NA.MWANDISHI
WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama leo
Machi 2, 2019 amefungua warsha ya mafunzo kuhusu Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi
la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanga, Tanzania.
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wadau 70 wakiwemo
viongozi Waandamizi na Watendaji Wakuu wa Mkoa wa Tanga, Wafanyabiashara wa
mkoa huo pamoja na wanahabari na kufanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa
kufungua warsha hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku mbili (Machi 02 na 03,
2019),Mhagama alisema Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kutumia fursa ya
mradi huo katika kujiletea maendeleo yao nan chi kwa ujumla.
“Mkutano huu wa leo ni matumaini kuwa, utaleta mageuzi
makubwa ya mipango mikakati yetu ili kuangalia fursa za ujio wa mradi huu kwa
kuzingatia ni moja kati ya mradi unaotarajiwa kuwa na manufaa mengi kwa nchi katika kuzalisha ajira,
kuendeleza urithishaji wa ujuzi na teknolojia pamoja na ubia kati ya makapuni
ya Tanzania na wageni,”alisema Mhagama
Waziri aliongezea kuwa, inawapasa wananchi kutumia
warsha hiyo kujadili na kuweka mikakati bora ya kuzitumia fursa zitakazotokana
na mradi kwa kuzingatia malengo mahususi ikiwemo kujadili maendeleo ya mradi na
fursa za ushiriki wa Watanzania katika ujio ya mradi pamoja na kuwa na majadiliano
kati ya Sekta Bonafsi ya Umma ili kuchochea maendeleo endelevu ya kiuchumi
Aliongezea kuwa, mradi huo utasaidia jamii kushiriki
kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia kuwa, ni zaidi ya robo
tatu ya Bomba hili litapita Tanzania na kuwanufaisha wananchi wake.
“Matarajio ni makubwa kwa kuzingatia mradi huu
unatarajiwa kupita katika mikoa 8 ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora,
Singida, Dodoma, Manyara na Tanga ambapo litapita katika Wilaya 24, Kata 134 na
Vijiji zaidi 180 hivyo hatuna budi kuchangamkia fursa kwa kuongeza jitihada za
ongezeko la ushiriki wetu,”alisistiza Mhagama
Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Mhe.Martine Shiga aliendelea kuhimiza watendaji wake kushiriki kikamilifu
katika hatua zote za maandalizi kama Mkoa ili kuona namna bora za kushiriki
katika fursa hiyo kubwa ya kujileea maendeleo yao.
Naye Katibu Mtendaji, Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa alieleza jitihada za
Baraza ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data ya nguvu kazi ambayo inachukua takwimu
za wafanyabiashara ili kiuwatambua kwa lengo la kushirikisha katika program na
kuona namba bora ya kuwashirikisha katika fursa hizo.
“Niwaombe watanzania
kuendelea kujisajili katika kanzi data ya nguvu kazi ili tuweze kuwatambua,
uwezo na changamoto zenu na kuwashirikisha katika miradi mbalimbali ukiwemo huu
wa bomba la mafuta pamoja na kutatua changamoto hizo,” alisisitiza Beng’i
AWALI
Warsha ya mafunzo hayo imeratibiwa na Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa ufadhili wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF)
kupitia BEST Dialogue Tanzania kwa lengo la kuwezesha viongozi na
Wafanyabiashara wa Mkoa huo kufahamu maendeleo na fursa zitakazotokana na mradi
huo.Bomba hilo la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki lina urefu wa KM 1,443 kati
ya hizo KM 296 zipo nchini Uganda na KM 1,147 zipo Tanzania
=MWISHO=
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.