
Awali, Mkuu wa wilaya ya Mkinga Bw Yona Maki alisema ujenzi wa jengo hilo ulianza Julai 2011 hadi Septemba 2014 na lilianza kutumika Agosti 2015 likiwa na taasisi 16 za Serikali zinazofanyakazi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nyumba 62 za watumishi, maji safi na salama pamoja na upungufu wa watumishi.
Majukumu ya kituo hicho ni pamoja na kusimamia, kudhibiti uingiaji na utokaji wa raia wa Tanzania na wageni, kufanya doria na misako hasa kwenye vipenyo ambako wale wasiopenda kufuata taratibu hupenda kutumia.
Wakati huo huo,Waziri Mkuu ameendelea kusisitiza watu wote wanaoingia nchini kupitia mipaka mbalimbali wapimwe afya zao ili kulikinga Taifa na maambuki ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano na Serikali kwa kutoa taarifa za watu wanaoingia nchini bila ya kufuata taratibu. “Lazima tulinde nchi yetu katika kupambana na kuzuia magonjwa mbalimbali kwa kuhakikisha watu wote wanaingia nchini wawe salama.”
Pia, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga kuimarisha doria katika maeneo ya mpakani ikiwa ni pamoja na kukagua maroli kwa kuwa yanahusika na ubebaji wa wahamiaji haramu.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kutojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kuwa madhara yake ni makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Amesema wananchi wakatae kutumika katika kupitisha dawa za kulevya na atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. “Usikubali gari lako likatumika kubeba wahamiaji haramu wala dawa za kulevya kwani ukikamatwa linataifishwa.”
Waziri Mkuu amesema mwaka jana dawa za kulevya aina ya heroine gramu 746, bangi kilo 485, mirungi kilo 880 zilipitishwa katika wilaya hiyo kiawango ambacho ni kikubwa, hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya aimarishe doria. 
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Bw. Dunstan Kitandula alitaja changamoto zinazoikabili wilaya hiyo ikiwemo ya ukosefu wa maji safi na salama, ambapo Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imeshaanza kushughulikia suala hilo.
Read More

Sunday, March 1, 2020

MAJALIWA AWASILI TANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo  ameanza ziara ya kikazi ya Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza maelekezo  ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (kulia) aliyoyatoa kwa Watanzania ya kutosalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana ikiwa ni tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.  Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akisalimiana na Marubani na wahudumu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kuelekea Tanga , Machi 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo  ameanza ziara ya kikazi ya Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza maelekezo  ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (kulia) aliyoyatoa kwa Watanzania ya kutosalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana ikiwa ni tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati alipoowasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga,Machi 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo  ameanza ziara ya kikazi ya Mkoa wa Tanga kwa kutekeleza maelekezo  ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (kulia) aliyoyatoa kwa Watanzania ya kutosalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana ikiwa ni tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati alipoowasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga,Machi 1, 2020.


Read More

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA TIMU YA UCHUNGUZI WA MKONGE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali katika tasnia ya kilimo cha mkonge mkoani Tangana kuagiza mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yakiwemo ya kurejeshwa Serikalini kwa nyumba na. 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Bw. Salum Shamte yafanyiwe kazi.

Nyumba nyingine zilizopendekezwa kurejeshwa Serikalini ni pamoja na nyumba kumi zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone, Bombo, Nguvumali na Market street ambazo zilinunuliwa na watumishi hao kwa udanganyifu.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Machi 1, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri za mkoa wa Tanga, viongozi wa taasisi mbalimbali, wadau wa zao la mkonge pamoja na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa hoteli ya Naivera.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wawekezaji ambao wanamiliki mashamba ya mkonge yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 2,000 ambao hawajayaendeleza wayaendeleze wakishindwa yatachukuliwa na kugawiwa kwa wananchi.

Timu hiyo maalum ya uchunguzi iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani Tanga kuanzia tarehe 29/11/2019 hadi tarehe 07/02/2020. Timu hiyo iliyokuwa na  wajumbe 13 ilihusisha maafisa kutoka ofisi mbalimbali za Serikali.

Uchunguzi huo maalum ulihusu masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge mkoani Tanga ambayo ni pamoja na uzalishaji wa mkonge, bei ya zao la mkonge katika soko la ndani na nje ya nchi.

Pia, ilichunguza kuhusu mali za iliyokuwa Mamlaka ya mkonge nchini, ubia kati ya Kampuni ya Katani Limited na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Utendaji kazi wa Kampuni ya Katani Ltd na pia Utendaji kazi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB). 

Awali,Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. Gerald Kusaya alisema timu ilibaini kuwa Kampuni ya Katani Ltd tokea mwanzo ilikuwa na mgongano wa kimaslahi na kupelekea kuhujumu uchumi kwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake Bw. Salum Shamte alikuwa mtumishi wa umma na alishiriki vikao vyote vya ubinafsishaji wa Mamlaka ya Mkonge ilhali akijua kuwa ana maslahi kwenye Kampuni inayonunua. 
“Kwa kuwa uchunguzi umebaini viongozi na wanahisa wa Katani Ltd waliohusika kuingia mikataba walikuwa watumishi wa Mamlaka ya Mkonge wakati wa mchakato wote wa ubinafsishaji hivyo walitumia vibaya madaraka yao kwa kuishawishi Serikali kuingia mkataba huo usiokuwa na tija kwa Serikali bali kwa manufaa yao binafsi. Hivyo, Timu imeandaa taratibu kwa ajili ya wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.”

Bw. Kusaya amesema timu hiyo inapendekeza kuwa Serikali itoe fedha kwa ajili ya kazi ya kuyapima upya mashamba matano ya Mwelya, Ngombezi, Hale, Magunga na Magoma ili wananchi wanaoendelea kutumia mashamba hayo kwa kukodishwa na Bodi ya Mkonge kama ilivyokubalika kwenye Baraza la Mawaziri mwaka 2005 ili waweze kupewa Hati ndogo (leasehold tittle);

Alisema timu inapendekeza nyumba 30 zilizopo eneo la Muheza, ambazo baadhi zilitolewa kwa wananchi waliokuwa watumishi wa Mamlaka ya Mkonge na baadhi kuachwa kwa ajili ya makazi ziendelee kuwa mali ya wananchi hao kwa kuwa eneo hilo kwa sasa lipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.

“Nyumba 22 zilizoko ndani ya mashamba ya mkonge na maeneo ya kiwanda cha TANCORD ziendelee kubaki mali ya Serikali na nyumba iliyoko katika kiwanja Na. 176 eneo la Bombo iliyohamishwa kwenda kwa Ndg. Salum Shamte irejeshwe Serikalini kwa njia ya urekebishaji wa daftari la Msajili wa Hati.”

 Kwa upande wao, viongozi wa mkoa wa Tanga wakiwemo wabunge wamemshukuru Waziri Mkuu kwa kuunda timu hiyo ya uchunguzi wa zao la mkonge kwa kuwa mapendekezo yake yamejibu changamoto zilizokuwa zinalikabili zao hilo.

Wamesema mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yanakwenda kufufua kilimo cha zao la mkonge hivyo kuongeza tija kwa wakulima wa mkonge mkoani Tanga.

 (mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU AFUNGUA HUDUMA YA KUCHUJA DAMU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mradi wa huduma ya kuchuja damu  katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na kupunguza gharama ya kuwasafirisha wagonjwa wenye matatizo ya figo kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kufuata hiduma hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amefungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Makorora-Msambweni (km nne) iliyojengwa kwa thamani ya sh. bilioni 5.9 ambayo itarahisisha mawasiliano kwa wakazi wa kata za Msambweni, Makorora, Mzingani na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Waziri Mkuu amezindua miradi hiyo kwa nyakati tofauti jana (Jumapili, Machi 1, 2020) wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara  ya kikazi mkoani Tanga, ambapo alisisitiza azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaletea maendeleo wananchi wote. 

Alisema sekta ya afya imepiga hatua kubwa ukilinganisha na miaka minne iliyopita na Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na maboresho ya stahili za watumishi. Amewataka watumishi waendelee kuwa watulivu wawe na Imani na Serikali yao.

Alisema ni vema kwa watumishi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanafanyakazi kwa uaminifu na uadilifu ili wagonjwa wenye matatizo ya figo pamoja na matatizo mengine ya kiafya wapate huduma bora  bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Pia, Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao kuandaa utaratibu wa kutoa elimu kila siku asubuhi juu ya umuhimu wa kujikinga na magonjwa yanayoambukiza na  yasiyoambukiza ambayo ni hatari na ya gharama kubwa.

“Suala la mazoezi ni tiba muhimu na nyie wataalamu ambao mnajua ugonjwa huu tunautibu vipi ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, hivyo  andaeni nafasi ya dakika tano hadi kumi za kutoa elimu na kuhamasisha watu wajenge tabia ya kufanya mazoezi. Magonjwa mengine yanaweza kutibika kwa kufanya mazoezi na kubadilisha mitindo ya maisha.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imeboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi wake zikiwemo za afya, hivyo aliwaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali wahakikishe hakuna mwananchi anayekwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma na kukosa dawa au vipimo.

Akizungumza kuhusu barabara ya Makorora-Msambweni, Waziri Mkuu alisema mbali na kurahisisha mawasiliano pia itaboresha usalama na mazingira ya wananchi kutokana na uwepo wa taa za barabarani jambo litakaloongeza thamani ya makazi.

Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema huduma za figo nchini zilikuwa zinatolewa katika vituo 19 vya binafsi na hospitali tano za Serikali ambazo ni Hospitali za Kanda za Rufaa Muhimbili, Mbeya, Bugando, KCMC na Benjamin Makapa.

Waziri Ummy alisema hadi 2016 asilimia 90 ya huduma za kusafisha figo zilikuwa zinatolewa na sekta binafsi na asilimia 10 taasisi za umma. “Hali hii inasababisha huduma za usafishaji figo kuwa na gharama kubwa na kukosa uwiano wa huduma hasa kwa wananchi waishio mikoa ya pembezoni.”

Alisema Serikali imepanga kutanua huduma hizo ili ziweze kutolewa katika hospitali zote za rufaa za mikoa, ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo imeanza kwa hospitali za rufaa za mikoa ya minane ambazo ni Bombo-Tanga, Meru-Arusha, Mtwara, Iringa, Bukoba-Kagera, Maweni-Kigoma na Sekoutoure-Mwanza.

Waziri Ummy alisema uanzishwaji wa kituo kimoja cha kutolea huduma ya kuchujia damu hadi kuanza kufanya kazi kama kilivyo cha Bombo kinagharimu sh milioni 574,794,177, hivyo kwa vituo hivyo nane ambavyo mwezi huu vinataanza kutoa huduma vitagharimu sh. bilioni 4.5.

Kwa upande wao,wagonjwa wenye matatizo ya figo waliishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma ya kuchuja damu katika hositali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga kwa kuwa awali walilazimika kutumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Muhimbili.

Pia, Wagonjwa hao licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma, pia wameiomba iangalie uwezekano wa kupunguza gharama ili watu wengi waweze kumudu matibabu hayo kwani kwa sasa gharama ya session moja ni sh. 250,000.

(mwisho)

Read More

MAJALIWA AFUNGUA KITENGO CHA KUCHUJA DAMU KATIKA HOSPITALI YA BOMBO-TANGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua kitengo cha kuchuja damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Tanga ya Bombo, Machi 1, 2020.  Wa tatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Mwita Waitara na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua kitengo cha kuchuja damu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo, Machi 1, 2020. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela,  wa tatu kulia ni Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa pili kulia ni Mganga Mfawidhi  wa hospitali hiyo, Dkt. Naima Yusuf.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Christopher Nyange mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika  kitengo cha kuchuja damu baada ya kufungua kitengo hicho katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mganga ya Bombo, Machi  1, 2020.


Read More

MAJLIWA AFUNGUA BARABARA YA MAKORORA - MSAMBWENI JIJINI TANGA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kufungua  barabara ya Makorora-Msambweni jijini Tanga yenye uerfu wa kilometa  nne iliyogharimu sh. bilioni 5.9,  Machi 1, 2020 .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua barabara ya Makorora-Msambweni jijini Tanga yenye urerfu wa Kilometa  nne iliyogharimu sh. bilioni 5.9,  Machi 1, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Wa tatu Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu na wa nne Kulia ni Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Mwita Waitara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua barabara ya Makorora-Msambweni jijini Tanga yenye urerfu wa Kilometa  nne iliyogharimu sh. bilioni 5.9,  Machi 1, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Wa tatu Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu na wa nne Kulia ni Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Mwita Waitara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipofungua  barabara ya Makorora-Msambweni jijini Tanga yenye urerfu wa kilometa  nne iliyogharimu sh. bilioni 5.9,  Machi 1, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela baada ya kufungua  barabara ya Makorora-Msambweni jijini Tanga yenye urerfu wa kilometa  nne iliyogharimu sh. bilioni 5.9,  Machi 1, 2020.



Read More