Saturday, March 30, 2019

WADAU WA AFYA MOJA WAJENGEWA UWEZO WA KUFANYA TATHIMINI YA VIMELEA HATARISHI VYA MAGONJWA KWA DHANA YA AFYA MOJA


Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akifafanua umuhimu wa Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya nchini , Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 25- 28 Machi, 2019 Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wawezeshaji wa  mafunzo ya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja,wakifuatilia mafunzo hayo,  kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka Makao Makuu FAO, Sophie Von Dobchuetz, Mwakilishi  Makao makuu WHO, Caroline Ryan,wakifuatilia mafunzo hayo yaliyoofanyika , Jijini Dar es salaam. 
Mwakilishi kutoka Makao Makuu FAO, Sophie Von Dobchuetz akiendesha mafunzo ya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya nchini, Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wawezeshaji wa hapa nchini Tanzania na wamashirika ya Kimataifa  wakiendesha mafunzo ya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya nchini, Jijini. 
Baadhi ya washiriki wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa sekta za Afya juu ya namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakifanya majadiliano wakati  wa mafunzo hayo, Jijini Dar es salaam
Mwezeshaji kutoka Dawati la Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jubilate Bernad, akiendesha mafunzo ya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya nchini, Jijini Dar es salaam
Washiriki wa  mafunzo ya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (katikati) mara baada ya kufungua mafunzo hayo, Jijini Dar es salaam.
Read More

MAFUNZO YA TATHIMINI YA VIMELEA HATARISHI VYA MAGONJWA KWA DHANA YA AFYA MOJA YAFANYIKA KWA MARA YA KWANZA BARANI AFRIKA NCHINI TANZANIA.

Kwa mara ya kwanza Barani Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kufanya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Afya moja juu ya namna ya  kufanya tathmini ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia dhana ya Afya moja. Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalam na wadau wa Afya moja kutoka sekta mbalimbali, hususan sekta za afya ya binadamu, wanyama, kilimo na mazingira.

Kufuatia nchi ya Tanzania kuwa imepiga hatua katika uratibu wa  masuala  ya Afya moja, ambayo ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu, hali hiyo imechagiza kuchaguliwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa wataalam wa sekta za  Afya hapa nchini kupewa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 25-28 Machi, 2019, Jijini Dar es salaam, yaliendeshwa na wataalamu kutoka Makao makuu ya  Shirika la Afya Duniani (WHO), Makao makuu ya Shirika la Chakula Duniani (FAO), pamoja na Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (IOE). Wataalamu hao wameweza kuwapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya hapa nchini juu ya namna ya kufanya tathmini hiyo kwa magonjwa ya Kichaa cha mbwa, Kimeta na Homa ya Mafua ya ndege.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, alibainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha amefafanua kuwa  dhana hiyo inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa  yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu na hata mimea (mazingira) na kusababisha magonjwa na hata usugu wa vimelea vya magonjwa.
 
Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo  hayo wamebainisha kuwa  wamekuwa wakifanya tathmini za vimelela hatarishi vya magonjwa hapa nchini lakini tathmini hizo zimekuwa ni za kisekta kwani hazikuwa zinazingatia ushirikiano kwa maana ya dhana ya Afya moja. Aidha walifafanua kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kuandaa nyenzo ya kitaifa ya kufanya Tathimini kwa Dhana ya Afya Moja ambayo itawaongoza Wataalamu  hususani wanapokuwa katika maeneo halisi yanakotokea magonjwa.

Aidha, washiriki  hao walieleza kuwa Dhana ya Afya Moja inatumika zaidi kwa kuzingatia kuwa vimelea vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu asilimia (60%) vinatoka  kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari. Hata hivyo, kwa nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa kuzingatia kuwa Bara la Afrika hususan sehemu zinazokaribia mapori makubwa ya wanyama (Congo Basin) ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa(RVF), Marburg na mengineyo.

Walibainisha kuwa, Kupitia matokeo ya mwingiliano kati ya wanyama na binadamu, wadau wa afya moja wanawajibika kupanga mikakati mbalimbali ya udhibiti, ulinzi na usalama katika kuzuia, kujiandaa na kukabali magonjwa ambukizi. Moja ya mkakati ulioibuliwa Kitaifa na kimataifa ni kujiandaa kwa kuwafundisha  wataalam wa sekta mbalimbali za  afya jinsi ya kufanya tathmini ya  hatari ya vimelea vya magonjwa ambukizi kwa ushirikiano. 

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na WHO, FAO, IOE na wadau wengine wa Afya moja waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.

 MWISHO
Read More

Wednesday, March 27, 2019

UJENZI WA MJI WA SERIKALI WAKAMILIKA KWA 99%-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nia ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli ya kujenga upya mji wa Serikali imetekelezwa baada ya mji huo kukamilika kwa asilimia 99.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Machi 27,2019) alipotembelea mji mpya wa Serikali unaojengwa katika eneo la Mtumba, Jijini Dodoma. Majengo ya wizara 20 yamekamilika.

Katika ziara yake hiyo, Waziri Mkuu ametembelea na kukagua majengo ya Wizara 13, ambapo amesema ameridhishwa na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika maeneo mengi.

Hata hivyo katika maengo hayo ya wizara 13 aliyoyatembelea, Waziri Mkuu, alibaini kasoro kwenye mlango wa kuingilia katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amemuagiza mkandarasi anayejenga jengo hilo auondoe na aweke mwingine kwa kuwa mbao zilizotumika zipo chini ya kiwango na haupendezi.

Kadhalika, kuhusu ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambayo bado haikamilika, Waziri Mkuu amemuongezea siku 10 mkandarasi na kumtaka akamilishe.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu wahakikishe kazi iliyosalia ambayo ni ya kuboresha mazingira ya nje ya ofisi hizo iwe imekamilika ifikapo Apriri 15, mwaka huu. Mji huo unatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt. Magufuli.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema ujenzi wa mji huo ulianza Desemba mwaka jana na ulitarajiwa ukamilike Februari mwaka huu lakini utakamilika Mei mwaka huu.

Waziri Jenista alisema ujenzi wa majengo ya wizara tatu ambayo hayajakamilika ikiwa ni pamoja na OR-TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Wenye Ulemavu yatakamilika Mei mwaka huu.

 (mwisho)
Read More

Tuesday, March 26, 2019

WIZI WA MITIHANI UNALIVUNJIA TAIFA HESHIMA-MAJALIWA

*Awaonya Maafisa wanajihusisha na wizi waache mara moja

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaoshirikiana na waliamu kujihusisha na wizi, udanganyifu na uvujaji wa mitihani waache mara moja tabia hiyo na mwenendo huo kwa sababu unalivunjia heshima na hadhi Taifa.

“Kamati za Mitihani za Mikoa na Wilaya ziendelee kusimamia sheria, kanuni na taratibu bila ya woga, upendeleo na tusiyumbishwe na hatua za kinidhamu na kiutumishi kwa mujibu wa sheria.Hatua ziendelee kuchukuliwa dhidi ya wote wanaobainika kukiuka sheria, taratibu na miongozo inayotolewa”.

Waziri Mkuuametoa onyo hilo leo (Jumanne, Machi 26, 2019) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Sita wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya(REDEOA), uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo inasema “Elimu Bora Itatufikisha Katika Uchumi wa Kati Ifikapo 2025”

AmesemaBaraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni chombo ambacho kwa muda mrefu kimejijengea sifa kubwa sana nchini na barani Afrika, ambapo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali ili kukifanya chombo hiko kuwa imara na cha kisasa. 

Waziri Mkuu amesema hali hiyo imezifanya nchi mbalimbali kuja nchini kujifunza masuala ya upimaji na uendeshaji wa mitihani. “Nimejulilishwa pia hivi sasa hapa nchini wapo Viongozi wa Mabaraza ya mitihani kutoka nchi za Afrika Mashariki”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema suala la tatizo la nidhamu mbaya ya wanafunzi ni jukumu la walimu wote, hivyo wanatakiwa watekeleze majukumu yao ya kufundisha, kulea, kuwaongoza na kuwaendeleza wanafunzi kimwili, kiakili na kiroho kwa uadilifu na kuzingatia sheria. 

Waziri Mkuu amesema Serikali imesikitishwa sana na matukio ya hivi karibuni ya athari ya viboko kwa wanafunzi shuleni ikiwemo kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu pamoja na tukio la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa shule ya msingi Kibeta Mkoani Kagera. 

“Ninatambua si kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi lakini tukubaliane kuwa kuna udhaifu katika utaratibu wa utoaji na usimamizi wa adhabu ya viboko shuleni. Maafisa Elimu kawakumbusheni walimu wote nchini wazingatie mwongozo wa kutoa adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha sheria ya Elimu sura 353 pamoja na kanuni zake”.

“Adhabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule heshima. Na adhabu hii itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi. Nina hakika tukisimamia utaratibu, matukio haya yaliyoanza kuonekana yatakoma”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya hao kwa sababu wanafanya kazi kubwa ambayo imechangia kupandisha ufaulu wa kidato cha sita na cha nne nchini. Amewasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii.
Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka maafisa hao wawe wanatoa taarifa sahihi kuhusu idadi ya wanafunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.
Awali, Mwenyekiti wa REDEOA, Germana Mung’aho amesema umoja wao unatekeleza majukumu yao ya kusimamia elimu kikamilifu nchini, lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli, ambaye anasisitiza watu wafanye kazi.
Amesema umoja huo una wanachama zaidi ya 400 na ulianzishwa ili kusimamia utoaji wa elimu nchini. Katika mkutano huo wanatarajia kujadiliana changamoto mbalimbali za sera ya elimu na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Kadhalika, Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali iwapatie magari maafisa hao watakayoyatumia kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya elimu kwenye maeneo yao ya kazi, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

(mwisho)
Read More

Monday, March 25, 2019

YAMETIMIA TANZANIA YAFUZU MICHUANO YA AFCON

*Ni baada ya kuifunga Uganda the Craines magoli 3-0
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars, imekuwa miongoni mwa timu nne zilizofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kuifunga Uganda  'The Crane' magoli matatu kwa sifuri.

Mechi hiyo dhidi ya Taifa Stars na Uganda the Craines imechezwa katika Uwanja wa Taifa leo (Jumapili, Machi 24, 2019) ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwaongoza Watanzania kushuhudia mechi hiyo.

Taifa Stars imefuzu michuano hiyo itakayofanyika mwaka huu nchini Misri baada ya kupita miaka 39 tangu mara ya mwisho kucheza michuanohiyo.Timu hiyo kwa sasa imeungana na Burundi, Kenya na Uganda kufuzu michuano hiyo.

Magoli ya  Simon Msuva, Erasto Nyoni na Agrey Morris yalichangia kuivusha Taifa Stars, ambapoMsuva alianza kwa kuipatia gori timu ya Taifa ya Tanzania dakika ya 20 baada ya mechi hiyo kuanza, Nyoni aliipatia Taifa Stars goli la pili dakika ya 50 na dakika sita baadae Moris aliipatia timu ya Taifa goli la tatu.

Kufuatia ushindi huo wachezaji wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania wamejihakikishia kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 kutoka kwaKamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na wachezaji hao jana wakati Waziri Mkuu alipotembelea kambi yao, Makonda ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala yeye aliwaahidi kuwapeleka katika mbuga yoyote ya wanyama watakayoichagua kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

(mwisho)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezana na Rais wa TFF,  Wallace Karia baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha kumaliza mechi kati Taifa Stars na Timu ya Taifa ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salam, Machi 24, 2019.  Taifa Stars ilishinda 3-0.

Read More

Sunday, March 24, 2019

MAJALIWA ASHUHUDIA USHINDI WA TAIFA STARS DHIDI YA YA UGANDA

Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Boko akichanja mbuga kuelekea lango la Timu ya Taifa ya Uganda katika Mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Machi 24, 2019. Taifa Stars ilishinda 3-1.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Boko akichanja mbuga kuelekea lango la Timu ya Taifa ya Uganda katika Mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Machi 24, 2019. Taifa Stars ilishinda 3-1.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Machi 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Machi 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia bao la tatu la Taifa Stars katika mechi ya kufuzu kuingia katika michuano ya mataifa ya Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Machi 24, 2019.

Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA STARS

*Kamati yaahidi milioni 10 kwa kila mchezaji, iwapo watavuka 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa na kuwaeleza kwamba Serikali na wananchi wanamatumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa maendeleo makubwa yanayoendelea kupatikana katika soka nchini.

Waziri Mkuu ametembelea kambi hiyo leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) jijini Dar es Salaam na amewaeleza kuwa Serikali inaimani nao na kwamba wasiwe na wasiwasi kwa sababu hawana tofauti yoyote na wachezaji wa timu nyingine duniani.

“Macho yote ya Watanzania yameelekezwa katika mechi ya kesho na Serikali inamatumaini makubwa na timu ya Taifa, hivyo waelewe kwamba kesho ni siku muhimu sana. Lengo letu ni kufikia hatua ambayo mataifa mengine yamefikia”.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kamati yake itatoa sh. milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu hiyo iwapo timu itafuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON)

Makonda amesema Watanzania wanachokijua kwa sasa ni kwamba AFCON 2019 ni zamu yao, hivyo amewaomba wachezaji wa timu ya Taifa wahakikishe wanawapa furaha kwa kuifunga timu ya Taifa ya Uganda na kwamba wananchi wengi wamehamasika kwenda kuwashangilia.

Nae, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala ameahidi kuwapeleka katika mbuga ya wanyama kwa ajili ya mapumziko iwapo wachezaji hao wataibuka na ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda hapo kesho.

Dkt. Kigwangala amesema Serikali ipo pamoja na wanamichezo, ambapo amewataka wachezaji hao wa timu ya Taifa wakapigane kweli kweli kwa ajili ya Taifa lao. “Kesho muingie uwanjani kama askari wa nchi. Mkapiganie ushindi wa Taifa letu”.

Awali, Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samata amesema,”Ninafuraha si kwa sababu ya ukubwa wa mechi ya kesho bali ni kwa sababu naona kesho nakwenda kuongoza nchi. Tupo tayari kuliletea Taifa ushindi”.

(mwisho)
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TAIFA STARS

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa ya Soka - Taifa Stars jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala  na kulia ni Mwenyekiti wa TFF, Wallas Karia.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa  ya Soka – Taifa Stars baada ya kuzungumza nao  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. Wa tano kulia (mstari wa mbele), ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala  na wa sita ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.  Wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa  ya Soka - Taifa Stars, Mbwana Samata  baada ya kuzungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa  ya Soka - Taifa Stars, Mbwana Samata  baada ya kuzungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019.


Read More

Saturday, March 23, 2019

MHE. WAZIRI MKUU AKIHAMASISHA WATANZANIA KUISHANGILIA TAIFA STARS

Tukutane Taifa kesho bila kukosa 

Read More

WAZIRI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ZAMBIA, ITALIA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mheshimiwa Balozi Hassan Simba Yahya, ambapo amemtaka akaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.

Amekutana na Balozi Yahya leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na Zambia.

Pia, Waziri Mkuu amemtaka akakutane na wafanyabiasha wa Zambia na awahamasishe waje wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda. Amesema Balozi huyo anaweza kuandaa kongamano la biashara na uwekezaji kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Zambia ili kuboresha uchumi.

Kwa upande wake, Balozi Yahya amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia waje wawekeze nchini na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha. Ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Balozi Roberto Mengoni.

Akizungumza na Balozi huyo Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi hiyo. “Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo tunawakaribisha wafanyabiashara waje wawekeze”.

Amesema Tanzania iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote yaweze kufaidika, ambapo Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki yuko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.

Naye, Balozi Mengoniameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Italia, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza na amesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Mhe. Hassan Simba Yahya kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni  jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Italia Nchini, Mhe. Roberto Mengoni, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Italia Nchini, Mhe. Roberto Mengoni, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Machi 23, 2019. 
Read More

Friday, March 22, 2019

MAJALIWA AFUNGUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO LINDI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limkited (CSTC) baada ya kukifungua kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashra, Joseph Kakunda na wa pili kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga.  
ziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfuko wenye unga wa muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah.  Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga na kushoto ni Shift Leader wa CSTC, Samwel Ponera.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald Billet (kulia) wakifungua  kiwanda cha kuchakata muhogo cha CSTC kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye  Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa pili kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick   Clavier. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa pili kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick   Clavier.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya uchakataji muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata mhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi Machi 22, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah, Naibu Waziri wa kilimo, Omari Mgumba, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Mwenyekiti wa CSTC, Gerald Billet, Balozi wa ufaransa nchini, Frederick Clavier, Mkurugenzi Mtendaji wa CSTC, Christophe Gallean na kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzani Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.  Wa tatu kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier, wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CSTS, Christophe Gallean.


Read More

Thursday, March 21, 2019

SEKTA ZA AFYA NCHINI ZA SHAURIWA KUITEKELEZA AFYA MOJA


Maafisa viungo wa Afya moja kutoka Wizara, Idara, Taasisi,  Mashirika ya serikali na ya Kimataifa, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya Uongozi wa  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
Na. OWM,  MOROGORO
Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.

Kwa kutambua  umuhimu wa  Afya moja nchini, sekta za Afya zenye kujumuisha wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wametakiwa kuanza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia dhana hiyo ili uimarishaji wa Afya ya binadamu uwe wa Ufanisi na matokeo bora.

Akiongea wakati wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja kutoka Wizara, Idara, Taasisi,  Mashirika ya serikali na ya Kimataifa, mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Matamwe Jimmy, amefafanua kuwa tayari wataalamu hao wanao Mkakati wa kuzileta pamoja  Sekta za Afya kwa ajili ya kuzuia, kukinga na kuthibiti madhara na magonjwa yanayoikumba nchi yetu, yaani magonjwa ambukizi kati ya wanyama na binadamu pamoja na usugu wa vimelea vya magonjwa hivyo ni wakati wa kutekeleza mkakati huo kwa  kuitumia dhana ya Afya moja.

“Ninaamini kwamba, wote mnafahamu kuhusu tishio kubwa la magonjwa kama vile homa ya bonde la ufa, kwenye nchi za Afrika Mashariki , virusi vya Ebola Afrika Magharibi, kusambaa kwa kiasi kikubwa cha ugonjwa wa mafua ndege, (HPAI), matatizo ya kupumua yanayosababishwa na virusi vya Corona, mlipuko wa homa ya Lassa huko Africa Magharibi na homa ya Zika huko Amerika ya Kusini, kwa hiyo mifano michache magonjwa hayo yamekuwa tishio kubwa kwa afya ya binadamu na wanyama duniani kote.” Amesisitiza Kanali Matamwe.

Wakiongea wakati wa warsha hiyo wataalamu wa sekta za Afya hizo wamebainisha kuwa tayari wamekubaliana mfumo wa kutoa taarifa na kuhuisha utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na USAID na   Chemonics International wameandaa mkutano wataalam hao.
MWISHO.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akieleza  jambo wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
Mtaalamu wa Afya moja toka sekta ya Afya ya Mifugo, Dkt. Joseph Masambu akichangia juu ya  umuhimu wa dhana ya Afya moja nchini wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
Baadhi ya Wataalamu wa sekta za Afya , sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira  wakifuatilia  warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.

Mtaalamu wa Afya moja toka sekta ya Afya ya Binadamu, Profesa. Japhet kilewo akichangia juu ya  umuhimu wa dhana ya Afya moja nchini wakati  wa warsha ya  maafisa viungo wa Afya moja mjini Morogoro leo tarehe 26, Februari, 2019.
Read More

Tuesday, March 19, 2019

MAJALIWA AFUNGUA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO KANDA YA ZIWA JIJINI MWANZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua   Benki ya Mendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Ziwa kwenye Mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud Kwiruja  na wapili kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua   Benki ya Mendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Kanda ya Ziwa kwenye Mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud Kwiruja  na wapili kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo baada ya kufungua  Benki ya Maendeleo ya Kilimo  Kanda ya Ziwa kwenye Mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud Kwiruja na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo baada ya kufungua  Benki ya Maendeleo ya Kilimo  Kanda ya Ziwa kwenye Mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud Kwiruja na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) Kanda ya Ziwa lililofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.

Read More