WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Tanzania nchini Zambia, Mheshimiwa Balozi Hassan Simba Yahya, ambapo
amemtaka akaimarishe mahusiano baina ya nchi zote mbili.
Amekutana
na Balozi Yahya leo (Jumamosi, Machi 23, 2019) katika Ofisi ya Waziri
Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine
amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia
kati ya Tanzania na Zambia.
Pia,
Waziri Mkuu amemtaka akakutane na wafanyabiasha wa Zambia na
awahamasishe waje wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.
Amesema Balozi huyo anaweza kuandaa kongamano la biashara na uwekezaji
kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Zambia
ili kuboresha uchumi.
Kwa upande wake,
Balozi Yahya amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote
aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara pamoja na kuboresha
ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia waje
wawekeze nchini na Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha. Ameyasema
hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini,
Balozi Roberto Mengoni.
Akizungumza
na Balozi huyo Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es salam, Waziri
Mkuu amesema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi
hiyo. “Serikali imedhamiria
kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza uchumi na kufikia wa kati
ifikapo 2025, hivyo tunawakaribisha wafanyabiashara waje wawekeze”.
Amesema
Tanzania iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha
wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote
yaweze kufaidika, ambapo Ofisi yake kupitia Waziri mwenye dhamana ya
Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki yuko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia
wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.
Naye, Balozi Mengoniameishukuru
Serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Italia,
hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza na amesema wapo
tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa
kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa.
|
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.