NA.MWANDISHI
WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde amewaasa wanawake
kudumisha upendo na umoja katika kushiriki shughuli za maendeleo nchini kwa
kushikamana pamoja bila kujitenga.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2019 katika Viwanja vya
Mashujaa Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista Mhagama.
Maadhimisho ya mwaka huu yana
kauli mbiu inayosema “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa
Maendeleo Endelevu”
Naibu Waziri alibainisha
miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanawake ni pamoja na
kukosekana kwa umoja, upendo na ushirikiano ambao unawaga katika makundi na kusababisha
wanawake kutokuwa na maendeleo ya pamoja.
“Niseme ukweli japokuwa
hamtaupenda kwa leo, miongoni mwa sababu zinazowakwamisha katika kuendelea ni tabia
ya chuki miongoni mwenu, umbeya na makundi yasiyoleta tija za
kimaendeleo,”alieeza Mavunde
Aliongezea kuwa, wanawake
wanapaswa kubalidi mitazamo na tabia ambazo zinawaga na kuondoa upendo kati yao
na kujikuta wanajitenga hivyo, kupunguza nguvu kazi ya pamoja katika uzalishaji
na kuchangia kusuasua kwa maendeleo yao.
Aidha Mavunde alieleza kuwa,
kwa kuzingatia mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo nchini ni vyema
wakaishi kwa upendo na umoja ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania ya
Viwanda.
“Kimsingi wanawake ni nguzo
imara inayotegemewa na Taifa kwa kuzingatia uthubutu na namna Mungu alivyowapa roho
ya kuvumilia na kuwaamini katika utendaji wenye uadilifu,”alisisitiza Mavunde
Aidha alieleza kuwa kwa
kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu jamii haina budi kutathmini hatua
tulizofikia kama Taifa katika masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji
wanawake na wasichana na kutumia maadhimishi hayo kama fursa ya namna bora ya
kukabili changamoto zinazowakabili wanawake katika kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Kamati ya Wanawake TUCTA Bi.Rehema Ludanga alieleza furaha yake kwa mwitikio
mkubwa wa Wanawake Mkoani Dodoma kwa ushiriki wao pamoja na kuipongeza Serikali
kwa jitihada zake za kuendelea kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa kuanzisha
madawati ya jinsia ambayo yanatoa fursa za kutetea haki za wanawake nchini.
“Kipekee nawapongeza
wanawake wote waliojitokeza kuiadhimisha siku hii muhimu pamoja na Serikali
yetu sikivu kwa jitihada zake za kuendelea kuwaangalia wanawake na haki zao kwa
kuanzisha madawati ya jinsi 422 nchini yanayotoa fursa za kusikiliza masuala
yanayowakabili wanawake nchini,”alisisitiza Rehema
=MWISHO=
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.